Jina
langu ni Tahir na hii ni safari yangu kutoka kwenye Uislamu hadi kwenye Ukristo.
Mara
baada ya kufika Marekani nikitokea Palestina miaka 14 iliyopita, nilimwoa
msichana mzuri wa Kikristo. Msichana huyu alijaribu kuwa Mwislamu ili
kunifurahisha mimi, lakini kadiri alivyojitahidi kufanya hivyo, ndivyo
nilivyozidi kuwa mbali naye. Tulizaa mtoto mmoja, lakini ndoa yetu haikudumu
maana ni vigumu sana kupenda wakati moyo wako umejaa chuki. Chuki ndicho kitu
ambacho nilifundishwa wakati wa kukua kwangu kule Palestina – chuki dhidi ya
Wayahudi, Wakristo na hata dunia nzima. Ukiwa kama Mpalestina, unafundishwa
tangu ziku ya kwanza kwamba dunia yote ndiyo inayohusika na mateso yetu, na
hasa Wayahudi na Wakristo.
Baada
ya kuachana, baadaye mke wangu huyo wa zamani alikuja kuniambia kuwa amembatiza
mwanangu. Nilikasirika mno kiasi kwamba nilienda kuingia moja kwa moja kanisani,
nikamtukana mchungaji aliyefanya ubatizo ule, na nikamwambia kuwa angeenda
jehanamu kwa sababu ya kitendo kile. Sikutaka kabisa mwanangu akue akiwa
Mkristo!. Matokeo yake nilipigwa marufuku na mahakama kumtembelea mwanangu
maana mke wangu alihofia kuwa ningeweza kuja kumteka mwanangu na kumpeleka
Palestina. Hivi sasa sipati nafasi ya kumuona mara kwa mara.