Wednesday, June 26, 2013

Swali kwa Waislamu Kuhusu Kupotoshwa kwa Biblia




Je, Biblia ni Kitabu Kilichopotoshwa na Wanadamu?



Waislamu wanashikilia SANA kwamba Biblia imepotoshwa; na kwamba Quran ndicho kitabu cha kweli chenye ujumbe wa kweli wa Mungu aliye hai.

Baada ya Yesu kuondoka Duniani, Quran ilikuja miaka zaidi ya 600 baadaye. Biblia ilishakuwapo kwa maelfu ya miaka kabla ya hapo.

Baada ya Quran kuandikwa, ikasema mengi kuhusiana na Biblia, yakiwamo machache yafuatayo:


1. Al- Imran 3:2-3

Allah! Hakuna mungu isipokuwa Yeye, aliye hai na wa milele. Amewafunulia kitabu chenye ukweli kinachothibitisha yale yaliyokitangulia; na ameshafunua Torati na Injili kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu, na kwa ajili ya kutofautisha kati ya jema na baya. [Allah! There is no god but Him, the Living, the Ever-existent One. He has revealed to you the Book with the truth confirming what preceded it; and He has already revealed the Torah and the Gospel for the guidance of men, and for the distinction between right and wrong.]



Je, tunaweza kusema kuwa andiko hili linaonyesha kwamba Biblia ni kitabu kilichopotoshwa au linaonyesha kwamba ni kitabu sahihi kabisa? Je, ni andiko linaloonyesha kuwa Biblia ni ujumbe kwa ajili ya Wakristo, Wayahudi au wanadamu wote?
 

Aya hii inaonyesha kuwa Torati na Injili (Biblia) zililetwa kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu WOTE (si Wakristo) ili waweze kujua lipi jema na lipi baya.


2. Yunus 10:94

Endapo mna shaka juu ya yale tuliyowafunulia, waulizeni wale waliosoma Kitabu kabla yenu. [If you are in doubt of what We have revealed to you, ask those who have read the Book before you.]

Kitabu hapa ni Torati na Injili na waliokisoma ni Wakristo na Wayahudi.



Kwa nini Quran iliagiza kwamba mashaka ya Waislamu yapelekwe kwenye Biblia? Unadhani lengo lilikuwa ni ili wakapotoshwe? Je, Quran ingefanya hivyo kama kitabu kingekuwa kimepotoshwa?


3. Al-Bayyina 98:6-7

Wale wasioamini miongoni mwa Watu wa Kitabu na wapagani wataungua milele katika moto wa jehanamu. Hao ni waovu kuliko viumbe wote. Lakini wale wanaoikumbatia imani na kutenda mema ni waadilifu kuliko viumbe wote. [The unbelievers among the People of the Book and the pagans shall burn forever in the fire of Hell. They are the vilest of all the creatures. But those that embrace the faith and do good works are the noblest of all creatures.]

Aya hii inaeleza kwamba, miongoni mwa Watu wa Kitabu, yaani watu wanaoamini Biblia, na pia miongoni mwa wanadamu WOTE, wale wanaoamini Biblia kikamilifu, yaani Wakristo wa kweli ndio viumbe wema kuliko viumbe wote wa Mungu.



Je, anawezaje mtu kuwa kiumbe bora kuliko viumbe wote (yaani kuliko hata Mwislamu mzuri kuliko wote) kutokana na kitabu kilichopotoshwa?


4. Al-Nisa 4:136

Enyi mlioamini, iweni na imani kwa Allah, na kwa Kitabu alichomfunulia Mtume wake, na kwa Kitabu alichokifunua kabla. [O believers, have faith in Allah and His Apostle, in the Book He has revealed to His Apostle, and in the Book He formely revealed.]


Na Kitabu alichofunua kabla ni Torati ya Musa na Injili ya Isa/Yesu.



Je, Waislamu wangepewa agizo hili kama wakati wa kuandikwa kwa aya hii Biblia ingekuwa imepotoshwa?


5. Al- Ahqaf 46:12

Na bado, kabla yake kulikuwa na Kitabu cha Musa, mwongozo na baraka kwa wanadamu wote. Kitabu hiki kinakithibitisha. [Yet before it there was the Book of Musa, a guide and a blessing to all men. This Book confirms it.]



Bila shaka ‘kitabu cha Musa’ hapa ni Agano la Kale au tuseme Torati. Je, kitabu kilichopotoshwa kinaweza kuwa baraka na mwongozo kwa wanadamu WOTE?


Historia ya maandishi kwa mwanadamu ilianza maelfu ya miaka, hata kabla ya Biblia na Quran kuandikwa. Kwa mfano, Wamisri na watu wa Mesopotamia, Wachina, n.k. walikuwa tayari wana maandishi.

Hivi leo yapo maandishi mengi tu yaliyoandikwa na watu hao. Unaweza kuona baadhi ya mifano kwa kubofya HAPA, na HAPA, na HAPA - au sehemu nyingine yoyote kwenye mtandao.

Sasa, kama nilivyosema hapo juu, Quran ilikuja miaka 600 baada ya Yesu. Na Quran hiyo ikasema mambo mengi kuhusiana na Biblia kama tulivyoona mifano hapo juu.

Kwa mfano, Quran inaposema katika Al- Imran 3:2-3 kuwa Mungu: ameshafunua Torati na Injili kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu, na kwa ajili ya kutofautisha kati ya jema na baya; hii ina maana kuwa Injili iliyokuwapo wakati maneno haya yanaandikwa ilikuwa ni Injili sahihi yenye sifa hizi zinazotajwa na andiko hili.

Kama Quran ni ya kweli, ina maana kuwa hadi miaka 600 baada ya Yesu, Biblia ilikuwa haijapotoshwa. Kama Biblia ingekuwa imepotoshwa wakati ule, basi Quran isingesema maneno haya. Pia isingewaagiza Waislamu katika surat Yunus 10:94:

Endapo mna shaka juu ya yale tuliyowafunulia, waulizeni wale waliosoma Kitabu kabla yenu. [If you are in doubt of what We have revealed to you, ask those who have read the Book before you.]

Agizo hili ni ushahidi kwamba, wakati maneno haya yanaandikwa kwenye Quran, Biblia ilikuwa iko sahihi kama ambavyo Mungu aliifunua kwa wanadamu.



Kwa kifupi ni kuwa, kutokana na aya za Quran nilizonukuu hapo juu, tunajifunza yafuatayo:


(a)       Wakati Quran inaandikwa (miaka zaidi ya 600 baada ya Kristo), Biblia ilikuwa na Neno lilelile la Mungu wa Israeli ambalo aliwafunulia wale walioliandika. Ndiyo maana Quran ikalitambua Neno hilo kwamba ndiyo mwongozo sahihi wa wanadamu wote.

(b)      Waislamu hawana uwezo na wala haileti mantiki kwa upande wao kulaumu Biblia iliyokuwapo hadi kufikia mwaka 600 BK, yaani kabla ya Quran kuandikwa, maana kwa kufanya hivyo watakuwa wanaikana Quran yao wenyewe na kuonyesha kuwa Mungu wao ni mwongo; na pia ina maana kuwa wao wanajua zaidi kuliko Mungu wao.
(c)       Kama ni kweli Biblia imepotoshwa, NI LAZIMA upotoshaji huo uwe umefanywa BAADA ya Quran kuwa imeandikwa, yaani labda kwenye mwaka 700 baada ya Kristo au zaidi.
(d)      Kama Biblia imepotoshwa, ni lazima zitakuwapo nakala ambazo zilikuwa zina hiyo inayoitwa na Waislamu ‘Biblia sahihi’, japo hata vipande vichache.

Kama Waislamu wakiweza kuonyesha jinsi Biblia ya sasa inavyotofautiana na Biblia ya mwaka 600 BK kurudi nyuma, hoja yao itakuwa na maana.


Kama Wakristo tukiweza kuonyesha kuwa Biblia iliyokuwapo mwaka 600 BK na kurudi nyuma ndiyo iliyopo leo, hoja ya Waislamu inakuwa haina maana yoyote.
 

Hiyo mnayoita Biblia yenye Neno la kweli la Mungu iko wapi? Hebu tujiulize swali la msingi la kawaida tu. Maandiko yaliyoandikwa na watu wa Misri, Mesopotamia, Uchina n.k., maelfu ya miaka kabla ya Kristo yanapatikana hadi leo.

Je, inawezekanaje tuamini kuwa eti maandiko ya Biblia (yaani hiyo mnayoita ninyi kuwa ni Injili sahihi) yaliyokuwapo juzijuzi, yaani miaka 500 baada ya Yesu yatoweke duniani kote na asipatikane mtu hata mmoja wa kuyabainisha?

Ni lazima Waislamu au mtu yeyote atuonyeshe hiyo mnayoita ninyi Injili ya kweli ili watu waweze kuamini kwamba kile mnachokisema [kuwa eti Biblia imepotoshwa na wanadamu] ni cha kweli.


Mbona kuna maandiko ya watu kama akina Plato yaliyoandikwa miaka takriban 500 kabla ya Kristo na leo yapo? Haya si ndiyo yalitakiwa yasijulikane kabisa kwamba yaliwahi kuwapo?  Hayo mnayoita Maandiko ya ‘kweli’ ya Biblia yaliyokuwapo miaka 1000 baadaye yako wapi, enyi ndugu Waislamu?

Inawezekanaje kitabu (vitabu) vilivyokuwapo miaka 500 baada ya Kristo vikatoweka KABISA duniani kote, wala asiwepo mwanadamu hata mmoja wa kukiona hata kipande kimoja cha ukurasa wa vitabu hivyo? Hii yote ni jitihada ya kujaribu kuhalalisha Quran ambayo nayo haihalalishiki isipokuwa kwa maneno na hoja za kutunga!! 

Mbona kila siku watu wanafukua masalia ya nyumba, mavazi, vyakula, mifupa ya watu, miji, na kadhalika; kwa nini hata siku moja hatusikii wamefukua masalia ya kitabu cha Musa kilicho tofauti na hiki tunachokijua? Badala yake wataalamu wa akiolojia wanaendelea kuthibitisha ukweli wa Biblia mstari kwa mstari kutokana na masalia ya nyakati za Biblia yanayofukuliwa sehemu mbalimbali - iwe ni Israeli, Misri au kwingineko kote kunakotajwa ndani ya Biblia?

Au basi mnataka kutuambia kuwa kile kilichopotea ndiyo hiyo Quran? Kwamba Quran ilivyo leo ndiyo iliyokuwa Biblia hapo mwanzo; Wakristo wakaitowesha duniani kote, lakini Allah akairudisha tena kupitia Muhammad?

Wapendwa, Biblia haijawahi kubadilika tangu Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo alivyoanza kuifunua kupitia wale aliowachagua. Biblia bado ni Neno la kweli la Mungu; na bado ndiyo mwanga na njia pekee ya kufika mbinguni. Iko vilevile tokea mwanzo.

Sisi tunao uwezo wa kuthibitisha kwamba Biblia iliyokuwapo wakati Quran inaandikwa, [ambayo Quran ilikuwa inaikubali na kusema kuwa ndiyo njia ya wanadamu wote kujua jema na baya], kuwa ndiyo hiyohiyo iliyopo leo – endelea tu kufuatilia blog hii.

Hoja ya kwamba Biblia imepotoshwa na wanadamu; hoja kwamba ujumbe uliotoka kwa Mungu kwanza si huu ulio kwenye Biblia ya leo, ni hoja ambayo haina maana, haina uthibitisho, haina nguvu, na wala haina ukweli hata chembe.


Tafakari

Jihoji

Jiulize

Jibu limo ndani mwako.

...........................................................................

Nyongeza:

Soma pia HAPA uone jinsi ambavyo huo unaoitwa ujumbe wa mtume wa mwisho wa Mungu unavyoleta mateso kwa watu waliofungwa nao. Ni uchungu mkubwa sana kuona jinsi watu wa Mungu wanavyosumbuka kwa sababu hawajajua kuwa uhuru, furaha, amani na wokovu vimo ndani ya BIBLIA pekee.

No comments:

Post a Comment