Ibrahim alikuwa Mwislamu wa imani kali. Alikuwa mtoa mihadhara katika misikiti mbalimbali nchini Misri. Alikutana na Injili ya Yesu. Moyo wake ulitikiswa. Hakujua amwamini nani – je, ni Yesu au ni Muhammad? Nani angemwambia njia ya kweli ni ipi? Aliinua moyo wake juu mbinguni. “Yehova, nionyeshe njia ya kweli nami nitaifuata kwa gharama yoyote ile,” alisema kwa machozi.
Bwana Yesu mwenyewe alikuja kusema
na Ibrahim katika ndoto. Ibrahim aliachana na Uislamu na kumkumbatia Mwokozi. Lakini
kundi la Waislamu wenye imani kali la Muslim Brotherhood wangemwacha tu? Vipi kuhusu
familia yake?
Kumfuata Kristo kuna gharama. Lakini
huwezi kumbadilisha mtu anapomjua Mungu wa kweli ingawaje utampiga, utamfunga,
na kumtesa kwa kila namna. Endelea kusoma ushuhuda huu wa kutia moyo na Mungu
wa mbinguni atasema na moyo wako kwa njia ya ajabu ambayo itabadilisha kabisa
maisha yako....!