“Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa
katika
ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa
yote; hapo ndipo ule mwisho
utakapokuja”
(Mathayo 24:14).
Ukisoma kurasa mbalimbali za kwenye mtandao juu ya
kukua kwa dini ya Kiislamu, utakuta wengi wanasema kwamba Uislamu ni dini inayokua
kwa kasi sana. Je, hilo ni kweli? Ni jambo gani linaloonyesha ukweli wa hoja
hiyo?
Lakini tunao ushahidi wa Neno la Kristo kwamba siku za
mwisho (yaani hizi tulizo nao), Injili itahubiriwa ulimwenguni kote. Pia, Mungu
Yehova anaahidi kuwa hizi ni siku za kumwaga Roho wake kwa wanadamu wote.
Hakika hizi ni nyakati za Injili ya Yesu Kristo kusonga mbele na kushinda na
kubomoa kila upinzani na ukuta uliojengwa na adui ili kuwazuia wanadamu kumjua
Mungu wa kweli na Mwokozi pekee, Yesu Kristo.