Sunday, May 25, 2014

Je, Kanisa ni Kiti cha Enzi cha Shetani?
Biblia inasema: “Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani…” (Ufunuo 2:13)


Waislamu “WAHUBIRI WA BIBLIA”, kama kawaida ya “injili” yao potofu hawaachi kuzipotosha njia za Bwana zilizonyooka; lakini kama hawataki kutubu, hukumu yao inakimbia mbio kuwajilia. Wahubiri hawa hutumia andiko hilo hapo juu kuonyesha eti Kanisani ni mahali akaapo shetani, wakimaanisha kuwa Wakristo wote tunapoenda kuabudu Kanisa, basi tunakuwa kwa shetani!

Lakini andiko hili maana yake ni nini?

Sunday, May 18, 2014

Je, Wakristo Waliokufa Wakimwamini Yesu kama Mungu Wamepotea?
Kama kawaida ndugu zangu wa Kiislamu niwapendao sana wanazidi kuzama kwenye dimbwi la udanganyifu. Wananukuu kitabu cha Wakorintho na kusema KWA UJASIRI MKUBWA kwamba tumepotea kwa kumwamini Kristo.

Mungu Muumba wa mbingu na nchi anasema wazi kwenye Biblia kuwa:

“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.” (Hosea 4:6).


Andiko hili halisemi WANAANGAMIA kama ambavyo watu wengi hulitamka; bali linasema WANAANGAMIZWA.

Sunday, April 20, 2014

Je, Yesu Alitumwa kwa Israeli Peke Yake?
Waislamu “wanahubiri” kuwa Yesu  hakuja kwa ajili ya ulimwengu wote bali alikuja kwa ajili ya Wayahudi peke yao. Kisha wanasema kuwa Muhammad ndiye mtume sahihi kwa sababu huyo alikuja kwa ajili ya ulimwengu wote. Andiko wanalotumia kupinga utume wa Yesu kwa ulimwengu ni lile alilolisema Yesu wakati akiongea na mwanamke Mkananayo (yaani asiye Myahudi), ambaye alikuwa anaomba Yesu amponye mwanawe.

Imeandikwa:
Akajibu akasema,  Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:26).

Friday, April 18, 2014

Eti Wakristo Hula Mkate Wenye Mavi (au Mashonde)

Waislamu wanaojaribu kuitoa makosa Biblia bado wanaendelea na mahangaiko yao ya kujaribu kuipa uhalali quran kupitia upotoshaji mkubwa wa Maandiko ya Biblia. Kama kwaida, hawana hoja mpya wala za kufikirisha, bali ‘wana-recycle’ maswali yaleyale toka januari hadi desemba. Haya ni maswali ambayo yalibuniwa na watu fulanifulani, basi na wao wanayabeba bila hata ya kuchuja na kujua endapo yana ukweli au la. Hata hivyo, kila jambo wanalolisema kinyume na Biblia ni UONGO mtupu SIKU ZOTE - NA USHAHIDI WA UONGO HUO TUNAO WAZIWAZI!

Katika kitabu cha Ezakieli imeandikwa:

…. Nawe utakila kama mkate wa shayiri, nawe utakioka mbele ya macho yao juu ya mashonde yatokayo katika mwanadamu. (Eze 4:12).
[Maana ya mashonde ni kinyesi]

Monday, April 7, 2014

Je, Yesu alisema kuwa Yeye ni Mungu?
“Wahubiri wa injili” wa Kiislamu huwa wanapinga kuwa Yesu ni Mungu na unapowakatalia wanakwambia, “Lete andiko.” Maandiko yapo mengi sana ndani ya Biblia juu ya ukweli kwamba Yesu ni Mungu. Ni mengi mno!

Ukishawapa andiko, wanabadilika na kusema, “Nataka maneno aliyoongea Yesu mwenyewe.”

Hiki ni kigezo POTOFU na si cha kibiblia hata kidogo. Ukweli ni kwamba, Biblia YOTE ni Neno la Mungu. Haijalishi amezungumza Musa, Isaya, Yohana, Petro au Yesu mwenyewe. Imeandikwa:
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. (2Petro 1:21).


Hivyo, kudai kwao eti, “Nataka maneno aliyosema Yesu mwenyewe,” ni kigezo batili na kisicho na mantiki hata kidogo.

Wednesday, April 2, 2014

Eti Biblia inataja mashehe, kwa hiyo inaunga mkono Uislamu!
Wahubiri wa ‘injili’ wa Kiislamu wanaendelea kuhaha kuhalalisha quran kupitia Biblia. Nasema ‘kuhaha’ kwa sababu hakika kabisa wana juhudi kubwa mno lakini inasikitisha kwa sababu hakuna hata siku moja waliyowahi kusema jambo lenye ukweli kibiblia linalounga mkono quran kama wasemavyo wao – Mungu ni shahidi yangu. Mara waseme Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia; mara waseme Yesu aliposema kuwa ataletwa Msaidizi basi alimaanisha Muhammad, n.k. Ni kituko kimoja baada ya kingine. Na wanayemdanganya ni wao wenyewe pamoja na Wakristo wachache wasiojua Biblia.

Monday, March 31, 2014

"Sikuja kutangua torati" maana yake ni nini?
Bwana Yesu alisema: Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii, la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.(Mt. 5:17-18). Ni nini maana ya andiko hili?

Friday, March 28, 2014

Eti Mungu wa Biblia ni Kahaba Kulingana na Isaya 23:17-18
Kama kawaida yao, Waislamu wanaendelea kudanganywa na walimu wao na kujipa matumaini kuwa wako kwenye njia ya uzima kutokana na kile wanachoamini kuwa Biblia si Neno la Mungu bali Quran ndiyo Neno la Mungu.

Kwa sababu wanaonekana ni watu wasiokuwa na utayari wa kuchunguza kile wanachoambiwa, basi wanaamini kila uongo na udanganyifu wanaopewa na kuubeba kama ulivyo na kuutangaza kwa ujasiri kabisa kana kwamba ndiyo kweli halisi!

Thursday, March 27, 2014

Unabii wa Kifo cha Yesu Kupitia Ibrahimu na Isaka
Kuzaliwa na kufa kwa Bwana Yesu si jambo lililoibuka tu. Hili lilikuwa ni jambo ambalo tangu wakati wa kosa la Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni lilitolewa unabii na Mungu mwenyewe. Mungu alimwambia shetani:“nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” (mwanzo 3:15).

Hakuna mwanadamu anayeitwa uzao wa mwanamke. Uzao huwa unahesabiwa kwa manamume siku zote na duniani kote. Lakini ni Yesu peke yake ambaye hakuzaliwa na baba wa kibinadamu kama wanadamu wengine ndiyo maana anaitwa uzao wa mwanamke.

Wakati wa  Ibrahimu, Mungu alitoa tena unabii juu ya kufa, kufufuka na kulipa dhambi kwa Bwana Yesu. Unabii huu ulitolewa kupitia mtoto wa Ibrahimu, yaani Isaka. Je, ilikuwaje?

Tuesday, January 14, 2014

Eti Yesu Amelaaniwa Hawezi Kuokoa
Kwenye facebook kuna hoja nyingi zinazozungumziwa humo. Nikakutana na ndugu mmoja mwislamu anatoa hoja kwamba Yesu amelaaniwa, hivyo hana uwezo wa kuokoa mtu. Na anatoa kabisa maandiko ya Biblia, eti kuthibitisha hoja zake - si kwa kudhihaki, bali kwa kuamini kabisa kwamba hivyo ndivyo ilivyo! Na hivi ndivyo hali ilivyo kabisa kwa Waislamu linapokuja suala la kutafuta sababu za wao kuukataa wokovu wa Yesu Kristo.

Monday, January 6, 2014

Maswali yangu kwako Mwislamu
Tarehe 21 Desemba 2012 niliuliza maswali yafuatayo HAPA. Lakini umepita mwaka mzima bado sijapata jibu japo kwa swali hata mojawapo tu! Ina maana maswali haya hayana majibu kutoka kwenye Quran au labda ndugu zangu Waislamu hawajayaona? Of course mimi binafsi najua kuwa hawawezi kuyajibu kwa sababu Uislamu hauna majibu juu ya masuala ya rohoni.

Hata hivyo, ningependa niyaulize kwa mara nyingine tena hapa tunapoanza mwaka huu wa 2014 ili iwe changamoto kwa Mwislamu uwaye yote – ujihoji, ujiulize na ujipime kule uendako.