Sunday, April 21, 2013

Je, Mtume Muhammad Yuko Wapi Hivi Leo?






Mungu hutufunulia mambo mbalimbali kupitia watumishi wake mbalimbali ili kutujulisha yale yaliyopo na hata yajayo; katika ulimwengu huu na pia ule ujao. Wapo watu wengi ambao Mungu amewatumia kutufahamisha juu ya mbingu na hata juu ya kuzimu.

Bo Ra Choi ni mchungaji kutoka Korea ya Kusini. Mchungaji huyu amekuwa akionyeshwa maono mbalimbali na Mungu kuhusu mambo ya ulimwengu wa roho. Mojawapo ya maono aliyoonyeshwa yanamhusu Muhammad, mtume wa Uislamu.

Je, Muhammad yuko wapi hivi leo? Katika video hii, mchungaji Bo Ra Choi anafikisha kwetu ujumbe kwa namna ambavyo alisikizishwa Muhammad akisema kule aliko sasa.

Kwa maana nyingine, ananukuu moja kwa moja maneno ya Muhammad ili kwamba iwe ni kama vile tunamsikia Muhammad akizungumza.

Tafadhali zikiliza kwa makini video hii, kisha utaupata ujumbe wa Mungu anaouleta kwetu kupitia mtumishi wake, Mchungaji Bo Ra Choi.

........................

Lakini anachosema Muhammad humo ni nini hasa?
 



Kifuatacho ndicho anachokisema Muhammad humo
kwa kilio kikubwa:
...........................
Mnajua mimi ni naniiiiiii?
Mimi ni Muhammad
Nilitenda dhambi kubwa sana
Nilifanya makosa makubwa mno
Nilikuwa mjinga
Nimetenda dhambi kubwa sana
Watu wengi sana wamekuwa wakitumbukia kuzimu kwa sababu yangu.
Nilitenda uhalifu mkubwa kuliko wote
Nilitenda dhambi kubwa kuliko zote
Nilitenda makosa
Nilitenda makosa
Yesu, nilifanya makosa.
Nilifanya hivyo kwa sababu nilikuwa maskini sana.
Nilitaka kuwa kiongozi wa watu wengi na nilitaka kuwa kama Yesu.
Nilifanya uhalifu mwingi sana wa kiovu
Niliua watu wengi sana
Msijikusanye pamoja
Mtakufa kama mkikusanyika kwa ajili yangu, Muhammad.
Tawanyikeni! Msijikusanye pamoja!
Kama mkijikusanya pamoja, shetani atawatumia!
Shetani atawatumia zaidi kama mkikusanyika kwa ajili ya Muhammad.
Bila ya Yesu, wote wanaishia kuzimu
Kuna joto kali!
Kuna joto kali!
Kuna joto kali!
Nitoe humu!
Nitoe humu!
Hakuna pepo ambayo mnaifikiria.
Kuna mbinguni na kuzimu tu.
Mafundisho hayo yamesambazwa kwa uongo. 
Uislamu umebadilishwa.
Haiwezekani!
Msipoteze maisha yenu namna hiyo.
Hakuna pepo ambayo Waislamu wanaiamini.
Mimi sikuzungumza juu ya mafundisho hayo ya uongo.
Yamebadilishwa.
Someni Biblia.
Inaonyesha namna ya kwenda mbinguni.
Hakuna mbingu katika Uislamu.
Mimi sikuandika theolojia hizo za uongo.
Mambo hayo yaliandikwa na watu waliokuwa wakijaribu kuniiga mimi.
Mambo hayo yamekuwa ni Biblia ya Uislamu ambayo inadhoofisha neno la Yesu.
Haiwezekani!
Sikuyaandika hayo!
Tafadhali, nisikilizeni!
Niko hapa kuzimu.
Niko hapa kwenye moto wa kuzimu.
Ninateseka kwa adhabu hii kubwa sana kwa sababu shetani alinitumia.
Msitupe maisha yenu kwa shetani!
Msiwe watii kwangu mimi, Muhammad.
Hiyo ni njia ya kwenda kuzimu.
Shetani atawatumia.
Tokeni humo kwenye Uislamu.
Mimi sikutaka haya.
Nilitaka tu kuwa mtawala wa taifa.
Lakini mambo yalienda vingine.
Hiki sicho nitakacho.
Sitaki vita.
Nilianzisha mapigano mengi ili kuunda taifa langu mwenyewe.
Mnajua ni kwa nini?
Ni kwa sababu nilikuwa maskini sana nilipokuwa mtoto.
Nilianzisha vita nyingi sana ili kuunda taifa langu.
Nilitaka tu kuongeza nguvu zangu ili kushinda vita.
Kwa nini Uislamu umebadilika hivyo?
Kama kweli mnataka kuwa watii kwangu,
Tawanyikeni na msiwasikilize viongozi wenu (wa dini).
Wanawaongoza kuelekea kwenye njia mbaya sana.
Wanaharibu maisha ya watu.

…………………………………….

Tafakari

Pima mambo

Chukua hatua
 

79 comments:

  1. Hivi nyie wakristo mna akili timamu kweli?
    sio bure yaani nyie ni nusu au vichaa kamili. Kwa nini nasema hivyo? Yaani nyie hampo hata chembe moja na maagizo ya mungu. Alafu, mfahamu ya kwamba, mnaposema uongo kwa mujibu wa biblia mnatenda dhambi.
    We Muhammad aende motoni amefanya nini? Toeni hoja msiwe na chuki binafsi kwa kuona kwamba iman ya Muhammad nabii aliesomeshwa na mungu, inazidi kupanda zaidi duniani. Alafu nyie mnachekesha kweli, hivi mtu akisema kaota akilala na mkeo ndio tayari keshalalanae?
    Yaani, nyie mmeshindwa kwa hoja na kwa kila kitu badala yake mnaleta matusi ambayo hayatawasaidia.
    Mimi nikisema mungu wenu kwa ushahidi wa biblia ni malaya mtakataa?
    ISAYA 23:17.
    Nikisema Yesu kalaaniwa kwamujibu wa biblia mtasemaje?
    YEREMIA 22:24-30. Hizo ndizo hoja za kwangalia kimakini kwa kuweka mshangao na kuona kwamba hivi kweli mnaabudu kitu sahihi?
    Mtamaliza maneno lakini ukweli unabaki palepale kwa ushahidi wa maandikob sio kubunibuni tuuuuuuuu! wanafiki maskini wa hoja.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ubarikiwe ndugu kwa kumtukana Bwana Yesu aliyetukuka mbinguni na duniani kumbuka alikufa kwa ajili ya ulimwengu wote ila jambo moja tu naweza kukuambia ndugu ipo siku utafunguliwa na utamjua huyu unae mtukana leo na utamkiri kuwa Bwana na Mwokozi wako kama ilivyo kwa waislamu wengine walio kuwa wanamtukana Bwana na sasa wameona wokovu mkuu Mungu wetu ni warehema na mapenzi tele kwa hivyo Bwana wa Majeshi na alie Mkuu sana akusamehe na siku moja aokoe moyo wako nakupenda ndugu katika Kristo.

      Delete
    2. Ibra asante kwa maoni yako. Biblia inasema kwamba: Maana ikiwa tumerukwa na akili zetu, ni kwa ajili ya Mungu; au ikiwa tunazo akili zetu timamu, ni kwa ajili yenu. (2 Wakor 5:17). Hiki ambacho huyu mchungaji alionyeshwa ni mambo ambayo Mungu huyaonyesha kila uchao. Yapo mengi sana ya aina hiyo. Hivyo, mimi sikukatalii kabisa. Ama huu ni ukichaa au ni uzima. Lakini kwa kuwa bado tunaishi, nadhani tuache muda utufikishe kwenye jawabu.

      Kuhusu suala la kuota, kama mtu akisema KAOTA kalala na mke wangu, yataishia tu hapo. Lakini kama HAKUOTA, basi itabidi nijiulize. Kama mchungaji huyu alikuwa anaota, basi ni wa kupuuza tu. Lakini swali ni kwamba, je, alikuwa anaota?

      Umesema kuwa Mungu wetu ni Malaya, jibu ni hapana kabisa, Ibra. Andiko ulilonukuu linasema hivi: Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, Bwana ataizuru nchi ya Tiro, NAYE atarudi apate ujira wake, ATAFANYA UKAHABA pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia. Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa Bwana, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za Bwana, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari. (Isaya 23:17-18).

      Hayo maneno NAYE na ATAFANYA yanaonyesha kana kwamba yanamrejea Bwana. Lakini hii ni kwa sababu katika Kiswahili hayabainishi jinsi ya kike au ya kiume. Ukisoma kwa Kiingereza imeandikwa hivi: And it shall come to pass after the end of seventy years, that the LORD will visit Tyre, and SHE shall turn to her hire, and shall commit fornication with all the kingdoms of the world upon the face of the earth. And HER merchandise and HER hire shall be holiness to the LORD: it shall not be treasured nor laid up; for HER merchandise shall be for them that dwell before the LORD, to eat sufficiently, and for durable clothing.


      Kwa hiyo, ni wazi kuwa aliye kahaba hapa ni mji wa Tiro. Ukahaba unapotajwa kwenye Biblia kuhusiana na nchi au watu wote kwa ujumla, ina maana kumwacha Mungu aliye hai na kwenda kutafuta msaada ama kwa miungu mingine au kwa nchi nyingine. Tazama Ezekieli 16:1-16. Je, Ibra, bado unadhani Mungu wetu ni kahaba?


      Kuhusu Yesu kulaaniwa ambapo umenukuu YEREMIA 22:24-30, anzia kusoma sura ya 21 kabisa. Kote hapo Mungu anaongelea hukumu juu ya wale wasiotaka kutii maagizo yake – wawe ni wafalme au watu wa kawaida. Kutokana na kutotii huko, ndipo anasema kuwa atawaleta wabaya wao waje kuwahamisha, wafalme wao watachukuliwa mateka na wale wanaotaka kutawala nao hawatafanikiwa. Kwa hiyo, hukumu na laana hizi zinawahusu wasiotii amri za Bwana.

      Lakini hebu ona Yer 22:15-16 inavyosema juu ya wale walio watii: Je! Utatawala kwa sababu unashindana na watu kwa mierezi? Baba yako, je! Hakula na kunywa, na kufanya hukumu na haki? Hapo ndipo alipofanikiwa. Alihukumu maneno ya maskini na mhitaji; hapo ndipo alipofanikiwa. Je! Huku siko kunijua, asema Bwana?

      Hapa anamwambia mfalme Shalumu, mwana wa Yosia. Maana yake ni kuwa Yosia alibarikiwa lakini Shalumu alikutana na laana. Sasa swali ni kwamba, Je, Yesu alikuwa mtii au muasi wa neno la Mungu? Kama alikuwa muasi, basi laana hizi moja kwamoja zinamhusu. Kama alikuwa mtii, laana hizi hazimhusu. Jibu liko wazi.

      Lakini upande wa pili, Biblia inasema hivi: Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti (Wagalatia 3:13).

      Yesu alilaaniwa si kutokana na dhambi zake, maana hakuwa na dhambi hata moja, bali alibeba dhambi zetu sote, kisha laana ya dhambi hizo ikawa juu yake – maana SOTE tuna dhambi na tumelaaniwa kwa sababu ya dhambi hizo. Baada ya hapo, Yesu akauawa ili sisi tupone. Ukiamini hilo, unapokea uzima wa milele. Ukikataa unabaki na dhambi zako na laana zinazoambatana na dhambi; na mwisho wake unajulikana.

      Kwa hiyo, laana ya Yeremia 22 haimhusu Yesu hata kidogo kama ambavyo ilikuwa haimhusu mfalme Yosia. Laana inayomhusu Yesu ni nyingine kabisa ambayo ilikuwa kwa ajili ya uzima wangu na wako.

      Delete
    3. Hatuna cha kukueleza umepokeya ujumbe safi kabisa na wewe usipomgeukiya Yesu Kristo utafata Muhammad aliko. Hayo majini ambayo waarabu Kawasaki kuyatasfiri kwenye lugha nyingine kwa sababu usifahamu ukweli(yanayo kuongoza) yatakudhihaki na kukutukana siku moja. Ole wako unaelekeya upotovu.

      Delete
    4. Hayo mafungu mpendwa unayoyasema ni ya falme za zamani kwa sasa hazipo yesu alifanya kazi yake akamaliza mwisho ni ufufuo we uhisi huyo kahaba atajiuza kwa farume zipi mwisho wa dunia ukishatimia

      Delete
  2. Mr.James huyo mchungaji habari zake hizi hapa:
    ISAYA 56:10-11 ''10 Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.

    11 Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote''.
    Kuhusu ISAYA 23:17-18 UMECHEMKA NDUGU YANGU.
    Kwa nini nasema hivyo? Lugha iliyotumika hapa ni sanifu kabisa, na wala haina mafumbo yeyote kama yaliyotumika kwenye ezekiel. Kwa hiyo, NAYE NA ATAFANYA, ni wazi kabisa inamhusu mh. mungu wenu.
    Ndugu yangu, hiyo Yer.22:24-30 usisome kwa jazba. Hautaelewa ni nini kinamaanisha! Hapo kuna habari ya KONIA au YEKONIA.
    MTU HUYU KALAANIWA NA MUNGU PAMOJA NA UZAO WAKE WOOOOTE! HAUTAFANIKIWA KUKETI KATIKA KITI CHA ENZI CHA DAUDI.
    SASA IWEJE BASI, YESU ATAWALE WAKATI YEYE NI MMOJA KATI WAZAO WA KONIA? AU MUNGU WENU NI KIGEUGEU? MATH.1:11
    Ndugu yangu, kuwa makini na imani yako, anza kutafakari na chukua hatua.
    YESU KRISTO kwa mujibu wa biblia ametenda dhambi ya KUONGOPA kwa kuwa kwa sheria ya mungu kwa wana wa israeli, UONGO ni dhambi!
    1) Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.
    Yohana 17.3-4
    Maneno haya yanantoka yesu kinywani mwake. Kwa hiyo hapa anaongopa kwa sababu wakristo wanaamini kuwa yesu ni mungu, sasa kauli hii inamlenga mungu gani? kwa nini asijisemee mwenyewe?
    Kama yesu ni mungu basi, amevunja amri ya USISEME UONGO!
    UONGO MWINGINE WA YESU:
    Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.
    Yohana 7.28-29.
    Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.
    Marko 9.37

    Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.
    Yohana 4.34
    Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu.
    Yohana 7.16-18
    WAONGO WENGINE KWENYE BIBLIA NI HAWA HAPA:
    Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.
    Matendo 3.26
    Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.
    Matendo 3.13
    Matendo 3.13
    Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.
    Matendo 4.29-30
    Sasa basi, kama binadamu wote tuna dhambi, na mungu wenu yesu anao dhambi kwa sababu ameongopa kwa kujikwepesha nafsi ya uungu, na pia hata wale waandishi wenu pia ni waongo! mkweli ni TITO tu pekeake, yaani tito ni zaidi ya mungu wenu.
    Na hii ya kuuwawa yesu ili sisi tupone sidhani kama ina pumzi ya mungu. Hapa inamaanisha kwamba, yesu anaenda motoni na nyinyi mnaenda peponi. duh! hiyo kali.
    Uzima wa milele ninaotaka mimi ni ule aliohubiri yesu wa kusema, MPENDE BWANA MUNGU WAKO UMWABUDU YEYE PEKEAKE, MPENDE JIRANI YAKO, USIUWE,,,NK.

    ReplyDelete
  3. Ibra naamini u mzima wa afya kabisa na nina-appreciate sana shauku yako na juhudi yako ya kumpenda na kumtumikia Muumba wako. Mimi binafsi unanipa changamoto kubwa sana.

    Kuhusu huyo mchungaji kuwa mbwa mwenye choyo, n.k., kama nilivyosema mara ya mwisho, time will tell. Tumeshaona watu wengi sana ambao hata miujiza ya kawaida anayofanya Bwana Yesu wanasema walokole wamewapa pesa ili mseme mmeponywa. Lakini Bwana huwa anakuja kuwakamata kirahisi sana. Kisha unaona mtu anamwaga ndoo ya machozi akisema, "Sikujua!" Kwa hiyo, usijali rafiki yangu, Ibra, Roho Mtakatifu ni mwaminifu kuthibitisha Neno lake - siku inakuja KATIKA JINA LA YESU!

    Kuhusu uongo unaousema kuhusiana na Biblia na Yesu, nafahamu kuwa tumeshazungumza sana juu ya suala la Mungu wa Biblia kujibainisha katika nafsi tatu, tofauti na Mungu wa Quran. Kwa hiyo, ukimchukulia kwa vigezo vya Quran, ni lazima ataonekana mwongo. Lakini kwa vigezo vya Biblia, Yesu si mwongo hata chembe. Japokuwa maneno yake yanaonekana kutenganisha kati ya Mungu (aliye mbinguni) na Yeye (akiwa duniani), hilo halina kamwe mkanganyiko; maana Mungu wetu ni Mkuu sana. Anaweza kuwa kokote kwa wakati uleule - na hivyo ndivyo alivyo. Kwa hiyo, mimi nisingependa tuanze moja tena kwenye suala ambalo tumeshalipitia kwa kina sana.

    Mwisho naomba nikuulize: Kwenye Quran, Allah mara nyingi sana haseni "NILIfanya hivi au vile", bali husema "TULIfanya hivi na vile." Kulingana na mantiki ya hoja zako, Allah ni mwongo pia, maana ninyi mnasisitiza sana juu ya Allah kuwa Mungu mmoja asiye na mshirika wala nafsi mbili au tatu.

    Je, kwa nini anaongea katika wingi? Najua utasema ni kutokana na ukuu wake n.k. Lakini utakaposema hivyo, naomba useme kwa ushahidi wa maandiko yenu si kwa maoni au mtazamo wako.

    Asante, Mungu Ibrahimu, Isaka na Yakobo akubariki.

    ReplyDelete
  4. Ahahahahahaa! Yaani we unachekesha. Ehe ebu nambie ni mchungaji gani wa kilokole au yeyote yule anafanya miujiza ya yesu? Ndugu yangu, kama hujui leo hii nakujulisha ya kuwa hiyo ni bonge la sanaa wanaotumia hao wanaojiita walokole. Mfano: Yule mzee wa upako anavyotumia yale mafuta from nchi za kiarabu katika kuwaangusha watu. Sasa je! nikupe dili? Kuna mafuta, ambayo nyie mnayaita ya upako. Yale mafuta, bila kuombea, wala kufanya chochote kile, paka kwenye viganja vya mikono yako, halafu nenda kwenye umati wa watu, fanya kama unawapungia wale watu mikono yako, baada ya secunde chache utaona yeyote mwenye mashetani anaanguka chini. Baadae mwendee mmoja baada ya mwingine mwonyeshe tena ule mkono wako, na wale mapepo watakuwa wameondoka.
    Hayo machache tu, ukitaka nitakupa dili jinsi ya kumwamsha mtu kilema.
    Kwa hiyo sio nguvu ya mungu. Na ukitaka kujua hilo, katika eneo lenu we angalia wanapofika hao wenye kuponyesha, utaona wote wanaoponyeshwa hawajulikani na wenyeji.
    Na katika ile ya mungu kujisemea kiuwingi, inamaanisha utukufu wake. Jambo kama hili, si geni machoni petu. Kuna makabila mengine wana desturi za aina hiyo, ya mtu mwenye heshima, kama vile mama au baba ni lazima unapowalenga kwa mazungumzo uwajaze. mfano: WEWE unamjaza kwa NYINYI.
    Na kauli ya aina haiwezi kuwa ya uongo kwa sababu pale anaposema TULI...anajionyesha. Tofauti na YESU, ambaye anajikataa katakata kama yeye si muumbaji.
    JAMES! Hakuna kwenye biblia inapodhibitisha kwamba yesu ni mungu. Mi binafsi nimewahi kukuomba maandiko ya uungu wa yesu. Baada ya kutoa maandiko yote yanayokufanya wewe uamini kuwa yesu ni mungu, mimi nilikujibu kwa uzuri sana, nikiwa na maana kwamba, utetezi wako haukuwa na mantiki.
    James! Mimi naamini kitu kimoja, kwamba YESU alitumwa na mungu, kama maandiko yanavyosema.
    SASA katumwa nini?
    Kuwaletea waisraeli wokovu kama maandiko yanavyosema. Yaani, yesu alibeba ujumbe wa mungu kwa watu wake. Kwa hiyo, wakati wa yesu, ili mtu apate uzima wa milele ilikuwa lazima umsikilize yeye. Yaani yesu, kwa wakati huo, alisimama badala ya mungu kama walivyokasimama minabii wa nyuma yake yesu katika kulitangaza neno la mungu.
    Kwa hiyo, ukisema yesu ni mungu, tukubaliane ya kwamba sio muumba ila kwa kuwa alisimama badala ya mungu katika kufundisha neno lake, basi wale wataalamu wa lugha walitumia kumuita yesu mungu kimafumbo sio kiuhalisia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ibra naamini Mungu anaendelea kukupigania na u mzima wa afya tele. Naendelea kukushukuru sana kwa juhudi zako zenye nai njema. Kwa muda kitambo sasa nimekuwa sipo kwenye blog yangu kwa sababu ya majukumu fulani. Lakini niko mbioni kuyamaliza.

      Leo nimepata mwanya kidogo nimeona nijibu ujumbe wako huu. Kuhusu suala la uponyaji wa wachungaji feki, hilo mimi sikukatalii hata kidogo. Wala hilo si geni katika Biblia. Yafuatayo ni maonyo kutoka kwa Bwana wa mabwana, Yesu mwenyewe:

      Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. …….. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, HATUKUFANYA UNABII KWA JINA LAKO, NA KWA JINA LAKO KUTOA PEPO, NA KWA JINA LAKO KUFANYA MIUJIZA MINGI? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. (Mt 7:15 na 22-23). Yesu alisema hivi kwa sababu mambo hayo yangekuwapo, na leo tunayashuhudia wazi kabisa.

      Lakini sasa, mimi sikuwa naongelea wachungaji. Imani yetu ni kwa Yesu, si kwa mchungaji awaye yote. Unaposikia kuyatoa maisha kwa Yesu maana yake unamwamini Yeye katika kila kitu. Bwana Yesu ni halisi na yuko kazini saa 24. Atakuongoza kwenye njia salama. Kwa hiyo, Yeye ana miujiza yake iliyo ya kweli na salama. Na hiyo ndiyo ambayo wewe unaijumuisha pamoja na ile ya wachungaji fake. Achana na hiyo, zungumzia ya Yesu.

      Katika nyakati hizi za mwisho udanganyifu utakuwa mwingi hata zaidi. Na hata sasa bado haujafikia kwenye upeo wake haswa! Kwa yeyote ambaye shauku yake ni kusaka miujiza, atanaswa kirahisi mno. Hapo ndipo ibilisi anapopenyeza miujiza yake kupitia watumishi wake ambao wanajiita wachungaji. Lakini kwa yule anayemtafuta YESU, huyo yuko salama kabisa. Kwa hiyo, mimi ninapotaja miujiza ya Yesu, simaanishi miujiza ya kishetani.

      Kuwapo kwa miujiza ya kishetani hakuifanyi miujiza ya Yesu isiwepo; na wala hakufanyi wachungaji wote kuwa fake. Fake wapo na wa kweli nao wapo. Ni watu wale tu walio na Roho Mtakatifu wa Kristo ndio wanaweza kupambanua na kuwa salama. Njoo kwa Yesu rafiki.
      ………………………………………………
      Kuhusu suala la Allah kutumia wingi kujitambulisha, nilikuomba usinipe maoni yako bali unithibitishie kimaandiko (ya Quran) lkn umefanya kilekile nilichoomba usifanye - ulichonipa ni maoni yako tu. Kwa hiyo bado hujathibitisha hoja.

      ……………………………..
      Kuhusu kwamba Yesu hajawahi kutamka kuwa Yeye ni Mungu, mimi pia nilikujibu vizuri sana. Nilikuambia kuwa Biblia yote ni Neno la Mungu. Wewe unataka maneno yanayotoka moja kwa moja kinywani mwa Yesu, lakini hicho si kigezo cha kibiblia. Kibiblia, maneno ya Petro, Musa au Paulo au mtu yeyote aliyetumiwa na Roho Mtakatifu kuleta ujumbe wa Yesu, ni SAWASAWA kabisa na maneno aliyosema Yesu mwenyewe.

      Kwa hiyo, mimi sina haja ya kufuata kigezo chako wewe ili wewe ukubaliane na mimi. Neno la Mungu katika Biblia ndiyo sheria ya mwisho. Hivyo, ama tunaiamini au tunaikataa – si vigezo vyetu wenyewe. Huwezi kumwamrisha Mungu kwamba eti, kama unataka nikuamini ufanye hivi au vile. Hata ukimwambia, anaweza akafanya au asifanye. Yesu ni Mungu halisi na maandiko yako tele kuthibitisha hilo. Brother Ibra, si vibaya ukienda kusoma tena majibu yangu hayo maana yalikuwa kwa kina kiasi cha kutosha. Bwana Yesu akubariki sana.

      Delete
    2. JAMES JOHN katika kusoma kwangu maandiko matakatifu ya Bwana wetu Yesu Kristo nimegundua nilazima uwe na ROHO MTAKATIFU ndani yako yaani KRISTO ili uyaelewe maandiko vinginevyo nikazi bure.Hivyo hawa ndugu zetu hawana budi kumkiri Kristo kwanza na Yeye atawafunbua macho ya rohoni.Hata hivyo unafanya kazi nzuri sana ,Bwana Yesu apewe sifa zote

      Delete
  5. kaka james Ubarikiwe na Bwana kwa kulitetea Jina lake kuu lilo tukuka sana , sasa kaka tuletee shuhuda nyingine jamani tuzidi kufunguliwa sisi tunao muhitaji Mungu maishani mwetu kwani kupitia shuhuda mbalimbali tunazidi kusonga mbele kwa nguvu za Mungu wetu ali hai milele yote Ubarikiwe na Bwana katika yote.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shalom, shalom. Asante sana kwa ujumbe wako huu wa kutia moyo. Ninaandaa shuhuda nyingine ambazo nitaziweka hivi karibuni. Bwana akubariki, endelea kusimama imara, endelea kusonga mbele.

      Delete
  6. Mr.James, nilishawahi kukupa tahadhali juu ya kitabu chako cha biblia ya kwamba sio cha kwaminika. Ukisoma dibaji ya biblia utakubaliana na mimi ya kwamba mambo mengi yametengenezwa na wanadamu kwa kukidhi haja zao. Mfano, kwenye biblia kuna majina ya watu na maeneo zaidi ya 3500 yaliyofikiriwa tena.
    Taurat sasa hivi haipo, Kuna kumbukumbu ya taurat. Ipo wapi Taurat James?
    Biblia ya yerusalem katika kitabu cha daniel kuna aya 14 na ile ya protestant ina 12. Swali: Je, nani kabadilisha?
    Na unaposema maneno yote ya biblia yanatoka kwa mungu, unapingana na paulo alivyodai ya kwamba anenalo aneni agizo la mungu.
    Na jingine, MUNGU WAKO WEWE NI YESU, LAKINI MIMI, MUNGU WANGU NI YULE ALIEMTUMA YESU KWA WANA WAISRAELI. (sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya israel).

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ibra rafiki yangu, kwa nini unapenda tuzidi kuongelea jambo lilelile kila siku? Nimeshakujibu masuala haya si mara moja, si mara mbili. Nafikiri ni muhimu niandae kabisa makala kamili inayoonyesha kuwa Biblia ni ileile tangu mwanzo.

      Kimsingi, mnachozungumzia Waislamu si Biblia bali ni tafsiri au matoleo mbalimbali ya Biblia. Hicho ndicho kinachowapa shida.

      Na kuhusu majibu ambayo nimeshakupa, sina namna ya kukufanya uamini bali mimi ninachoomba tu, Roho Mtakatifu mwenyewe, ambaye ndiye Mwandishi halisi wa Biblia aseme nawe - iko tu siku Ibra, ambapo utakuja kusema, "Asante Yesu kwa kufungua macho ya moyo wangu kuhusiana na Neno lako." Ipo tuu!

      Na mimi naingoja kwa hamu kwelikweli.

      Delete
  7. James, naomba majibu kwa maswali yafuayo:
    -Biblia original kabisa iliyoandikwa na roho mtakatifu ina vitabu vingapi?
    -Imeandikwa kwa lugha gani?
    -Kitabu cha daniel kina sura 12 au 14?
    -Umesema biblia yote imeandikwa na roho mtakatifu. Hata hili pia?
    ''ninenalo silineni agizo la bwana''.
    -Biblia yenye vitabu 73 na ile ya 66 ipi ya kweli? Je! Hapa kuna mkono wa roho mtakatifu au ubinadamu?
    -Luka katika 1:1-3 anajieleza jinsi alivyopata ukweli. Ni kwa kusikia masimulizi ya watu ambao hawakuwa manabii wala mitume, unasemaje juu la hilo?
    Ukweli unabaki palepale kwamba biblia sio kitabu chakutegemea sana kwa mambo ya mungu. Hapa duniani biblia ninazojua mimi ziko zaidi ya tano. Na zote vimepishana kwa namba ya vitabu vilivyopo.
    Sasa hapo mimi nabaki nashangaa, niamini biblia gani kati ya hizi?
    Ubabaishaji, kweli haimo.
    Tafakari. Jihoji. Kweli imo ndani yako! Soma Qur'ni tukufu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari Ibra. Najua kuwa tulikubaliana kuwa nisiwe nakujibu kama makala, yaani nje ya mahali ulikouliza maswali, lakini naona wakati mwingine inakuwa vigumu kwa kuwa, pale ninapotaka kuweka LINKS, kwenye comments section hiyo option haipo. hivyo, maswali haya nimeyajibu kwenye makala isemayo JE, BIBLIA INA VITABU VINGAPI?

      Delete
  8. Ibra,.naskia mtume alikuwa hajui kusoma wala kuandika,.na mnadai aya za koran aliteremshiwa,.swali huwa ni nani aliyeiandika koran? Ukweli atakuwa sio mtume! Na kama sio mtume,aliweza kuprove vipi kama kilichoandikwa ndicho alichoteremshiwa? Vipi kama kilibadilishwa na kuandikwa uongo mtume mwenyewe aliweza vipi kukihakiki na kuprove kuwa kilichoandikwa ni kweli? Maana hajui kusoma wala kuandika,.

    Na koran inasema viumbe wa kwanza kuiamini koran ni majini,na ndio maana mnaamini kuwa kuna majini wabaya na wazuri,.kama majini ndo walikuwa wa kwanza kuamini koran,huoni kama hiyo korani iliteremshwa na shetani mwenyewe? Maana majini mkuu wao ni shetani,.

    Lakini pia ningependa kuweka sawa kuwa,mungu wa koran(wa waislam),ni tofauti kabisa na MUNGU wa kweli wa biblia(wa wakristo walioamini),.maana hata sifa zao ni tofauti kabisa!

    Na inaonyesha mtume alipenda sana wanawake,.alikuwa na wake wanne? Du? Kazi kwelikweli

    HONGERA JAMES KWA KUMTETEA YESU,.ibra,naamini neema ya MUNGU wa kweli ipo juu yako na ipo siku utakuwa chombo kiteule cha MUNGU

    ReplyDelete
    Replies
    1. MUUJIZA WA IDADI NDANI YA QUR-ANI TUKUFU:
      1:Limetajwa neno siku{kwa wingi} mara 365,na idadi ya siku ndani ya mwaka ni 365.
      2:Limetajwa neno Siku {kwa umoja} mara 30, na idadi ya siku ndani ya mwezi ni 30.
      3:Limetajwa neno Mwezi mara 12 ,na idadi ya miezi ndani ya mwaka ni 12.
      4:Limetajwa neno Imani mara 25,na neno kufuru limetajwa
      mara 25.
      5:Neno dunia limetajwa mara 115,na akhera pia imetajwa
      mara 115.
      6:Neno Malaika limetajwa mara 88,na shetani limetajwa mara 88.
      7:Neno Watu limetajwa mara 50,na Manabii limetajwa mara 50.
      8:Neno Wanaume limetajwa mara 24,na neno Wanawake limetajwa mara 24.
      9:Neno Maisha limetajwa mara 145,na mauti pia limetajwa
      mara 145.
      10:Neno Mema limetajwa mara 167,na Maovu pia limetajwa mara 167.
      11:Neno Mbingu limetajwa mara 7,na idadi ya mbingu ni 7.
      12:Neno Adhabu limetajwa mara 117,na neno msamaha limetajwa mara 234 yaani mara mbili zaidi.
      13:Neno maji, limetajwa mara 32, na neno ardhi limetajwa mara 13. Ukilinganisha kwa asilimia utapata maji=71.11111%=71% na ardhi=28.8888889%=29%. Hivi ni vipimo ambavyo wanasayansi wamevipata.
      We ndugu! unaona jinsi gani quran ilivyopangika? Ni mungu peke yake mwenye ustadi wa mpangilio huu.
      Hivi wewe, kwa uzoefu wako, mtu asiesoma anaweza kupangilia kitu kama hilivyo quran kikakubalika karibia miaka 1500 sasa?
      We mwenyewe ni shahidi, kwamba kitu ukristo, bila ya kukumbatiwa na wazungu ungeshamwagikana. Dalili zimejionesha kule ulikoanzia leo hii karibia haupo kabisa! unatawala uislam maeneo yote ya mashariki ya kati. Sasa hapo, jiulize, hawa watu wa mashariki ya kati, ukristo ulikoanzia kwanini wanakumbatia uislam?
      Kwa hiyo, uweza wa kuandika quran, ikawepo kama ilivyo unatoka kwa mungu mwenyewe. Mungu ameilinda ndo maana haijichanganyi.
      Halafu, nikwambie kitu? Nabii usomeshwa na mungu sio wanadamu. Ukimuona mtu kasoma, halafu adai yeye ni nabii, ni muongo anataka kuwadanganya watu na kutafsiri vibaya aya za mwenyezimungu kama ilivyotokea kwa Paulo.
      Neno kutoka kwa mungu linaeleweka na lile ambalo halitoki kwa mungu linajulikana pia. Mfano mmoja ni kuhusu utofauti wa ukoo wa yesu kwenye injili ya matayo na ile ya luka.
      Halafu, wewe inavyoonesha hujui kitu. Wenzako wanapotafuta ukweli wa mambo, hawangalii kaanza nani kuamini, wanaangalia inafundisha nini!
      Unasikia wewe, kama kweli una nguvu ya hoja, ichambue quran na useme, nini kinachokufanya wewe usiamini.
      Hapa ukileta hoja ya majini au shetani utapasuka kichwa. Hao majini unaowasema wewe, walikuwa makundi mawili, moja waliamini quran kama tunavyoamini sisi na jingine hawakwamini kama msivyoamini nyinyi, sasa tatizo liko wapi?
      Ndugu, hao mapepo walimwamini yesu pia wakisema kwamba wewe ni mwana wa mungu! Tatizo liko wapi?
      Mtume Paulo alintumia shetani katika kuwafanya watu wamjue mungu!(tim1:20)
      Mungu wenu alintumia shetani ili aweze kunjaribu yesu! Tatizo lenu nyie wakristo liko wapi? Mbona mnatusingizia habari ambazo nyie ndo watumizi?????????????????
      Kuhusu swala la usawa wa mungu wa waislam na yule wa wakristo mimi nakubaliana na wewe. Kwa sababu, mungu wenu nyie ni yesu na mungu wetu sie ni yule ambaye mungu wenu nyie (yesu) alikuwa anamtegemea na kumwabudu, kama vile alipokakaa usiku kucha akimwabudu mungu, na pale msalabani kabla hajakata roho mungu wenu nyie, alisikika akimlalamikia mungu wetu sie kwa kusema mungu wangu, mungu wangu, mbona umeniacha?
      Swala la wanawake mbona umefupisha? Mtume alikuwa na wake tisa kwa kukuweka sawa. Sasa jee! ni dhambi kuoa wake wengi? Andiko gani kwenye biblia yako inakataza? Mbona kuna nabii alioa wake 700 na vijumba 300, jumla buku.
      Tatizo lenu nyie wakristo, mnajitungia taratibu za maisha nyie wenyewe, matokeo yake mnaanza kuzini, karibu kila mwezi, lazima mchungaji au padre wafumaniwe na waumini wao wakizini.
      Huyo James wako ana lolote analokufundisha.
      NENO LA MUNGU HALITETEREKI!
      Nyie wakristo, orodhesheni vifungu kwenye quran tukufu, ambavyo mnaamini kwamba bila ya hivyo, mngekuwa waiislam!

      Delete
    2. Hakuna muujiza wowote hapa. Kwa kuwa kuna watu ambao ni wajuzi zaidi wa eneo hili, basi ni vizuri ukawasoma wanachokisema. Mmojawapo alikuwa ni mwislamu.

      Nakili link hii kwenye google kisha utakutana na ukweli juu ya 'muujiza wa kiislamu' kuhusiana na tarakimu: http://www.answering-islam.org/authors/masihiyyen/numerical_miracles_309.html

      Yesu ni juu ya milima yote. Yeye ndiye Mungu wangu na Mungu wako daima.

      Delete
  9. nimejifunza kitu kikubwa kwenye mahojiano haya.Kwanza nawashukuru wote mliochangia ingawa najua kua ukamilifu ni wa mungu.Moja ya nilichojifunza ni kwamba kuna watu ambao wanazungumza tu kutetea upande wao yaani ili mradi yupo kwenye kundi hilo basi hataki kinyume hata kama atapewa hoja za msingi hatairuhusu akili yake itafakari hoja hizo na kuupata ukweli bali anakua na mtazamo hasi tu.Naomba tutafakari hoja au changamoto anayokupa mwenzio na sio kutetea kitu ambacho kiutash hakileti maudhui! Hata katika dini tunafundishwa kuongea vitu ambavyo tuna ushahid navyo na sio kila unachosikia basi unakiamin! Napenda nitoe angalizo qurani haijamtaja muhammad pekeake,mitume wote waliokuja kabla wametajwa kwa utukufu wao,mariam pia ambae ni mama wa yesu katajwa,mateso ya israel yawetajwa,vitabu vyote vilivyokuja na manabii tofaut vimetajwa,yesu mwenyewe na miujiza yake katajwa,na pia katika uislam tunaamin kua atarud tena.Je haya unayaona ni ya kipuuzi kuliko ndoto ya huyo mwanadam?? Je unairuhusu akili yako kutafakari au unaishi kwa ndoto za wachungaji? Elimu ndogo ni sumu ndo maana mwenye akili hamwombi mungu utajiri au ukuu bali huomba maarifa!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakushukuru Mohammed kwa kutembelea blog hii na kutoa maoni yako. Ninadhani kushikilia msimamo juu ya jambo si kitu kibaya, maana kinyuma cha hapo mtu anaitwa HANA MSIMAMO. Na kwa kweli kutokuwa na msimamo ndilo hasa linaweza kuwa tatizo.

      Isipokuwa sasa, pale ambapo watu wawili wenye misimamo tofauti wanapokutana, hoja ndizo zinazoweza kumfanya mwenye msimamo A kuuacha na kupokea msimamo B. hilo ni jambo la kawaida kabisa - shida tu ni mtu mwenye msimamo mmoja KUMLAZIMISHA mtu mwingine kuukubali msimamo wa mlazimishaji hata kama mlazimishwa haelewi.

      Lakini tunavyoendelea kujdiliana, ndipo ufahamu wetu juu ya yale tusiyoyakubali unaongezeka na, huwezi kujua, labda iko siku nitakuwa mwislamu - ingawaje kwa sasa maombi yangu ni waislamu WOTE wasiishie tu kusema kuwa Yesu, Mariamu, n.k. wametajwa kwenye Quran, bali wawe na Yesu pamoja na wokovu wa Yesu mioyoni mwao.

      Yesu anaitwa Emanueli - yaani 'Mungu pamoja nasi.'
      Pia, jina 'Yesu' maana yake ni 'atakayewaokoa watu na dhambi zao.'

      Sasa, hata kama ametajwa kwenye Quran, je hizo maana zimo ndani ya Quran na ndani ya wale wanaoamini Quran?

      Delete
    2. James, kudanganya hakufai! Nionyeshe sehemu gani yesu ameitwa mungu pamoja nasi?
      Nionyeshe sehemu gani Yesu yaani, yehoshua ina maana ya atakaewaokoa watu wake na dhambi zao?
      Nasubiri jibu!

      Delete
    3. Shalom ndugu yangu Ibra. Miaka 700 kabla ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu, nabii Isaya alitabiri katika Isaya 7:14 akisema: Kwa hiyo, Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.

      Kisha Mathayo akaja kusema, akimnukuu Isaya: Tazama bikira atachukua mimba, naye atazaa mwana; nao watamwita jina lake Imanueli; YAANI MUNGU PAMOJA NASI. (Mt 1:23).

      Ukirudi hapo juu kidogo katika Mathayo 1:21 imeandikwa: Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, MAANA, YEYE NDIYE ATAKAYEWAOKOA WATU WAKE NA DHAMBI ZAO.

      ................

      Bwana Yesu akubariki.

      Delete
    4. Mr.James, haya ndio matatizo ya biblia. Tunaposema biblia sio neno la mungu, matokeo yake ndio haya! Huyu mwandishi Matayo, kakusudia kabisa kuwadanganya watu eti ''Imanueli'' ni Yesu bila hata ya aibu. Nyie wakristo, tafadhalini sana, maneno ya hawa waandishi inawabidi muyachunguze na kuyachukulia hatua. Msiamini moja kwa moja. Mnapotoka pale mnaposema kwamba, wamefunuliwa na roho mtakatifu wakati kuna version za bible chungu mzima, ina maana mnapofanya mabadiliko ya tafsiri huyo roho mtakatifu anakuwa wapi?
      Sasa basi, nikirudi kwenye hoja ya msingi, nasema hivi, nukuu ya mathayo ni batili. Sio kweli! Utabiri haumhusu Yesu kwa sababu zifuatazo:
      1) Maria, hakuwai kumwita mtoto wake jina la Imanueli, kama utabiri unavyotaka, badala yake, kwamujibu wa biblia yeye amemwita mtoto wake jina la Yesu, kama alivyoelekezwa na malaika wa mungu. (Math.1:25 na Luka 1:30-31).
      2) Tukisoma kifungu chenyewe, kuzaliwa na jina la mtoto ilikuwa kwa ajili ya ishara kwa mfalme Ahazi ya kwamba mungu alikuwa pamoja nao kwa kuwa falme mbili adui walitaka kuwavamia (Isaya 7:10-16). Ahadi hii ilikamilika kipindi icho icho cha nabii Isaya!(2wafalme 16:9).
      Jina Mungu pamoja nasi inamaanisha mungu atatusaidia!
      Isaya 7:10-16 ''10 Tena Bwana akasema na Ahazi akinena,
      11 Jitakie ishara ya Bwana, Mungu wako; itake katika mahali palipo chini sana, au katika mahali palipo juu sana.
      12 Lakini Ahazi akasema, Sitaitaka, wala sitamjaribu Bwana.
      13 Naye akasema, Sikilizeni sasa, enyi nyumba ya Daudi; Je! Ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia?
      14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.
      15 Siagi na asali atakula, wakati ajuapo kuyakataa mabaya na kuyachagua mema.
      16 Kwa maana kabla mtoto huyo hajajua kuyakataa mabaya na kuyachagua mema, nchi ile, ambayo wewe unawachukia wafalme wake wawili, itaachwa ukiwa.''
      2Wafalme 16:9 ''9 Na huyo mfalme wa Ashuru akamsikia; mfalme wa Ashuru akapanda juu ya Dameski, akautwaa, akawahamisha watu wake mateka mpaka Kiri, akamwua Resini.''
      3) Isaya 7:14 kwa Kiebrania haisemi bikira, bali mwanamke kijana. Neno la kiebrania almah, lina maana ya mwanamke kijan. Neno la bikira kwa kiebrania ni b'tulah.
      Jibu lako la pili najibu kwa kukutolea mfano huu:
      LEO, KAZINI KWETU TUTATEMBELEWA NA MGENI KUTOKA MAREKANI, JINA LAKE JORGE BUSH, MAANA YEYE NDIYE ATAKAYE TUFUNGULIA SHULE YETU YA MSINGI.
      kAZI KWAKO!

      Delete
    5. Shalom Ibra,
      Yesu ana majina mengi: Bwana wa mabwana, Mkate wa uzima, Simba wa kabila ya Yuda, jiwe kuu la pembeni, Mwana wa Mungu, Alfa, Omega, Neno, Hekima, Kristo, Mwanakondoo wa Mungu, Shina na Mzao wa Daudi, Mzabibu wa kweli, Mti wa uzima, Nuru, Mpatanishi, Kuhani Mkuu, Mzaliwa wa kwanza, Mfalme wa amani, Mfalme wa utukufu, Mwalimu, Mungu, n.k., n.k.

      Unasema kuwa Mariamu hakuwahi kumwita Yesu Imanueli: Je, ni wapi ambapo Mariamu alitaja kuwa Yesu ataitwa kwa majina hayo hapo juu? Kama hakutaja, ina maana kuwa haya si majina ya Yesu? Kwani ili jina liwe la Yesu ni LAZIMA awe limetajwa na Mariamu?
      ………………………..
      Kuhusu Isaya 7:10-16, hata kama unabii huu ulitimizwa wakati wa Ahazi, bado kibiblia kuna kitu kinachotwa ‘dual meaning of prophecy’. Kuna unabii mwingi sana ambao unatimizwa zaidi ya mara moja – katika kipindi ambapo unabii huo unatolewa na pia baadaye. Kwa mfano, ukisoma Yer 51:63-64, nabii Yeremia anatabiri juu ya hukumu ya Babeli ambao utazamishwa kabisa wala usiibuke tena. Inaeleweka kwamba ufalme wa Babeli haupo tena leo.

      Lakini jambo lilelile tunalikuta kwenye kitabu cha Ufunuo – yaani juu ya kuzamishwa milele kwa Babeli. Lakini safari hii haiongelei ufalme wa Babeli wa kibinadamu, bali utawala wa shetani. [Hebu linganisha Yer 51:63-64 na Ufunuo 18:21].

      Hivyo, hata kama ingekuwa kwamba unabii wa Isaya ulitimizwa wakati wa Ahazi, bado kulikuwa na mwendelezo wake ambapo huyo unayemwita ‘kijana mwanamke’ alitakiwa kumzaa Imanueli, yaani Mungu pamoja nasi……

      Nikikunukuu maoni yako, unasema: “Mnapotoka pale mnaposema kwamba, wamefunuliwa na roho mtakatifu wakati kuna version za bible chungu mzima.” Hii imekuwa ni hoja yako ya kila mara kwamba Biblia haiaminiki kwa kuwa kuna Biblia mbalimbali zinazotofautiana. Hapa unamaanisha kwamba Quran ni ileile kutokea mwanzo na katika ulimwengu wote wa Kiislamu.

      Katika makala yangu niliyoyaita “Je, ni kweli quran haijawahi kubadilika na wala haina mkono wa mwanadamu ndani yake?” nimetoa link mwisho kabisa juu ugunduzi wa nakala za Quran kwenye msikiti kule Yemen. Nikinukuu makala hayo, yanasema hivi: “Soon after the project began, it became clear that the “paper grave” is a resting place for, among other things, tens of thousands of fragments FROM CLOSE TO A THOUSAND DIFFERENT CODICES OF THE QURAN”!!! – yaani kuna aina karibu 1000 za Quran zinazotofautiana! Hivi mwislamu ana haki gani ya kutuhumu uhalali wa Biblia kwa kigezo cha ‘versions tofautitofauti’? of course ninajua kuwa utasema hizo ni nakala feki wala hazitoki kwa mtume, n.k., n.k. – maana sifa mojawapo kubwa sana ya uislamu ni DENIAL.
      ……………..
      Umetafsiri Mathayo 1:21 kwa kutumia mfano wa George Bush. Unapojifunza lugha ktk kipengele cha Semantics, kuna sentensi ambazo wanasema ni ‘tungo tata’- yaani inaweza kutafsirika kwa namna zaidi ya moja. Lakini pia katika kuamua maana kuna kile kinachoitwa ‘meaning of the speaker’ na ‘meaning of language’. Nikisema tungo tata itakuwa na maana yangu mimi niliyoikusudia lakini pia maana ya maneno menyewe ambayo sikuikusudia. Sasa huwezi kunilazimisha nikubali maana ambayo sikuwa nayo mimi ingawaje imo ndani ya maneno.

      Hivyo basi, unatafsirije pia aya zifuatazo: Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa, KWA KUWA YEYE NDIYE ALIYE MAMA YAO WOTE WALIO HAI. (Mwa. 3:20); Tazama, wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, MAANA BWANA AMESIKIA KILIO CHA MATESO YAKO. (Mwa 16:11); wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, KWANI NIMEKUWEKA UWE BABA WA MATAIFA MENGI (Mwa 17:5).

      Delete
  10. Kaka James nimefuatilia sana comment zako na naweza kusema yute hiyo ni kazi ya Roho Mtakatifu katika kukuongoza kuelimisha wenzetu(waislam) walio na msimamo wa uuaji na hasira kali juu ya wenzao.Kitu cha muhimu ni kuukubali ukweli kuwa Yesu ni MUNGU na ni mkombozi wa dunia hii.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shalom, shalom mpendwa. Asante kwa maoni yako na Bwana akubariki. Waislamu ni wapendwa wenzetu kabisa. mioyoni mwao wanaamini kwa dhati kabisa kuwa wako sahihi, maana wanadamu walio wengi hawangependa kwenda kuzimu, lakini ni kazi na wajibu wetu kuomba kwa ajili ya wote ili waweze kumjua Mwokozi wetu na wao, ambaye anatupenda SANA SANA wanadamu wote.

      Delete
  11. ibra ni mara ngapi umekosewa na kumsamehe aliyekukosea? bila shaka ni mara nyingi sana.kwa nini hukulipiza kisasi kama Q'tukufu inavyokuagiza? ni mara ngapi umemwona mwizi amekamatwa na hukuenda kumpiga mawe hadi afe kama Q' tukufu inavyokuagiza? naamini umewahi kutukanwa, kuibiwa, kupigwa nk lakini ukasamehe! huende nafsi yako ilikuambia samehe, puuza nk . hivyo wewe ni mfuasi mzuri sana wa yesu kilichobakia kwako ni kumkiri kwa kinywa chako ya kuwa yeye ni bwana na mwokozi wa maisha yako. yesu anasema samehe mara saba mara sabini, na ni yeye ndiye anatukataza kulipiza kisasi( na kusema kisasi ni cha bwana) na kusema usiue. hivyo unaiishi biblia takatifu na si Q'

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwab hiyo, kwa akili ya kwako wewe, unataka wote watendao maovu wasamehewe? Mwizi, mtu akizini na mkeo, mtu aje tu nyumbani kwako achome nyumba yako, ambake mtoto wako wa kike hadharani na we mwenyewe unaona. We unaona sawa tu? Sasa sikiliza kauli ya mungu wako:
      14 Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.
      15 Basi Bwana wa majeshi asema hivi, katika habari ya manabii, Tazama, nitawalisha pakanga, nitawanywesha maji ya uchungu; kwa kuwa kutoka kwa manabii hao wa Yerusalemu kukufuru kumeingia katika nchi yote.
      16 Bwana wa majeshi asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria; huwafundisha ubatili; hunena maono ya mioyo yao wenyewe; hayakutoka katika kinywa cha Bwana.
      17 Daima huwaambia wao wanaonidharau, Bwana amesema, Mtakuwa na amani; nao humwambia kila mtu aendaye kwa ukaidi wa moyo wake, Hamtapatwa na ubaya wo wote.
      Yeremia 23:14-18
      Mungu anasema, watu kama nyinyi, MNATIA NGUVU KWA WATENDAO MAOVU.
      Kwa maana hiyo wewe katika kufunua funua kwako vitabu vya mungu ukagundua quran ina makosa kwamrisha watu wauawe wanapotenda kosa?
      Biblia kitabu chako kinasemaje?
      7 Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
      8 Nanyi zishikeni sheria zangu, na kuzitenda; Mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi.
      9 Kwa maana kila mtu amlaaniye baba yake au mama yake hakika atauawa, amemlaani baba yake na mama yake; damu yake itakuwa juu yake.
      10 Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.
      11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.
      12 Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo uchafuko; damu yao itakuwa juu yao.
      13 Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.
      14 Tena mtu mume akimwoa mke pamoja na mama yake, ni uovu mkuu; watachomwa moto, yeye mume na hao wanawake pia; ili kwamba usiwe uovu kati yenu.
      Mambo ya walawi 20:
      Msikilize yesu mwenyewe:
      Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.

      Delete
    2. Ibra habari. Jibu lako kwa huyu ndugu, kwa ujumla wake unachomaanisha ni kwamba: Haitakiwi kusamehe kila kitu. Huu ndio msimamo wako, na of course ndio msimamo wa Uislamu, maana hivi ndivyo unavyosema: "Kwab hiyo, kwa akili ya kwako wewe, unataka wote watendao maovu wasamehewe? Mwizi, mtu akizini na mkeo, mtu aje tu nyumbani kwako achome nyumba yako, ambake mtoto wako wa kike hadharani na we mwenyewe unaona. We unaona sawa tu?"

      Lakini huu si msimamo wa Ukristo wala wa Bwana Yesu. Mimi na wewe ni binadamu. Hali ya asili kabisa ya mwanadamu kuhusiana na mambo uliyotaja hapo juu ni kukasirika, kuumia, na kutaka kulipa kisasi - ndiyo maana ni ajabu kwa Uislamu kuifanya kuwa ni hali ya kidini! Je, hata wapagani nao si wana-react kwa namna hiyohiyo wanapoudhiwa? Sasa ukiwa mwislamu na wewe ukafanya kama wapagani, tofauti yako na wao ni nini basi?

      Lakini Bwana wa uzima, Yesu Kristo anasema hivi: Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni ... Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? ... Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? (Mt 5:43-47).

      Kwa kuwa mimi na wewe ni wanadamu, nilazima tukiudhiwa tunakasirika. Lakini Kristo akiwa ndani yako, UNASHINDA YALIYOSHINDIKANA! Ndiyo maana imeandikwa: Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi. (Zekaria 4:6).
      ............

      Na kuhusu hiyo Walawi 20 uliyonukuu kwamba eti Yesu anasema: "Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu," ukitaka kumaanisha kwamba Yesu anaruhusu uuaji au kulipa kisasi, unajua kabisa kwamba you are wrong. Nilishakujibu kwa mapana kabisa juu ya hoja hiyo katika makala niliyoita: JE, YESU ALIAGIZA WAFUASI WAKE WAWAUE MAADUI WA YESU? Unachofanya wewe kwenye aya hii ni upotoshaji tu. Unamwekea Bwana Yesu maneno na maana ambayo hakuikusudia. Si vibaya uende ukasome tena makala hayo.

      Bwana akubariki.

      Delete
  12. I adore or appreciate James John na Ibrabura. Maana kupitia Maswali ya Ibra Injili inakolea ..Hakika injili ni Neno la Bwana liletao wokokovu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Thanks pal. God bless you and keep standing. The Lord is coming soon.

      Delete
  13. ibra asante kwa majibu mazuri kwa mujibu wa uelewa wako. kwa imani ya wakristo biblia nzima niNENO la MUNGU pamoja na walawi uliyonukuu.Ila injili ya yesu ambaye hakika ni mwana wa MUNGU tofauti na manabii waliomtangulia ililetwa kwa ajili ya wokovu na kukamilisha yote yaliyonenwa kabla yake ambayo yalionekana yanahitaji kuongelewa tena mfano, sheria iliyokuwepo ilikuwa ni kuwachukia adui, alisema tuwapende. kutofanya kazi siku ya sabato, alisema ni vyema kufanya jambo jema siku ya sabato, kuwapiga mawe waliozini, alisema ambaye hajazini awe wa kwanza kumpiga,kuhusu kutokula baadhi ya vyakula, alisema kiingiacho hakimtii mtu unajisi( kwani hutupwa chooni) bali kimtokacho mtu ndicho chamtia mtu najisi,nk. hivyo kama jambo lile lile lilinenwa hivi kabla ya yesu, naye kaja na akasema hivi ni wajibu wetu kufuata maagizo ya yesu. MFANO WA KIDUNIA. ulipokuwa darasa la tatu ulifundishwa 5 - 8 = haiwezekani. ulipofika darasa la tano ulifundishwa 5 - 8 = -3
    . kwa nini hukukataa majibu haya ya darasa la tano na uendelee kuamini majibu ya darasa la tatu mpaka leo? majibu ya haiwezekani kwa darasa la tatu yalikuwa ya ukweli kulingana na umri wao na uwezo wao wa kufikiri. majibu ya darasa la tano kwamba ni hasi tatu ndio sahihi
    mpaka phd jibu ni hilo. kwa hiyo walawi uliyonukuu ndiyo majibu ya darasa la tatu na injili ja yesu ndio majibu ya darasa la tano ambayo kila mmoja aliyekwisha fika la tano kuendelea anatakiwa ajibu anapoulizwa. ukifanya mtihani wa lasaba, form 2, form 4, form 6 , C/ kikuu na kuandelea kujibu 5 - 8 = haiwezekani, lazima ukoseshwe kwani wasahihishaji wanajua ulipaswa kujibu 5 - 8 = -3 na ndio jibu sahihi.kwa hiyo habari ya kupiga wawe wazinzi, kukata mikono wezi,kuchoma watu moto, kufukia watu kwenye mashimo nusu, kuuwa/ kuwachukia
    maadui, HAYAPO TENA MAANA SI MAJIBU SAHIHI NA HAYATARUDI TENA KUWA MAJIBU SAHIHI. tafadhali sana soma WARAKA KWA WEBRANIA sura ya nane yote ( attention mstari wa 6,7,9 na mstari wa 13) sura ya tisa yote ( attention mstari wa 1,9, 10,11,14,15 ,19 23, 24,25,26) na sura ya kumi yote. utaona misingi ya mfano wangu na meelezo yangu. welcome to JESUS, salvation and then HEAVEN.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hili jibu ni zuri SANA maana linaeleza kwa ufupi lakini kikamilifu sana maana ya Agano la Kale na maana ya Agano Jipya pamoja na uhusiano kati ya maagano hayo mawili. Nimeupenda mfano wa hesabu ya 5-8 na majibu yake ambayo ni sahihi lakini kulingana na majira na nyakati.

      Bwana Yesu akubariki mpendwa.

      Delete
  14. james mi naitwa castor, nilichangia mjadala wako na ndugu ibra, nikamuuliza kwanini hajawahi kumpiga mawe mzinzi, naye akanijibu kwa maandiko ktk walawi ambayo hakika ni neno la mungu
    ikabidi nitafute mfano mrahisi wa kidunia na wenye uhalisia kumuelewesha naamini ataelewa sasa kwanini ingawa walawi aliyonukuu inatutaka kuwapiga mawe wazinifu, kuwakata mikono wezi nk lakini wakristo hawatekelezi hayo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amen Castor. Nashukuru sana kwa maoni yako. Ubarikiwe na Bwana.

      Delete
  15. ibra unaitaji ukombozi

    ReplyDelete
  16. ibra bila shaka umeelewa vyema mfano wa hiyo hesabu hapo juu ndio maana uko kimya! hongera. yesu alishakukomboa kilichobaki ni wewe kuacha ubishi, aibu na kuungana nasi kumtangaza yesu kwa kila kiumbe. kama utapenda ntakupa namba ya aliyekuwa mbishi na siasa kali naamini zaidi yako sasa ni mfuasi mzuri wa yesu kristo mwana wa Mungu na kwaq kuwa alikuwa upande wenu zamani hakika yeye ana maelezo mazuri sana kwako pengine kutushinda.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hiyo hesabu, mimi nimeipata na nimeelewa vizuri sana. Umenifurahisha kwa kukiri kwako juu ya kile kinachoonekana ndani ya biblia katika kitabu cha mambo ya walawi 20:7-14, mungu wa biblia alivyoruhusu binadamu kuhukumiwa kwa namna tofauti tofauti kulingana na makosa mpaka kufikia ya KWUAWA. Bila ya shaka, aya hii inaweza ikafanana na hukumu itolewayo na mataifa ya kiislamu dhidi ya raia wao wafanyao makosa kama hayo!
      Lakini, katika kutetea imani yako, ukanitolea mfano wa hesabu ya 5-8=-3 na 5-8=''haiwezekani,". Ndugu yangu, mtu amejifunza hesabu ya 5-8 jibu likaja "haiwezekani" huwezi kumlinganisha na mtu wa dhama za nabii Mussa, kwa sababu, dhama hizo kulikuwepo taratibu za mungu za mtu kuupata uzima wa milele, lakini huyu wa hesabu, hawezi kuwa engeener kama ataendelea na utaratibu huo! Kwa hiyo ni tafauti wala haiyendani kabisa. Kwa kudhihirisha hilo, Yesu alisikika akisema kwamba yeye akuja kwa ajili ya wenye haki bali kwa wale waliopotea (walio nje ya utaratibu wa mungu). Soma Mt 9:11-13. Kwa hiyo, wale wote ambao walikuwa na mashiko wa taratibu za mungu walizoteremshiwa kupitia minabii kabla ya Yesu hakuwa na haja nao. Yaani Yesu hakuja na kitu kipya, ndio maana akahubiri yafuatayo katika matayo 5:17-20:
      "17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
      18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.
      19 Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
      20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni."
      Ndugu, kwa kuwa wewe unajinadi kuwa mtu wa Yesu, yafaa umsikilize yeye kama mwenyewe alivyodai kuliko kumsikiliza mtu mwingine!
      Kwa vipengele nilivyokuonyesha hapo juu, haina haja ya wewe kuwasikiliza akina Paulo, kwa yale aliyoandika katika waraka kwa waebrania. Sio mkweli, maneno mengi anapishana na Yesu. Hivi unajua kwamba huyu Paulo alikuwa anafanya kazi na shetani? Soma Timoteo I 1:20.
      Kwa hiyo sheria bado ipo kama ilivyoshushwa na mungu na haiwezi kuondoka mpaka pale mbingu na nchi zitakapoondoka kama alivyodai Yesu ambae ni mkuu kuliko Paulo.
      Na ujuwe kwamba sheria ya mungu anatenguwa mungu mwenyewe, sio binadamu. Sasa sehemu gani ndani ya biblia mungu anatengua hiyo sheria?
      Hivi we ndugu, yafaa nini kuwa na imani na mungu, bila ya kutekeleza mamrisho yake?
      Huu si ushetani ndugu? Maana shetani anamjua mungu kuliko hata unavyomjuwa ,ila akutaka kutekeleza amri zake. Soma yakobo 1:22-25.
      "22 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. 23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. 24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. 25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake."

      Delete
  17. Ndugu, hapa duniani, kuna matendo mengine yanakuwezesha kupata thawabu mbele za mungu ukiyatenda, lakini kama ukuyatenda, mungu hawezi kukuandikia dhambi. Mfano, Yesu alisikika akiwaambia wanafunzi wake maneno yafuatayo:
    38 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; 39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.
    Sasa hapa kuna kauli mbili, moja ni ya kisheria na jingine ambalo ni ya Yesu ambalo ukilifanya unaweza kupata thawabu na usipolitenda ukalitenda lile la kisheria huwezi kupata dhambi hata QURAN TUKUFU INATAMBUA.
    "40. Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu." QURAN 42:40
    Mi nawashangaa sana nyie wakristo, hivi maandiko hamuyaoni au mnafanya kusudi?
    Sasa angalia yesu anavyobariki:
    "29 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
    30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum." Matyo 5:29-30
    Jamani he! Labda niseme kitu kimoja, sisi pamoja na yesu hatufuati mawazo ya kibinadamu. Tunatekeleza kile ambacho ni amri kutoka kwa mungu pale inapobidi.
    Unaona jinsi gani maneno ya mungu yanavyolingana? Je! Umekubali kwamba maneno ya yesu sio msumeno?
    Hoja nyingine, nisingependa niyache ni juu ya utoto wa mungu wa Yesu. Jambo hili wakristo linawachanganya sana. Mimi sijui wanapokwama, yesu mwenyewe amewahi kusema kwamba "17 Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. Ndugu usiwe na akili ya kuvukia barabara tu, ebu waangalie na watoto hawa, sijui utasemaje!
    "22 Nawe umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu;
    23 nami nimekuambia, Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia, nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako."
    Kutoka 4:22-23.
    "Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa." Zaburi 2:7.
    "9 Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu." Yeremia 31:9.
    Mwisho kabisa ningependa niwashauri jambo. Angalieni kwanza pande zile ambako imani zetu zimechimbuka watu wake sasa hivi kwa %kubwa wana dini gani? Jibu ukilipata tafadhali sana lifanyie kazi kama wazungu wanavyofanya siku hizi.
    Naona umewahi kusikia kwamba uwanja wa emirate wa london ni marufuku kuingia bendera ya uingereza kwa sababu ina msalaba. Tafakari sana ndugu yangu, wacha ile dhana potofu inayokusumbua tafuta dini ya kweli.
    Kazi njema!

    ReplyDelete
  18. ibra ni vigumu kukuelewesha kwani wewe unasoma biblia katika mwili, biblia haikuandikwa kwa akili na utashi wa kibinadamu bali iliandikwa wakiongozwa na Roho wa Mungu/ Roho Mt/Roho wa Yesu nini cha kuandika hivyo hata kuielewa ni lazima usitumie akili za kimwili( kama ya kuvukia barabara kama ulivyosema) bali uisome ktk roho. kwa msingi huo hutaweza kuielewa biblia kwa sababu hata Roho Mt Hamuitambui na wala hamuiamini.yesu mwenyewe anathibitisha hili pale anaposema '' baba nakushukuru kwa sababu mambo haya umewaficha wenye akili na kuwafunulia watoto wadogo'' watoto wadogo wanawakilisha watu waendao ktk roho na si ktk akili kama unavyotaka tuenende. Paulo ni mtu ndio, lakini aliyokuwa akiyahubiri na kuyaandika hayakuwa ya kwake bali ya Yesu, kwani aliyemuita kutoka katika uhalifu wake ni yesu na ni yeye/ Roho wa yesu ndiye alikuwa akihubiri kupitia mwili wa paulo. kwa maana nyingine maneno ya paulo ni maneno ya yesu mwenyewe isipokuwa pale paulo alipotoa ushauri wa kwake mwenyewe. paulo si tu ninyi waislamu hamumuelewi bali hata wakristo wengi hawemuelewi kwani wanaona ujumbe wa paulo ni kaa la moto kichwani pao, kwa sababu wengi wanaenenda ktk mwili. AGANO JIPYA TOA PAULO NA NYARAKA ZAKE ni sawsaw na historia ya maisha na matendo ya yesu tu, nyaraka za paulo ndio dira na mtzamo wa maisha ya kila siku y a mkristo.( bila roho wa Mungu kamwe hutaweza kuelewa kaulihiyo) castor

    ReplyDelete
    Replies
    1. Castor, mimi nadhani majadiliano yetu, yanalenga juu ya IMAN YA KWELI itakayosababisha mtu apate uzima wa milele. Sote tunaamini kwamba Mungu alituma minabii, kwa ajili ya kuwalingania watu ili wamjue yeye ya kwamba ndiye apasaye kwabudiwa kwa haki na kila mtu. Na hao manabii, kwa majaaliwa ya mungu mwenyewe wakaona ni vema ujumbe wa Mungu uandikwe ili uwe fundisho kwa vizazi vijavyo. TAURATI, ZABURI, INJILI NA AL-QURAN vilipatikana.
      Mimi naamini kwamba sio lazima mtu awe na imani ndipo ailewe biblia. Ila imani anaipata baada ya kuisoma biblia na kuilewa. Ndo maana kuna mashirika fulani kutoka america walikujaga hapa tanzania kugawa biblia na akagawiwa kila mwenye kuwepo eneo husika bila ya kujali.
      Sasa unaponituhumu mimi kwamba nasoma biblia kimwili sisomi kiroho na hao waliotengeneza hizo biblia kwa ajili ya kuwagawia watu wasiokuwa na imani ile huyu roho wanampata wapi ili wao waamini? Jibu ni kwamba hakuna hizo ni jinsi wakristo wanavyojiaminisha wanapokutana makanisani mwao.
      Ndugu, hoja ya msingi katika majadilano yetu ni kitu gani kinachofanya wakristo msimwamini mtume muhammad kuwa ni mtume wa mwisho, yule ambae manabii wa nyuma walitabiri kuja kwake?
      Kwa madai yenu mnasema kwa sababu yeye ni mwuaji, yaani kitabu chake kinaruhusu kwua tofauti na biblia.
      Sasa mimi nimetoa andiko, wapi mungu wa biblia anaruhusu mauwaji, kama ilivyo kwenye quran alafu wewe unaniambia mimi nasoma biblia kimwili, kivipi hapo?
      Ndugu, sheria ya taurati bado ipo hai kwa ushahidi wa maneno ya yesu na mungu mwenyewe, sio mtu mwingine hapa!
      Mtu akifanya kosa, lazima ahukumiwe kutokana na kosa lake.
      Lakini pia, mtu akikukosea wewe kwa sababu sheria imeandikwa jino kwa jino, basi unaweza kumsamehe ili wewe ujinufaishe mbele za mungu.
      Ndugu, leo nataka nikupe faida kidogo kwamba mtu huwezi kuwa na imani ya kweli bila ya kufuata matendo. Na mtendaji wa matakwa, au maagizo ya mungu yuna imani ya kweli.
      Ndugu, shetani anamjua mungu kwamba ndiyo mwenye mamlaka yote, lakini yeye akapotea kwa sababu alishindwa kumtii mungu kwa maagizo yake. Sasa wewe ukiwa imani tu, basi upishani na shetani.
      Ufalme wa mbinguni unafanana kwa karibu na tawala zetu za hapa duniani. Wewe unaamini kabisa ya kwamba unatawaliwa na serikali fulani, unaamini pia kwamba hiyo serikali ina taratibu zake za utawala ambazo ukienda kinyume na hizo utahukumiwa bila kujali imani yako na serikali.
      Na kitu kingine, mimi nasema hivi Paulo sio, hatokuwa na hategei kuwa mtume wa yesu. Sasa basi ukitaka mada hii tuiamushe, mimi ushahidi ninao.




      Delete
  19. Ushabiki aufai maana waislamu wanaushabiki mbaya juu ya dini wala hawataki kweli.Nakwasasa blog hii wanaijua sana labda wanawezafunguliwa kupitia kwayo.james john Mungu akubariki kwani kupitia masomo/makala yako sasa imani yangu kiroho imekua 7x70.Bwana akuongoze.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amina rafiki mpendwa. Mungu akubariki nawe pia. Tuzidi kuomba kwa ajili ya hawa ndugu zetu, maana Kristo Yesu ni Mwokozi wao kama ilivyo kwetu.

      Delete
  20. Hahahaha...hivi kama injili yenyewe ingehubiriwa kama mnavyohubiri nyinyi, hata mtu mmoja msingempata. Kwa sababu hoja zenu ni dhaifu yaani hazina mashiko. Mnasema biblia ni neno la mungu iweje sasa, maagizo mengine muyakatae.
    Mada imewashinda mnaanza visingizio sasa. Kitu gani nimeshabikia? Wewe ndiye mshabiki eti 7x70. Ebu jiulize kwanza juu ya mikakati iliyokawekwa na watu wa imani yako kwenye mkutano wa niceia. Mojawapo haikuwa ya kuwauwa wale wote ambao wangepinga makubaliano yaliyokafikiwa kwenye huo mkutano?
    We nini bwana! Kila siku tunawaona wakristo kwenye mahakama wanadai nini na wao wameambia wasamehe? Eneo lenye wakristo wengi basi hapakosi ujambazi, ukahaba, mauwaji ya albino nk...
    Hii ni kutokana na ibada zenu na inafikia sehemu watu hawamuogopi mungu.
    Kumbuka maneno yangu "IMANI ZETU ZOTE ZIMEANZIA MASHARIKI YA KATI, LEO HII, % KUBWA YA WATU WAKE WANA DINI GANI?"

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lakini Ibra, unaongelea hapa WATU hauongelei Neno la Mungu (Biblia). Watu walio waovu hawataisha hadi mwisho wa ulimwengu. Ni sehemu moja tu ambako hakuna uovu - yaani Mbinguni kwa Bwana Yesu.

      Ukisema kwamba waliko Wakristo kuna ukahaba, mauaji ya albino, n.k., ni wapi kwenye Biblia ambako tumeagizwa kufanya ukahaba au kuua albino? Kwani huko yanakofanyika hayo hakuna Waislamu?

      Ongelea Biblia usiongelee watu?

      Hakuna sehemu yoyote kwenye Biblia ambako Mungu anaagiza watu watende uovu.

      Delete
    2. ibrabura Ushabiki ni Hahahaha...hivi kama injili yenyewe ingehubiriwa kama mnavyohubiri nyinyi, hata mtu mmoja msingempata. Kwa sababu hoja zenu ni dhaifu yaani hazina mashiko. Hapa inaonyesha ww upo radhi ili tu upate watu maana unasema tusinge pata mtu ila kwa mimi cmlazimishi mtu kuwa mkristo bali nitamfundisha kweli lakini suala la kufuata ni yeye mwenyewe. mengi ushajibiwa ila unaposema "IMANI ZETU ZOTE ZIMEANZIA MASHARIKI YA KATI, hapa unaonyesha unacho amini bado unamashaka nacho ila imani ilianzia huko, lakini lengo lilikuwa ni kwa watu wote sio kama ww dhana yako unasema sijui imeanzia mashariki utadhani ameianzisha mtu.Alafu kama hujui unauliza sio unatoa maana zako ambazo hazina weledi eti Kila siku tunawaona wakristo kwenye mahakama wanadai nini na wao wameambia wasamehe? ivi kama unarudi nyumbani na kukuta mtu amejimilikisha nyuma yako usamehe tu.Biblia haijatufunga kiivyo lakini tunasamehe nini?? Kwa mfano kunajambo ambalo haliwezi kunidhuru hapo sinabudi kuachana nalo nakuepusha malumbano ivi mbona inafahamika FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE. eti Eneo lenye wakristo wengi basi hapakosi ujambazi, ukahaba, mauwaji ya albino nk... ivi ujiulizi shehe ponda mbona anateseka hii ni kwasababu mfumo wa kiislamu haukubaliani na utaratibu wakibinadamu kamwe.gadafi,osama na sadamu huseni ambaye amenyongwa ni kwasababu tu hajakubali mfumo wa maisha ya binadamu tena mnaita mfumo kristo.ibrabura NI YESU KRISTO PEKEE NDO NJIA,KWELI NA UZIMA.

      Delete
  21. ibra, mohamad ni marehemu na mdhambi kama tu mababu wa kale walivyo, hata ninyi mnafahamu hili ndio maana mnajitahidi kumwombea rehema na amani huko ahera aliko ili yesu amrehemu. kama sivyo, ninyi si mnawaheshimu na kuwatambua manabii wote wa mwenyezi Mungu? kwa nini yeye mumuombee rehema peke yake na si yeye pamoja na manabii wengine kama yesu, ibrahimu, adamu nk? jibu ni simple kwamba ktk manabii wote yeye ndiye anahitaji rehema kwani ndiye mdhambi na yeye ndiye yuko kuzimu (wenzake wako mbinguni). kwa msingi huo nitamfuataje mfu, marehemu anayehittaji rehema kama babu yangu? namfuata aliye hai, aliyefufuka na yuko mbinguni na ambaye hukumu yote iko mikononi mwake ikiwemo kumhukumu muhamad. hata alipokuwa ktk mwili alimsamehe yule mama kahaba dhambi zake. ndio kazi yake kurehemu, kusamehe na kuhukumu kila kiumbe akiwemo muhamad. hivyo siwezi kumfuata marehemu muhamad kamwe kwani hana sifa za kufuatwa na watu wanaotaka kwenda mbinguni, wale tu wanaotaka kwenda kuzimu aliko ndio wapaswa kumfuata,hata hivyo yesu anawaonea huruma anawaita mumfuate ili aliko yeye nanyi muwepo. ni suala la muda tu, muhamad atawakaribisha wafuasi wake kuzimu huku yesu akiwakaribisha wafuasi wake wa kweli kweli kwa baba yake mbinguni.

    ReplyDelete
  22. I'm Alan Khassim,nlkuwa na iman flan badae nkawa na nyngne,nlchogundua mtu akokoka ni kbadlka mana ananza kuish maisha yasowaumza wnadam wenzke bal kwafaidsha.Sasa kwa hbar ya hiz iman 2 nmegndua kwamba Mr John anatamn aelewke ktk hoja zke(UKRSTO/INJLI) kptia Roh Mt na hsa kamua kusulubsha mwli na raha zupendzo ambzo si ktk nature ya kbinadmu Kma Yesu na magizo yke.Wkati huo Mr Ibra anafundsha imni yke kwa njia ya IMANI na SHERIA .Ssa hii inakua ngmu kelewna kwan UISLAM ni URITHI ambpo UKRISTO halsi utaktfu/ulokole ni kuamua bnafsi na kjikna na ndio mana wengi wanahsi ni wakristo lkini si halsi kwan hawakbar kbadlka.Kimsng tungelewan kma Roho mtaktifu anakpa sir za dunia hii na Mbngun Bw Ibra.So kwmba ssi walokole hatjui kuish maisha ya raha na ssi tunavyotaka,ni rahsi ila shda ni kumksa Mungu na kuwaudh wnadmu.Sasa ili kuamin si mnafamina?anza kfuatlina ktk matendo na life styles znu kwa sri au fuatilia mtu kama marehm Kulola au Mwaksege,wanampenda Mungu na wmemona ACHA UBISH YESU ANAOKOA.0753936742.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amen brother Alan. Asante kwa ushuhuda wako, maana wewe unaongea kutokana na practical experience. Unajijua ulivyokuwa kabla ya kumpokea Kristo Yesu na unajua ulivyo hivi leo.

      Kwa hiyo unafahamu vizuri kwamba wokovu si dini, maana dini ulikuwa nayo hata kabla. Kama ambavyo huhitaji dini ili kuwa na uhusiano mzuri na mzazi wako, ndivyo ambavyo huhitaji dini ili kuwa na uhusiano mzuri na Mungu. Dini si mbaya lakini si MSINGI wa kupokea uzima wa milele kutoka kwa Mungu.

      Uzidi kubarikiwa sana na Bwana Yesu.

      Delete
  23. Mr.James,Mr. Ibra, Mr. Castor na Mr. Alan Bwana Yesu asifiwe!! ukweli leo nimetiririka na mada nzima ilimuhusu Mohamad yaani Mtume wawa islam, ninapo shangaa ni pale Ibra anakuwa na Jazba wakati nikimsoma James ndo kwanza anacheka roho yako na sura yako inavyobadilikia hiyo screen bure............Kwanza kabisa nakupa hongera sana Ibra maana unataka kujifunza kuhusu huyu mwanaume shujaa tunayemsema habari zake ni njema kila paitwapo leo nae ni YESU. Mada ilikuwa Mohamad yuko wapi? Mimi nakujibu bila kuota au kuhisi yupo motoni ki ukweli maana Biblia inasema aaminiye na kubatizwa ataokoka, na asiye amini atahukumiwa je! Mohamad ameokoka? jibu ni Hapana? je misamaha ni ya nini mnamwomba Mungu kwa ajili yake? umewahi sikia mkristo yoyote anamwombea Yesu msamaha? jibu ni hapana!! Ibra usifanye jambo kwa jazba mpaka kufikia unamtukana Mungu, sikuzote ukitaka kujifunza/ kujuzwa kitu hebu nenda taratibu mpaka ufike mwisho kuliko kuwa hivyo. Kama umewahi sikia mkutano mkubwa wa injili hapo Tegeta alihubiri mmoja wawafuasi wenu aliye asi na kumkubali YESU kuwa ni Bwana na ni Mungu anaitwa ............. shekhe Abubakar? uzuri na ubaya wako unachukulia andiko mstari mmoja na kutembea nao jaribu kusoma maandiko mwanzo wa story mpaka mwisho........unanifafanuliaje huu mstari? 1kor 15:15 je unaamini Yesu kafufuka au unadhani hajafufuka? Bwana Yesu awabariki.

    ReplyDelete
  24. Jamani ushabiki tuweke kwanza pembeni. Nina jambo la kushauri its better kwa mkristo akausome uislam vizuri kwa ustadh anaejua na aulize maswali yake ya kutosha na muislamu nae amtafute kiongozi wa kikristo anaejua kisha aulize maswali yake then mtulete feedback. au pia kuna video zinazoonesha midahalo kama hii tuangalie but uhakikishe una bible inayokubaliwa na wakristo na qur`an iliyotafsiriwa na inayokubalika na waislam. nadhani hapo tutajifunza pia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shalom ndugu. Asante pia kwa ushauri wako. Lakini maoni yangu ni kwamba, ukienda kwa ustaadhi utaishia kwenye haya tunayoyaona leo duniani kote. Bwana Yesu alisema kwamba "Mti unajulikana kwa matunda yake." Matunda ya uislamu yako wazi duniani kote.

      Ukizungumza na huyo unayemwita 'ustaadhi anayejua', atakwambia kuwa uislamu ni dini ya amani. Lakini ukishaingia tu, ni marufuku kutoka; na ukitoka, huyo ustaadhi ndiye atakayekata kichwa chako.

      Ndugu, ni vema ukasoma mwenyewe utaujua ukweli kuliko kutegemea mtu akuambie kile kilichomo ndani ya uislamu. HAKIKA KABISA HAWATAKWAMBIA HATA CHEMBE YA HICHO KILICHOMO HUMO!! Matunda ya mti wa uislamu yanaongea zaidi kuliko maneno ya hao "maustaadhi wanaojua"

      Bwana Yesu akubariki.

      Delete
  25. amani !!!!! amani!!! uislamu huu huu au mwingine? kama ni huu ambao allah wao anapenda kuchinjiwa wakristo, amani hiyo itapatikana baada ya kuchinjiwa wakristo na wayahudi wote. hata hivyo bado hatatosheka na damu zao atahitaji damu ya waislamu wasio waaminifu kwake.akiwamaliza hao huenda hiyo amani itaeleweka.

    utasikia eti mtume katika vita vyoote alivyoviratibu hakuua hata mtu mmoja kwa mkono wake!!!! Mubarak alimuua nani kwa mkono wake, mbona kashtakiwa kwa muuhaji, mursi alimuua nani kwa mkono wake mbona kashtakiwa kwa mauaji,rais wa siria kamuua nani kwa mkono wake mbona analaumiwa kwa mauaji. mtume wenu aratibu na kuongoza vita vilivyoua watu ataponea wapi kuitwa muuaji na ingekuwa bado anaishi angeishi gerezani.

    ReplyDelete
  26. Asanteni sana WAUMINI kwa mjadala mzuri.
    Kwa kweli nahitaji kuingia name katika mjadala huu ili kupata elimu ya dini nikiamini kwamba binaadam sote ni wadhaifu na tunalazimika kupita njia sahihi ili kuutafuta ukweli.
    Kabla ya kwenda kwenye kitabu Kitakatifu cha QUR-AN, naomba niulize waumini hapa mswali yangu kutoka kitabu kitakatifu cha BIBLIA.
    Niliposoma Marko 11:12-14 nimepata wasiwasi kidogo kuhusu bwana Yesu. Jee alipokua anauendea huo mti kupata matunda alikua yeye kama BINADAM au MUNGU kwa wakati huo? kama alikua kama MUNGU, kwanini hakujua kwamba sio msimu wa matunda? kama alikua kama binadam kwa wakati huo MUNGU alikua wapi? au nani? ASANTENI SANA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shalom rafiki mpendwa. Asante sana kwa maoni yako na maswali yako kuhusiana na Marko 11:12-14.

      Swali lako tunaweza kulifananisha na mwalimu anavyofundisha darasani. Tuseme mwalimu anafundisha wanafunzi wa darasa la kwanza. Halafu akasema: machungwa mawili ongeza machungwa matatu tunapata machungwa mangapi?

      Sasa je, ni sahihi kwetu kuanza kusema: "Ina maana mwalimu mzima ambaye amemaliza elimu ya sekondari na elimu ya chuo hajui jibu la swali hilo hadi anauliza watoto wadogo kama hawa?"

      Bila shaka hatuwezi kujiuliza swali kama hilo? Kwa nini? Kwa sababu tuna UHAKIKA kwamba mwalimu aliuliza kwa lengo la kuwafundisha wanafunzi wake - yaani alifanya hivyo kwa faida ya wanafunzi si kwa faida yake, au sio?

      Yesu hakutoka mbinguni kuja kutafuta tini duniani. Wala hakuja kutafuta mikate au zabibu au nyama, n.k. Yote aliyofanya Yesu hapa duniani ilikuwa ni kwa faida yangu, yako na ya wanadamu wote. ALIKUJA KUTONYESHA JINSI MUNGU ALIVYO, ANAVYOTUWAZIA, ANACHOTEGEMEA KUTOKA KWETU NA ALICHO TAYARI KUFANYA KWA AJILI YETU.

      Ni kweli Yesu alijua kuwa mtini haukuwa na matunda lakini alikuwa na lengo la kufundisha somo muhimu sana. Swali lako halina tofauti na kusema hivi: Mungu anajua kuwa tuna shida mbalimbali - magonjwa, kesi, ada za shule, kodi za nyumba, viongozi wabovu, nk, kwa nini asiondoe tu hayo matatizo yote?

      HATAONDOA KAMWE HADI MTU APIGE MAGOTI NA KUOMBA, TENA KWA BIDII NA KWA IMANI.

      Kwa nini? Kwa sababu akifanya kimyakimya, hakuna mtu atakayejua kuwa amefanya. Badala yake kila kitu ambacho Mungu hufanya kimyakimya, wanadamu huita ni 'natural circumstances' au 'natural phenomena'! Je, hii si kashfa kwa Mungu?

      Sasa, hili ndilo somo ambalo Yesu alitaka kufundisha kwetu (si kwake) kupitia mtini:

      “Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka shinani. Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka. Yesu akajibu, akamwambia, MWAMININI MUNGU. AMIN, NAWAAMBIA, YE YOTE ATAKAYEUAMBIA MLIMA HUU, NG'OKA UKATUPWE BAHARINI, WALA ASIONE SHAKA MOYONI MWAKE, ILA AAMINI KWAMBA HAYO ASEMAYO YAMETUKIA, YATAKUWA YAKE. KWA SABABU HIYO NAWAAMBIA, YO YOTE MYAOMBAYO MKISALI, AMININI YA KWAMBA MNAYAPOKEA, NAYO YATAKUWA YENU.” (Marko 11:20-24).

      Kwa hiyo mpendwa, Yesu hakuwa anatafuta matunda ya mtini; alikuwa anatafuta kufundisha kanuni ya Imani ambayo ndiyo inayotufanya tupokee haja zetu mbalimbali toka kwa Mungu.
      Ubarikiwe na Yesu.

      Delete
  27. ibura tafadhal ueleze umma kupitia kitabu ktukufu cha kuran kwamba kwanin alikua akitumia wing katika kueleza mambo yake ukitudhbtishia kupitia vfungu vya kuran. swali hili umeulzwa huko juu hutak kulijbu

    ReplyDelete
  28. Waislamu Wanatakiwa wafahamu kuwa Allah ni mungu wa kutengenezwa, Mohamad ni mtume wa kujitakia/kutengenezwa na Islam ni dini ya kikafiri (inapinga ukristo.

    Kuran ina pande mbili, imejaa ulaghai rejea Kuran 9:5
    Bwana James Nitaungana na wewe kufundisha kuhusu Kuran maana kama Ibra haielewi biblia ni vigumu kwake kuielewa kuran. Wakati umefika tutumie Kuran kuwaelimisha waislamu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amen kamanda wa Bwana Yesu. Karibu katika mapambano na ibilisi ambaye haachi kuiba roho za watu wa thamani ambao Bwana aliwaumba. Ufahamu na maarifa ndiyo silaha muhimu kabisa ya kumtoa mtu kwenye kifungo cha uongo. Barikiwa na Bwana.

      Delete
  29. Amani iwe nanyi ndugu! Kaka Ibra wewe umebarikiwa kipawa kikumbwa cha kuueleza ukweli kupitia maandiko. Yaani ni zaidi ya aliyeenda chuo cha biblia. Insaallah Mola akuongezee na naamini kupitia wewe Mungu wangu atawafungulia hao wenye pepo wa kuota ndoto na kuzifanya ndio imani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amani iwe nawe pia ndugu katika jina la Yesu. Kwenye vyuo vya Biblia ndugu yangu huwa hawafundishwi uongo wala upotoshaji. KILA KITU anachoeleza Ibra humu ni uongo na upotoshaji mtupu. Kama kweli wewe ni mpenzi wa KWELI HALISI, basi linganisha hoja za pande zote mbili na kupima, kisha utaiona na kuitambua hiyo KWELI. Mungu wa kweli akubariki.

      Delete
  30. wakristo wote ni vipofu, viziwi na wanabeba imani pasipo kufikilia. Imani sio kufuata wazazi Bali in kufikilia. Embu naomba niambie ni sehemu gani kwenye biblia yes au Mungu amesema kuwa ukristo ni dini? binadamu wrote ni waislamu in nature. Na ndio maana wakristo huwabatiza ili kuwa kafiri. Dini ya yesu sio ukristo Bali ukristo umeanzishwa baada ya yesu kuondoka. na aliyeanzisha ukristo ni paul huko Antokia ambapo kwa kipindi hicho alijulikana kama Saul. Na wanafunzi wa yesu walikuwa wamekufa, paul hakuwahi kuwa mwanafunzi wa yesu kwahiyo mafunzo mengi aliyofundisha ni ya kipagani. Unayesema yesu amelaniwa kwa dhambi zako, hata hufikilii? Usijipe moyo kwa ujinga. Mungu amemuumba binadamu tofauti na viumbe wengine. Umepewa akili ya kujifunza na kufikiria. Yaani yesu alaniwe kwa dhambi za watu! Anayelaaniwa huwa anaenda motoni au peponi? biblia sio muongozo sahihi wa imani yako. Biblia sio kitabu cha Mungu. Vitabu vya Mungu ni Zaburi, torati, injili na Qurani. Vitabu vya Mungu vimeshushwa pamoja na mitume. Je biblia alipewa mtume gani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yesu hakusema Ukristo ni dini maana sisi hatuna haja na dini kama ninyi waislamu, wahindu na wabudha. ninyi ndio watu wa dini. Yesu sio dini bali ni Njia ya kwenda mbinguni.


      Mnajifariji kwamba eti binadamu wote ni waislmu by nature. Sasa kwa nini mtu akija kwenu mnamsilimisha? Kwa nini umsilimishe wakati ni muislamu tayari?


      Paulo hakuwahi kuwa mwanafunzi wa Yesu? Hiyo ni kwa mujibu wa Biblia au quran? Bwana Yesu alipokuwa anaondoka alisema: Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote KUWA WANAFUNZI, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu (Mathayo 28:19). Je, hapo alimaanisha nini? Je, alimaanisha wapelekwe mbinguni aliko ili wakawe wanafunzi wake huko?


      Paulo hakuanzisha Ukristo kama mnavyojidanganya. Andiko unalojaribu kuhangaika nalo linasema:
      hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. NA WANAFUNZI WALIITWA WAKRISTO KWANZA HAPO ANTIOKIA. (Matendo 11:26). Ni jina ndilo lililoanzia Antiokia. Hawa walikuwa ni wanafunzi wa Yesu tayari. Walikuwa tayari wakiyaishi mafundisho ya Yesu. Ukristo haukuanzia Antiokia. Huo ni uongo wa ibilisi.


      Kama Yesu hakulaaniwa kwa ajili ya dhambi za watu, kwa nini katika torati Wayahudi walipotenda dhambi walipeleka wanyama hekaluni ambao waliuawa na damu yao kumwagwa kwa ajili ya dhambi zao?


      Imendikwa: Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; NAMI NIMEWAPA NINYI HIYO DAMU JUU YA MADHABAHU, ILI KUFANYA UPATANISHO KWA AJILI YA NAFSI ZENU; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi. (Walawi 17:11). Huu ulikuwa ni unabii wa kifo cha Yesu. Ukikataa damu ya Yesu kwa ajili yako, utakufa na dhambi zako na jehanamu ni sehemu yako ya milele.


      Biblia inasema tuwasamehe maadui zetu na kuwaombea. Quran inasema muwaue na kuwalipiza kisasi maadui zenu. Mwenye akili ya kawaida anaona tu tofauti kipi cha Mungu na kipi si cha Mungu. Kati ya mambo hayo mawili, ni lipi ambalo hata ibilisi anaweza kulitenda? Je, ibilisi anaweza kumsamehe adui yake? au atamlipiza kisasi?

      KALAGA BAHO!!

      Delete
    2. naitwa Rose...ahaaaa...ahaaa.... yaani napenda sana mafundisho yako yananipa moyo na nguvu mimi ambaye ndo ninachipuka kuja huko kwa Jemedari wa vita, bwana wa bwana, mfalme wa wafalme, mwakondoo, Jaji mkuu yaani basi majina ni mengi sana siwezi yamaliza.

      unatoa majibu mazuri sana huku ukiongozwa na roho wa Mungu vizuri ubarikiwe sana maana roho wa Mungu yupo kwa ajiri ya kutuogoza na yote kwa kuwa ndiye tuliyeachiwa mpaka hapo..?!! mwisho wa dahari. @james John

      ntaendelea kusoma ili niwe na imani kuu na siku moja nije niuridhi ufalme ule.. tuohaidiwa AMEN.

      Karibuni ndugu zetu waislamu kwani hamuoni.. ama kweri kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzie ama wote watatumbukia shimoni. unajua hilo ni shimo lipi?? (ni shimo la uharibifu ndo maana yake) hayo ni maneno ya Yesu mwenyewe alisema.

      tatizo lingine wenzetu hawaelewi maana kuna mistari mingi Yesu anasema kwa mafumbo sasa wao wanachukulia hivyohivyo lilivyo eg. huo mti. na pia ukichukulia kwenye mathayo kwenye kusulibiwa kwake alitumia sana majibu ya mafumbo wakati akiwa kwenye mateso makali sana ili aniokoe mimi na wewe unayemkataa sasa etc.

      ndugu zangu waislamu na waabudu sanamu na wapagani karibuni mle raha huku. yaani mbinguni ni kugusa tu wewe tu na nafsi yako. ni rahisi ni kumkiri kuwa ndiye bwana na mwokozi wa maisha yako na kubatizwa basi ticket tayari. na hapa ndo mtihani ulipo kukiri... ni ishu sana kwa wenzetu ila najua atawatembelea mmoja baada ya mwingine. maana Yesu ahataki mpotee katika dhambi maana lile ziwa la moto ni kwa ajiri ya shetani na wenzake ambao ni majini na si kwa ajiri ya wanadamu. hivyo anapenda roho zote ziingie mbinguni kwenye nchi aliyoihaidi kuwa anakwenda kutuandalia.

      Delete
    3. Shalom Rose,

      Asante sana kwa maneno yako.Bwana azidi kukubariki na kukupa nguvu ya kusonga mbele katika wokovu huu wa thamani kubwa sana aliotupatia kwa njia ya mauti na damu yake.

      Jina lake liinuliwe daima.

      Barikiwa dada Rose

      Delete
  31. James naomba uthibitisho Wa kua Allah si Mungu ni shetani na Muhammad mfuasi wake

    ReplyDelete
  32. MUNGU NI ROHO, Bila roho mtakatifu kukufunulia, BIBLIA kwako ni NOVEL. Bwana Yesu Asifiwe. These are last days. Repent. Mabishano Mara zote hayatangazi Injili, yanafanya jina la Bwana litukanwe.

    ReplyDelete
  33. kujua allah si mungu ni shetani na mtume wake muhamad ni mfuasi wake. angalia sifa za shetani alafu angalia sifa za mungu.

    ReplyDelete
  34. abubakar shekeu wa boko haram kasema allah kamuagiza kwenye quran awauze wale mabinti aliowateka,mtume wa allag muhamad naye alifanya hivyo.wewe si muhamad wala si allah lakini je unaweza kumteka mtu ,kumlawiti,kumbaka, na kumuuza? naanimi huwezi kwani una hofu ya mungu ndani yako inakwambia ni dhambi kufanya hivyo. kwa msingi huo wewe ni mwema, mwenye huruma na upendo kumshinda allah na mtume wake.kama wewe binadamu unamshinda allah kwa kufanya mema je allah ni nani? shetani .na wajumbe wake ni mapepo,majininbokoharam,isis, alshaabab,muhammad n.k

    ReplyDelete
  35. Waislam kwa nini ni wagumu kuelewa?1.Quran ni kitabu kinachokosoa vitabu vya dini nyingine na yenyewe kujiona iko sawa kwa kila kitu kitu ambacho si kweli ni uongo!
    2:Ndicho kitabu kinachosema hakina shaka na aya zake zipo wazi wazi lakini pia huu ni uongo kwani waislam wengi hawajua maana ya ayah nyingine ndio mana kuna vitabu vya tafsiri.
    3:Waislam hata uwape ushahidi vipi kua qurani ni uongo na fikra za muhamamad tu hawatakubali kwa kua hata kipindi cha mtume kuna watu walimbishia na alikua anawabishia na kusema ukimtii yeye ni sawa umemtii Mungu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndioinakukosoa ili uendane na mafundishoya mungu mfanoyesu hajawahi kuwa mungu waka hatokua mungu. Masanamhayaruhusi ktk ibada hiyo ipo humo humoktk biblia lakini hamuelewiiiiiiiiiiiiiii

      Delete
    2. mchungaji ambae anaeza kukuambia ukweni ni yule ajuae vitabu vyote vinne lakini kama mchungaji wako wa kichochoroni hama hio kanisa uende ingine muulize mchungaji wako niipi njia ya kuenda peponi hio njia anyoijua ni muislamu na mchungaji wa kweli pekee

      Delete
  36. 2:4
    Na ambao wanayaamini yaliyo teremshwa kwako, na yaliyo teremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo.

    2:5

    Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio walio fanikiwa

    Jamani naomba kufahamishwa, maandiko yaliyoteremshwa kabla ya Muhamad ni yapi? Yako wapi?

    ReplyDelete
  37. katika moja wapo ya lugha ya mama yangu inasema usipo muogopa ng'ombe utaambiwa wewe ni ng'ombe.sasa kama nyinyi muna mchungaji na sisi hatuna mchungaji sababu sisi ni wanaadam hatuezi chungwa.wala hatuna tabia ya kujibizana kwasababu ALLAH kesha tuambia wala musikashif dini zingine kwaio sasa tafakari mwanaadam hashindani na anaechungwa anashindana mchungaji kama hujaelewa(we dnt deal with a dog we deal with it master)🗡🗡🗡⚔

    ReplyDelete
  38. Bwana Yesu Kristo Asifiwe milele, ukweli Ni kwamba Hawa waislamu wanahitaji kuombewa Sana.

    ReplyDelete
  39. Allah si mungu wa kweli hajawai sema Hana uwezo wa waislam kuswali kwake ila yeye allah na malaika wanamsalia nabii na Kama anamsalia huyo anamsalia KWA nni (KWA yehova) nani mkubwa allah na muhamad Quran 33:56 Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu

    ReplyDelete
  40. Qurani 2:2 kitabu kisicho na Shaka ndani yake Mimi naona nikitabu Cha kukopi KWA biblia ili ujue mwandishi wa Quran anajichanganya swali mwislam wa kwanza wa uislam kusilim alikuwa nani
    *Ibrahim
    *Musa
    *Adam
    *Yesu
    Au nani

    ReplyDelete
  41. Qurani 2:2 kitabu kisicho na Shaka ndani yake Mimi naona nikitabu Cha kukopi KWA biblia ili ujue mwandishi wa Quran anajichanganya swali mwislam wa kwanza wa uislam kusilim alikuwa nani
    *Ibrahim
    *Musa
    *Adam
    *Yesu
    Au nani
    Quran 6:163 - Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu.
    *Quran 6:14
    *Quran39:11-12
    Quran.2:132 - Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu,
    wanyenyekevu.
    ***3:52 - Isa alipo hisi kuwa kati yao pana ukafiri alisema: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wake wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu.
    ****Haya Ni mashaka makubwa muhamadi Ni wakwanza wa uislam kusilim anawezaje kumtaja Ibrahim isa nawengine waliopita inaonyesha uongo

    ReplyDelete