Sunday, April 21, 2013

Mamilioni ya Waislamu Afrika Wanamkimbilia Yesu Kristo Isivyo Kawaida

 “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika 
ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa 
yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja” 
(Mathayo 24:14).

Ukisoma kurasa mbalimbali za kwenye mtandao juu ya kukua kwa dini ya Kiislamu, utakuta wengi wanasema kwamba Uislamu ni dini inayokua kwa kasi sana. Je, hilo ni kweli? Ni jambo gani linaloonyesha ukweli wa hoja hiyo?

Lakini tunao ushahidi wa Neno la Kristo kwamba siku za mwisho (yaani hizi tulizo nao), Injili itahubiriwa ulimwenguni kote. Pia, Mungu Yehova anaahidi kuwa hizi ni siku za kumwaga Roho wake kwa wanadamu wote. Hakika hizi ni nyakati za Injili ya Yesu Kristo kusonga mbele na kushinda na kubomoa kila upinzani na ukuta uliojengwa na adui ili kuwazuia wanadamu kumjua Mungu wa kweli na Mwokozi pekee, Yesu Kristo.

Je, Mtume Muhammad Yuko Wapi Hivi Leo?


Mungu hutufunulia mambo mbalimbali kupitia watumishi wake mbalimbali ili kutujulisha yale yaliyopo na hata yajayo; katika ulimwengu huu na pia ule ujao. Wapo watu wengi ambao Mungu amewatumia kutufahamisha juu ya mbingu na hata juu ya kuzimu.

Bo Ra Choi ni mchungaji kutoka Korea ya Kusini. Mchungaji huyu amekuwa akionyeshwa maono mbalimbali na Mungu kuhusu mambo ya ulimwengu wa roho. Mojawapo ya maono aliyoonyeshwa yanamhusu Muhammad, mtume wa Uislamu.

Je, Muhammad yuko wapi hivi leo? Katika video hii, mchungaji Bo Ra Choi anafikisha kwetu ujumbe kwa namna ambavyo alisikizishwa Muhammad akisema kule aliko sasa.

Kwa maana nyingine, ananukuu moja kwa moja maneno ya Muhammad ili kwamba iwe ni kama vile tunamsikia Muhammad akizungumza.

Tafadhali zikiliza kwa makini video hii, kisha utaupata ujumbe wa Mungu anaouleta kwetu kupitia mtumishi wake, Mchungaji Bo Ra Choi.

........................

Lakini anachosema Muhammad humo ni nini hasa?
 Kifuatacho ndicho anachokisema Muhammad humo
kwa kilio kikubwa:
...........................
Mnajua mimi ni naniiiiiii?
Mimi ni Muhammad
Nilitenda dhambi kubwa sana
Nilifanya makosa makubwa mno
Nilikuwa mjinga
Nimetenda dhambi kubwa sana
Watu wengi sana wamekuwa wakitumbukia kuzimu kwa sababu yangu.
Nilitenda uhalifu mkubwa kuliko wote
Nilitenda dhambi kubwa kuliko zote
Nilitenda makosa
Nilitenda makosa
Yesu, nilifanya makosa.
Nilifanya hivyo kwa sababu nilikuwa maskini sana.
Nilitaka kuwa kiongozi wa watu wengi na nilitaka kuwa kama Yesu.
Nilifanya uhalifu mwingi sana wa kiovu
Niliua watu wengi sana
Msijikusanye pamoja
Mtakufa kama mkikusanyika kwa ajili yangu, Muhammad.
Tawanyikeni! Msijikusanye pamoja!
Kama mkijikusanya pamoja, shetani atawatumia!
Shetani atawatumia zaidi kama mkikusanyika kwa ajili ya Muhammad.
Bila ya Yesu, wote wanaishia kuzimu
Kuna joto kali!
Kuna joto kali!
Kuna joto kali!
Nitoe humu!
Nitoe humu!
Hakuna pepo ambayo mnaifikiria.
Kuna mbinguni na kuzimu tu.
Mafundisho hayo yamesambazwa kwa uongo. 
Uislamu umebadilishwa.
Haiwezekani!
Msipoteze maisha yenu namna hiyo.
Hakuna pepo ambayo Waislamu wanaiamini.
Mimi sikuzungumza juu ya mafundisho hayo ya uongo.
Yamebadilishwa.
Someni Biblia.
Inaonyesha namna ya kwenda mbinguni.
Hakuna mbingu katika Uislamu.
Mimi sikuandika theolojia hizo za uongo.
Mambo hayo yaliandikwa na watu waliokuwa wakijaribu kuniiga mimi.
Mambo hayo yamekuwa ni Biblia ya Uislamu ambayo inadhoofisha neno la Yesu.
Haiwezekani!
Sikuyaandika hayo!
Tafadhali, nisikilizeni!
Niko hapa kuzimu.
Niko hapa kwenye moto wa kuzimu.
Ninateseka kwa adhabu hii kubwa sana kwa sababu shetani alinitumia.
Msitupe maisha yenu kwa shetani!
Msiwe watii kwangu mimi, Muhammad.
Hiyo ni njia ya kwenda kuzimu.
Shetani atawatumia.
Tokeni humo kwenye Uislamu.
Mimi sikutaka haya.
Nilitaka tu kuwa mtawala wa taifa.
Lakini mambo yalienda vingine.
Hiki sicho nitakacho.
Sitaki vita.
Nilianzisha mapigano mengi ili kuunda taifa langu mwenyewe.
Mnajua ni kwa nini?
Ni kwa sababu nilikuwa maskini sana nilipokuwa mtoto.
Nilianzisha vita nyingi sana ili kuunda taifa langu.
Nilitaka tu kuongeza nguvu zangu ili kushinda vita.
Kwa nini Uislamu umebadilika hivyo?
Kama kweli mnataka kuwa watii kwangu,
Tawanyikeni na msiwasikilize viongozi wenu (wa dini).
Wanawaongoza kuelekea kwenye njia mbaya sana.
Wanaharibu maisha ya watu.

…………………………………….

Tafakari

Pima mambo

Chukua hatua
 

Friday, April 5, 2013

Upande Mwingine wa Maisha Katika Nchi za Kiislamu
Hii si video ya kidini. Haielezei Ukristo wala Uislamu. Lakini ni video inayoonyesha maisha ya watu wa Irani ambayo ni nchi ya Kiislamu. Kwa jinsi ambavyo Uislamu unajinadi mbele ya ulimwengu, mtu ungefikiria kwamba watu wa nchi kama hizo wana furaha na utawala wa kidini wa nchi zao. Lakini je, hivyo ndivyo ilivyo?

Thursday, April 4, 2013

Ndoto Yamfanya Al-Haji Mohammed Ampokee Yesu
Al-Haji Mohammed Ahmed alikulia kwenye familia ya Kiislamu. Anaitwa al-Haji kwa sababu alishaenda Makka kuhiji.


Mohammed anasema:”Maishani mwangu mwote nilikuwa Mwislamu thabiti sana. Katika familia yangu, lengo letu kuu lilikuwa kujenga misikiti na kueneza Uislamu kila mahali.”