Historia ni kama ghala kubwa ambamo
kumehifadhiwa kila kitu. Tunapochungulia kwenye ghala hili, tunaweza kujifunza
kuhusiana na wapi tumetokea, na hatimaye wapi tuliko na kule tunakoelekea.
Bila shaka Biblia na Quran ni vitabu
viwili ambavyo vina umuhimu mkubwa sana kwa wanadamu na ulimwengu. Hivi ni
vitabu ambavyo ndivyo vinavyoumba maisha halisi ya idadi kubwa sana ya watu.
Haya si tu maisha ya kula, kunywa na kuvaa hapa duniani, lakini pia vinaaminika
kuwa vimebeba hatima ya milele yote kuhisiana na kila mwanadamu.
