Biblia
inasema: “Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani…” (Ufunuo 2:13)
Waislamu “WAHUBIRI WA BIBLIA”, kama kawaida
ya “injili” yao potofu hawaachi kuzipotosha njia za Bwana zilizonyooka; lakini
kama hawataki kutubu, hukumu yao inakimbia mbio kuwajilia. Wahubiri hawa
hutumia andiko hilo hapo juu kuonyesha eti Kanisani ni mahali akaapo shetani,
wakimaanisha kuwa Wakristo wote tunapoenda kuabudu Kanisa, basi tunakuwa kwa
shetani!
Lakini andiko hili maana yake ni nini?
Maneno haya yamo kwenye ujumbe wa Bwana Yesu
kwa Kanisa la Pergamo. Kwa kuwa Bwana Yesu anatoa ujumbe kwa Makanisa kadhaa,
hebu tuanzie nyuma kidogo ili tuweze kuona MUKTADHA wa matumizi ya maneno haya
kwa usahihi. Siku zote nasisitiza umuhimu wa kuangalia maandiko katika MUKTADHA
wake kwa kuwa bila kufanya hivyo, utadanganywa, utadanganywa tu na watumishi wa
shetani na roho yako itaangamia milele!!
Mstari wa nane wa sura ya pili ya Ufunuo
unasema:
“Na
kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye wa
kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai.” (Ufunuo 2:8).
Bwana analiambia Kanisa hili: “Naijua dhiki yako na
umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni
Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.” (Ufunuo 2:9).
Haihitaji ufahamu wowote mkubwa kutambua kuwa
hapa kuna pande mbili – tena zinazopingana. Kuna upande wa Kanisa la Smirna
linalomwamini Yesu Kristo; na kuna upande unaopingana vikali na Kanisa hilo,
yaani upande wa Sinagogi la Shetani.
Kwa maneno mengine, Bwana Yesu anasema: “Wewe
Kanisa uko Smirna, lakini shetani na kundi lake nao wapo hapohapo Smirna. Yaani
hawa wana wa ibilisi ambao wanajidai kuwa wanahubiri neno la kweli la Mungu
kumbe ni ujumbe utokao kuzimu kwa shetani, ambao kwa nje unaonekana kama ni
maneno ya Mungu lakini ni ujumbe wa mauti.
Ufunuo 2:10 inasema: “Usiogope
mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili
mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami
nitakupa taji ya uzima.”
Hapa Bwana anasema kwa hilo Kanisa la Smirna,
“Wewe Kanisa, kwa kuwa hapo Smirna ulipo kuna pia kundi la shetani, kaa ujue
kuwa shetani amepanga mabaya juu yako na atayatekeleza. Lakini pamoja na uovu
wake huo, VUMILIA HATA KAMA ATAWAUA (angekuwa allah angesema, “Msikubali,
chukueni mapanga mjilipize kisasi!”).
Hilo ni Kanisa la Smirna. Hebu sasa tugeukie
Kanisa jingine kuhusiana na andiko linalotumiwa kwa hila na wahubiri wa ‘injili’
ya kiislamu. Hilo ni Kanisa la Pergamo.
Kwa mantiki ileile ya Kanisa la Smirna,
mstari wa 13 unatoa maelekezo ya Bwana Yesu kwa Kanisa la Pergamo. Anasema:
“Napajua ukaapo, NDIPO PENYE KITI CHA ENZI CHA
SHETANI; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata
katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo
akaapo Shetani.” (Ufunuo 2:13).
Hapa tunaona kuwa, Bwana anatoa tahadhari kwa
Kanisa hili. Anachosema ni kuwa: “Wewe Kanisa la Pergamo, hapo Pergamo ulipo
ndipo pia yaliko makao makuu ya shetani.”
Kwa kila Kanisa, Bwana anakuwa anaeleza uzuri
wa Kanisa husika kisha upungufu wake. Kwa Kanisa la Pergamo, uzuri wao ni huu: “walishika
sana jina langu, wala hukuikana imani yangu.”
Kwa hiyo, ukitazama mtiririko ulivyo kupitia
makanisa haya tu mawili, unaona kuwa Bwana Yesu anatenganisha WAZIWAZI kati ya Kanisa
lake na kundi la shetani ambalo linaleta upinzani kwa Kanisa.
Kwa kifupi ni kuwa, Kanisa la Kristo SI MAHALI
PA SHETANI HATA KIDOGO bali shetani ni mpinzani anayeingia Kanisani ili
kuwaangusha watakatifu kupitia wale
wanaoikana Injili ya kweli ya uzima ya Bwana Yesu!!
Ushauri wangu kwako Mwislamu ‘unayehubiri’
Biblia: kama unadhani ni muhimu kupinga Ukristo, fanya hivyo kwa kutumia hoja ZA
KWELI (kama zipo) na sio kutumia hoja ZA UONGO; mambo ambayo Biblia hata
haiyasemi!
Mgonjwa wa ebola akitumainia uongo wa kusema,
“Mimi sina kabisa ebola mwilini mwangu” wakati anayo, kwanza hamdanganyi yeyote
bali ni yeye mwenyewe!! Pili, ATAKUFA yeye mwenyewe na sio wale anaowaambia
uongo huo.
Hoji mambo
Uongo unaua
Na ujinga (ignorance) ni barabara ya kwenda
kuzimu
Tafakari
Chukua hatua!!
Nilifikiria utatowa maelezo sahihi ya Aya hiyo kumbe malalamiko na shutma. Kiti cha enzi maana yake makao makuu si ndio kinapatikana kwenye Hilo kanisa
ReplyDeleteEmeni Asante YESU mbaliki mtumishi WAKO kwakazi njema
ReplyDeleteHuna hoja ata moja ulie ongea apo zaidi tu ya kulalamika, ilo andiko niko wazi kbs , kiti ca Enzi kinapo patina ni kanisani tu 🙄 poleni
ReplyDelete