Mwanamke
wa Saudia aliyeamua kuumwaga
moyo
wake wote
Ni jambo lililo wazi
kwamba wanawake katika nchi za Kiislamu wananyanyaswa kupita kiasi. Maisha yao
hayana uhuru wala amani kwa kuwa sheria za dini yao zinawakandamiza wao na
kuwapendelea wanaume. Hata hivyo, baadhi yao wanatambua hali hiyo na
wanapambana kujaribu kuibadilisha. Lakini, ni wazi pia kuwa
mapambano yao hayo hayawezi kuwasaidia sana kwa kuwa huko ni sawa na kusema
Quran ibadilishwe. Je, hilo linawezekana kwa nchi hizo? Maana tatizo si wanaume au serikali; tatizo ni maagizo ya Mungu wanayemwabudu.
Katika video hiyo hapo
juu, tunamwona mwanamke mtangazaji wa kituo kimojawapo cha TV kule Saudi Arabia,
akimhoji mwanamke mwingine, Bi. Buthayna Nasser, ambaye naye ni mtangazaji
kwenye kituo cha TV. Mahojiano yanahusu mjadala uliokuwamo kati ya wanazuoni wa
Saudia juu ya wanawake kuonyesha nyuso zao kwenye TV ya Saudia.