Thursday, October 19, 2017

Mafarisayo na wayahudi walishika sharia (Torati)


 

Yesu alipokuja, Wayahudi – wakiwamo Mafarisayo, Masadukayo na watu wa kawaida – waliamini torati, kwa mfano jino kw ajino, jicho kwa jicho, kupiga mawe wazinzi, nk, kama ambavyo Waislamu wanaamini leo.

Lakini cha ajabu, Yesu (ambaye waislamu wanadai wanafuata aliyofuata na kwamba alikuwa mwislamu kama wao) alisema hivi kuhusu maandiko:

Mwayachunguza maandiko, kwa sababu MNADHANI kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. (Yoh 5:39).


Sijui kama umemwelewa vizuri.
Yaani anasema, Ninyi washika torati, mnasoooooma maandiko kwenye vitabu hivi vya Mungu, halafu MNADHANI kwa kusoma na kushika huko eti ndio mtapata uzima.

He! Sasa kosa liko wapi Bwana Yesu?

Anafafanua kwamba, kosa lenu hamjatambua kuwa Maandiko hayo hayahusu jino kwa jino, kupiga mawe, kutawadha, nk, BALI YANANIHUSU MIMI.

Aya ya 40 anasema: Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima.

Yaani maana yake ni kuwa, mnasoma maandiko halafu mnaenda kupiga watu mawe, mnakalia kutawadha, kwa kuwa HAMUELEWI maana yake. Mngekuwa mnaelewa, baada ya kuyasoma hayo yote, MNGEKUJA KWANGU ili mpate uzima.

Kwa hiyo, Torati yote (au kwa lugha nyingine Agano la Kale lote) haliongelei kutawadha, kupiga mawe, kukata mikono wezi, nk BALI LINAMWONGELEA YESU.

Unaposoma humo mambo kama vile:

- kunawa kwa maji
- kuchinja kondoo au mbuzi
- kupigana vita
- masuala ya wafalme
- masuala ya makuhani
nk, nk, nk.

Yooote hayo NI ALAMA zinazomhusu YESU KRISTO; ndio maana akasema: NA HAYO NDIYO YANAYONISHUHUDIA. (Yoh 5:39).

Kama unasoma na humuoni Yesu ujue umeshapotea.

Uamuzi ni wako.
Uzima umo ndani ya Yesu.
Ukiukataa, hasara yake utaibeba peke yako.
Tafakari.
Chukua hatua.

No comments:

Post a Comment