Ulimwengu wa Kiislamu,
kama kawaida yake, unatia juhudi kubwa sana katika kuuchafua Ukristo ili
angalau uweze kuendelea kuwashikilia walio ndani yake; na pale inapowezekana,
kuwadanganya Wakristo wasiojua Ukristo wala Uislamu.
Kuna mambo mawili makubwa
ambayo huwa yananishangaza sana kuhusiana na masuala ya kiroho. Kwanza ni jinsi
ambavyo wakuu wa dini wa Kanisa Katoliki wanavyotumia miaka na miaka kusomea
dini na Biblia, kisha wanakuja kuishia kufundisha mambo yaliyo nje ya Biblia!!!
Kwa mfano, wanawaambia waumini wao kuwa wafu wanatuombea kule mbinguni au
kwamba unaweza kufanya misa huku duniani halafu ndugu yako aliyekufa akiwa na
dhambi na, kwa ridhaa yake alikataa wokovu, eti atasamehewa dhambi na Mungu
atamuingiza mbinguni!!!
Jambo la pili
linalonishangaza sana ni kitendo cha Uislamu na Waislamu kutumia uongo kwa juhudi kubwa sana ili
kutetea dini yao na kuwafanya waumini wao waendelee kubakia kwenye Uislamu.
Kama dini yenyewe haiwezi kujitetea kwa njia ya neno inalolihubiri, bali inabidi uisaidie kusimama kwa kutumia uongo, kwa nini basi unaitetea? Na kwa nini hasa unaiamini?
Siwashangai wale wasioelewa, lakini nawashangaa wale wanaojua kuwa, “Hapa ninasema uongo ili kumtetea Allah!” Yaani, wanafanya makusudi kusema uongo kwa lengo la kumtetea Mungu ambaye tunatarajia na tunaamini kuwa ana uwezo wote!!!!
Kama dini yenyewe haiwezi kujitetea kwa njia ya neno inalolihubiri, bali inabidi uisaidie kusimama kwa kutumia uongo, kwa nini basi unaitetea? Na kwa nini hasa unaiamini?
Siwashangai wale wasioelewa, lakini nawashangaa wale wanaojua kuwa, “Hapa ninasema uongo ili kumtetea Allah!” Yaani, wanafanya makusudi kusema uongo kwa lengo la kumtetea Mungu ambaye tunatarajia na tunaamini kuwa ana uwezo wote!!!!
Ama kweli duniani kuna
mambo!!!
Nikirudi sasa kwenye mada
ya leo, mojawapo ya silaha za uongo inayotumiwa
na Waislamu kwa lengo la kuinua dini yao ni kusambaza na kuhubiri kile
kinachojulikana kama “Injili ya Barnaba.”
Injili
ya Barnaba ni nini?
Hiki ni kitabu
kikubwa (karibu sawa na injili zote nne za Biblia zikijumuishwa pamoja - maana kina sura 222). Kitabu hili kinaeleza maisha ya Yesu na kudai kwamba kimeandikwa na mmoja wa mitume wa
Yesu aliyeitwa Barnaba.
Nakala za zamani kabisa za kitabu hiki ambazo zinajulikana ni mbili – moja kwa Kiitaliano na nyingine kwa Kihispania. Zote zinaonyesha kuwa ziliandikwa kwenye karne ya 15 au 16 baada ya Kristo.
Nakala za zamani kabisa za kitabu hiki ambazo zinajulikana ni mbili – moja kwa Kiitaliano na nyingine kwa Kihispania. Zote zinaonyesha kuwa ziliandikwa kwenye karne ya 15 au 16 baada ya Kristo.
Kwa
nini injili ya Barnaba ni ya bandia?
Unaposoma injili hii,
unagundua kuwa ni ‘forgery’ au ni ya bandia kutokana na sababu mbalimbali. Baadhi ya
sababu ziko wazi lakini zingine zinahitaji jicho la karibu zaidi ili kuzitambua.
Zifuatazo ni baadhi ya sababu hizo:
Zifuatazo ni baadhi ya sababu hizo:
1. Mwanzoni
tu mwa injili hii, Yesu anaitwa ‘Kristo’ (Christ). Imeandikwa: “Dearly beloved the great
and wonderful God hath during these past days visited us by his prophet Jesus Christ …” Lakini unavyoendelea kusoma unakuta
kwamba Yesu anakataa kwamba yeye si ‘Masihi’. Kwa mfano, katika sura ya 42
imaendikwa: Jesus confessed, and said the truth: "I am not the
Messiah."
Neno
‘Kristo’ (Christ) ni tafsiri ya Kigiriki ya neno
la Kiebrania ‘masihi’ (Messiah). Kwa hiyo, Kristo na Masihi ni neno lilelile. Licha ya
hivyo, katika maisha yao yote, Wayahudi walikuwa wakimtarajia Masihi. Hivyo,
hili lisingekuwa ni neno geni kwao kiasi cha kumfanya mwandishi ashindwe kulielewa.
Mbali na hayo, Barnaba halisi anayejulikana kwenye Biblia aliishi kwenye kisiwa cha Kipro (Cyprus) ambako wenyeji wake walizungumza Kigiriki. Na Barnaba mwenyewe alikuwa ni Mwebrania. Kwa hiyo, asingeweza kamwe kushindwa kuelewa kuwa maneno haya yanabeba maana ileile katika lugha mbili tofauti ambazo alizizungumza zote.
Mbali na hayo, Barnaba halisi anayejulikana kwenye Biblia aliishi kwenye kisiwa cha Kipro (Cyprus) ambako wenyeji wake walizungumza Kigiriki. Na Barnaba mwenyewe alikuwa ni Mwebrania. Kwa hiyo, asingeweza kamwe kushindwa kuelewa kuwa maneno haya yanabeba maana ileile katika lugha mbili tofauti ambazo alizizungumza zote.
Kwa
hiyo, huu ni ushahidi kwamba mwandishi wa Injili ya Barnaba ni mtu ambaye
hakujua Kigiriki ndiyo maana mwanzoni tu mwa injili yake hii anamwita Yesu ni Christ, ilhali ndani anamfanya Yesu aseme kuwa yeye si Messiah!
2. Quran
inasema kwamba Yesu ni Masihi. (Tazama Sura 3:45). Na Biblia nayo inasema kuwa
Yesu ni Masihi. Kama wewe Mwislamu unaamini kuwa Quran ni kitabu cha kweli; na
kwamba kile inachokisema ni kweli, iweje basi uamini injili ya Barnaba
inayosema kuwa Yesu si Masihi na usiamini Biblia inayosema kuwa Yesu ni Masihi
kama ambavyo Quran yako inasema?
3. Katika
sura ya 3, ‘barnaba’ huyu anatuambia kuwa Herode na Pilato walitawala Yudea
wakati Yesu alipozaliwa. There reigned at that time in Judaea Herod, by decree
of Caesar Augustus, and Pilate was governor in the priesthood of Annas and
Caiaphas. Wherefore, by decree of Augustus, all the world was enrolled;
wherefore each one went to his own country, and they presented themselves by
their own tribes to be enrolled. Joseph accordingly departed from Nazareth, a
city of Galilee, with Mary his wife, great with child, to go to Bethlehem (for
that it was his city, he being of the lineage of David), in order that he might
be enrolled according to the decree of Caesar…….. While Joseph abode there the
days were fulfilled for Mary to bring forth.
Herode
alitawala Israeli kati ya mwaka 37-4 kabla ya Kristo. Unaweza kusoma HAPA au
kwingineko kokote. Lakini Pilato alitawala miaka zaidi ya ishirini baadaye, yaani
kati ya 26-36 baada ya Kristo. Unaweza kusoma HAPA. Sasa, kwa kuwa Barnaba
aliishi pamoja na Yesu, wakati ambapo Pilato alikuwa mtawala, inawezekanaje
akafanya kosa lililo wazi kama hili? Hili ni kosa linaloweza tu kufanywa na
mwandishi ambaye hakuishi nyakati za Yesu au nyakati za Pilato.
4. Katika
sura ya 20 tunaambiwa na ‘barnaba’ kwamba Yesu alisafiri baharini kutoka
Galilaya hadi Nazareti. Imeandikwa: Jesus went to the sea of Galilee, and
having embarked in a ship sailed to his city of Nazareth. Hebu tafuta Nazarethi
kwenye ramani HAPA, kisha uangalie kama mtu anaweza kusafiri kwa chombo cha
majini kutoka kwenye Bahari ya Galilaya hadi Nazarethi.
Nazarethi
iko kilometa takriban 14 kutoka Bahari ya Galilaya. Ni mtume gani wa Yesu
angeweza kusema jambo kama hili – ukichukulia kwamba Yesu na mitume wake
walikuwa wakitembea sana kwenye maeneo haya? Hii inaonyesha tu kwamba mwandishi
wa injili ya Barnaba hajui jiografia ya Nazarethi au Galilaya.
5. Yehova
aliagiza kwenye Biblia kwamba watu washerehekee mwaka wa Yubile kila baada ya
miaka 50. Imeandikwa: Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa
mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile. Mwaka huo
wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho
kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa (Walawi
25:10-11).
Mwaka
1300 B.K, papa Boniface VIII alitangaza kimakosa kuwa Wakristo wanatakiwa
washerehekee siku hiyo kila baada ya miaka 100. Lakini, mwaka 1350 B.K, papa
aliyefuata, yaani Clement VI, alirudisha utaratibu wa kawaida wa kusherehekea
yubile kila baada ya miaka 50. Kwa hiyo, kwa kipindi cha miaka 50, yaani
kuanzia 1300 hadi 1350, watu walikuwa wakijua kwamba yubile inasherehekewa kila
baada ya miaka 100. Soma HAPA.
Na
huyu mwandishi wa Injili ya Barnaba kwenye sura ya 82, anamwekea Yesu maneno
mdomoni kwamba eti alisema: “insomuch that the year of jubilee, which now comes
every hundred years, shall by the Messiah be reduced to every year in every
place."
Hivi, kama ukiona sinema ambayo mtu anakwambia hii ni ya mwaka 1910, na inaonyesha watu wamevaa mavazi ya zamani na nyumba ni za zamani, lakini humo ndani kwa nyuma ukaona bendera ya taifa la Tanzania inapepea utawaza nini?
Hivi, kama ukiona sinema ambayo mtu anakwambia hii ni ya mwaka 1910, na inaonyesha watu wamevaa mavazi ya zamani na nyumba ni za zamani, lakini humo ndani kwa nyuma ukaona bendera ya taifa la Tanzania inapepea utawaza nini?
Kihistoria
inajulikana kabisa kwamba bendera hiyo haikuwapo mwaka 1910. Maana ya kuwapo
kwake kwenye sinema hiyo ni moja tu – kwamba hiyo ni sinema ya uongo!
Sasa,
suala la yubile ya kila miaka 100, kwa mara ya kwanza, lilikuja mwaka 1300. Halafu
waislamu mnataka kuwaambia watu kuwa injili ya Barnaba iliandikwa na mtume
aliyeishi na Yesu kwenye karne ya Kwanza, yaani miaka 1300 kabla ya jambo hili
linalohusiana na yubile ya kila miaka 100 kutokea. Au huyu mheshimiwa 'barnaba' alikuwa anaongea kinabii?
Kwa
msomaji unayependa KWELI, hili linakuonyesha kitu gani? Bila shaka jibu liko
wazi kwamba mwandishi wa injili hii aliishii baada ya mwaka 1300. Amka!!!
Barnaba
wa karne ya 1 asingeweza kamwe kuandika au kusema jambo kama hili; na zaidi ya
yote Yesu…?!
6. Katika
sura ya 178, injili ya Barnaba inatuambia kuwa ili ufike paradiso ni lazima
uvuke mbingu 9. Ikimaanisha kuwa, paradiso ni ya kumi. Imeandikwa: Truly I say
to you that the heavens are nine, ……. And truly I say to you that paradise is
greater than all the earth and all the heavens together.
Katika
karne ya 14 kule Italia kulikuwa na mshairi maarufu aliyeitwa Dante Alighieri. Katika
mojawapo ya vitabu vyake, Dante anazungumzia jambo hilihili. Yaani anasema kuwa
ili kufika paradiso unatakiwa kuvuka mbingu tisa!!! Unaweza kusoma HAPA.
Na
inajulikana, kama nilivyosema mwanzo wa makala haya kuwa, nakala za zamani
kabisa zinazojulikana za injili ya Barnaba ni mbili – moja ya Kiitaliano na
nyingine ya Kihispania. Na hizi zinajulikana kuwa ni za kwenye takriban karne
ileile ya Dante. Waswahili wanasema, mwenye macho haambiwi tazama!!
7. Sura
ya 193 ya Injili ya Barnaba inaongelea juu ya kifo cha Lazaro ambaye
alifufuliwa na Yesu. Kisha Yesu anasema kuwa saa yake (ya kufa) ikifika naye
atalala vilevile kama Lazaro na atafufuliwa mara moja. Imeandikwa: 'My hour is
not yet come; but when it shall come I shall sleep in like manner, and shall be
speedily awakened.'
Lakini
unapofika kwenye sura ya 216 na 217, wakati ambapo Yesu amekamatwa ili auawe, tunaambiwa
kuwa Mungu alimwondoa kimiujiza (kama Quran inavyosema) na badala yake mungu huyu (anayeonekana kuwa ni mwongo) akamvika Yuda sura ya Yesu na Yuda akauawa kwa kuwa watu waliomjia Yesu
walidhani kuwa Yuda ndiye Yesu.
Swali
ni kuwa, je, si Yesu katika sura ya 193 ndiye aliyesema kwamba angekufa na
kufufuliwa? Mbona basi Mungu anamkimbiza na kumficha badala ya kutimiza lile
ambalo Yesu alilisema?
Mwenye
macho haambiwi tazama!!
8. Sura
ya 54 inasema kuwa mafarisayo walikuwapo wakati wa nabii Eliya. Lakini historia
inaonyesha kuwa Mafarisayo walitokea kuanzia karne ya pili kabla ya Kristo. Soma
HAPA au kwingineko.
Lakini
nabii Eliya aliishi kwenye karne ya 9 kabla ya Kristo. Soma HAPA. Hiyo ina
maana kuwa aliishi takriban karne 7 kabla mafarisayo hawajatoke. Sasa iweje
huyu barnaba atuambie kuwa mafarisayo walikuwapo nyakati za Eliya?
9. Sura
ya 80 inatumbia kwamba Danieli alichukuliwa na Nebukadreza kupelekwa Babeli
akiwa na miaka miwili. Imeandikwa: Daniel as a child, with Ananias, Azarias,
and Misael, were taken captive by Nebuchadnezzar in such wise that they were
but two years old when they were taken; and they were nurtured among the
multitude of idolatrous servants.
Unaposoma
Biblia inatuambia kwamba: Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake
Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake
ukamwacha. (Dan. 2:1).
Matokeo
yake Nebukadreza alitaka waganga na wataalamu wa kutafsiri ndoto wamwambie
maana ya ndoto ile. Kila mmoja alishindwa lakini Danieli alitafsiri ndoto ile
baada ya kumwomba Yehova.
Matokeo
yake, Biblia inasema: Ndipo Nebukadreza, mfalme, akaanguka kifudifudi,
akamsujudia Danieli, akatoa amri wamtolee Danieli sadaka na uvumba. Mfalme
akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana
wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii. Basi
mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa
mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye
hekima wa Babeli. (Dan. 2:46-48).
Sasa,
Nebukadreza aliota ndoto hii akiwa katika mwaka wa pili wa kutawala kwake. Kama
alimchukua Danieli kutoka Israeli katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake,
hiyo ina maana kwamba, Danieli alitafsiri ndoto ile akiwa na miaka mitatu; na
pia alifanywa kuwa liwali (mbunge) akiwa na miaka hiyohiyo mitatu!
10.
Jambo
jingine ambalo ni kichekesho kikubwa kuhusiana na hii injili ya Barnaba ni kuwa
Yesu hakuwahi kuwa na mtume aliyeitwa Barnaba. Mitume wa Yesu wanajulikana. Unaweza
kusoma Mathayo 10:2-4; Luka 6:13-14.
Sasa, Barnaba ni nani?
Huyu alikuwa ni mwanafunzi aliyemwamini Yesu baadaye wakati Yesu tayari alishafufuka na kupaa kurudi mbinguni. Wakati mitume alioacha Yesu walipohubiri injili ya Yesu, mmoja wa watu waliosikia na kuiamini na kuokolewa alikuwa ni Yusufu (Joseph), mwenyeji wa Kipro (Cyprus).
Huyu alikuwa ni mwanafunzi aliyemwamini Yesu baadaye wakati Yesu tayari alishafufuka na kupaa kurudi mbinguni. Wakati mitume alioacha Yesu walipohubiri injili ya Yesu, mmoja wa watu waliosikia na kuiamini na kuokolewa alikuwa ni Yusufu (Joseph), mwenyeji wa Kipro (Cyprus).
Huyu aliuza shamba lake akaleta fedha kwa
mitume ili wenye uhitaji waweze kugawiwa. Mitume walimpa jina la Barnaba likiwa
na maana ya ‘mwana wa faraja.’
Imeandikwa: Na mitume wakatoa ushuhuda wa
kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. Wala
hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote
waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile
vilivyouzwa, wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya
alivyohitaji. Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa
faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro, alikuwa na shamba akaliuza,
akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume. (Matendo ya Mitume 4:33-37).
Kwa hiyo, Barnaba hakuwa mmoja wa mitume wa
Yesu!
Je, unadhani baada ya
ushahidi huu kidogo (maana upo zaidi) bado utashikilia kuwa Injili ya Barnaba
ni ya kweli? Unafikiri ni nani aliiandika? Kama umewahi kuisoma injili hii, ni kitu
gani kitakachokufanya upinge hoja kwamba injili hii iliandikwa na mwislamu
aliyeishi Italia katika karne ya 14, 15 au 16 ambaye alikuwa anajaribu
kumhalalisha Muhammad kama ambavyo ninyi Waislamu mmeendelea kufanya hadi hivi leo – maana injili yenyewe 'inamfagilia' Muhammad?
Waswahili husema: Mwenye
macho haambiwi tazama na pia sikio la kufa halisikii dawa. Je, wewe ni mwenye
macho au ni sikio la kufa?
Jiponye
mwenyewe.
Utadanganywa
hadi lini?
Tafakari.
Hoji
mambo.
Chukua
hatua.
ok pole kwa kuumiza kichwa ili kupata ukweli wa mambo magumu kama haya
ReplyDeleteamina. tuendelee kupeleka Keli ya Kristo ili watu watoke gizani
Deleterudi tena mafunzoni.... nahisi unajaribu kufumba macho kukwepa kuona ukweli. lakini kama wataka kujua ukweli isome qur ani vizuri soma injili ya barnaba soma na biblia..
DeleteNakala ya Injili ya miaka 1500 iliyopita na ambayo imepatikana tena katika kanisa moja nchini Uturuki baada ya kupotea kwa muda wa miaka 12, ina utabiri wa kuja Mtume wa Uislamu, Nabii Muhammad SAW baada ya Masihi Issa yaani Yesu AS.
DeleteVyombo vya habari vimeripoti kuwa, nakala hiyo ya zamani sana ya Injili imeandikwa kwa lugha ya Kiarami na vyombo vya habari vinasema kuwa, ilikuwa imefichwa kwa muda wa miaka 12.
Tayari viongozi wa Vatican wameonesha hamu kubwa ya kuipata Injili hiyo na Papa Benedict wa 16 ametoa mwito wa kufanyiwa uchunguzi maandishi ya Injili hiyo.
Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni wa Uturuki, Ertuğrul Günay amesema kuwa, bei ya Injili hiyo ni dola milioni 22 za Kimarekani na kwa vile utabiri wa kuja Mtume Muhammad SAW unapatikana kwenye Injili hiyo yenye lugha ya Nabii Issa AS, ilikuwa imefichwa ili watu wasiione.
Amesema maneno yaliyomo kwenye Injili hiyo ya miaka 1500 iliyopita yanafanana sana na maneno ya Qur'ani Tukufu na kiujumla maneno yake yanakaribiana sana na mafundisho ya Uislamu.
Sehemu moja ya maneno yaliyomo kwenye Injili hiyo yanamtaja Yesu kuwa ni mwanadamu na kumnukuu Nabii huyo wa Mwenyezi Mungu akisema kuwa, Mtume atakayekuja baada yake anaitwa Muhammad. Sehemu ya maneno ya Injili hiyo ya miaka 1500 iliyopita yana maana isemayo: Kuhani mmoja alimuuliza Masihi Yesu kuhusu mtu atakayekuja kuchukua nafasi yake na Yesu akajibu: "Muhammad (SAW) ndilo jina lake lililobarikiwa, anatoka katika kizazi cha Ismail, baba yangu Mwarabu."
Waziri wa Utamaduni wa Uturuki pia amesema, tayari Papa Benedict wa 16 ametuma maombi rasmi ya kutaka wapatiwe Injili hiyo iliyopatikana kwenye visiwa vya Uturuki vilivyoko kwenye bahari ya Mediterranean. Imeelezwa kuwa watu waliopatikana na Injili hiyo walikuwa wana nia ya kuiuza kimagendo na hivi sasa wanashikiliwa katika mahakama za Uturuki.
Wakati huo huo kasisi Ihsan Uzbek, mmoja wa viongozi waandamizi wa Kikristo nchini Urutuki amesema kuwa Injili hiyo ni ya zama za mtakatifu Barnaba aliyeishi na Nabii Issa na ambaye alikuwa mfuasi wake wa karibu.
Huko nchini Uturuki nako kumetolewa mwito wa kufanyika uchunguzi wa kitaalamu wa kuweza kujua tarehe hasa ilipoandikwa Injili hiyo.
Habari zinazofanana: Uturuki kuonyesha Injili inayotabiri kudhihiri Mtume Muhammad SAW.
Uislamu ni maneno tu hakuna matendo kwa huyo Mungu wake--- MANENO TU NA AHADI HEWA------------- Yesu yuko kazini usiku na mchana na tunaona matendo yake sawasawa na ahadi alizotoa miaka 2000 iliyopita.
DeleteHatuna haja na allah. Hakuna mtume aliyeitwa Barnaba.
Sasa kwa nini wewe unatoa HITIMISHO ilhali unasema hiyo "injili" wanataka kuifanyia uchunguzi? Au tuseme uchunguzi tayari.
Kufanana na quran si tatizo, maana hata "injili" ya barnaba nayo ni quran tupu humo ndani.
ALLAH ANAHANGAIKA!!!!!!!!!!!!!
BARNABA Aliokoka kwa kuhubiriwa na wakina Petro, sasa aje aandike kupinga na kumuweka Muhammad ndani take duu! Changa la macho hili, injli hazitofautiani hata siku moja.
DeleteAhsante sana kuchambua injili hii ya Barnabas ambayo hakika ni kanyaboya kama Quran ilivyokuwa kanyaboya. Uandishi wa Quran hautofautiani na Barnabas. Hii inakueleza tu kuwa aliyeandika Barnabasa alikuwa na elimu ya Quran ila akataka kuihalalisha Quran kwa kuweka imani ya Quran kwenye kitabu hiki akakikiita kitabu cha Kikristo kuwapotosha watu. Waislamu mnapotea na mnapotezwa hivi hivi na watu wanaowalaghai. Huu ulaghai uliotumika kuandika Barnabas hata Quran imetumika tu huo ulaghai kuiandika.
ReplyDeleteamen. ulichosema ndugu ni cha kweli. Biblia haina mtu wa kui-challenge hata kidogo. Hilo ni NENO la Mungu wa kweli.
DeleteNdugu James John
ReplyDeleteUmefanya vyema kuijadili injili feki ya barnaba hapa. Lakini ili usionekane kuwa "asiyemwaminifu" katika Habari ya Uinjilishaji ni vyema kujifunza kwanza jambo kabla hujaliweka ili usionekane mpotoshaji kama nabii wa uongo mohamad.
Kanisa Moja Takatifu Katoliki La Mitume Halifundishi kama Ulivyosema katika nukuu Hii
"Kuna mambo mawili makubwa ambayo huwa yananishangaza sana kuhusiana na masuala ya kiroho. Kwanza ni jinsi ambavyo wakuu wa dini wa Kanisa Katoliki wanavyotumia miaka na miaka kusomea dini na Biblia, kisha wanakuja kuishia kufundisha mambo yaliyo nje ya Biblia!!! Kwa mfano, wanawaambia waumini wao kuwa wafu wanatuombea kule mbinguni au kwamba unaweza kufanya misa huku duniani halafu ndugu yako aliyekufa akiwa na dhambi na, kwa ridhaa yake alikataa wokovu, eti atasamehewa dhambi na Mungu atamuingiza mbinguni!!!
Si kila mfu hutuombea ila WATAKATIFU TU. Mama Bikira Maria, Mtakatifu Stephano, Paulo, Petro, Yuda Thadeus, Baba Mt. Yohane Paul wa Pili na Watakatifu wengineo wengi hawa ndio ambao hutuombea kwani Wapo karibu na Mungu Mkuu. Na hii Ni Neema ya Mungu Kwa wanadamu Wote wenye Mapenzi Mema na Ni Fundisho Lenye Uongozi wa Roho Mtakatifu.
Si Kila mfu huombewa. Kanisa huwaombea wale waliokufa katika hali ya Neema wakiwa na Tumaini La Ufufuko kwa njia ya Yesu Kristu Bwana Wetu. Kama mtu hakufa katika hali ya neema, yaani iwe alikufa katika hali ya dhambi mf. katika ujambazi, kujiua, mafarakano, ulevi n.k huyu hatumuombei kwani amekwisha hukumiwa.
Kanisa Linafundisha watu kujitahidi kuishi kitakatifu kama wafuasi waaminifu wa Yesu Kristu kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu.
Ndugu James Nirudie kukukumbusha Kujifunza kwa bidii kutoka Kwa Wakristu popote Ulimwenguni ili uweze Kuinjilisha katika Uaminifu kwa Bwana wetu Yesu Kristu na kwa Kanisa lake Takatifu.
Wako Katika Umoja wa Yesu Kristu
Innocent Julius
Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo
Kanisa Moja Takatifu katoliki la Mitume.
Kijenge, Arusha, Tanzania
shalom shalom Innocent
DeleteNakushukuru kwa maoni yako ambayo nayaheshimu.
Asante pia kwa angalizo lako.
Ningependa kuanza kujifunza kutoka kwako.
Tafadhali naomba unithibitishie KIMAANDIKO juu ya ukweli wa hayo uliyoyasema yaani watakatifu wanaostahili kuombwa; na wale wabaostahili kuombewa.
Asante na Bwana akubariki.
Shalom Ndugu
DeleteKwanza nitoe angalizo tena.
Mungu Mwenye - Enzi ndiye Mpaji wa Vyote m.f Uzima, Msamaha, Mali n.k. Mahitaji yetu yote Mungu ndiye anayetupatia tumuombapo.
Kwa watakatifu TUNAOMBA WAUNGANE NASI KATIKA SALA NA MAOMBI YETU, yaani WATUOMBEE. Ndiyo Maana Utasikia Mkatoliki anamtaja Mtakatifu Fulani kisha anasema UTUOMBEE.
Kamwe hatuwaombi watakatifu wafu, Kwani tunaamini wote walio Mbinguni wana Uzima Tele zaidi Yetu.Bwana Mungu wetu si wa wafu bali wa walio hai.
Maombi ya Mtu mwenye haki yana nguvu sana Yak 5:16. Hao walioko Mbinguni ni wenye haki kwa sababu kisicho safi hakiwezi kuingia mbinguni Ufunuo 21:27.
Watakatifu Mbinguni ni sehemu ya Mwili wa Kristu hivyo hawatengwi nasi tulio pia sehemu ya Mwili wa Kristu kwa Kifo\Mauti ya kimwili, bali wanatuzunguka kama wingu kubwa la mashahidi Waebrania 12:1
Wanasimama katika Ufalme wa Mungu na kutolea Maombi yetu Kwake Ufunuo 5:8, na kufanya tuwe na utulivu katika kukaza mwendo kuifikia taji.
Washiriki katika Mwili wa Kristu wakiombeana ni jaambo linalompendeza Mungu 1 Tim 2:1-4 na Ndivyo alivyoamrisha katika amri ya mapendo Yohana 15:17.
Watakatifu walio Mbinguni wana Mapendo thabiti, sasa kwa nini wasituombee? Kristu Ni Mzabibu, Nasi tuu Matawi; Kama sisi na watakatifu twaungana naye, basi sote twashikamana kwa pamoja bila kutengwa.
Mtakatifu Paulo Mtume na Shahidi wa Yesu Kristu aliuliza 'je Jicho laweza kuuambia Mkono 'sikuhitaji'?" Hivyo nasi hatuwezi kusema hatuhitaji maombi ya ndugu zetu katika Kristu walio hapa duniani na hata walio mbinguni. Tukijua kuwa Wokovu ni kwa familia ya Mungu/Taifa la Mungu.
Na Kwa kuwa sote tuu taifa la Mungu, Hivyo Ni Vyema kuziombea Roho za Marehemu wetu waliokufa katika Kristu.
Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu Akubariki
Wako Katika Umoja wa Yesu Kristu
Innocent Julius
Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo
Kanisa Moja Takatifu katoliki la Mitume.
Kijenge, Arusha, Tanzania
Amina Innocent. and James. Nimejifunza mengi mno. It was worthy my time. Mungu awabariki.
DeleteInnocent rudi jifungie ndani soma tena Biblia yako,upagani umeingizwa Karoliki,shtuka
ReplyDeletenapenda kujua tofauti ya wakristo na wakristu
ReplyDeleteShalom Klauss
DeleteTofauti ya maana hakuna bali ni namna tu ya utamkaji. Wakatoliki wanapendelea kutumia Kristu na protestants wanapendelea Kristo. Lakini yote yana maana ileile.
Hahahahahahaha. Eti nakala imegunduliwa ilikuwa imepotea miaka 12. Kabla ya miaka12 mbona hatukuisikia. Wanatengeneza ushahidi
ReplyDeleteJames kuwa makini na kitu imani, hivyo usipate shida sana... eleza kwa kiwango chako na kufunuliwa na roho.. kwa nini roho.. James yamekuwepo mafundisho ya ajabu yakutisha yakusikitisha na hata KUCHEKESHA, Biblia inatamka wazi na bila ubishi roho ikishamtoka mtu haina uwezo wa kutubu tena.. Mungu akasema kunatofauti gani ya kufa mnyama na kufa binaadamu maana jinsi afavyo huyu ndivyo afavyo huyu? nani alikwambia Mwanaadamu anapokufa roho yake huenda juu naya mnyama henda chini nani kakwambia? lakini leo ypo mtu mmoja kwa kuchafua tu imani za watu wengine kadai amekwenda kuzimu akamuon Marti Lutha, Kanumba na wengine (kasoro YUDA)eti wnanakula nyama za watu.. ahera kunapikwa akamchukua mwanamuziki maarufu duniani aliyefariki takribani miaka 5 iliyopita akapita pori kwa pori akampeleka mbinguni jamani... LABDA MBINGU YA DSM... si mbingu Yesu aliyoiongelea... Comedian tupu zile picha za horror tulizozoea kuziona zimehamia kwenye mafundisho... inafikia mkuu wa kanisa Katoliki anatamka wazi kisa cha Hawa kula tunda bustani ya edeni ni kisa cha habari bandia BBC nukuu... Injili ya Barnaba ni Propaganda... muombe roho akufunulie.
ReplyDeleteMtakuja jua ukweli siku mkitolewa roho zenu
ReplyDeleteKama watu wanaweza chambua hili tuliweke na hili tusiliweke inamaanisha nini? Kwamba biblia ilichambuliwa kwanza na kuonwa na watu kwamba hili linafaa tuliweke na hili halifai. Kwa ninavyojua mimi maneno ya Mwenyezi Mungu hayapangiwi na mwanadamu. Tuzidi kufanya uchunguzi ili tuweze kuitambua njia iliyonyooka.
ReplyDeleteUmesema neno masihi na kiristo ni kitu kimoja. Sio kweli. Kristo ni jina la yesu.
ReplyDeleteNukuu ktk bibilia, Yule mwanamke akasema "najua kua yuaja masihii aitwae kristo. Kwamantiki hio kristo ni jina la yesu yaaninyesu kristo.
Msipate shida, neno la Mungu linanguvu wala haliitaji kutetewa. Kama kanisa lako au dini yako ina mafundisho potovu haiwezi kuwa na nguvu za Mungu hata kutoa pepo kwa Jina lake Yesu. Mtaishia kutumia akili zenu wenyewe huku mafundisho yenu yaki lenga kuhalalisha tamaa za miili yenu.
ReplyDelete1. Kwa Habari ya kuombea wafu ni uzushi ulioingia kanisani(Luka 16: 19-31) Usipoishi maisha ya kumpendeza Mungu hapa duniani huwezi ingia mbinguni.
2. Kwa waislamu;
Kama tulivyo wakristo, waislamu nao wanadai kumuabudu Mungu wa wayahudi. Lakini Biblia haipingani na kitabu cha wayahudi lia Quran inapingana kwa mambo mengi. Hakuna nabii aliyetumiwa na Mungu akashindwa kuandika au kusoma alichoambiwa na Mungu. Mohamed yatima(mkoresh) aliye lelewa na mjomba wake anapata ajira kwa mwanamke Tajiri Kisha anamuoa na kuanzisha uislamu ambao baadae watu wa mecca walipopingana na uislamu Mohamed anaamua kuhama na kwenda Medina akawateka watu wa Medina na kuwafanya watumwa. Jeshi lake lilipopata nguvu akarudi kuivamia mecca na kuiteka Kisha akaua wayahudi wengi lakini mwanamke myahudi alipika chakula akaweka sumu kulipa kisasi cha mauti ya mume wake na watu wake. Mohamed akala, akaanza kuumwa na mwisho akafa mikononi mwa Aisha binti aliyemuoa akiwa na miaka 9. Soma Quran utajua ukweli wa dini hii ya mpinga kristo.
Kama huelewi kiarabu ingia yutube andika Christian prince, huyu ni muarabu anaichambua Quran kwa kina.