Marehemu Ahmed Deedat
Waislamu wanashikilia
kwamba Muhammad alitabiriwa kwenye Biblia. Andiko lao kuu wanalotumia kutetea
hoja hii ni Kumbukumbu la Torati 18:18. Andiko hilo linasema:
Mimi nitawaondokeshea
nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu
kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.
Haya ni maneno ambayo aliambiwa Musa na Yehova.
Mmojawapo wa watu ambao walijaribu sana kuonyesha kuwa
andiko hili lilimhusu Muhammad, alikuwa ni mwanaharakati wa Kiislamu, marehemu
Ahmed Deedat wa Afrika Kusini.