Ishmaeli na mama yake (Hajiri)
wanafukuzwa nyumbani kwa Ibrahimu
Katika makala yangu yenye kichwa
kisemacho: Je, Muhammad Ametabiriwa Kwenye
Biblia? – Sehemu ya II, ndugu yangu Ibra amenipa changamoto kadha wa kadha
ambazo naziheshimu na nimezitafakari vizuri. Unaweza kuzisoma kwa ukamilifu
wake kwenye sehemu ya ‘comments’ mwisho kabisa wa makala yaliyo hapa.
Mjadala wangu na Ibra
unatokana na hoja yake kwamba Muhammad
alitumwa kwa watu wote lakini,
Ibra anasema, Yesu alitumwa kwa ajili ya
wana wa Israeli tu, kitu ambacho mimi nimemweleza kuwa si kweli kwamba Yesu
alitumwa kwa Israeli tu. Hoja zake na majibu yangu viko kwenye sehemu ya hiyohiyo ya maoni
(comments) mwishoni mwa makala yaliyo
hapa.
Lakini nimeona ni vema
nitoe majibu ya changamoto hizo kama makala kamili kwa ajili ya faida ya wengi,
maana maswali haya yanajirudiarudia tena na tena kutoka kwa ndugu zangu
Waislamu walio wengi.
Ibra umeanza kwa kunionya
kwamba niache tabia ya kuwa nabii wa uongo maana Mungu hapendi na ni mkali sana
juu ya upotoshaji wa Neno lake. Ninashukuru kwa hilo rafiki yangu Ibra. Ni kweli
kabisa Neno la Mungu si la kuchezea hata kidogo. Ukilipindisha utakutana na
mapigo makubwa mno maana si tu kwamba unasema uongo, bali pia unasababisha watu
wa Mungu waishie jehanamu ya milele kutokana na uongo huo. Mungu hawezi kuwa
radhi na tabia hiyo. Kwa hiyo, Ibra, ninakubali maonyo yako; lakini hadi sasa,
ninapoangalia, sijadanganya mahali kokote katika yale niliyokwisha kuyasema. Yote
ni mambo ambayo yana ushahidi wa kimaandiko juu ya ukweli wake.
Vilevile, Ibra umesema
kuwa unashindwa kuelewa ni kwa nini mimi ni mgumu wa kuelewa maandiko, na pia
ninayatafsiri kama ninavyotaka mimi. Ukaniuliza, “Kwa nini lakini unapingana na
Mungu? Maandiko yako wazi kabisa we unamn'gan'gania Isaka kivipi? Mungu atafanya
agano lake imara na la milele kwa Isaka kwa ajili ya uzao wake. Sasa hapo
wewe unahusika kivipi hapo? We ni uzao wa Isaka?
Majibu
yangu:
Najua Ibra, hapa unalenga
kwenye maneno uzao wake. Unachomaanisha
ni kwamba, mbona mimi ni Mswahili wa mbali huku? Je, ninahusika vipi na andiko
hili wakati mimi si Myahudi?
Ibra, napenda nikujulishe
wewe pamoja na wengine kuwa mimi ni uzao wa Isaka kabisa! Tena si mimi tu, bali
hata wewe ni lazima uwe uzao wa
Isaka, kama una nia ya kuingia mbinguni. Haya si maneno au mawazo yangu, bali
ni maagizo ya Muumba wetu.
Kila mara nimekuwa
nikisisitiza jambo hili ambalo namwomba Roho Mtakatifu aweze kuwafunulia ndugu
zangu Waislamu ili muweze kutoka kwenye kifungo kilichowafunga.
Wapendwa wangu, mnajua
kabisa kwamba Mungu ni roho, mbingu ni mahali pa kiroho, na hivyo hata ujumbe
wa Mungu ni wa kiroho. Lakini mara zote ninyi mnaishia kuona mambo kimwili. Hapo
ndipo mnakopigwa chenga kubwa sana inayowagharimu uzima wa milele.
Maandiko yanasema hivi: Kilichozaliwa
kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. (Yohana 3:6). Ukiishia kuwaza kwamba
Mungu alipotumia neno ‘uzao’ alimaanisha kuzaliwa kimwili, basi ni lazima
utakwama tu. Mambo ya mwili ni ya hapa duniani. Lakini mambo ya Mungu si ya
hapa duniani. Ni mambo ya mbinguni ambayo ni ya kiroho.
Sasa mimi ni wa uzao wa
Isaka kwa vipi? Hebu soma andiko lifuatalo:
Maana yeye si Myahudi
aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;
bali yeye ni Myahudi
aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko;
ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu. (Warumi 2:28-29).
Hii ina maana kuwa kuna Wayahudi wa
aina mbili: wale wa nje na wale wa ndani. Myahudi wa nje ni yule anayezaliwa
kimwili; ni damu kabisa ya Isaka. Lakini Myahudi wa ndani ni yule wa rohoni. Anayezaliwa
na Roho Mtakatifu kupitia Neno la Kristo, yaani kupitia kuiamini Injili.
Hilo ndilo linalonifanya mimi, wewe
na mwingine kuwa uzao wa Isaka. Na ndiyo maana basi, Mungu akamwambia Ibrahimu
kwamba:
Ibrahimu atakuwa
taifa kuu, hodari, na katika yeye
mataifa yote ya dunia watabarikiwa? (Mwanzo 18:18).
nami nitakufanya wewe
kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami
nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. (Mwanzo 12:2-3).
na katika uzao wako mataifa yote ya dunia
watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu. (Mwanzo 22:18).
Hebu niambie, Ibra, mataifa yote
yanaingiaje ndani ya baraka za Ibrahimu wakati (kwa mtazamo wako) hajawazaa
yeye?
Na ni kwa vipi basi Mungu alimwambia
Ibrahimu kwamba: Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe
utakuwa baba wa mataifa mengi (Mwanzo 17:4)?i
Ubaba wake unakujaje? Kwani alituzaa
sote kimwili kama unavyojaribu kutafsiti neno ‘uzao’? Bila shaka hapana.
Ibrahimu ni baba yetu kwa njia nyingine tofauti na uzazi wa kimwili. Ni watoto
wake kwa njia ya kiroho. Na kama ni watoto wake, basi sisi ni uzao wake; na ni
uzao wa Isaka pia.
Na kama ni uzao wake, basi tunarithi
baraka zake alizoahidiwa na Mungu. Na huo uzao wa Ibrahimu na Isaka, ndio ambao
Yesu Kristo aliujia. Maana Yesu anasema: Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba
ya Israeli.
(Mathayo 15:24).
Kila anayekataa kuingia kwenye uzao
wa Isaka, hana nafasi katika mbingu za Mungu aliyeumba mbingu na nchi. Hana! Hana!
Hana!
*****************
Ibra amenukuu Biblia
katika Mwanzo 16:12 inayosema:
Mkono wake (yaani wa Ishmaeli) utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote.
Kisha Ibra akaniambia, “Tafsiri
basi na aya hiyo. Mungu anamaanisha nini hapo?”
Ibra, nadhani andiko hili
liko wazi kabisa. Na pia linaonyesha jinsi Biblia ilivyo kweli ni Neno la Mungu
aliye hai. Hebu fikiria mwenyewe, andiko hili limeandikwa takriban miaka 1400 kabla ya Kristo.
Biblia inapoongelea Ishmaeli
hapa, inaongelea uzao wake. Na wewe unajua uzao wa Ishameli ni nani – ni Waarabu
kimsingi. Na unajua nini kinachoendelea leo.
Muhammad alitokea miaka
600 baada ya Kristo. Hiyo kusema, alikuja miaka 2000 baada ya andiko hili. Na kuanzia
pale ndipo uhalisia na utimilifu wa andiko hili ulipokuwa wazi.
Je, si kweli kwamba uzao
wa Ishmaeli (Waarabu/Waislamu) wako kinyume na dunia yote kiasi kwamba wako
tayari hata kuua kwa jina la dini na la Mungu? Je, si kweli kwamba uzao huu
unamwona kila asiyekubaliana na wao kuwa ni kafiri na adui? Na je, si kweli kuwa,
kutokana na kwamba kile wanachojaribu kufundisha hakifundishiki na
hakikubaliani hata na asili ya mwanadamu, matokeo yake inabidi wakilazimishe kwa
nguvu? Na je, si kweli kwamba dunia nayo haikubaliani na hilo? Unaona sasa,
Ibra, jinsi Biblia ilivyo Neno hai na la kweli la Mungu?
*****************
Ibra
anasema:
Ndugu yangu maagano ya Mungu
(sio ya shetani kama ulivyodai) yapo mawili: la Isaka kwa ajili ya uzao wake na Ishmaeli kwa ajili ya watu wote ambalo, amerithi kutoka kwa
baba.
Anachodai Ibra ni kuwa,
Isaka (na hatimaye Yesu, walikuwa ni kwa ajili ya Israeli tu. Lakini Ishmaeli
(na hatimaye Muhammad), walikuwa ni kwa ajili ya ulimwengu wote. Kwa hiyo, Ibra
ametoa nukuu kadhaa za Biblia ili kuthibitisha hoja yake kama ifuatavyo:
Mwanzo 15:4. Nalo neno la
Bwana likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako
ndiye atakayekurithi.
Ishmaeli ni mtoto wa kiuno
na Isaka ni mtoto wa ahadi. Kwa hiyo mrithi atatoka katika viuno.
Jibu langu:
Inaonekana rafiki yangu
Ibra, wewe unafikiri kuwa andiko hili linamhusu Ishmaeli. Si hivyo. Hili linamhusu
Isaka.
Lakini kabla hatujaangalia maana halisi ya andiko hili,
hebu tuangalie kwanza muktadha uliozaa andiko lenyewe. Imeandikwa kwamba:
Baada ya mambo hayo
neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni
ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.
Abramu akasema, Ee
Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki
nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski?
Abramu akasema,
Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.
Nalo neno la Bwana
likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye
atakayekurithi.
(Mwanzo 15:1-4).
Hapa Ibrahimu alikuwa anamwambia
Mungu kuwa, kwa kuwa hajapata mtoto na ameshakuwa mzee, basi wale waliozaliwa
nyumbani kwake, (yaani wasio damu yake – watoto wa watumishi na wajakazi wake,
maana alikuwa nao wengi), hao ndio angelazimika kuwaachia urithi wake.
Ndipo Mungu akampa majibu hayo hapo
juu.
Lakini najua kuwa Ibra utasema, “Sasa
aliyetoka kwenye viuno vya Ibrahimu na anayetakiwa kuwa mrithi wa baraka na
kila kitu si ni Ishmaeli?”
Hata Ibrahimu naye aliwaza kwamba ni hivyo. Baada ya
Ishmaeli kuzaliwa, na kabla Isaka hajazaliwa, imeandikwa kwamba: ''Ibrahimu
akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako.
Lakini Mungu akasema: Sivyo, lakini Sara mkeo
atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano
langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.
(Mwanzo 17:18-20).
Kwa hiyo, agano la milele kati ya
Mungu na Ibrahimu halikumhusisha Ishmaeli hata kidogo japokuwa alikuwa naye ni
mwana wa Ibrahimu. Kwa maana hiyo, halimhusu
Muhammad. Agano linatoka kwa Mungu –
Ibrahimu – Isaka – Yakobo – Yesu. Si
Ishmaeli wala Muhammad!
Maana yake ni nini? Maana yake ni kuwa mwanadamu yeyote akitaka kuingia kwenye
agano la kulindwa, kubarikiwa, kuponywa na kupata uzima wa milele, ni lazima apitie upande wa Isaka na kamwe si upande wa Ishmaeli.
*******************
Ibra ameniuliza:
Sasa basi, Ishmaeli
anarithi nini kutoka kwa baba?
Jibu
langu:
Kulingana na maandiko,
Ishmaeli hana urithi wowote kutoka kwa Ibrahimu. Imeandikwa kwamba:
Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa
maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. (Wagalatia 4:30). Ishmaeli
alikuwa mwana wa mjakazi, yaani Hajiri; na Isaka alikuwa mwana wa mwungwana,
yaani Sara.
Ibra umenukuu
maandiko yafuatayo:
Mwanzo
17:2-4. Nami
nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.
Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema,
Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi.
Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema,
Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi.
Mwanzo 12:2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka.
Mwanzo
17:20. Na
kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami
nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe
taifa kuu.
Wagalatia 4:21-25. Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria?
Wagalatia 4:21-25. Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria?
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana.
Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi.
Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.
Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto.
Ibra
anamalizia kwa kuniuliza, “Hapo napo inahitaji chuo?”
Jibu
langu:
Asante sana Ibra kwa
changamoto hizi. Ni wazi kwamba maandiko yote haya yanazidi kuonyesha jambo lilelile
kwamba baraka na urithi wa kiroho unaweza kutufikia tu kupitia Isaka na si
kupitia Ishmaeli.
Kwa upande wa Ishmaeli,
alichopata tu kutoka kwa Mungu ni kuwa taifa kubwa. Na hili liko wazi hata
sasa. Waarabu na hatimaye Waislamu ni jeshi kubwa kabisa. Lakini hapo ndio
mwisho wa ahadi na baraka za Mungu.
Lakini kwa kuwa shina la
yote ni Ibrahimu, tumeona katika Wagalatia 4:30 hapo juu kuwa, ahadi ya Mungu
kwa Ibrahimu hakupewa mwana wa mjakazi. Badala yake, huyo alifukuzwa. Kwa hiyo,
hana baraka hasa ile ambayo Mungu alisema kuwa hata mataifa yote watajibarikia.
Lakini nashangaa Ibra
huogopi kunukuu Wagalatia 4:21-25!
Hebu itazame nukuu hiyo
tena kwa makini:
Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria,
je! Hamwisikii sheria?
Je, Ibra, andiko hili linawasifu
au linawakemea wanaotaka kuwa chini ya sheria? Ni wazi kuwa linawakemea. Mwandishi
anawashangaa watu hawa ambao wanaacha kukumbatia uhuru badala yake wanakimbilia
kujiweka chini ya kongwa la sheria.
Sasa, ni nani anayetaka
kuwa chini ya sheria leo? Je, si wewe Ibra na Waislamu wenzako? Mnataka kuwa chini ya sheria ambazo mnajua fika kuwa ninyi
wenyewe hamjawahi kuzitimiza hata siku moja. Ndipo sasa anawauliza, kwa nini
mnataka kuwa chini ya utumwa badala ya kuwa huru? Hebu tuendelee kulisoma
andiko hilo:
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi.
Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.
Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto.
Ishmaeli na Isaka ni wana
wa baba mmoja. Lakini pia kati wao Mungu ametupatia mfano. Ishmaeli alizaliwa
kimwili. Yaani ni mtoto tu kama watoto wengine.
Lakini Isaka alitokana na
ahadi ya Mungu mwenyewe. Maana mama yake (Sara) alikuwa tasa. Hivyo,
kibinadamu, au kimwili, hakuwa kabisa na uwezo wa kuzaa. Kuzaliwa kwake ilikuwa
tu ni kwa mwujiza wa Mungu, kwa sababu Mungu alishatoa ahadi kwa Ibrahimu.
Ni kwa vipi basi mambo
haya ni mfano? Kwenye Mlima Sinai ndiko Musa alikopokea torati. Na Yerusalemu
ndiko Bwana Yesu alikoleta Injili.
Ishmaeli ni ishara ya
utumwa na kukataliwa, licha ya kwamba kwa kawaida mtoto wa kwanza ndiye
aliyekuwa na haki ya kuwa mrithi wa baba yake. Vivyo hivyo, torati ni sheria
ambazo kazi yake pekee ni
kumwonyesha mwanadamu jinsi ambavyo amepungukiwa mbele za Mungu. Na mwanadamu yeyote
anayejidanganya kuwa anaweza kutimiza sheria
yote ya Mungu, huyo yuko chini ya utumwa na laana na kukataliwa – maana hakuna
mwanadamu anayeweza kutimiza sheria yote
ya Mungu kwa ukamilifu wote – hata wewe Ibra ni shahidi katika maisha yako
mwenyewe.
Isaka ni ishara ya uhuru
na kukubaliwa. Vivyo hivyo, Injili ya Yesu Kristo ni habari njema inayotangaza
kusamehewa dhambi na kukubaliwa na Mungu kwa sababu yuko mmoja ambaye alibeba
dhambi zetu, ili kwa kumwamini tu, sisi, japo hatustahili mbingu kutokana na
dhambi zetu, tuweze kusamehewa bure.
Na kwa msingi huu, yeyote
anayekumbatia Quran, (ambayo asili yake ni Ishmaeli au Uarabuni), anakumbatia
utumwa na kukataliwa na Mungu. Lakini yule anayekubali Biblia (ambayo asili
yake ni Isaka au Yerusalemu), anakumbatia uhuru na kukubaliwa na Mungu.
Tafakari.
Jihoji.
Jipime.
Chukua
hatua.
****************
Mwisho ndugu yangu Ibra na
Waislamu wengine, naomba majibu ya maswali yaliyoko hapa.
Mr.James
ReplyDeleteMimi sijui wewe umekwama wapi. Nimekuonya mara ya kwanza juu ya kutaka kwako kuyapindisha aya za mungu.
MITHALI 30:5-6 ''Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.
6 Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.''
Mr.James pamoja na biblia kuwa na utata mwingi, swala la Ibrahim linaeleweka vizuri. Hapa ndipo penye msingi wa imani.
Ni kweli kabisa kwamba, Ishmaeli na mama yake walifukuzwa nyumbani kwa Ibrahim. Aliyowafukuza ni Sara, sio Ibrahim, baada ya yeye(Sara) kupata mtoto ambaye ni Isaka, ili mali za nyumbani arithi Isaka peke yake (Mwanzo 21: 9 Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka.
10 Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.
11 Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe. )
Mungu kwa kuepusha shari, kwa mambo kama haya ya kibinadamu, akamwambia Ibrahim akubaliane na matakwa ya Sara.
14 Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.
Sasa je! baada ya kutengwa na Sara, mungu na Ibrahim waliwatenga (Hajiri na mtoto wake)?
Neno la mungu linasema hapana, hawajatengwa.
Mwanzo 21:13 Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako.
Mwanzo 21:15 Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja.
16 Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia.
17 Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.
18 Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.
19 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
20 Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
Maandiko ya wazi kabisa, mungu akawa pamoja na huyo kijana.
19 Basi Ibrahimu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Ibrahimu akakaa huko Beer-sheba.
Kwa maana hiyo Ibrahim yupo beer-sheba aliko Ishmaeli.
KWA HIYO ISHMAELI NA MAMA YAKE WAMEFUKUZWA NA SARA NYUMBANI KWA IBRAHIM KWA SHINIKIZO LA SARA. SIO MUNGU WALA IBRAHIM. AHADI YA MUNGU IPO PALEPALE YA KUMFANYA ISHMAELI KUWA TAIFA KUU KAMA BABA YAKE IBRAHIM. MTOTO HUYU, ANARITHI BARAKA ZA BABA YAKE.
Mwanzo 18:18 AKIWA IBRAHIM ATAKUWA TAIFA KUU, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa?
Mwanzo 17:20 Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, NAMI NITANFANYA AWE TAIFA KUU.
Mwanzo 16:12 Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote.
KWA AYA HII, YEYOTE YULE ANAEJIJUWA KWAMBA NI MTU INAMHUSU, NDUGU( ISAKA NA WENGINE), INAWAHUSU PIA. NDIO MAANA YA TAIFA KUU. HAPA NDIO CENTER WA IMANI ZOTE, MWISHO WA IMANI. HAPA HACHAGULIWI MTU, WOTE NI SAWA KATIKA KUMWABUDU MUNGU.
Ndugu Ibra, Mungu akubariki kwa jitihada zako na shauku yako ya kutaka kuhakikisha kwamba KWELI ya Mungu inapewa kipaumbele. Kwa kuwa hoja zako za kumtetea Ishmaeli zinatokana na Biblia (na si Quran), basi ni vizuri, kama ulivyoanza kuiamini Biblia katika aya hizi, uamini Biblia yote.
DeleteNasema hivi kwa sababu, anayezungumza katika kitabu cha Mwanzo ndiye huyohuyo anayezungumza katika vitabu vyote – hadi kitabu cha Ufunuo. Maana yake ni kuwa, tunapoongelea aya YOYOTE katika Biblia, NI LAZIMA kuitazama katika muktadha wa Biblia nzima. Hadi hapa nimeshakupatia ushahidi unaoonyesha kuwa Ishmaeli hayupo kwenye urithi wa baraka za Ibrahimu ambazo Mungu alimuahidi Ibrahimu.
Safari hii umesema kuwa aliyemfukuza Hajiri hakuwa Ibrahimu wala Mungu, bali ni Sara. Pia unasema kwamba, “Mungu kwa kuepusha shari, kwa mambo kama haya ya kibinadamu, akamwambia Ibrahim akubaliane na matakwa ya Sara.”
Ibra, kusema kwamba Mungu alikuwa anaepusha shari, hayo ni maneno yako mwenyewe wala hakuna sehemu yoyote kwenye Biblia ambapo Mungu anasema hivyo. Lakini badala yake nilikuonyesha sababu ya kufukuzwa kwa Hajiri. Ngoja niirudie tena hapa. Ibrahimu alitaka Ishmaeli arithi baraka ambazo Mungu alimuahidi. Tunasoma kwamba: ''Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako.”
Lakini ni lipi lilikuwa jibu la Mungu? Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake. (Mwanzo 17:18-20).
Nirudie kusema tena kwamba, Ishmaeli hayupo kwenye ramani ya kiroho ya ukombozi wa mwanadamu. Si kwamba alikuwa mtu mbaya, hapana. Ila tu lile agano LA MILELE (yaani linalovuka maisha haya ya duniani), linapatikana upande wa Isaka tu.
…………………………..
Jambo jingine linalothibitisha kwamba Ishmaeli hana nafasi kwenye wokovu wa mwanadamu ni namna Mungu anavyoitwa kwenye Biblia yote. Utakuta anaitwa Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Hakuna hata nusu mstari, achilia mbali aya nzima, inayosema kuwa Mungu ni Mungu wa Ibrahimu na Ishmaeli. Tazama mifano ifuatayo:
Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, MUNGU WA IBRAHIMU baba yako, na MUNGU WA ISAKA; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. …, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. (Mwanzo 28:13-14)
Hapa Mungu anasema na Yakobo. Na unaona kuwa Mungu anamwambia, “katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.” Ni ahadi ileile ya Ibrahimu, babu yake.
………………………………………
Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, MUNGU WA IBRAHIMU, MUNGU WA ISAKA, NA MUNGU WA YAKOBO. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu. (Mwanzo 3:6)
ili kwamba wapate kusadiki ya kwamba Bwana, MUNGU WA IBRAHIMU, MUNGU WA ISAKA, MUNGU WA YAKOBO, amekutokea (Mwanzo 4:5)
Ee Bwana, MUNGU WA IBRAHIMU, NA WA ISAKA, NA WA ISRAELI, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, …. (1 Wafalme 18:36)
Ee Bwana, MUNGU WA IBRAHIMU, NA WA ISAKA, NA WA ISRAELI, …(1 Nya 29:18)
Enyi wana wa Israeli, mrudieni Bwana, MUNGU WA IBRAHIMU, NA ISAKA, NA ISRAELI, …(1 Nya 30:6)
Mimi ni MUNGU WA IBRAHIMU, NA MUNGU WA ISAKA, NA MUNGU WA YAKOBO? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. (Mt. 22:32)
…Mimi ni MUNGU WA IBRAHIMU, NA MUNGU WA ISAKA, NA MUNGU WA YAKOBO? (Mk. 12:26)
… hapo alipomtaja Bwana kuwa ni MUNGU WA IBRAHIMU, NA MUNGU WA ISAKA, NA MUNGU WA YAKOBO. (Lk. 20:37)
MUNGU WA IBRAHIMU NA WA ISAKA NA WA YAKOBO, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, … (Matendo 3:13)
Vilevile Ibra, Mungu anaitwa ni MUNGU WA ISRAELI. Israeli ni jina jingine la Yakobo. Na Yakobo ni mwana wa Isaka, mwana wa Ibrahimu. Unaweza kuona mifano michache tu kwenye aya zifuatazo: (1 Wafalme 22:53, 2 Wafalme 9:6, 18:6, 19:15, 21:12, 1 Nya. 5:26, 15:14, 2 Nya. 2:12, Lk 1:68).
Kwa hiyo rafiki yangu Ibra, bado ukweli uko palepale kwamba wokovu wa mwanadamu unapita kwenye mstari wa Ibrahimu – Isaka – Yakobo – Yesu. Basi!
nahitaji kuuliza kitu nje ya mada
DeleteMwanzo 29:20-30 inaelezea habari za Nuhu pamoja na kukaa uchi na kulewa
suala langu 'Kaanani alilaaniwa na Nuhu na baadae Nuhu na Mungu wakashirikiana na kusema Kanaani awe mtumwa kwa ndugu zake, Jee Kaanani kafanya kosa gani?
Umeeleweka Jems John. Mungu akutie nguvu ili uendelee kutuelimisha
ReplyDeleteUbarikiwe sana James
ReplyDeleteNeno la MUNGU kulielewa ni lazima uongozwe na roho Mtakatifu. Nawashauri wote wanaosoma neno la Mungu yaani Biblia waombe kwanza Roho Mtakatifu awaongoze kulielewa, tofauti na hapo wataishia kulipinga tu na si kulielewa.
James ubarikiwe mtumishi kazi yako njema
ReplyDelete