Thursday, March 21, 2013

Aliyekuwa Ustaadhi na Hakimu wa Mahakama ya Sharia Akutana na Injili ya Yesu Kristo na Kuokoka – Sehemu ya 2



Ahmed alikuwa ni injinia. Baadaye alishawishiwa na Ulama mmoja na kupandikiziwa chuki dhidi ya Wakristo na Wayahudi kiasi kwamba aliamua kuacha kazi yake na kwenda kusomea masomo ya dini ya Kiislamu (licha ya mama yake kupinga sana).

Masomo hayo yalimwezesha kuwa hakimu wa mahakama ya sharia. Kutokana na ukandamizaji mkubwa aliouona kwenye mahakama hizo na kukosekana kwa haki na pia kukosekana kwa msimamo juu ya tafsiri sahihi ya sheria za kiislamu, moyo wake ulikosa kabisa amani.

Kwa neema za Yesu Kristo, Ahmed alifunguliwa macho yake na sasa anajiuliza ilikuwaje akaamini Uislamu?

Ufuatao ni ushuhuda wake kwa maneno yake mwenyewe ambao ameupa kichwa cha habari: “Njia ya Allah Kuelekea Jehanamu au Njia ya Yesu Kuelekea Mbinguni.”

Kwa kuwa hii ni sehemu ya 2, ili kupata picha kamili, tafadhali anza na Sehemu ya 1 HAPA.

*********************

Njia ya Allah Kuelekea Jehanamu au Njia ya
Yesu Kuelekea Mbinguni

Hadithi ya Kweli

Mafunzo yangu ya uhandisi yalinipa uwezo wa kuchambua jambo mojamoja.  Mtume Muhammad hakuwa na unabii wowote kabla yake, lakini Yesu Kristo alikuwa nao. Allah hakuwahi kuzungumza moja kwa moja na nabii Muhammad (isipokuwa kwa kupitia malaika). Lakini Yesu Kristo alizungumza naye na alikuwa Mwana wa Mungu. Moja ya adhabu alizotoa Mtume Muhammad kwa mwizi ilikuwa ni kunyofoa macho ya mtu huyo (kulingana na Hadith za Bukhari), ambapo Kristo Yesu hakuwa na kingine zaidi ya msamaha na upendo kwa mtu yoyote. Wanawake katika Biblia hawalaumiwa kwa maovu yote katika ulimwengu huu kama ilivyo katika Uislamu, na wao na wanaume wanaangaliwa kwa usawa katika Ukristo. Allah alionekana yuko mbali sana, ilhali Yesu Kristo alionekana yuko karibu sana. 


Katika Sura 3.7 ya Qur'ani, Allah anasema kuwa ni yeye tu ndiye anayeweza kutafsiri Quran vizuri. (Kwa mujibu wa Hadithi, ni aya takribani 700 tu kati ya aya zaidi ya 6,000 za Quran ndizo zinazoeleweka kwa mwanadamu – yaani ni chini ya 12%). Basi ni kwa nini Allah alitupatia Quran hiyo ambayo hakuna mtu anayeweza kuitafsiri sawasawa? Je, Qur'an si kwa ajili ya mwanadamu kama ilivyo Biblia? Tofauti na Biblia, aya nyingi za Qur'ani zinatafsirika kwa namna nyingi (open ended), hivyo zinafanya kuwepo na kubuni kwingi.  (Hata kwa Mwarabu, haiwezi kueleweka wazi, kwa sababu imeandikwa kwa Kiarabu cha zamani - ni kama kwa Mwingereza wa sasa kujaribu kuelewa Kiingereza cha zamani au Kiingereza cha wakati wa Shakespeare).

Wanaakiolojia hawawezi kufanya kazi zao kwa kutegemea Qur'an, maana ndani yake hakuna historia yoyote au jiografia. Ni aya tu kuhusu yale ambayo Allah anatarajia kutoka kwa mwanadamu pamoja na adhabu kwa asiyefanya mambo hayo, n.k. Lakini Biblia imejaa simulizi kuhusiana na wanadamu, na hata leo, nasikia, wanaakiolojia hufanya kazi zao kwa kusoma kwanza majina ya sehemu na matukio yanayotajwa kwenye Biblia.

Mtume Muhammad hakuwa amesoma, ambapo Yesu Kristo alikuwa mwalimu akielimisha wengine. Mtume Muhammad alikuwa na wake 12, masuria wengi, wake wengi wa muda na watumwa wa kike wengi (aliowapata kwa kuwakata vichwa waume zao), na mmoja wa wake zake (Aisha) alikuwa na umri wa miaka 8 tu wakati yeye alipokuwa na miaka 52. (Baada ya yeye kulishwa sumu, kwa mujibu wa Hadith ya Bukhari, alikufa akiwa mikononi mwa mke huyu, Aisha). Yeye alifanya ngono na mtumwa wa mkewe (nje ya ndoa) na kumwacha mkewe akisikitika. Kwa leo tungemwita mtu kama huyo ‘sex-maniac’, ambapo Yesu Kristo alikuwa mtu safi.

Katika Sura 18.86 ya Qur'an, Allah anasema jua hutuama kwenye dimbwi la maji machafu duniani. Kama Mwenyezi Mungu ni muumba, ni jinsi gani Mwenyezi Mungu huyo afanye makosa ya namna hii? Je, si Mwenyezi Mungu ndiye aliyetakiwa kujua kuwa dunia ni duara na kwamba jua halizami ndani ya bwawa la maji machafu duniani kila siku? Labda kama Allah si Mungu na Qur'an si kutoka kwa Mungu. Katika Quran, Sura 2.106 na 16.101, Allah anasema kuwa alirekebisha aya katika Qur'ani na kutangua au kubatilisha aya zingine ili kuweka zilizo bora zaidi. Kama Allah ni Mungu, basi hakukuwa na haja ya kubadili kile alichokiandika mwanzo, kwa sababu tangu mwanzo kilitakiwa kiwe kikamilifu. Lakini kuandika upya Quran inaonekana kuwa si Mungu kwangu na Allah ni kama mtu tu, ambaye anafanyia masahihisho kazi yake mwenyewe. (Huyu Allah anaweza kuwa alitumia  'Liquid Paper' nyingi sana). Nani anayeweza kuamini kwamba Allah anahitaji kusahihisha kazi yake mwenyewe? Lakini hiki ndicho hasa anachosema Allah katika Sura hizi za Quran.

Katika Sura 11.114, 17.78-79, 20.130, na 30.17-18 za Qur'an, Allah anasema kila mwislamu analazimika kuomba mara 3 kwa siku. Lakini katika Hadith anasema ni mara 5 kwa siku. Je, Allah asingeweza kuwa na uamuzi mmoja tu? Kwa nini utata namna hii? Kuna utata mwingi, kiasi kwamba mimi sikuweza kuamini, na hivyo ni yule mama mzee wa Kikristo ndiye aliyekuja kunifungua macho na nikaweza kuona makosa haya (blunders). Uislamu sasa ulionekana kama kichekesho kamili kwangu. 

Kwa upande mwingine, Biblia haiagizi kukata watu mkono wa kulia na mguu wa kushoto kwa sababu ya wizi, au kumwua mtu kwa vile ameacha dini yake, au kuua makafiri, [kama Allah ndiye muumba wa mwanadamu, basi kwa nini aagize Waislamu bilioni 1, yaani 1/6 ya watu duniani kuwaua 5/6 ya wanadamu waliobakia. Inaonekana ni kichekesho (ridiculous) kwangu sasa] au kumpiga mawe mzinifu hadi afe, au kujilipua vipandevipande, ili yamkini ukapate raha kule mbinguni kama mfiadini, huku ukiwa na mabikira 70, mito ya ulevi, asali, matunda mapya, n.k.  Inaonekana ni kichekesho, ukatili (barbaric) na machukizo (gruesome). 

Katika Sura 19.71-72 ya Qur'ani, Allah anasema kuwa waislamu wote watakwenda motoni (Mwislamu yeyote unayesoma ushuhuda huu, mwulize ustaadhi wako maana ya Sura 19.71-72). Hiyo ina maana kuwa, yeyote anayefuata njia hii ya Uislamu, hakika atakwenda motoni (labda kama utajilipua vipandevipande kwa bomu kama mfiadini). Huu unaonekana ni ukatili (barbaric) na machukizo (gruesome) kwangu. (Waislamu daima hukosoa Wakristo Watao, Wahindu na Wabudha kwamba wanaabudu sanamu. Lakini katika Hadith za Bhukari, inaelezwa kuwa Mtume Muhammad alisaidia makabila mbalimbali kubadilisha sanamu takriban 30 ndani ya Kaabah kule Makka, baada ya kupanuliwa na kujengwa upya. Baadhi ya sanamu zimevunjikavunjika kutokana na joto kali la miaka mingi. Wao wana ujasiri wa kukosoa dini zingine wakati Waislamu wenyewe huomba na kuabudu sanamu).

Muda ulipita huku nikiwa kwenye hali hii ya utata; na kadiri nilivyozidi kusoma Biblia, ndivyo nilivyozidi kushawishika kwamba hakika hii ndiyo njia sahihi ya kufika kwa Mungu, na kwamba Qur'an haitoki kwa Mungu, au Allah alitengenezwa tu na "this barbarian", Muhammud, na kudai kuwa yeye ni Mtume au ni Shetani mwenyewe akiwa amejificha. Kama Uislamu utampeleka tu mtu kuzimu, basi hii si njia sahihi kwangu. Katika Ukristo, ninalo tumaini la kufikia mbinguni, na sina ulazima wa kwenda Jehanamu. (Kama Uislamu ni mzuri kama unavyosemwa, basi ungeweza kuziunganisha nchi za kiislamu. Lakini, historia yote inaonyesha kuwa  nchi za kiislamu zimekuwa katika vita baina yao). Lakini mimi nahitaji mwongozo sahihi ili kuthibitisha kushawishika kwangu ili niweze kuendelea mbele zaidi.

Siku moja, niliteleza mbele ya duka moja. Mtu mmoja asiyenifahamu, mara moja alinyosha mkono wake na kunishika ili nisianguke. Nilikuja kujua kuwa jina lake ni Maria, Mkristo Mkatoliki. Alikuwa hajaolewa, na ikatokea tu alikuwa mfanyakazi kama karani, katika benki ileile niliyokuwa nakwenda. Niliweza kumweleza hadithi yangu na kumwomba kama anaweza kunisaidia. Yeye alikataa kabisa. Hata hivyo sikuweza kumlaumu, maana nilikuwa nimefuga ndevu nyingi, nimevaa barghashia, na kanzu. Nilionekana ninatisha, hivyo ningeweza kumwogopesha mtu yeyote. Mbali na hivyo, Mkristo atajiingiza kwenye mataizo kama ikijulikana amemsababisha Mwislamu kuacha dini yake.

Siku chache baadaye, nilikutana tena na Maria na tuliongea kwa muda mfupi, na niliweza kuhisi kuwa alianza kuniamini. Baadaye alisema kuwa angenisaidia tu wakati akiwa na muda. Haikuchukua muda mrefu, tulianza kwenda pamoja kweny nyumba ya rafiki yake iliyokuwa imejitenga, mara giza linapoanza na ninakuwa sivai barghashia wala kanzu yangu. Kutoka kwangu na Maria, kwa mara ya kwanza, kulikuwa zaidi ni kwa ajili ya kupata mafunzo na si suala la uhusiano wa kimapenzi. Lakini nilianza kuvutwa naye kadiri muda ulivyopita. Ikawa dhahiri kwangu wakati huu kwamba nisingeweza tena kudanganya kwa ajili ya Allah na Uislamu. Nilijua kuwa sehemu hii ya maisha yangu ndiyo ilikuwa imefika mwisho. 

Baadaye, nilifanya safari nyinginyingi kwenye benki ya Maria, kupeleka hundi zangu, na kuweka fedha. Lakini, ukweli ni kuwa lengo langu lilikuwa kwenda tu kumwona huyu binti mrembo aliyekuwa kwenye miaka ya ishirini hivi.  Kaka zangu na dada yangu walimpenda Maria pale nnilipomleta nyumbani, (lakini wakati baba yangu na mke wake wa pili wanapokuwa hawapo nyumbani). Nilihudhuria pia masomo ya dini na Biblia kwa siri, mara nyingi nikiwa pamoja na Maria. Haikuchukua muda mrefu tukawa tumependana, lakini daima tulikuwa waangalifu mbele za watu. Kaka zangu na dada yangu pia walikuwa na wasiwasi sana kuhusu usalama wangu.

Katika siku ya wapendanao, nilimtumia Maria kifurushi, kikiwa na maua ya waridi, pete na kadi inayosema "Chukua waridi kwa ajili ua uzuri na harufu, lakini pete kwa ajili ya moyo wangu wenye shauku na upendo wangu kwa ajili yako." Siku hiyo, kama ilivyopangwa, nilikwenda kumchukua Maria kwa ajili ya chakula cha jioni. Kwa furaha, Maria aliinua pete yake kunionyesha wakati alipokuwa anaingia kwenye gari langu, na akaninong’oneza sikioni mwangu, "Ndoto huwa zinatimia; lakini sikutarajia kuwa ingekuwa ni kutoka kwa aliyekuwa ofisa wa Kiislamu."

Mimi nami nilimnong’oneza kwamba,  "Asante kwa kuniokoa kutoka njia ya Allah ya kuelekea jehanamu, na kunionyesha njia ya Yesu Kristo kuelekea Mbinguni." Miezi kadhaa baadaye, Maria na mimi tulikwenda kwenye mji mkuu wa nchi yetu, huku kila mtu akipita njia yake (ili watu wasianze kutushakia). Tulikwenda huko kwa ajili ya Ubatizo wangu katika Kanisa Kuu. Hili lilipangwa na kanisa. Baada ya Ubatizo, ilikuwa ni kama vile jua limefika kwenye Kanisa Kuu hilo, na kila kitu kilikuwa na mng’ao na amani. Mimi hata nilijisikia ni mwepesi. Kila mtu alinipongeza. Baada ya kula chakula cha mchana kwenye bwalo la chakula la Parokia, Maria alirudi kwenye mji wetu, lakini mimi nilibakia ili kutafuta kazi katika mji huu mkuu.

Niliweza kupata kazi kama mhandisi wa ubunifu, katika mji mkuu wa nchi hii kupitia rafiki, mbali na mji wangu, kwa ajili ya usalama wangu. Najua kile ambacho Waislamu watafanya kwa mtu anayeasi Uislamu (nacho ni kuniua).  Nilichofanya baada ya hapo ilikuwa ni kunyoa (hakuna ndevu wala masharubu). Kisha nikatoka kwenda kuonja kila chakula nilichoweza kula. Unajua, Mwislamu anatakiwa kula tu hakula halali (kilichopikwa na Mwislamu mwingine), vinginevyo kitakuwa ni haramu (haramu na ni dhambi). Bila ya barghashia, ndevu na kanzu, hakuna hata mtu aliyenitazama ninapokula chakula haramu. Nilijisikia huru sana kutoka kwenye kongwa la Uislamu. Mwanzoni nilikuwa siwezi kufanya mambo mengi. Uislamu ulikuwa umenifunga kabisa kwa kutumia sheria nyingi. Ilikuwa ni kama mzigo mzito sana umeondolewa kwangu. Maisha yakaonekana mazuri sana. Sikuwa tena na haja ya kuwaza hili au lile kabla ya kufanya jambo lolote. Nilianza hata kuimba mara nyingi.

Usiku mmoja, wakati wa maombi yangu, nililia kwa Yesu kwa furaha, kwa ajili ya yote aliyonitendea, na nikatumaini kuwa kaka zangu na dada yangu, siku moja wataweza kushiriki furaha yangu katika Yesu Kristo, ambaye hajanipa kingine chochote isipokuwa furaha na faraja. Chuki yote katika moyo wangu ilitoweka, na nikawa tu na upendo, kwa wanadamu wenzangu (hata waislamu). Niliwapatia Biblia wadogo zangu watatu wa kiume na dada yangu.  (Mdogo wangu mmoja na dada yangu tayari wameshaigundua njia ya kweli na sasa ni Wakristo. Mungu awabariki).

Miezi miwili baadaye, nilipoenda kumfuata Maria, alifurahi sana kuniona, hasa bila ndevu zangu. Akiwa anapapasa mashavu yangu kwa mikono yake, alisema, "Sasa unaendana na ndoto zangu, juu ya shujaa wangu anayevutia." Aliendelea kupapasa mashavu yangu taratibu. Mimi na  Maria tulienda kumtembelea yule bibi Mkristo na mtoto wake. Walishtuka sana na hawakuweza kuamini kuwa nilikuwa mtu yuleyule, (bila ndevu zangu, barghashia na kanzu). Kabla ya kuwaaga, sote tulipiga magoti mbele ya madhabahu yao na kuomba, huku tukimshukuru Yesu kwa baraka zake; na yule bibi alifanya maombi maalum kwa Yesu ili aweze  kutuweka salama na kutulinda daima. Kisha akamgeukia Maria, akamshika mikono yake na kumwambia kwamba atamkumbuka siku zote katika sala zake.

Mimi na Maria tulioana katika sherehe ya kimyakimya katika Kanisa Kuu la mji mkuu wa nchi hiyo. Kaka zangu na dada yangu, na wazazi wa Maria, kaka na dada zake nao walihudhuria kwenye harusi yetu kwa kuja katika gari nililokodi.  Ingawaje sasa, tuna watoto watatu wazuri wa kiume, Maria hajakata tamaa ya kupata binti. Kila jioni huwa tunaomba kama familia pamoja na Maria amekuwa ni mshauri wangu na ngao ya familia, kwa neema za Bwana wetu, Yesu Kristo.

Ninapotafakari nyuma, kwa siku hizo zote, nadhani haikuwa ni bahati tu mimi kumwona yule bibi wa Kikristo, au Maria kunishika mkono na kuniepusha kuanguka, bali ilikuwa ni kazi ya ajabu na ya siri ya Bwana wangu, Yesu Kristo, na sijawahi kuacha kumshukuru yeye, kwa ajili ya zawadi zake zote za ajabu, za kuyafanya maisha yangu kuwa mazuri sana kama nilivyotamani. Asante Yesu, Mwokozi wangu wa ajabu.

Ahmed Simon

Tafadhali: Kama wewe ni Mwislamu mwanamume, amini nakwambia, njia yako inaweza kukupeleka kwenye furaha na Mbinguni, kama utatupilia mbali kongwa la Uislamu na kuchukua njia ya Yesu Kristo.

Kama wewe ni Mwislamu mwanamke, (kutokana na uzoefu niliopata kupitia mama yangu mwenyewe na kazi yangu ya awali kama ustaadhi na hakimu), najua yale unayopitia (maumivu, mateso na udhalilishaji) na kweli kabisa naweza kuelewa hali uliyomo. Lakini haitakiwi kuwa hivyo, si ndiyo? Haujachelewa, kama utaamua kuwa huru kutokana na kongwa hili, ambalo limekufunga.

Wanaume na wanawake, achaneni na dunia yenu ya uongo na chuki (kama mimi), na kufungua mioyo yenu na kujiweka huru wenyewe leo, na kuweza kupokea upendo na furaha kwa njia ya Yesu Kristo. Chukua hatua sasa na, amini nawaambia, kamwe hamtajuta.

*******************

Ushuhuda huu umetafsiriwa kutoka kwenye Kiingereza. Kama ungependa kuusoma kwa Kiingereza, tafadhali bofya HAPA.

3 comments: