Yafuatayo ni mahojiano kati ya mtangazaji, Sid Roth na
Akef Tayem. Akef Tayem anatokea Palestina. Alikuwa ni Mwislamu lakini sasa
anamwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi wake. Pia anawapenda sana Wayahudi ambao
zamani aliwachukia kwa moyo wake wote. Je, nini kilitokea? Hakika Bwana Yesu
anahusika humo! Karibu ukutane na Bwana wa mabwana anayeweza kubadilisha maisha
yako kwa namna ya kushangaza.
……………
Sid
Roth:
Akef, hebu nieleze mtazamo wako ulivyokuwa kuhusiana na
Wayahudi wakati wa ujana wako.
Akef:
Nilikua huku nikiwa nawachukia Wayahudi, maana
walichukua ardhi yetu na kutuondoa kwenye makazi yetu. Baba yangu alikuwa amefanikiwa sana kule
Haifa, Israeli. Lakini alishindwa sasa
hata kuihudumia familia yake. Hivyo, niliwachukia Wayahudi.
Sid
Roth:
Familia yako ilihamia Cyprus na kuanza upya. Lakini
familia yenu ilikuwa ya watu imara sana, maana watoto wote waliweza kwenda
kusoma Marekani. Na ulipokuwa Marekani, ulikutana na msichana mzuri wa Kikristo
pale na akakueleza kuhusu Yesu. Hilo ni sawa, lakini jambo lililokuwa
linakusumbua ni masuala ya miujiza. Kwa nini miujiza?
Akef:
Ni kwa sababu suala lenyewe lilikuwa halileti mantiki.
Nilikuwa nikisomea Hisabati na Kemia; na unajua kwenye Uislamu, Muhammad hakuwahi
kufanya miujiza yoyote. Kwa hiyo, kwetu miujiza si jambo lenye nguvu sana.
Sid
Roth:
Msichana yule alikukaribisha kwenye mkutano wa injili.
Kwa nini ulienda?
Akef:
Nilienda kwa sababu niliamini kuwa huyo mhusika alikuwa
ni mhubiri wa uongo tu. Kimsingi nilikuwa siamini kuwa miujiza hutokea.
Sid
Roth:
Ulipofika pale, uliona nini? Uliwaza nini?
Akef:
Kilichovuta hisia zangu, ilikuwa zaidi ni kama shoo –
kuna magitaa pale, steji na watu wanamsifu Bwana …
Sid
Roth:
Kwani hawafanyi hivyo msikitini?
Akef:
Hapana. Hapana. Kwenye Uislamu zaidi ni kuonyesha
heshima, tunasujudu. Kwangu lilikuwa ni jambo geni kabisa. Lakini alipoanza
kuongea kuhusiana na miujiza, kulikuwa na mtu kwenye kiti cha magurudumu, na mhubiri
akasema angemwombea na angesimama.
Sid
Roth:
Kwa hiyo alimwombea na akasimama?
Akef:
Ndiyo.
Sid
Roth:
Kwa hiyo ulishuhudia muujiza?
Akef:
Sijui!
Sid
Roth:
Unamaanisha nini unaposema hujui?
Akef:
Nilijua hiyo ni sehemu ya ile shoo. Kisha alimwita
mwanamke aliyekuwa kipofu, akamwombea. Na mara akawa anaona. Kila kitu
kilionekana kama kimepangwa tu. Kimsingi mambo hayo hayakunigusa hata kidogo.
Kilichokuja kugusa moyo wangu, ilikuwa ni mtoto wa miaka kama 7 hivi. Na mtoto
huyu hakuwa mbali na nilikokaa. Na mguu wake mmoja ulikuwa mfupi kuliko
mwingine. Niliushuhudia maana walimpitisha karibu na nilikokaa. Mguu ulikuwa
umepinda na ni mfupi.
Na yule mhubiri alisema kuwa wampeleke kwenye jukwaa;
na kwamba angemwombea; na kwamba Mungu angemponya. Na cha ajabu, mhubiri huyo
alisema, “Wale ambao hamuamini kuhusu miujiza, njooni huku mtaona jambo.”
Nikaona kuwa hiyo ilikuwa ni fursa yangu. Niliruka na kwenda kwenye jukwaa.
Sid
Roth:
Ukaona nini sasa?
Akef:
Alimkalisha mtoto yule mbele yake kwenye kiti mbele
yangu. Kisha alishika mguu wa mtoto kwenye mikono yake. Na mimi nilisimama kwa
pembeni ili niweze kuona vizuri. Alipoanza kuomba, ‘Katika jina la Yesu,’ ule mguu ulianza kurefuka hadi ukafikia urefu
wa mguu mwingine, kisha ukakomea hapo. Na mwazoni mwangu nilikuwa nimewaza
labda ungepitiliza. Jambo hilo sikuwa na uwezo wa kulikana! Kisha ukawa kama
umejazwa hewa ‘puu’.
Sid
Roth:
Uliona haya kwa macho yako mwenyewe?
Akef:
Niliona kwa macho yangu kabisa! Na cha kushangaza,
mtoto yule alisimama na hakuweza kuukanyagia mguu ule sawasawa. Ilikuwa na kama
amepata mguu mpya. Ilibidi ajifunze kuutumia. Ilimchukua dakika chache
kung’amua kwamba kumbe anaweza kuukanyagia mguu ule. Na hatimaye akaanza
kukimbia. Hilo, sikuweza kulikana!
Sid
Roth:
Sasa, ukawa muumini wa Yesu Kristo. Familia yako
ilichukuliaje hilo?
Akef:
Oh, oh. Ilikuwa msukosuko. Walinikataa. Walimwambia
kaka yangu ambaye tulikuwa wanafunzi sote kunishawishi niachane na Ukristo.
Alijaribu mara kadhaa. Alisema, “Umefanya hili. Baba hajafurahia.” [Maana
alikuwa akigharamia mahitaji yangu yote]. “Unatakiwa urudi kwenye imani yetu.”
Lakini sikuweza kufanya hilo. Kwa hiyo walinikataa.
Sid
Roth:
Je, walikutemea mate?
Akef:
Unajua, hiyo ndiyo mila yetu. Inabidi wakutemee mate.
Hiyo ndiyo namna ya kukukataa.
Sid
Roth:
Kwa hiyo, ulikuwa kwenye msukosuko mkubwa.
Akef:
Ndiyo.
Sid
Roth:
Baba yake alimkataa. Akef hakuingia kwenye mfungo,
lakini alikosa kabisa hamu ya kula. Alikaa zaidi ya siku 40 bila kula chakula
zaidi tu ya kunywa maji. Kisha muujiza ulitokea kwake!!
……………………………
Ndugu msomaji, kuna mambo makubwa yaliyotokea kwa Akef
baada ya kupita kwenye kipindi hicho cha kutokula kwa siku hizo zote. Je, ni
mambo gani hayo?
Tafadhali fuatilia sehemu ya pili ya ushuhuda huu wenye
nguvu. Bwana Yesu ni halisi kama ambavyo Biblia inasema. Bofya HAPA.
..........................
Tafakari
Jiulize
Hoji
mambo
Chukua
hatua.
..........................
Bonus reading: click HERE.
No comments:
Post a Comment