Nadereh ni mwanamke
aliyekuwa Mwislamu ambaye aliishi kulingana na sheria na taratibu za dini ya Kiislamu.
Lakini katika maisha yake ya kumtafuta Mungu, alikutana na vikwazo au upungufu
kadhaa. Hatimaye, alijikuta akibadili mwelekeo wake na kupokea wokovu wa Yesu
Kristo. Je, ni nini kilitokea? Ni kwa nini hajutii uamuzi wake huo? Ungana naye
ili uweze kujifunza jinsi Mungu anavyokupenda na kile alichokuandalia kwa ajili
ya maisha haya na yale yajayo.
******************
Nilikuwa Mwislamu na
nilimwamini Allah. Allah kwangu alikuwa Mungu na niliamini; lakini Mungu ambaye
alikuwa hafanyi chochote kwangu. Hakuwa maishani mwangu. Sikuwa na uhusiano na
Mungu huyo.
Mungu huyu alikuwa kwenye ‘kabati’
ndani. Kila nilipokuwa nina hitaji fulani, ninamwambia halafu nasahau. Kwa
hiyo, sikuwa na uhusiano naye ila tu ninapokuwa nina hitaji, ninamwomba. Hivyo,
huo ndio uliokuwa uhusiano wangu na Allah.
Kwa kweli, nilikuwa mtupu
ndani; hakuna amani, hakuna furaha kabisa! Japokuwa nililelewa kwenye familia
nzuri na yenye upendo, lakini ndani yangu nilikuwa mtupu, mwenye huzuni, mkavu kabisa!
Kilichonifanya nianze
kumjua Kristo ni mwujiza ulionitokea maishani mwangu. Mimba ya mwanangu wa
kwanza iliharibika. Kisha baadaye nilipata mtoto wa kwanza. Nilipata ujauzito
tena na baada ya miezi mitano, nilianza kutokwa damu, na nikampoteza tena mtoto
yule hospitalini.
Baada ya hapo, nilijawa na
huzuni sana. Nilimkarikia sana Mungu. Sikutaka kusikia chochote kuhusu Mungu;
kuhusu Allah, maana nilikuwa na huzuni kubwa sana!
Kwa hiyo, nilikuwa
nikilia, na hata nikaamua kujiua. Wakati huo sikutaka kuongea na mume wangu au
hata na mwanangu. Nilikuwa najifungia ndani na kulia sana kwa huzuni.
Miezi michache baadaye,
mume wangu, kwa kuwa aliona nilivyo na huzuni, alipendekeza kwamba tusafiri na
aninunulie zawadi ili kunifanya niwe na furaha. Lakini sikupata furaha.
Baada ya muda, nilipata
ujauzito tena. Baadaye nikaanza kutokwa damu tena. Wakati huo nilikutana na
mama mmoja Mkristo ambaye anamwamini Yesu. Alinihubiria Injili na akaniambia,
“Kwa nini usimwambie Mungu akuambie kweli?”
Nikasema, “Una maana
gani?”
Akasema, “Wewe mwombe tu
akuonyeshe ukweli.”
Kusema kweli,
nilishangazwa sana na pendekezo hilo aliloniambia. Nakumbuka usiku ule nilipiga
magoti pembeni mwa kitanda changu na kumlilia Mungu. Nikamwambia, “Nionyeshe
kweli. Wewe ni nani? Wewe ndiwe uliyeniumba. Unaweza kunionyesha kweli. Sitaki
kufuata tu dini yoyote. Maana hakuna anayeweza kubadili moyo wangu. Kama wewe
ni wa kweli, basi nionyeshe ile kweli.”
Na nakumbuka nililala na
niliamka usiku na damu zilizokuwa zikinitoka ziliacha kutoka! Na siku
iliyofuata nilienda kwa daktari. Alisema, “Kila kitu kiko sawa; mtoto yuko
vizuri kabisa. Ni muujiza! Sijui ni kitu gani kimekutokea!”
Nikasema, oh, oh. Kuna
jambo limetokea kwangu. Ilikuwa ni muujiza kwangu. Kwa mwingine inaweza isiwe
ni muujiza lakini kwangu ulikuwa ni muujiza maana nilimwomba Mungu
ajidhihirishe kwangu. Kwa hiyo, nilimpigia simu yule mama Mkristo. Ilikuwa ni
jumapili. Nikamwambia, imani yako ni ipi? Napenda kuisikia. Nilienda nyumbani
kwake. Alianza kunieleza juu ya Injili ya Yesu Kristo; kwamba alikuwa ni Mungu
katika mwili; ambaye alikuja na kufa kwa ajili yangu; kwa ajili ya dhambi zangu
na kila kitu. Alilipa gharama kwa ajili yangu.
Niliguswa sana. Nikasema, “Sina
Mungu wa namna hiyo. Mungu ninayemfahamu ni wa tofauti sana. Ninapenda nimjue
Mungu huyo aliyekufa kwa ajili yangu. Napenda aje moyoni mwangu. Je, nifanye
nini? Niende tu kanisani? Au nijue Biblia yote?”
Akasema, “Hapana.
Mkaribishe tu Yesu moyoni mwako nawe utakuwa huru, utaokoka na utaponywa.”
Nilishangaa sana na
nilijawa na furaha sana. Nikasema, “Aha! Nifanye nini sasa?”
Akasema, “Wewe omba pamoja
na mimi sala hii.”
Tuliomba sala fupi tu.
Nilimkaribisha Yesu moyoni mwangu. Na mara tu nilipomaliza kuomba, nilijisikia
furaha kubwa sana; amani kubwa sana ambayo sikuwa nimewahi kuwa nayo! Na tangu
wakati ule, maisha yangu yalibadilika kabisa.
Nimekuwa Mkristo kwa miaka
18 sasa. Yesu amebadili ufahamu wangu na kila kitu ndani yangu – uhusiano na mume
wangu, uhusiano na wanangu, uhusiano na marafiki zangu au hata na watu wengine.
Kila kitu ambacho nilikuwa napambana nacho, Yesu amebadili. Ni kwa sababu Yeye
ni Mungu na amekuja kwenye maisha yangu na kubadili kabisa moyo wangu.
Nilikuwa na kila kitu
maishani mwangu – mume mzuri, mtoto, wazazi wazuri, lakini ndani yangu sikuwa
na furaha! Na mara nilipomkaribisha Yesu moyoni, nilipata furaha kubwa sana.
Na nilipofika nyumbani,
nilikuwa naogopa kumweleza mume wangu juu ya jambo lile. Niliomba kwa wiki
mbili ili niweze kumweleza. Nilipokuja kumweleza mume wangu, nilikuwa ni mtu
niliyebadilika sana kiasi kwamba alifurahi sana. Hata yeye alikiri kuwa ndani
ya zile wiki mbili aliona mabadiliko makubwa.
Kabla ya hapo sikuwa na
furaha kabisa. Nilikuwa na kila kitu lakini sikuwa na furaha. Na binti yangu
nilimzaa salama, sikutokwa na damu tena. Na binti zangu wanampenda Kristo.
Siku moja nilikwenda
kwenye nyumba ya rafiki yangu na binti yao alikuwa na kansa. Ana miaka 22 na
wao ni Waislamu. Nikawaeleza kuhusiana na uponyaji na amani na furaha na kweli
ambayo wanaweza kuzionja.
Nilimweleza kuwa, Yesu
alisema, kama ukitaka kuujua mti, basi angalia matunda yake. Na nikasema, wakati
nilipokuwa kwa Allah, sikuwa na matunda yoyote. Sikuwa na furaha, hakuna amani,
hakuna upendo, hakuna kitu! Nilikuwa mtupu! Na nikawaambia kuwa wanaweza kuona
hata ndani yao ni hivyo hivyo – maana hata wao hawana kitu. Huo ndio ukweli.
Lakini sasa naweza
kuwaeleza kuwa, kwa kumkaribisha Yesu mioyoni; kwa kuikubali kweli, ile kweli inakuweka
huru. Kweli inakuponya na kukupa furaha – yote hayo yanaletwa na kweli maishani
mwako. Wewe pokea tu.
Nikasema, mimi nilikubali
na maisha yangu yakabadilika. Kwa nini na ninyi msipokee? Mkaribishe tu Yesu
moyoni na uone jinsi ilivyo rahisi. Huwa nawashirikisha watu Injili. Na mara
nyingi huwa naongea na Waislamu; na wengi wao unapowaeleza, kile wanachowaza ni
kuwa labda unataka kuwaambia wabadili dini yao.
Mara zote huwa nasema,
mimi siongelei kuhusu dini. Ninaongea kuhusiana na wokovu. Mungu anazungumza
kuhusiana na wokovu. Si kuhusiana na dini. Maana Muhammad au mtu mwingine
yeyote wanacholeta ni dini. Na Mungu hajaongea kuhusiana na dini. Yesu hakuwahi
kuongea kuhusu dini. Tunaongea kuhusiana na wokovu. Kweli ndiyo inayokuweka
huru.
**********************
Ndugu msomaji wa blog hii,
umemsikia na kumsoma Nadereh. Unawaza nini juu ya maisha yako? Unampenda Mungu
au unapenda dini?
Tafakari
Hoji
mambo
Chukua
hatua.
No comments:
Post a Comment