Showing posts with label uislamu na ukristo. Show all posts
Showing posts with label uislamu na ukristo. Show all posts

Monday, January 6, 2014

Maswali yangu kwako Mwislamu




Tarehe 21 Desemba 2012 niliuliza maswali yafuatayo HAPA. Lakini umepita mwaka mzima bado sijapata jibu japo kwa swali hata mojawapo tu! Ina maana maswali haya hayana majibu kutoka kwenye Quran au labda ndugu zangu Waislamu hawajayaona? Of course mimi binafsi najua kuwa hawawezi kuyajibu kwa sababu Uislamu hauna majibu juu ya masuala ya rohoni.

Hata hivyo, ningependa niyaulize kwa mara nyingine tena hapa tunapoanza mwaka huu wa 2014 ili iwe changamoto kwa Mwislamu uwaye yote – ujihoji, ujiulize na ujipime kule uendako.

Sunday, April 21, 2013

Mamilioni ya Waislamu Afrika Wanamkimbilia Yesu Kristo Isivyo Kawaida





 “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika 
ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa 
yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja” 
(Mathayo 24:14).

Ukisoma kurasa mbalimbali za kwenye mtandao juu ya kukua kwa dini ya Kiislamu, utakuta wengi wanasema kwamba Uislamu ni dini inayokua kwa kasi sana. Je, hilo ni kweli? Ni jambo gani linaloonyesha ukweli wa hoja hiyo?

Lakini tunao ushahidi wa Neno la Kristo kwamba siku za mwisho (yaani hizi tulizo nao), Injili itahubiriwa ulimwenguni kote. Pia, Mungu Yehova anaahidi kuwa hizi ni siku za kumwaga Roho wake kwa wanadamu wote. Hakika hizi ni nyakati za Injili ya Yesu Kristo kusonga mbele na kushinda na kubomoa kila upinzani na ukuta uliojengwa na adui ili kuwazuia wanadamu kumjua Mungu wa kweli na Mwokozi pekee, Yesu Kristo.

Sunday, March 24, 2013

Juhudi za Kupinga Ukristo za Mwanaharakati wa Kundi la Ahmadiah Kutoka Pakistani Zamfanya Aachane na Uislamu



Nusrat Aman alikuwa ni mwanaharakati wa kiislamu wa kundi la Ahmadiah kule Pakistani. Siku moja aliamua kuingia kanisani ili akamwulize mchungaji ni kwa nini hasa hataki kuwa mwislamu ilhali unabii wote umeshatimizwa ndani ya Muhammad? Nusrat aliishia kupata aibu, hasira na hatimaye wokovu …!


Je, ilikuwaje? Endelea kusoma ushuhuda wake wenye kichwa kisemacho "Kwa nini niliamua kuwa Mkristo?" ambao unafungua macho na mioyo kwa kuwa ni watu wengi walio katika kundi alimokuwa Nasrat hapo zamani.

Sunday, March 17, 2013

Maswali Yanayonitatiza Kuhusiana na Quran



Ibra na Waislamu wengine, kumekuwa na kawaida kwa ulimwengu wa Kiislamu kufanya kila juhudi kuonyesha kwamba Biblia imepotoshwa, ingawaje jambo hilo si kweli hata kidogo. Ukiachilia mbali makosa ya kibinadamu ya hapa na pale ambayo yanaingia kutokana na ukweli kwamba Biblia imetafsiriwa na inaendelea kutafsiriwa mara nyingi sana, hakuna makosa ya makusudi yanayofanywa ili kupotosha au kuficha ukweli.

Na juhudi hizi zote zinafanywa ili kutaka kuonyesha kwamba  Quran ni neno la Mungu la kweli ambalo halijapotoshwa hata kidogo. Basi mimi naomba mnisaidie majibu ya maswali haya machache kati ya mengi:

Friday, March 15, 2013

Majibu Yangu kwa Ibrabura - Sehemu ya 1




Katika makala haya, ninajibu hoja zako rafiki yangu Ibra, ambazo umezitoa kwenye sehemu ya ‘comments’ kwenye makala yangu mengine yenye jina:  Je, Yesu aliagiza wafuasi wake wawaue maadui wa Yesu? Unaweza kusoma HAPA.


Ninatoa majibu yangu kama makala tofauti kwa sababu kuu mbili. Kwanza ni kuwapa fursa watu wengine waweze kujifunza kutokana na mjadala wetu na hata kuchangia au kutusahihisha pale tunapokosea. Pili, kutokana na urefu wa majibu yangu, ni rahisi kuyatoa kama makala kuliko maoni (comments), maana maoni ya mara moja hayatakiwi kuzidi herufi takribani 4,000 hivi.

Sunday, February 10, 2013

Baada ya Kuijua Njia ya Kweli, Mwana wa Kiongozi wa Hamas Auacha Uislamu na Kumgeukia Yesu Kristo







Mosab Hassan Yousef ni kijana wa kipekee ambaye ana ushuhuda usio wa kawaida. Baba yake ni mmoja wa waliokuwa viongozi wenye ushawishi mkubwa sana ndani ya kundi la kijeshi la Hamas kule Ukanda wa Magharibi (Palestina). Mosab alikulia kwenye familia iliyoshikilia Uislamu kwa nguvu sana.

Akiwa na umri wa zaidi ya miaka 30 sasa [yaani wakati ushuhuda huu ukiandikwa], ni mshirika wa Kanisa la Kikristo, Barabbas Road kule San Diego, Calif. Aliikana imani yake ya Uislamu, akaiacha familia yake kule Ramallah na anatafuta hifadhi ya kisiasa kule Marekani.

Hadithi ya maisha yake inashangaza sana - uwe unakubaliana au hukubaliani na mtazamo wake. Video ifuatayo inaonyesha mahojiano kati ya Mossab na kituo cha FOX News, akieleza yeye mwenyewe namna Muislamu kutoka Ukanda wa Magharibi alivyogeuka na kuwa Mkristo wa Pwani ya Magharibi.

Friday, February 8, 2013

Kutoka Kwenye Uislamu Hadi Kwenye Ukristo



Jina langu ni Tahir na hii ni safari yangu kutoka kwenye Uislamu hadi kwenye Ukristo.

Mara baada ya kufika Marekani nikitokea Palestina miaka 14 iliyopita, nilimwoa msichana mzuri wa Kikristo. Msichana huyu alijaribu kuwa Mwislamu ili kunifurahisha mimi, lakini kadiri alivyojitahidi kufanya hivyo, ndivyo nilivyozidi kuwa mbali naye. Tulizaa mtoto mmoja, lakini ndoa yetu haikudumu maana ni vigumu sana kupenda wakati moyo wako umejaa chuki. Chuki ndicho kitu ambacho nilifundishwa wakati wa kukua kwangu kule Palestina – chuki dhidi ya Wayahudi, Wakristo na hata dunia nzima. Ukiwa kama Mpalestina, unafundishwa tangu ziku ya kwanza kwamba dunia yote ndiyo inayohusika na mateso yetu, na hasa Wayahudi na Wakristo.

Baada ya kuachana, baadaye mke wangu huyo wa zamani alikuja kuniambia kuwa amembatiza mwanangu. Nilikasirika mno kiasi kwamba nilienda kuingia moja kwa moja kanisani, nikamtukana mchungaji aliyefanya ubatizo ule, na nikamwambia kuwa angeenda jehanamu kwa sababu ya kitendo kile. Sikutaka kabisa mwanangu akue akiwa Mkristo!. Matokeo yake nilipigwa marufuku na mahakama kumtembelea mwanangu maana mke wangu alihofia kuwa ningeweza kuja kumteka mwanangu na kumpeleka Palestina. Hivi sasa sipati nafasi ya kumuona mara kwa mara.

Sunday, February 3, 2013

Muhubiri wa Kiislamu Kutoka Misri Aokoka Baada ya Yesu Kusema Naye Kupitia Ndotoni



Ibrahim alikuwa Mwislamu wa imani kali. Alikuwa mtoa mihadhara katika misikiti mbalimbali nchini Misri. Alikutana na Injili ya Yesu. Moyo wake ulitikiswa. Hakujua amwamini nani – je, ni Yesu au ni Muhammad? Nani angemwambia njia ya kweli ni ipi? Aliinua moyo wake juu mbinguni. “Yehova, nionyeshe njia ya kweli nami nitaifuata kwa gharama yoyote ile,” alisema kwa machozi.

Bwana Yesu mwenyewe alikuja kusema na Ibrahim katika ndoto. Ibrahim aliachana na Uislamu na kumkumbatia Mwokozi. Lakini kundi la Waislamu wenye imani kali la Muslim Brotherhood wangemwacha tu? Vipi kuhusu familia yake?

Kumfuata Kristo kuna gharama. Lakini huwezi kumbadilisha mtu anapomjua Mungu wa kweli ingawaje utampiga, utamfunga, na kumtesa kwa kila namna. Endelea kusoma ushuhuda huu wa kutia moyo na Mungu wa mbinguni atasema na moyo wako kwa njia ya ajabu ambayo itabadilisha kabisa maisha yako....!

Thursday, January 17, 2013

Yesu Mwenyewe Asema na Mwanamke wa Kiislamu



Mungu alinijibu Mimi!

Huu ni ushuhuda wa kweli kuhusiana na maisha ya mtu aliyekuwa anamtafuta Mungu.

Habari yako na Mungu akubariki. Jina langu ni Amal na ninashuhudia kwamba kile ambacho unaenda kusoma ni cha kweli kabisa na sahihi kwa kadiri ya kumbukumbu zangu maana Mungu mwenyewe ni shahidi yangu. Maombi yangu ni kwamba Mungu aseme  na moyo wako na kutumia ushuhuda huu kukubariki wewe kwa namna ya pekee maishani mwako.

Kimsingi mimi nilikulia kwenye familia ya Uislamu mkali. Baba yangu ni Mpalestina kutoka Israeli. Mama yangu ana asili ya Brazili. Alikuwa ni Mkatoliki. Baba yangu alikutana naye Brazili. Walioana na mama yangu alibadili dini na kuwa Mwislamu.

Sunday, January 13, 2013

Mwanamke Mwislamu Aliyemkimbilia Yesu Kristo


Hii si picha ya Siti mwenyewe. Ni picha tu kutoka kwenye mtandao.

Ushuhuda wa Siti Zainab

Assalam-mualaikum.

Jina langu ni Siti Zainab. Mimi ni mwanamke wa Kiislamu kutoka Malesia, kusini mashariki mwa Asia.  Nilizaliwa kwenye familia ya Kiislamu, iliyokuwa ikifuata taratibu za Kiislamu kwa nguvu sana. Tokea mwanzo, nilipata elimu ya Kiislamu ambayo ilikuwa imara na ya ndani sana.

Pamoja na elimu yangu ya msingi, nilipelekwa pia kwenye madrasah ya Kiislamu, yaani shule ya dini, na nikaanza kusoma na kukariri Quran tangu mapema; huku nikijifunza maadili na misingi ya Uislamu wa Kisuni, kutoka kwa walimu waliobobea wa Kiislamu. Huko nilijifunza kumwogopa na kumtii Allah s.w.t. na pia kufuata mafundisho na mifano ya Mtume Muhammad (hususani yale yaliyo kwenye Hadithi zinazokubalika). Pia nilikuwa nina uwezo wa kusoma Quran yote, jambo ambalo liliwafurahisha wazazi wangu. Kwa kifupi, nilikuwa nina msingi imara na imani ya ndani ya dini kama Muslimah mwaminifu na aliyejitoa kwa moyo wote.

Saturday, January 12, 2013

Kwa Nini Niliacha Uislamu na Kumpokea Yesu?




Mutee'a Al-Fadi alikuwa ni Mwislamu mwenye msimamo mkali wa Wahabbi ambao alisomea kule Saudi Arabia. Lakini baada ya kukutana na upendo wa Yesu, moyo wake uligeuka kabisa na akaanza kuitafuta kweli iliko. Hatimaye alitambua kuwa Yesu ndiye Njia, Kweli na Uzima. Ufuatao ndio ushuhuda wake: