Muhammad si tu kwamba ni mtume ambaye
hashuhudiwi na binadamu mwingine yeyote bali pia namna alivyokuwa akipata
ufunuo (wahyi) wake ni jambo linalotia mashaka makubwa sana.
Hashuhudiwi na binadamu mwingine yeyote
kwa sababu mambo yote aliyosema yanatoka kinywani mwake peke yake na hakuna mtu
wa pili wa kusimama kama shahidi ili kuonyesha kuwa alichosema ni kweli kinatoka kwa Mungu wa mbinguni.
Yaani shahidi wa mambo yake ni yeye
peke yake.
Na hakimu wa mambo yake ni yeye peke
yake.