Friday, July 5, 2013

Je, Biblia Ina Vitabu Vingapi?




Vitabu 73 au 66?
Leo duniani kuna Biblia yenye vitabu 73 na yenye vitabu 66. Waislamu wamekuwa wakitumia suala hili kama silaha ya kushambulia Biblia kwamba ni kitabu kisichoaminika, wala hakiwezi kumfikisha mtu mbinguni.

Kwa mfano, ndugu yangu Ibra ambaye amekuwa msomaji na mchangiaji mzuri sana wa blog hii ameniuliza kama ifuatavyo:
James, naomba majibu kwa maswali yafuatayo:
-Biblia original kabisa iliyoandikwa na roho mtakatifu ina vitabuvingapi?
-Kitabu cha Danieli kina sura 12 au 14?
-Biblia yenye vitabu 73 na ile ya 66 ipi ya kweli? Je! Hapa kuna mkono wa roho mtakatifu au ubinadamu?
Ukweli unabaki palepale kwamba biblia sio kitabu cha kutegemea sana kwa mambo ya mungu. Hapa duniani biblia ninazojua mimi ziko zaidi ya tano. Na zote zimepishana kwa namba ya vitabu vilivyopo.
Sasa hapo mimi nabaki nashangaa, niamini biblia gani kati ya hizi? Ubabaishaji, kweli haimo.
Tafakari. Jihoji. Kweli imo ndani yako! Soma Qur'ani tukufu.