Monday, April 7, 2014

Je, Yesu alisema kuwa Yeye ni Mungu?




“Wahubiri wa injili” wa Kiislamu huwa wanapinga kuwa Yesu ni Mungu na unapowakatalia wanakwambia, “Lete andiko.” Maandiko yapo mengi sana ndani ya Biblia juu ya ukweli kwamba Yesu ni Mungu. Ni mengi mno!

Ukishawapa andiko, wanabadilika na kusema, “Nataka maneno aliyoongea Yesu mwenyewe.”

Hiki ni kigezo POTOFU na si cha kibiblia hata kidogo. Ukweli ni kwamba, Biblia YOTE ni Neno la Mungu. Haijalishi amezungumza Musa, Isaya, Yohana, Petro au Yesu mwenyewe. Imeandikwa:
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. (2Petro 1:21).


Hivyo, kudai kwao eti, “Nataka maneno aliyosema Yesu mwenyewe,” ni kigezo batili na kisicho na mantiki hata kidogo.
  

Ufuatao ni ushahidi wa kibiblia kwamba YESU KRISTO  ni Mungu.

Yohana 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye IBRAHIMU ASIJAKUWAKO, MIMI NIKO.

NIKO ni jina la Mungu peke yake. Tunakutana na jina hilo pale Musa alipoongea na Mungu na kutumwa kuwakomboa wana wa Israeli kutoka Misri. Imeandikwa:
Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n'nani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO (Kutoka 3:13-14).

Mwanadamu yuko kwa sababu Mungu alisababisha awepo. Gari liko kwa sababu injinia au mbunifu alisababisha liwepo. Nyumba ipo kwa sababu fundi alisababisha iwepo. Lakini Mungu YEYE YUKO TU!! Hayupo kwa kusababishwa na yeyote! Ndiyo maana akasema MIMI NIKO AMBAYE NIKO! Yesu ni NIKO. Kwa hiyo, Yeye ni Mungu.

Yohana 10:30
Mimi na Baba tu umoja.

Waislamu wana msemo wao kwamba eti, Yesu na Mungu ni wamoja katika malengo, si katika asili yao. Basi huwa nawauliza swali kuhusu aya ifuatayo ya Isaya, nao wanazimika na kukosa jibu:

Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu MTOTO amezaliwa, Tumepewa MTOTO MWANAMUME; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, Mfalme wa amani.

Aya hii iko wazi kabisa. anayetajwa ni Yesu kwamba Yeye ni Mungu mwenye nguvu.


Yohana 14:9
Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?

Maneno haya Yesu aliyasema baada ya kuulizwa swali lililo wazi kabisa, ambalo lilikuwa na lengo la kumjua MUNGU BABA! Imeandikwa:
Filipo akamwambia, Bwana, UTUONYESHE BABA, yatutosha.  Ndipo Yesu akajibu waziwazi: ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA. Maana yake ni kuwa, “Mimi ndio Baba mwenyewe.”

Ufunuo 1:17 na Ufunuo 22:13
Mimi ni wa kwanza na wa mwisho
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.


Ni Mungu TU ndiye mwenye uwezo wa kuwa wa kwanza na wa mwisho; Yesu ni Alfa na Omega. Kwa hiyo Yeye ni Mungu.

Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye NENO ALIKUWA MUNGU.

Andiko hili Waislamu hawalipendi kabisa. ni kwa sababu liko wazi mno. Yesu ni Neno; na Neno ni Mungu; hivyo, Yesu ni Mungu!

Yohana 20:28
Tomaso akajibu, akamwambia, BWANA WANGU NA MUNGU WANGU!

Tomaso aliposema hivi, Bwana Yesu hakukanusha na kusema, “Mimi sio Mungu.” Badala yake: Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki. (Yoh 20:29). 


Matendo 20:28
Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, ALILOLINUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE.

Ni Mungu gani mwenye damu huyu? Jibu liko wazi. Huyu ni Yesu Kristo. Huyu ndiye aliyetoa uhai wake na kumwaga damu yake msalabani; na hapo ndipo alipoanzisha Kanisa.


Wakolosai 1:16
Kwa kuwa KATIKA YEYE VITU VYOTE VILIUMBWA, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.


Katika Yeye Yesu vitu vyote viliumbwa. Ina maana kuwa vitu vyote vilitokana na Yesu; maana Yesu ni Neno la Mungu. Na tunajua kuwa Muumba wa vitu vyote ni Mungu; hivyo, Yesu ni Muumba – Yeye ni Mungu!!

Wakolosai 2:9
Maana KATIKA YEYE UNAKAA UTIMILIFU WOTE WA MUNGU, kwa jinsi ya kimwili.


Sisi sote ni watu wasio wakamilifu. Tunaanguka tena na tena kwenye dhambi. Kwa hiyo, hakuna mwanadamu wa kawaida ambaye anaweza kujigamba kwamba yeye ametimia kama alivyo Mungu. Lakini katika Yesu “utimilifu WOTE wa Mungu unakaa.” Kwa nini? Kwa sababu Yeye ndiye Mungu huyohuyo.

1Timotheo 3:16
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. MUNGU ALIDHIHIRISHWA KATIKA MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.


Ni Mungu gani aliyedhihirishwa katika mwili? Jibu liko wazi. Ni Yesu Kristo peke yake.

Tito 2:13
….tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU

Yesu Kristo ni Mungu Mkuu!!

Shida KUU ya Waislamu ni hii: Wanampima Mungu kwa vigezo vya kibinadamu. Mungu anasema: Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza? (Yer 32:27) 

Jibu liko wazo. HAKUNA!
Lakini utakuta Waislamu wanauliza maswali ya ajabu sana. Eti, kama Yesu ni Mungu, wakati amekufa, nani alikuwa anaangalia dunia?

Hili ni swali linalofaa kuulizwa juu ya kiumbe. Kama tungesema kuwa mwanadamu fulani alikuwa amekufa, ndipo kuna mantiki kuuliza kwamba, wakati amekufa nani alikuwa anatunza familia yake? Maana hili ni swali linalohusu tabia za kibinadamu kwa kuwa mwanadamu hawezi kuwa mahali kuwili au zaidi kwa pamoja. MUNGU SI MWANADAMU! ANAWEZA YOTE – NA HASA MUNGU WA IBRAHIMU, ISAKA NA YAKOBO!

YESU NI MUNGU MILELE NA MILELE!!

HALELUYA!!

Tafakari

Hoji mambo

Chukua hatua!

22 comments:

  1. Unaonekana jinsi gani ulivyo na akili kama ya kuku. Kwa yeyote anayesema hivyo ni kwamba ni mvivu wa kusoma, kujifunza na kufuatilia vitu. Fuatilia ujue jinsi biblia alianzishwa na nani? na walifanyeje? na ni nani aliyeanzisha ukristo. Na je ukristo ulianzishwa kabla ya yesu au baada? pia fuatilia ni wakina nani waliohusika kujadili maneno ya waandishi kisha kuongeza na kupunguza? pia fuatilia ujue kuna waandishi wangapi walioandika gospel (injili) na waandishi wangapi walioandika biblia? na pia fuatilia ujue kuna version ngapi za biblia? mwisho fuatilia matendo na ibada waliyokuwa wanafanya wapagani kipindi hicho kisha linganisha ukristo. fuatilia sikukuu ya chrismass tarehe yake inahusiana na siku gani? Tusijidanganye jamani Mungu ni mwenye busara, hekima, muadirifu sana. Haiwezekani kuwa muislam tu ndio uende peponi au kuwa mkristo tu ndio uende peponi. Wengi wetu tumekuwa waislamu au wakristo bakutokana na wazazi wetu. Kwahiyo Mungu anasema hautakiwi kujisifia kuwa ni muislam au mkristo Bali unatakiwa kuwa mwenye kuamini. Na kuamini ni kwamba kaa tafakari juu ya uumbaji wake, ulimwengu, na angalia ishara za mwenyezi Mungu kwa binadamu. Najua jinsi tulivyokuwa kwa asili ni kwamba Muislamu humchukia sana mkristo na kujiona yupo sahihi alikadharika mkristo humchukia sana muislam naye hujiona yupo sahihi. Kuna ishara nyingi sana za Mungu zilizopo waziwazi kuonesha kuwa yeye ndio Muumba wa vitu vyote ulimwenguni. Tuache kuwa na mapokeo tuu na kushikwa macho na masikio jamani tufuatilie vitu. Tusidangangike kwa vitu vilivyowazi. Elimu na ufuatiliaji ni kitu cha msingi sio kuvaa msalaba au kuwa na sijida kubwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. shalom, shalom rafiki.

      Mimi nasema, bora kuwa na akili kama kuku inayoongea vitu kwa ushahidi wa Maandiko kuliko kuwa na akili ya "profesa" iliyojaa maoni na mitazamo binafsi.

      Umesema mengi lakini ni maoni yako tu ambayo hayana ushahidi hata wa neno moja kutoka kwenye maandiko - au hata kutoka kwenye historia ya kawaida.

      Nakukaribisha uongee kwa ushahidi ndipo mtu anaweza kutilia maanani usemacho.

      Delete
    2. Shalom Shalom James!

      Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa ajili ya madhabahu hii, sofa utukufu heshima ni vyake. Ninauhakika Mungu haitaji msaada wa mawazo, hekima, na mitazamo ya kibinadamu; na mahali tunapopatafuta hatuwezi kupafikia kwa nguvu za ushawishi wa dunia hii unaotokana na elimu ya dunia hii ambayo ipo kinyume kabisa.

      Hivyo naomba Mungu amsaidie huyu ndugu na wengine wa namna yake kuwa hapa kwenyekwenye hii madhabahu hatuongelei elimu ya masokwe kubadilika na kuwa watu!!!! ILA ILA tunaongelea ELIMU ya BABA WA MBINGUNI inayotokana na NENO lake kwa ROHO MTAKATIFU.

      Kwa hali hiyo hiyo bila kunyenyekea kwa Roho wa hatuwezi kwenda mahali popote. Kwahiyo angalizo kwako unayefikiri MUDA unapotezwa bure hapa! Unakosea kabisa, mahali hapa TUNAUOKOA MUDA ili wengi wasiachwe na MUDA. Hivyo tafadhari tafadhari nafasi ya MTU kutumika ili kuupoteza MUDA KUPITIA MADHABAHU HII HANA NAFASI. KAMA UNAHITAJI KUJIFUNZA INGIA KWENYE MAANDIKO.

      Shalom Shalom.

      Delete
    3. Shalom Shalom James!

      Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa ajili ya madhabahu hii, sofa utukufu heshima ni vyake. Ninauhakika Mungu haitaji msaada wa mawazo, hekima, na mitazamo ya kibinadamu; na mahali tunapopatafuta hatuwezi kupafikia kwa nguvu za ushawishi wa dunia hii unaotokana na elimu ya dunia hii ambayo ipo kinyume kabisa.

      Hivyo naomba Mungu amsaidie huyu ndugu na wengine wa namna yake kuwa hapa kwenyekwenye hii madhabahu hatuongelei elimu ya masokwe kubadilika na kuwa watu!!!! ILA ILA tunaongelea ELIMU ya BABA WA MBINGUNI inayotokana na NENO lake kwa ROHO MTAKATIFU.

      Kwa hali hiyo hiyo bila kunyenyekea kwa Roho wa hatuwezi kwenda mahali popote. Kwahiyo angalizo kwako unayefikiri MUDA unapotezwa bure hapa! Unakosea kabisa, mahali hapa TUNAUOKOA MUDA ili wengi wasiachwe na MUDA. Hivyo tafadhari tafadhari nafasi ya MTU kutumika ili kuupoteza MUDA KUPITIA MADHABAHU HII HANA NAFASI. KAMA UNAHITAJI KUJIFUNZA INGIA KWENYE MAANDIKO.

      Shalom Shalom.

      Delete
    4. Ubarikiwe sana mtumishi wa Bwana Revocatus. Hakika ni kweli Bwana ndiye mwenye sifa zote. Na nje yake ni vigumu sana kujua tofauti kati ya giza na nuru. Bwana ataendelea kuwafikia watu wake popote pale walipo huku Roho wake akiweka nuru ya Kristo ndani ya mioyo ya watu kupitia Kweli yake.

      Shalom shalom mtumishi.

      Delete

  2. Mimi, nawasikitikia sana ndugu zangu katika Adamu, Wakristo. Hivi kwanini mnayatukuza sana mafundisho ya wanadamu kuliko ya Mungu Mwenyezi? Ni watu gani nyie? Mnajifanya Biblia mnaiyelewa kumbe wote ni mbumbumbu maskini ya Mungu. Hakuna mnachoelewa hata kimoja! Umewajaa UPAGAN vichwani mwenu,basi amtaki hata la kwambiwa.
    Kinacho nishangaza mimi, maagizo ya Mungu kwenye biblia yenu mnayaona na hamtaki kutekeleza, badala yake, mnaenda kinyume chake.
    Ahadi ya Mungu kwa Waisraeli ni kuwaletea mwokozi wa zambi zao, binadamu Yesu, kutoka ukoo wa Nabii Daudi.Kwa maneno mengine, Mungu kamtuma Yesu kama alivyokawatuma akina Mussa, Daudi, Mohammad na wengine, kuubeba ujumbe maaluum kutoka kwake Mungu kwa ajili ya kuwaokoa jamaa zake na zambi zao. Kwa hiyo, Musa, Daudi,Yesu na Muhammad kwa sababu walibeba ujumbe wa Mungu kwa wanadamu wa enzi zao walikuwa wawakilishi wa Mungu Mwenyezi hapa duniani.
    Mungu ni mkuu kuliko yeyote yule mpaka Yesu: Yn.14:28”Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.”
    Mungu anaemwabudu Yesu ni yule yule wetu sisi:Yn.20:17 “Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.”
    Kifungu cha Yn.8:58 hakiwezi kuwa kigezo cha Yesu kuwa Mungu kwa sababu, kuna watu wengine wenye sifa kama hizo na bado hawajawa Miungu:
    Nabii Suleimani anaripotiwa katika Mithali 8:23-27, ya kuwa amesema, “Nalitukuka tokea milele, tangu awali, kabla haijawako dunia. Wakati visipokuwako vilindi nalizaliwa, Wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa maji. Kabla milima haijawekwa imara, Kabla ya vilima nalizaliwa. Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makonde, Wala chanzo cha mavumbi ya dunia; Alipozithibitisha mbingu nalikuwako…"
    Kwa mujibu wa Ayubu 38:4 na 21, Mungu amemtambulisha Nabii Ayubu kama ifuatavyo: “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa unafahamu.”
    Yn.10:30: kifungu hiki hakiwezi pia kumfanya Yesu awe Mungu. Tukiangalia kifungu kingine cha Yn.17:21-23 tunakuta kwamba kumbe nao wanafunzi wa Yesu wana umoja na Mungu na Yesu:”21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
    22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.
    23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.”
    Kuhusu Isaya 9:6 umezidi kujichanganya ndugu yangu, maana ujui unachokijadili. “...Mtoto ATAITWA JINA LAKE Mshauri wa Ajabu, Mungu mkuu...”ndio iwe sababu ya yeye kuwa mungu? Yani wewe ukiitwa jina lako DUNIA, utakuwa dunia? Hili si jina tu!!? Wakristo mnatia aibu!!!
    Kifungu cha Yn.14:9 tukienda sambamba na akili zako zinavyokutuma kitakuwa kinapingana ni hivi hapa:
    kutoka 33:20, Mungu anamwambia Musa: "Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi".
    Yohana 5:37, ambapo Yesu anasema: "Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Nanyi hamjapata kamwe kusikia sauti Yake, wala kuuona uso wake".
    ITAENDELEA

    ReplyDelete
    Replies
    1. POLE SAna ndugu hujui hata moja unatemblea kuikariri ,, unahitaji kujifunza elimu ya utatu wa Mungu ndipo utaelewa kwa nn Yesu alizungumza hayo ,, bible haijakosewa wala Yesu hajakosea na hawez kujikataa kuwa yy sio Mungu , waislamu bado sana ktk elimu ya roho mpo kimwili

      Delete
  3. INAENDELEA
    Lakini kwa mtu mtaalamu wa lugha kwake yeye ni rahisi sana kuelewa nini alikuwa anakusudia Yesu aliposema “ALIYENIONA MIMI AMEMUONA BABA”.
    Sikilizeni nyie wakristo mbumbumbu, Mungu Mwenyezi ni MUUMBA WA KILA KIUMBE. Kwa maana hiyo,yeye sio KIUMBE.
    YESU, kwa kuwa yeye ana UMBO,ina maana AMEUMBWA NA MUNGU. Na kwa kuwa yeye KAUMBWA na MUNGU, basi HAWEZI KUWA MUNGU!
    MFANO: Mwanadamu kaumba computer, lakini mwanadamu hawezi kuwa computer, na computer haiwezi kuwa mwanadamu.Ila, Mwanadamu anaweza kuchagua computer moja, kwenye system ya computer 10 au zaidi,iwe kiongozi wa zingine ili kurahisisha mipangilio yake. Kwa hiyo, ile computer kiongozi haiwezi kuwa Mwanadamu eti kwa sababu inafanya kazi za Mwanadamu. NEVER!!!!
    Mwisho kabisa, ningependa kuwasii ndugu zangu Wakristo kwamba, Mwenyezi Mungu anapotaka kufanya jambo lenye manufaa kwa wanadamu anakuwa na kawaida ya kutoa ahadi. Na ahadi ya Mungu kwa Waisraeli ni kuwapelekea mtume sio Mungu kama inavyohubiriwa na wasioelewa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yani mnapokosea ni kuzani kutukana watu ndio kuwaelewesha kiasi gani unaonekana una umejaa Jazba unawaita mbumbumbu mara wapumbavu hiyo ndio hakima ya elimu yako ya kiislam je sisi tunao jifunza kwako kwa hakima hii tutakuelewa kweli, mbona Mtoa mada hana Jazba wala shaka na huja yake kaileta kwa heshima bila kumtusi mtu?

      Delete
  4. mtoa mada ni mpumbavu..

    Akili huna

    ReplyDelete
    Replies
    1. NYIE WAKRISTO NI MBUMBUMBU KWELI KWELI, SOMA HII KAMA UJASILIM BASI TENA SUBIRI MOTOOOOO TU

      90 Verses says: Jesus is not God
      Compiled by TMAI
      All four Gospels record Jesus as saying, "Blessed are the peace-makers; they will be called sons of God."
      The word ‘son’ cannot be accepted literally because in the Bible, God apparently addresses many of his chosen servants as ‘son’ and ‘sons.’ The Hebrews believed God is One, and had neither wife nor children in any literal sense. Therefore, it is obvious the expression ‘son of God’ merely meant ‘Servant of God’; one who, because of faithful service, was close and dear to God as a son is to his father.
      Christians who came from a Greek or Roman background, later misused this term. In their heritage, ‘son of God’ signified an incarnation of a god or someone born of a physical union between male and female gods. This can be seen in Acts 14: 11-13, where we read that when Paul and Barnabas preached in a city of Turkey, pagans claimed they were gods incarnate. They called Barnabas the Roman god Zeus, and Paul the Roman god Hermes.
      Furthermore, the New Testament Greek word translated as ‘son’ are ‘pias’ and ‘paida’ which mean ‘servant,’ or ‘son in the sense of servant.’ These are translated to ‘son’ in reference to Jesus and ‘servant’ in reference to all others in some translations of the Bible. So, consistent with other verses, Jesus was merely saying that he is God’s servant.
      Additional problems with Trinity
      To a christian, God had to take human form to understand temptation and human suffering, but the concept is not based on any clear words of Jesus. In contrast, God does not need to be tempted and suffer in order to be able to understand and forgive man’s sins, for He is the all knowing Creator of man. This is expressed in the verse:
      ‘And the Lord said: ‘I have surely seen the affliction of My people that are in Egypt, and I have heard their cry because of their taskmasters; for I know their pains.’ (Exodus 3:7)
      God forgave sin before Jesus’ appearance, and He continues to forgive without any assistance. When a believer sins, he may come before God in sincere repentance to receive forgiveness. Indeed, the offer to humble oneself before God and be saved is made to all humankind.
      ‘And there is no God else beside Me; a just God and a Savior; there is none beside Me. Look to Me, and be saved, all the ends of the earth; for I am God, and there is none else.’ (Isaiah 45:21-22, Jonah 3:5-10)
      Biblically, people can receive forgiveness of sins through sincere repentance sought directly from God. This is true at all times and in all places. There has never been a need for the so-called inter cessionary role Jesus plays in attaining atonement. The facts speak for themselves. There is no truth to the Christian belief that Jesus died for our sins and salvation is only through Jesus. What about the salvation of people before Jesus? Jesus’ death brings neither atonement from sin, nor is it in any way a fulfillment of biblical prophecy.
      Christians claim that in the birth of Jesus, there occurred the miracle of the incarnation of God in the form of a human being. To say that God became truly a human being invites a number of questions. Let us ask the following about the man-God Jesus. What happened to his foreskin after his circumcision (Luke 2:21)?

      Delete
    2. Inaalillaaah wainna ilayh raajiuun mmepotea ndg znu et yesu n mungu subhaanallaah daah wkt yesu mwenyewe alwaambia watu wa izrail wamwabudu Allah mola wng n mola wenu nyny xx mbn mwajtia adhabun ndg zangun funguken nyny

      Delete
    3. Weweh ni mbumbumbumbumbumbu zere%

      Delete
  5. Nyie mnaojiita wakristo (waabudu mungu - mtu Kristo) acheni kujitia ujinga na kuondoa uwezo wenu wa kufikiria sawasawa. Yesu angikuwa Mungu angewaambia wafuasi wake kuwa yupo baba ambaye ni mkuu (soma Yohana). Mwandishi anasema eti ametupatia mtoto tena mtoto wa kiume. Hivi kweli mungu anaweza kuzaliwa kutoka kwa mwanamke kama tulivyo binadamu wengine. Nawashauri msome quran vizuri kama hamuwezi bora msome vitabu vya mashahidi wa Yehova huenda vitawasaidia kuujua ukweli. Acheni kudanganyika na uchambuzi uchwara ambao haujengi hoja za msingi kuwa yesu ni mungu. Mjue kuwa mnamchukiza sana Mungu kwa kumpa daraja la Yesu. Ukristo wenu ni upagani uliofanyiwa maboresho kidogo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kisicho uchwara kwako si lazima kiendane na quran? hakuna uzima humo bali mauti tupu. Kama huna Yesu, Biblia inasema UMEKUFA. Na hiyo ni kweli iliyo wazi wala haihitaji tochi kuiona.

      Delete
    2. hivi we james john tatizo lako huoni maandiko au hua unakimbilia yale yenye utata utata kuyasoma ili uwadanganye watu wasioelewa lugha vizuri halafu ukielekezwa una panik tu wala hayo maandiko ya hapo juu hujayakosoa ila una dili na mchangiaji mda tu ila sio kupinga maandiko waliyokutolea me naona we upo kwa ajili ya kulazimisha watu ili nuendelee kubishana halaf unajifanya kama huoni unachofundishwa? hebu rejea yale maneno aliyosema yesu mwenyewe alipowekwa msalabani(heloi heloi ........) na uniambie yana maana gani?

      Delete
    3. Kaka ang james umepotea soma uelewe sio unakurupuka

      Delete
  6. Kwenye Amri zenu kumi inabidi isisomeke tena"Usiwe na miungu mingine ila mimi" iwe na wingi "Usiwe na miungu mingine ila sisi"

    ReplyDelete
  7. Yesu siyo Mungu umeeleza mengi Ila Akuna ukweri hapo

    ReplyDelete
  8. Yesu ni Mungu one day nyie wote mtaamini tu

    ReplyDelete
  9. Kwanini ndugu zetu mnakuwa wagumu wa mioyo je hamfatilii shuhuda za waislamu wenzenu jinsi yesu alivyowaokoa na kuwatokea je hamuoni waganga na wachawi wengi walikiri nguvu za yesu acheni ubishi tulizeni akili pigeni goti umuombe Mungu atawaonesha imani ya kweli.mungu awabariki

    ReplyDelete