Allah
alitokea wapi?
Uislamu unajinadi kwamba
Allah ndiye Mungu yuleyule aliyejishughulisha ya Wayahudi tokea nyakati za Ibrahimu
katika Agano la Kale. Je, jambo hilo ni kweli?
Uislamu ulianza na
Muhammad kwenye miaka 600 baada Kristo. Je, kabla yake imani za Waarabu
zilikuwaje? Je, yako mambo yoyote kutoka kwenye imani hizo ambayo yaliingia
kwenye Uislamu? Kwa maneno mengine, je, Uislamu hauna upagani ndani yake?
Fuatana nami kwenye makala
haya marefu yanayochambua chimbuko la Uislamu ili tuweze kuona iwapo upo uhusiano
wowote kati ya Uislamu na upagani uliokuwa ukitawala miongoni mwa jamii za Waarabu
kabla ya kutokea kwa Muhammad?