Mpendwa msomaji na mpenzi
wa blog hii, naamini ulishasoma sehemu ya 1 na ya 2 za ushuhuda huu wa Akef. Hii
ni sehemu ya 3 na ya mwisho inayoonyesha ukuu, upendo na uweza wa Mungu wa
Ibrahimu, Isaka na Yakobo, yaani Yesu Kristo. Karibu usome sehemu hii na Bwana
Yesu akubariki.
Showing posts with label ukristo na uislamu. Show all posts
Showing posts with label ukristo na uislamu. Show all posts
Sunday, June 9, 2013
Monday, May 13, 2013
Kutoka Kwenye Uislamu Hadi Kumkubali Yesu Kristo
Naeem alikuwa ni Mwislamu tangu
utoto wake. Ulifika wakati ambapo alikutana na Yesu Kristo. Matokeo yake,
aliweza kuyajua makusudi ya kuumbwa kwake. Na sasa anamshangilia Mwokozi na
Muumba wake ampendaye, yaani Yesu Kristo. Je, ilikuwaje? Tafadhali soma
ushuhuda wake ufuatao:
Sunday, March 24, 2013
Juhudi za Kupinga Ukristo za Mwanaharakati wa Kundi la Ahmadiah Kutoka Pakistani Zamfanya Aachane na Uislamu
Nusrat Aman alikuwa ni
mwanaharakati wa kiislamu wa kundi la Ahmadiah kule Pakistani. Siku moja
aliamua kuingia kanisani ili akamwulize mchungaji ni kwa nini hasa hataki kuwa
mwislamu ilhali unabii wote umeshatimizwa ndani ya Muhammad? Nusrat aliishia kupata
aibu, hasira na hatimaye wokovu …!
Je, ilikuwaje? Endelea kusoma
ushuhuda wake wenye kichwa kisemacho "Kwa nini niliamua kuwa Mkristo?" ambao unafungua macho na mioyo kwa kuwa ni watu wengi walio
katika kundi alimokuwa Nasrat hapo zamani.
Sunday, March 17, 2013
Maswali Yanayonitatiza Kuhusiana na Quran
Ibra na Waislamu wengine,
kumekuwa na kawaida kwa ulimwengu wa Kiislamu kufanya kila juhudi kuonyesha
kwamba Biblia imepotoshwa, ingawaje jambo hilo si kweli hata kidogo. Ukiachilia
mbali makosa ya kibinadamu ya hapa na pale ambayo yanaingia kutokana na ukweli
kwamba Biblia imetafsiriwa na inaendelea kutafsiriwa mara nyingi sana, hakuna
makosa ya makusudi yanayofanywa ili kupotosha au kuficha ukweli.
Na juhudi hizi zote
zinafanywa ili kutaka kuonyesha kwamba Quran ni neno la Mungu la kweli
ambalo halijapotoshwa hata kidogo. Basi mimi naomba mnisaidie majibu ya maswali
haya machache kati ya mengi:
Friday, February 8, 2013
Kutoka Kwenye Uislamu Hadi Kwenye Ukristo
Jina
langu ni Tahir na hii ni safari yangu kutoka kwenye Uislamu hadi kwenye Ukristo.
Mara
baada ya kufika Marekani nikitokea Palestina miaka 14 iliyopita, nilimwoa
msichana mzuri wa Kikristo. Msichana huyu alijaribu kuwa Mwislamu ili
kunifurahisha mimi, lakini kadiri alivyojitahidi kufanya hivyo, ndivyo
nilivyozidi kuwa mbali naye. Tulizaa mtoto mmoja, lakini ndoa yetu haikudumu
maana ni vigumu sana kupenda wakati moyo wako umejaa chuki. Chuki ndicho kitu
ambacho nilifundishwa wakati wa kukua kwangu kule Palestina – chuki dhidi ya
Wayahudi, Wakristo na hata dunia nzima. Ukiwa kama Mpalestina, unafundishwa
tangu ziku ya kwanza kwamba dunia yote ndiyo inayohusika na mateso yetu, na
hasa Wayahudi na Wakristo.
Baada
ya kuachana, baadaye mke wangu huyo wa zamani alikuja kuniambia kuwa amembatiza
mwanangu. Nilikasirika mno kiasi kwamba nilienda kuingia moja kwa moja kanisani,
nikamtukana mchungaji aliyefanya ubatizo ule, na nikamwambia kuwa angeenda
jehanamu kwa sababu ya kitendo kile. Sikutaka kabisa mwanangu akue akiwa
Mkristo!. Matokeo yake nilipigwa marufuku na mahakama kumtembelea mwanangu
maana mke wangu alihofia kuwa ningeweza kuja kumteka mwanangu na kumpeleka
Palestina. Hivi sasa sipati nafasi ya kumuona mara kwa mara.
Sunday, February 3, 2013
Muhubiri wa Kiislamu Kutoka Misri Aokoka Baada ya Yesu Kusema Naye Kupitia Ndotoni
Ibrahim alikuwa Mwislamu wa imani kali. Alikuwa mtoa mihadhara katika misikiti mbalimbali nchini Misri. Alikutana na Injili ya Yesu. Moyo wake ulitikiswa. Hakujua amwamini nani – je, ni Yesu au ni Muhammad? Nani angemwambia njia ya kweli ni ipi? Aliinua moyo wake juu mbinguni. “Yehova, nionyeshe njia ya kweli nami nitaifuata kwa gharama yoyote ile,” alisema kwa machozi.
Bwana Yesu mwenyewe alikuja kusema
na Ibrahim katika ndoto. Ibrahim aliachana na Uislamu na kumkumbatia Mwokozi. Lakini
kundi la Waislamu wenye imani kali la Muslim Brotherhood wangemwacha tu? Vipi kuhusu
familia yake?
Kumfuata Kristo kuna gharama. Lakini
huwezi kumbadilisha mtu anapomjua Mungu wa kweli ingawaje utampiga, utamfunga,
na kumtesa kwa kila namna. Endelea kusoma ushuhuda huu wa kutia moyo na Mungu
wa mbinguni atasema na moyo wako kwa njia ya ajabu ambayo itabadilisha kabisa
maisha yako....!
Subscribe to:
Posts (Atom)



