Ibra na Waislamu wengine,
kumekuwa na kawaida kwa ulimwengu wa Kiislamu kufanya kila juhudi kuonyesha
kwamba Biblia imepotoshwa, ingawaje jambo hilo si kweli hata kidogo. Ukiachilia
mbali makosa ya kibinadamu ya hapa na pale ambayo yanaingia kutokana na ukweli
kwamba Biblia imetafsiriwa na inaendelea kutafsiriwa mara nyingi sana, hakuna
makosa ya makusudi yanayofanywa ili kupotosha au kuficha ukweli.
Na juhudi hizi zote
zinafanywa ili kutaka kuonyesha kwamba Quran ni neno la Mungu la kweli
ambalo halijapotoshwa hata kidogo. Basi mimi naomba mnisaidie majibu ya maswali
haya machache kati ya mengi:
1. Sura
54:19 inasema kuwa mji wa Aad uliharibiwa kwa siku moja na sura 69:6,7 inasema
kuwa uliharibiwa kwa 'usiku' sita na siku nane (seven nights and eight days).
Hapo kuna mkanganyiko au la?
2. Sura
19:17 inaonyesha kuwa malaika alimtokea Mariamu lakini sura 3:42 inasema
walikuwa malaika wengi.
3. Sura
28:40 inasema kuwa farao alizama na kufia kwenye maji lakini sura 10:92 inasema
kuwa farao huyo alipona.
4. Sura
18:86 inasema kuwa jua huzama kwenye chemchemi ya maji yenye tope. Unadhani hii
ni sahihi. Jua lina joto la zaidi ya nyuzijoto 6000 kwenye uso wake. Lakini maji
yakifika nyuzijoto 100 yanageuka mvuke. Je, maji yanayotajwa kwenye sura hii ni
maji gani? Unadhani ni Mungu aliyeumba jua na maji ndiye anayesema haya?
5. Sura
15:19 inasema kuwa dunia ni bapa kama meza (flat). Kama Mungu ndiye aliumba
dunia na ndiye alileta Quran, anaweza kusema jambo kama hili?
6. Sura
86:6,7 inasema kuwa manii ya mwanamume
hutokea kati ya uti wa mgongo na mbavu. Hii ni sayansi ya wapi? Ni kutoka kwa
Mungu aliyeumba wa mbingu na nchi na uti wa mgongo na mbavu kweli? Kama haitoki
kwa Mungu basi hata kitabu chenyewe nacho hakitoki kwa Mungu, au siyo?
7. Sura
19:27,28 inasema kuwa Mariamu alikuwa ni dada wa Haruni. Lakini tangu Haruni
aishi ilipita miaka 1300 ndipo alipozaliwa Mariamu. Ni Mungu gani basi
anayeweza kusema maneno kama haya?
8. Sura
28:8 inasema kuwa farao na Hamani waliishi wakati mmoja na mahali pamoja. Lakini
historia iko wazi kwamba kuna tofauti ya miaka takribani 1000 kati ya watu
hawa. Vilevile, farao aliishi Misri wakati Hamani aliishi Uajemi kwenye ngome
iliyoitwa Shushani.
MAONI
YANGU
Biblia
na Quran zote zina makosa fulanifulani ya kibinadamu yalioyoingia humo wakati
wa kuandikwa kwa vitabu hivyo. Kwa upande wa Biblia (sijui sana upande wa
Quran), huwa nakutana na makosa kadhaa, kwa mfano kukosewa kuandikwa kwa neno,
kutafsiriwa vibaya kwa neno, kukosewa kwa takwimu, n.k. Mimi nadhani kuwapo kwa
makosa ya aina hii si ishara kwamba kitabu hiki hakitoki kwa Mungu. Ingekuwa ni
kweli kwamba makosa haya yaliingizwa ili kuficha au kupindisha ukweli fulani,
basi huko ndiko kungekuwa ni kupotosha maandiko.
Kwa
upande wangu kipimo kikuu cha kutambua iwapo neno fulani ni la Mungu au la, ni
MAFUNDISHO ya Mungu anayehusika. Kwa mfano, hapo juu nimetoa mfano wa Sura
54:19 inayosema kuwa mji wa Aad uliharibiwa kwa siku moja ilhali sura 69:6,7 inasema
kuwa uliharibiwa kwa 'usiku' sita na siku nane (seven nights and eight days).
Mimi sioni kama hiki ni kigezo cha kusema kuwa Quran si kitabu cha Mungu wa kweli. Au aya moja kusema farao alizama maji na nyingine ikasema hakuzama. Aina hii ya ukinzani kwangu si kigezo cha kubatilisha kitabu.
Lakini tunapoenda kwenye mafundisho yanayohusu mwenendo wa kuishi na wanadamu wenzako, vigezo vya utakatifu, wajibu wa muumini kwa Mungu, wanadamu wenzake na jamii kwa ujumla, n.k., hapo ndipo ninaona kuna uwezekano wa kutenganisha kati ya ujumbe wa Mungu wa kweli na usio wa Mungu wa kweli.
Kama Mungu mmoja anasema wachukie wanadamu wasio na imani kama yako, waue; halafu kuna Mungu mwingine anasema wapende, wasamehe, waombee, wavumilie, n.k., bila shaka hapa ndipo penye uwanja sahihi wa kutenganisha pande hizi mbili.
Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo akubariki ndugu msomaji.
Tafakari.
Hoji mambo
Chukua hatua.
******************
Bado naendelea kungoja kwa hamu kubwa majibu ya maswali niliyouliza HAPA. Sijapata mtu wa kunijibu hadi sasa.
Ukisoma 19:17 malaika alikuwa mmoja na 3 anzia 39 utaona kuwa malaika in mmoja aliyemletea maryam ubashiri ukija 42 hawakuwa wakibashiri wale malaika Bali wakimueleza maryam ya kuwa amebarikiwa.
ReplyDeleteLabda ungelejea Quran yako kwa utulivu na so kwa akili ya kihitikadi maana 10:92 na 28:40 zinaeleza maana moja.
ReplyDeleteUkisoma 15 kuanzia 16 utaelewa 19 inaeleza kuwa kilichotandazwa ni ardhi.soma 2:2 kwa faida yako
ReplyDelete