Kuzaliwa na kufa kwa Bwana
Yesu si jambo lililoibuka tu. Hili lilikuwa ni jambo ambalo tangu wakati wa
kosa la Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni lilitolewa unabii na Mungu
mwenyewe. Mungu alimwambia shetani:“nami nitaweka uadui kati yako na huyo
mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na
wewe utamponda kisigino.” (mwanzo 3:15).
Hakuna mwanadamu anayeitwa
uzao wa mwanamke. Uzao huwa unahesabiwa kwa manamume siku zote na duniani kote.
Lakini ni Yesu peke yake ambaye hakuzaliwa na baba wa kibinadamu kama wanadamu
wengine ndiyo maana anaitwa uzao wa mwanamke.
Wakati wa Ibrahimu, Mungu
alitoa tena unabii juu ya kufa, kufufuka na kulipa dhambi kwa Bwana Yesu.
Unabii huu ulitolewa kupitia mtoto wa Ibrahimu, yaani Isaka. Je, ilikuwaje?