Friday, October 13, 2017

Naapa kwa uhakika! Gabrieli hakutumwa kwa Muhammad



Malaika Gabrieli tunayemjua ni:
-       mpole
-       mnyenyekevu
-       ametulia
-       mtaratibu
       -      HAKABI WATU.



Mwanadamu yeyote akikutana na kiumbe wa rohoni, lazima ataingiwa na hofu kwa kuwa hilo si jambo la kawaida. Lakini kuna TOFAUTI ya kuingiwa na hofu kwa sababu UMEONA kisicho cha kawaida; na kuingiwa na hofu kwa sababu sit u umeona kisicho cha kawaida, lakini pia kwa kuwa KIMEKUKABA hadi ukaishiwa pumzi.


Hebu mwangalie Gabrieli wa kweli alivyo:

Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka. NDIPO AKANIAMBIA, USIOGOPE, DANIELI; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. (Danieli 10:11-12)


Naye Bwana akamjibu yule malaika aliyesema nami KWA MANENO MAZURI, MANENO YENYE FARAJA. (Zekaria 1:13)


Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. Lakini yule malaika akamwambia, USIOGOPE, ZAKARIA, MAANA DUA YAKO IMESIKIWA, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. (Luka 1:12-13)


Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika akamwambia, USIOGOPE, MARIAMU, KWA MAANA UMEPATA NEEMA KWA MUNGU. (Luke 1:28-30)


Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. MALAIKA AKAWAAMBIA, MSIOGOPE; KWA KUWA MIMI NINAWALETEA HABARI NJEMA YA FURAHA KUU itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. (Luka 2:8-11)
 
……………
Huyo ndio Gabrieli ninayemjua.
Huyo ndio Gabrieli wa kweli.
Huyo ndio Gabrieli wa mbinguni.


Lakini vipi kuhusu Jibril ambaye Uislamu unasingizia kuwa ni Gabrieli wa Biblia?
Tunasoma katika Sahih Bukhari Vol 1, Bk 1, No. 3:
The Prophet added, "The angel caught me forcefully and pressed me so hard that i could not bear it any more.”


Maana yake:
Mtume akaongeza, “Malaika alinikamata kwa nguvu na kunigandamiza kwa nguvu sana hadi nikawa siwezi kupumua tena.”

“Aliyeenda kwa Muhammad:
SIO Gabrieli.
Sio!
Hata siku moja!

Bwana Yesu anasema:
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye HATAKWENDA GIZANI KAMWE, bali atakuwa na nuru ya uzima. (Yohana 8:12)

Usidanganywe.
Tafakari.
Chukua hatua.

No comments:

Post a Comment