Mpendwa msomaji na mpenzi
wa blog hii, naamini ulishasoma sehemu ya 1 na ya 2 za ushuhuda huu wa Akef. Hii
ni sehemu ya 3 na ya mwisho inayoonyesha ukuu, upendo na uweza wa Mungu wa
Ibrahimu, Isaka na Yakobo, yaani Yesu Kristo. Karibu usome sehemu hii na Bwana
Yesu akubariki.
……………………….
Sid
Roth:
Ulipomgusa yule mtu
aliyekuwa kwenye kiti cha magurudumu, nini kilitokea?
Akef:
Inashangaza. Mimi hata
sikuwaza kwamba amngeponywa. Nilijua ingetokea
kwangu. Nilijua kuwa miujiza hutokea kupitia wachungaji lakini si kwa mtu kama
mimi. Lakini alikuja mbele akanyosha mkono wake, nami nikamshika. Na mara aliinuka kutoka kwenye kiti chake cha
magurudumu.
Sid
Roth:
Kwa nini ulimgusa?
Akef:
Sijui. Nilijisikia tu shauku aondoke kwenye kiti
kile.
Sid
Roth:
Alitembea?
Akef:
Ndiyo. Alianza kwa kunyanyuka polepole, kisha akaanza
kutembea mle kanisani. Kisha akatoka nje, akarudi ndani na kila mtu kwenye lile
kanisa la Kibaptisti alishangaa. Na kwa namna fulani, kila mtu alitamani kuja
mbele na kugusa mkono wangu. Mchungaji alikuja akauangalia mkono wangu – maana uligeuka
mwekundu na wenye joto. Aliwaonyesha waumini na kuwaambia waje mbele kuugusa.
Sid
Roth:
Pamoja na ukubwa wa
muujiza ule, Akef ananiambia kuwa kulikuwako na jambo jingine kubwa zaidi. Lilikuwa
ni jambo gani?
Akef:
Lilikuwa ni jambo ambalo lilinifanya
nijue ninakosimama; nijue iliko imani yangu. Chuki ambayo nilikuwa nayo dhidi
ya Wayahudi; ambayo niliibeba; uzito ule, uliondoka! Uliondoka na kiukweli
nilianza kujisikia mzigo moyoni kwa ajili ya Wayahudi. Na nikaanza kuwaza
kwamba, kama kuna njia yoyote ya kuwasaidia, basi niko tayari kuwasaidia. Na nilijua
kuwa hili ni jambo lililo nje kabisa ya uwezo wangu! Nisingeweza kamwe kufanya
hivi! Sasa jambo hili limetokea wapi? Ni nani aliyenibadilisha jinsi
nilivyolelewa; kile nilichoamini? Nini kilichotokea? Ni nguvu ya Bwana.
Sid
Roth:
Akef, mimi ni Myahudi. Mimi
ni Mzayuni. Nina uraia wa aina mbili. Mimi ni Mwisraeli. Ninaamini kuwa watu
wangu wana haki na ardhi ya Israeli ambayo Mungu amewaahidia kwenye Biblia
yake. Je, unawaza nini juu yangu?
Akef:
Mimi si mjuzi sana wa
mambo ya kisiasa …
Sid
Roth:
Unawaza nini juu yangu!
Akef:
Ninakupenda! Na nilitamani
kukutana na wewe, na nilishakutana nawe muda mrefu uliopita kwenye akili yangu,
kwenye moyo wangu. Wewe ni kaka yangu katika Kristo, na kupitia Ibrahimu, baba
yetu.
Sid
Roth:
Napenda niwaambie (watazamaji)
jambo. Kuna machozi yanayotiririka machoni mwangu hivi sasa. Na hili ni jambo
lisilo la kawaida linalotokea leo. Huwa halitokei mara nyingi kama ambavyo
ningependa, lakini linanitokea sasa. Na pale
linapotokea, ni wakati wa Mungu mimi kukuambia – uwe ni Myahudi, Mwarabu au
Mhindu – Mungu ni mkuu sana kuliko yale uliyoambiwa. Mungu ni mwema sana; Mungu
ni upendo.
Anakupenda, hataacha
kukupenda. Lakini kuna jambo linalokuzuia kupokea utimilifu wa pendo lake. Jambo
hilo ni dhambi. Na kama ukimwambia Mungu unatubu dhambi zako … mwambie kuwa
unatamani kubadilika lakini hauna nguvu, kisha umwombe nguvu ya kuwekwa huru. Atafanya
hivyo. Lakini ni lazima umwendee kwa njia ya Jina pekee ambalo tumepewa
wanadamu kwa ajili ya kuokolewa. Jina hilo kwa Kiebrania ni Yeshua, yaani Yesu.
Kama ukisema sala ifuatayo
kwa kumaanisha, Mungu atakutakasa, atakufanya upya, atakupa makusudi ya maisha
kama alivyofanya kwa Akef. Yeye ni Mungu wa miujiza. Na Yeye ni Mungu wa nafasi
ya pili. Omba sala ifuatayo pamoja nami:
Ee
Mungu,
Mimi
ni mwenye dhambi,
Nimekutenda
dhambi Wewe peke yako,
Nami
ninatubu.
Ninaamini
kuwa damu ya Yesu
Inaniosha
dhambi zangu zote,
Na sasa mimi ni safi.
Na
sasa kwa kuwa niko safi,
Ninatamka
kwa ujasiri,
Kwamba
Yesu ni Masihi wangu na Bwana wangu.
Bwana
Yesu,
Karibu
ndani yangu,
Tawala
maisha yangu,
Uwe
Bwana wa maisha yangu.
Katika
Jina la Yesu.
Amen.
Sid
Roth:
Akef, nikuulize swali moja
la harakaharaka. Kwa nini Waislamu hawasomi Agano Jipya, na hasa Injili?
Akef:
Hawasomi Injili kwa kuwa
wanaamini kwamba, Mungu, Allah alimpa Yesu Injili. Na wanaamini kuwa Injili ile
ambayo Allah alimpatia Yesu, ilipotea.
Sid
Roth:
Kwa nini hilo halina
ukweli?
Akef:
Halina ukweli kwa kuwa
halina mantiki. Hii ni kwa sababu Injili hii ilikuwapo kwenye miaka ya 600 hadi
700 baada ya Kristo. Iweje basi kitabu hiki kipotee tu duniani kote kwa ghafla
hivyo? Hakuna aliyewahi kukiona! Yaani vitabu ambavyo viliandikwa maelfu ya
miaka kabla ya hapo vipo halafu hiki cha juzi tu ndicho kisiwepo kabisa!!
………………………………….
Ndugu msomaji wa ushuhuda
huu, umemsikia au kumsoma Akef.
Tafakari,
Hoji
mambo,
Jiulize
maswali,
Chukua
hatua.
No comments:
Post a Comment