Friday, October 13, 2017

Je, Yesu Alitawadha Wanafunzi Wake Kama Waislamu Wanavyofanya?

 
Katika Yohana 13:4-5 tunasoma kuhusu Yesu kuwa:
aliondoka chakulani … akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.
Kutokana na tendo hili, waislamu hudai kuwa wao wako karibu na Yesu zaidi ya wakristo kwa kuwa wao hutawadha ilhali sisi hatutawadhi.
Lakini hebu tutazame mambo mawili muhimu hapa:

1. Yesu aliwatawadha SIO wao walijitawadha
2. Ilikuwa wakati wa chakula SIO wakati wa ibada



Kwa hiyo, tendo hili halina uhusiano kamwe na kile kinachofanywa na Waislamu. Kama wanadhani linafanana, je:
1.     Nyie huwa mnatawadhwa na mashekhe wenu kama Yesu alivyowatawadha wanafunzi wake?
2.     Nyie huwa mnatadha wakati wa kula chakula?
Jibu ni hapana.
Sasa kwa nini Yesu aliwatawadha wanafunzi wake miguu?

Katika Yohana 13:14-16 Bwana Yesu anaeleza MAANA ya tendo hili alilolitenda. Anasema:
Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.

Anasema:
1.     mimi Bwana na Mwalimu – maana yake mimi ni mkubwa, aliye juu, kiongozi Yaani: sikujali ukubwa au cheo changu nimejishusha na kuwa MTUMISHI wenu. Jueni kuwa cheo SIO u-boss. Ninyi mtakuwa viongozi wa Kanisa. Basi mkawe WATUMISHI na SIO MABOSI.
2.     Nimewapa kielelezo – maana yake huu ni mfano tu. Msikariri. Kielelezo ni kitu kinachotoa picha ya jambo kubwa. Hapa siongelei kutawadha, bali naongelea utumishi kwenye maeneo YOTE.


Kwa hiyo, ni WAZI kwamba jambo alilofanya Bwana Yesu HALINA KAMWE uhusiano na tendo la kubeba makopo ya maji na kuelekea uani kwenda kutawadha.

Ninyi mnaposoma maji katika Torati mnaona maji. Sisi tunamwona Yesu.
Maana amesema katika Yohana 5:39 - 40
Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; NA HAYO NDIYO YANAYONISHUHUDIA. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima.
Maana yake, maandiko hayajaandikwa ili kushuhudia MAJI, bali yameandikwa kumshuhudia Yesu.

Ukiona maji ni Yesu.
Ukiona damu ni Yesu.
Ukiona vita ni Yesu.
Ukiona chakula ni Yesu, nk.
Nje ya hapo unatembea gizani.
Ndugu zetu Waislamu,
acheni kuangamizana kwa uongo
Kwa kupindisha maneno ya Mwalimu Yesu.
Tafakari
Chukua hatua.

2 comments: