“Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa
katika
ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa
yote; hapo ndipo ule mwisho
utakapokuja”
(Mathayo 24:14).
Ukisoma kurasa mbalimbali za kwenye mtandao juu ya
kukua kwa dini ya Kiislamu, utakuta wengi wanasema kwamba Uislamu ni dini inayokua
kwa kasi sana. Je, hilo ni kweli? Ni jambo gani linaloonyesha ukweli wa hoja
hiyo?
Lakini tunao ushahidi wa Neno la Kristo kwamba siku za
mwisho (yaani hizi tulizo nao), Injili itahubiriwa ulimwenguni kote. Pia, Mungu
Yehova anaahidi kuwa hizi ni siku za kumwaga Roho wake kwa wanadamu wote.
Hakika hizi ni nyakati za Injili ya Yesu Kristo kusonga mbele na kushinda na
kubomoa kila upinzani na ukuta uliojengwa na adui ili kuwazuia wanadamu kumjua
Mungu wa kweli na Mwokozi pekee, Yesu Kristo.
Uzuri ni kwamba, hili si jambo la mwanadamu. Hii ni
kazi ya Mungu, Muumba mbingu na nchi Yeye mwenyewe. Ukristo si kama dini
zingine ambazo zinajipigania zenyewe. Ukristo ni kazi ya Kristo mwenyewe! Kuipinga
kazi hii ni kupingana naye. Na kuikataa kazi hii ni kumkataa Yeye mwenyewe.
Mamilioni ya Waislamu wametambua sasa ni wapi uzima uliko.
Je, ndugu msomaji, umeshaingia kwenye safina ambayo ni
Yesu Kristo? Usikubali kuachwa nje ya safina. Hakuna wokovu kwa mwingine awaye
yote ila kwa Yesu Kristo peke yake!
Suala si dini. Suala ni maisha ya amani na furaha na
mafanikio hapa duniani na kisha uzima wa milele mbinguni baada ya maisha haya.
Dini hazitusaidii lolote kamwe – iwe ni Ukristo au dini nyingine!
Kama ingekuwa ni kuhesabu mafanikio ya dini katika
historia nzima ya mwanadamu, basi dini zimefanikiwa sana kuleta mafarakano,
chuki na uhasama baina ya wanadamu. Hakika hicho ndicho ambacho dini
zimefanikiwa kufanya! Lakini Yesu – ah Yesu! Bwana wa amani! Bwana wa upendo!
Bwana wa uzima na uzima tele! Yeye ni njia, ni kweli, ni uzima! Dini bila Yesu
ni kupoteza kila kitu …!
Yafuatayo ni mahojiano kati ya mtangazaji Maher
Abdallah wa kituo cha Al-Jazeera na Sheikh Ahmad Al Katani kuhusiana na suala
la Waislamu milioni 6 kuingia kwenye Ukristo kila mwaka.
****************
Mtangazaji
Maher:
Idadi ya Waislamu hivi sasa haizidi theluthi ya watu wa
bara lote la Afrika. Hii inatilia
maanani pia ukweli kwamba, sehemu kubwa ya Waislamu katika Afrika ni Waislamu
wa Kiarabu. (Yaani ambao wanapatikana kaskazini mwa Afrika).
Ni wazi kuwa suala la uinjilisti na kuwageuza watu kuwa
Wakristo kunakofanywa na Wakristo vimesaidia katika kugeuza hali hii ya mambo
katika bara hili.
Katika kujadili mada hii, ninayo furaha kumkaribisha mtu
ambaye ni mtaalamu wa suala hili la uinjilisti
na kuwageuza watu kuwa Wakristo katika Afrika. Atalenga kwanza kuzungumzia
zaidi suala la kuenea kwa Ukristo. Shekhe Ahmad Al Katani, rais wa Companions
Lighthouse for Science in Libya, ambayo ni taasisi iliyojikita kwenye kusomesha
maimamu na wahubiri wa Kiislamu.
Shekhe
Ahmad:
Katika hali halisi, maneno haya (yaani ya Maher)
hayasemi kikamilifu kile kinachotakiwa kusemwa. Kama tulivyosema mwanzoni, kila
mtu anayo haki ya kuwakaribisha wengine kwenye dini yake; hiki ndicho
kinachojulikana kama kuhubiri dini. Na kuhusu uenezaji wa Ukristo, hakuna mtu
mwenye haki ya kuwatoa Waislamu nje ya dini yao, na umeuliza kuhusu rejea na
rejea ziko nyingi sana.
Uislamu ulikuwa ni dini kuu ya Afrika na kulikuwa na
lugha 30 za Kiafrika ambazo zilikuwa zikiandikwa kwa maandishi ya Kiarabu.
Idadi ya Waislamu imepungua Afrika hadi milioni 316, ambapo nusu ya hao ni
Waarabu wa Afrika Kaskazini. Kwa hiyo, katika eneo la Afrika ambalo
tunalizungumzia, eneo lisilo la Waarabu, idadi ya Waislamu haizidi watu milioni
150. Tunapotambua kwamba Afrika ina watu bilioni moja, tunaona kwamba idadi ya
Waislamu imepungua sana kutoka idadi iliyokuwapo mwanzoni mwa karne iliyopita.
Kwa upande mwingine, idadi ya Wakristo imeongezeka
kutoka milioni moja mwaka 1902 hadi milioni 329, 882,000, au tuseme milioni 330
mwaka 2000.
Kila saa moja, Waislamu 667 wanaingia kwenye Ukristo.
Kila siku moja, Waislamu 16,000 wanaingia kwenye Ukristo. Kila mwaka mmoja,
Waislamu milioni 6 wanaingia kwenye Ukristo. Idadi hii ni kubwa sana.
Mwandishi
Maher:
Hebu subiri
kidogo. Unamaanisha ni Waislamu milioni 6 wanaingia kwenye Ukristo au wanaingia
kwenye dini zingine?
Shekhe
Ahmad:
Dini zingine haziwekwi kwenye kundi la kufanywa
Wakristo; bali zinawekwa kwenye kundi la uinjilishaji. Dini nyingine katika
Afrika ni upagani. Kwa hiyo ni Uislamu, Ukristo au upagani. Hakuna kitu kama
kule Asia, kwa mfano, ambako kuna Ubudha au Uzoroasta. Kwa Afrika ni makundi
haya matatu tu. Kwa hiyo, unapozungumzia kuhusu kuwafanya watu kuwa Wakristo,
kunalenga dini nyingine pekee ya mbinguni, ambayo ni Uislamu.
*******************
Nini
maana ya hali hii?
[Maelezo yangu mimi blogger]
[Maelezo yangu mimi blogger]
Maandiko Matakatifu yako wazi kwamba: wa kwanza atakuwa
wa mwisho (Mathayo 19:30). Ulaya na
Marekani zilianza kuupokea Ukristo na kiwango kikubwa sana. Lakini hivi sasa
wamemkataa Bwana Yesu na wanazidi kuzama zaidi na zaidi kwenye giza nene.
Afrika, ambayo ilikuwa katika giza nene la ibilisi la
kutomjua Bwana huko nyuma, (kwa maana kwamba ilikuwa ya mwisho), katika nyakati
hizi za mwisho, ndiyo inayokuwa ya kwanza. Nuru ya Injili inasambaa kama moto
wa nyika. Na hili ni jambo linalotoka kwenye kiti cha enzi cha mbinguni
kwenyewe kama nilivyosema hapo mwanzo.
Hata kama adui atajaribu kujiinua kwa kiasi gani, Neno
la Bwana, kama kawaida yake, ni lazima
litimie! Hata nukta moja haitaanguka hadi yote yatimie.
Ndugu msomaji, hebu jiulize mwenyewe, Ukristo haujawahi
kushindana na mwanadamu ili kuwaingiza wanadamu kwa nguvu ndani yake. Haujawahi
kushika panga wala bunduki ili kuwaingiza wanadamu kwenye imani hii! Sasa ni
kitu gani kinachoufanya ukue kwa kasi namna hii? Mbona imani ya Kikristo ni
imani ya upole, huruma, msamaha na maelewano lakini wakati huohuo inasonga
mbele kwa kasi namna hii?
Bila shaka iko nguvu nyingine iliyo nyuma ya kundi
hili. Nguvu hiyo ni Roho Mtakatifu, ambaye ni Mungu mwenyewe. Vita ya kanisa la
Kristo siku zote imekuwa dhidi ya ulimwengu wa giza wa ibilisi. Na kwa sababu
silaha zetu ni za kiroho (si za kimwili), hizo ni silaha za ushindi daima.
Kanisa kamwe halishindani na wanadamu.
Bwana anatupenda sana wanadamu wake aliotuumba, ndiyo
maana alikuja duniani na kuishi na kufa kwa ajili yetu. Mtu yeyote anayeshindana
na Bwana hawezi kufika kokote. Tena ukichukulia kwamba mtu mwenyewe anashindana
kwa silaha za kimwili dhidi ya silaha za kiroho!
Tafakari.
Jiulize.
Hoji
mambo.
Chukua
hatua.
Huu ni uongo wa dhahiri ili kuupigia debe ukiristo.Iwapo watu 667 wanaingia kwa ukiristo kwa saa,na 327 milioni kwa mwaka,sidhani kama kungekuwa na Uislamu duniani kwa sasa.You are saying the direct opposite of that.
ReplyDeleteKama huu ni uongo, basi hilo ni jambo la ajabu kuliko kawaida. Shekhe Ahmad ni mwislamu, anaishi kwenye nchi ya kiislamu, na anaamini kuwa uislamu ndiyo njia ya kufika mbinguni. Huyuhuyu ndiye anayesema maneno haya, si kwa kukisia, lakini kutokana na utafiti waliofanya kitaalamu.
DeleteVinginevyo ndugu, labda unataka kutuambia kuwa huyu anayesema hivi ni mkristo ambaye amejipachika jina la kiislamu ili kuuchafua uislamu, au siyo?
Lakini kama ni mwislamu, anapata faida gani au uislamu unapata faida gani kwa maneno yake haya kama si watu kuukimbia zaidi?
Nilidhani yeye kama mwislamu, alitakiwa aseme kinyume chake kwa ajili ya kulinda heshima na jina la uislamu.
Mimi nikiwa kinyume nawe, halafu ikatokea nataka kusema uongo juu yako, siwezi kusema uongo ambao utakujenga; nitasema uongo unaokubomoa!
Mie Regy....Mungu akubariki James kwa nguvu ulizonazo za kuutetea ukweli siku zote, ninachotaka kusema ni hiki yumkini alikosea tuu hesabu kwani sie si binadamu? maana nimesoma mada hapo juu inajieleza vizuri sana tuu cha msingi tuwe waelewa na kuwaombea Mungu wasio mjua Yesu wabadilike ishu sio kumpinga mwingine na kumwita mwongo,, haya kaandika amepata faida gani? maana sidhani kama James kamlipa kwa uongo wake............tuwe watu wenye akili jamani sii kukurupuka tuu nakutamka maneno yasiyo na kibali mbele za Mungu. unajua Imani ni kitu Kidogo sana watu wengi wanadharau lakini ni jambo kubwa sana ukiamini maana kama Bikira Mariam kama hakumuamini yule malaika basi leo asingekuwa mama wa Yesu na kupata heshma kubwa yakumbeba mfalme.....angalia hata parapanda isije ikapigwa ukaambiwa ukakataa ukadhani ni mabomu ya mbagala. Mimi nakushauri ndg msomaji usiwe mwepesi wa hasira, kinywa chako kikatawaliwa na chachu ya ibilisi ukajikuta unapata gharama yakutengeneza na Mungu. Mungu akubariki kama umenielewa.
ReplyDeleteAmen Regy.
DeleteAsante kwa maoni na Bwana akubariki.