Sunday, March 24, 2013

Juhudi za Kupinga Ukristo za Mwanaharakati wa Kundi la Ahmadiah Kutoka Pakistani Zamfanya Aachane na UislamuNusrat Aman alikuwa ni mwanaharakati wa kiislamu wa kundi la Ahmadiah kule Pakistani. Siku moja aliamua kuingia kanisani ili akamwulize mchungaji ni kwa nini hasa hataki kuwa mwislamu ilhali unabii wote umeshatimizwa ndani ya Muhammad? Nusrat aliishia kupata aibu, hasira na hatimaye wokovu …!


Je, ilikuwaje? Endelea kusoma ushuhuda wake wenye kichwa kisemacho "Kwa nini niliamua kuwa Mkristo?" ambao unafungua macho na mioyo kwa kuwa ni watu wengi walio katika kundi alimokuwa Nasrat hapo zamani.

Injili ya Barnaba - Beleshi Linalochota Waislamu na Kuwatupia Kwenye Shimo la KuzimuUlimwengu wa Kiislamu, kama kawaida yake, unatia juhudi kubwa sana katika kuuchafua Ukristo ili angalau uweze kuendelea kuwashikilia walio ndani yake; na pale inapowezekana, kuwadanganya Wakristo wasiojua Ukristo wala Uislamu.

Kuna mambo mawili makubwa ambayo huwa yananishangaza sana kuhusiana na masuala ya kiroho. Kwanza ni jinsi ambavyo wakuu wa dini wa Kanisa Katoliki wanavyotumia miaka na miaka kusomea dini na Biblia, kisha wanakuja kuishia kufundisha mambo yaliyo nje ya Biblia!!! Kwa mfano, wanawaambia waumini wao kuwa wafu wanatuombea kule mbinguni au kwamba unaweza kufanya misa huku duniani halafu ndugu yako aliyekufa akiwa na dhambi na, kwa ridhaa yake alikataa wokovu, eti atasamehewa dhambi na Mungu atamuingiza mbinguni!!!