Sunday, March 24, 2013

Injili ya Barnaba - Beleshi Linalochota Waislamu na Kuwatupia Kwenye Shimo la Kuzimu



Ulimwengu wa Kiislamu, kama kawaida yake, unatia juhudi kubwa sana katika kuuchafua Ukristo ili angalau uweze kuendelea kuwashikilia walio ndani yake; na pale inapowezekana, kuwadanganya Wakristo wasiojua Ukristo wala Uislamu.

Kuna mambo mawili makubwa ambayo huwa yananishangaza sana kuhusiana na masuala ya kiroho. Kwanza ni jinsi ambavyo wakuu wa dini wa Kanisa Katoliki wanavyotumia miaka na miaka kusomea dini na Biblia, kisha wanakuja kuishia kufundisha mambo yaliyo nje ya Biblia!!! Kwa mfano, wanawaambia waumini wao kuwa wafu wanatuombea kule mbinguni au kwamba unaweza kufanya misa huku duniani halafu ndugu yako aliyekufa akiwa na dhambi na, kwa ridhaa yake alikataa wokovu, eti atasamehewa dhambi na Mungu atamuingiza mbinguni!!!

Jambo la pili linalonishangaza sana ni kitendo cha Uislamu na Waislamu kutumia uongo kwa juhudi kubwa sana ili kutetea dini yao na kuwafanya waumini wao waendelee kubakia kwenye Uislamu. 

Kama dini yenyewe haiwezi kujitetea kwa njia ya neno inalolihubiri, bali inabidi uisaidie kusimama kwa kutumia uongo, kwa nini basi unaitetea? Na kwa nini hasa unaiamini? 

Siwashangai wale wasioelewa, lakini nawashangaa wale wanaojua kuwa, “Hapa ninasema uongo ili kumtetea Allah!” Yaani, wanafanya makusudi kusema uongo kwa lengo la kumtetea Mungu ambaye tunatarajia na tunaamini kuwa ana uwezo wote!!!!

Ama kweli duniani kuna mambo!!!

Nikirudi sasa kwenye mada ya leo, mojawapo ya silaha za uongo inayotumiwa na Waislamu kwa lengo la kuinua dini yao ni kusambaza na kuhubiri kile kinachojulikana kama “Injili ya Barnaba.”

Injili ya Barnaba ni nini?

Hiki ni kitabu kikubwa (karibu sawa na injili zote nne za Biblia zikijumuishwa pamoja - maana kina sura 222). Kitabu hili kinaeleza maisha ya Yesu na kudai kwamba kimeandikwa na mmoja wa mitume wa Yesu aliyeitwa Barnaba. 

Nakala za zamani kabisa za kitabu hiki ambazo zinajulikana ni mbili – moja kwa Kiitaliano na nyingine kwa Kihispania. Zote zinaonyesha kuwa ziliandikwa kwenye karne ya 15 au 16 baada ya Kristo.

Kwa nini injili ya Barnaba ni ya bandia?

Unaposoma injili hii, unagundua kuwa ni ‘forgery’ au ni ya bandia kutokana na sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu ziko wazi lakini zingine zinahitaji jicho la karibu zaidi ili kuzitambua. 

Zifuatazo ni baadhi ya sababu hizo:

1.  Mwanzoni tu mwa injili hii, Yesu anaitwa ‘Kristo’ (Christ). Imeandikwa: “Dearly beloved the great and wonderful God hath during these past days visited us by his prophet Jesus Christ …” Lakini unavyoendelea kusoma unakuta kwamba Yesu anakataa kwamba yeye si ‘Masihi’. Kwa mfano, katika sura ya 42 imaendikwa: Jesus confessed, and said the truth: "I am not the Messiah."  

Neno  ‘Kristo’ (Christ) ni tafsiri ya Kigiriki ya neno la Kiebrania ‘masihi’ (Messiah). Kwa hiyo, Kristo na Masihi ni neno lilelile. Licha ya hivyo, katika maisha yao yote, Wayahudi walikuwa wakimtarajia Masihi. Hivyo, hili lisingekuwa ni neno geni kwao kiasi cha kumfanya mwandishi ashindwe kulielewa. 

Mbali na hayo, Barnaba halisi anayejulikana kwenye Biblia aliishi kwenye kisiwa cha Kipro (Cyprus) ambako wenyeji wake walizungumza Kigiriki. Na Barnaba mwenyewe alikuwa ni Mwebrania. Kwa hiyo, asingeweza kamwe kushindwa kuelewa kuwa maneno haya yanabeba maana ileile katika lugha mbili tofauti ambazo alizizungumza zote.

Kwa hiyo, huu ni ushahidi kwamba mwandishi wa Injili ya Barnaba ni mtu ambaye hakujua Kigiriki ndiyo maana mwanzoni tu mwa injili yake hii anamwita Yesu ni Christ, ilhali ndani anamfanya Yesu aseme kuwa yeye si Messiah!

2.  Quran inasema kwamba Yesu ni Masihi. (Tazama Sura 3:45). Na Biblia nayo inasema kuwa Yesu ni Masihi. Kama wewe Mwislamu unaamini kuwa Quran ni kitabu cha kweli; na kwamba kile inachokisema ni kweli, iweje basi uamini injili ya Barnaba inayosema kuwa Yesu si Masihi na usiamini Biblia inayosema kuwa Yesu ni Masihi kama ambavyo Quran yako inasema?

3.  Katika sura ya 3, ‘barnaba’ huyu anatuambia kuwa Herode na Pilato walitawala Yudea wakati Yesu alipozaliwa. There reigned at that time in Judaea Herod, by decree of Caesar Augustus, and Pilate was governor in the priesthood of Annas and Caiaphas. Wherefore, by decree of Augustus, all the world was enrolled; wherefore each one went to his own country, and they presented themselves by their own tribes to be enrolled. Joseph accordingly departed from Nazareth, a city of Galilee, with Mary his wife, great with child, to go to Bethlehem (for that it was his city, he being of the lineage of David), in order that he might be enrolled according to the decree of Caesar…….. While Joseph abode there the days were fulfilled for Mary to bring forth.

Herode alitawala Israeli kati ya mwaka 37-4 kabla ya Kristo. Unaweza kusoma HAPA au kwingineko kokote. Lakini Pilato alitawala miaka zaidi ya ishirini baadaye, yaani kati ya 26-36 baada ya Kristo. Unaweza kusoma HAPA. Sasa, kwa kuwa Barnaba aliishi pamoja na Yesu, wakati ambapo Pilato alikuwa mtawala, inawezekanaje akafanya kosa lililo wazi kama hili? Hili ni kosa linaloweza tu kufanywa na mwandishi ambaye hakuishi nyakati za Yesu au nyakati za Pilato.

4.  Katika sura ya 20 tunaambiwa na ‘barnaba’ kwamba Yesu alisafiri baharini kutoka Galilaya hadi Nazareti. Imeandikwa: Jesus went to the sea of Galilee, and having embarked in a ship sailed to his city of Nazareth. Hebu tafuta Nazarethi kwenye ramani HAPA, kisha uangalie kama mtu anaweza kusafiri kwa chombo cha majini kutoka kwenye Bahari ya Galilaya hadi Nazarethi.

Nazarethi iko kilometa takriban 14 kutoka Bahari ya Galilaya. Ni mtume gani wa Yesu angeweza kusema jambo kama hili – ukichukulia kwamba Yesu na mitume wake walikuwa wakitembea sana kwenye maeneo haya? Hii inaonyesha tu kwamba mwandishi wa injili ya Barnaba hajui jiografia ya Nazarethi au Galilaya.

5.  Yehova aliagiza kwenye Biblia kwamba watu washerehekee mwaka wa Yubile kila baada ya miaka 50. Imeandikwa: Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile. Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa (Walawi 25:10-11).

Mwaka 1300 B.K, papa Boniface VIII alitangaza kimakosa kuwa Wakristo wanatakiwa washerehekee siku hiyo kila baada ya miaka 100. Lakini, mwaka 1350 B.K, papa aliyefuata, yaani Clement VI, alirudisha utaratibu wa kawaida wa kusherehekea yubile kila baada ya miaka 50. Kwa hiyo, kwa kipindi cha miaka 50, yaani kuanzia 1300 hadi 1350, watu walikuwa wakijua kwamba yubile inasherehekewa kila baada ya miaka 100. Soma HAPA.

Na huyu mwandishi wa Injili ya Barnaba kwenye sura ya 82, anamwekea Yesu maneno mdomoni kwamba eti alisema: “insomuch that the year of jubilee, which now comes every hundred years, shall by the Messiah be reduced to every year in every place." 

Hivi, kama ukiona sinema ambayo mtu anakwambia hii ni ya mwaka 1910, na inaonyesha watu wamevaa mavazi ya zamani na nyumba ni za zamani, lakini humo ndani kwa nyuma ukaona bendera ya taifa la Tanzania inapepea utawaza nini?

Kihistoria inajulikana kabisa kwamba bendera hiyo haikuwapo mwaka 1910. Maana ya kuwapo kwake kwenye sinema hiyo ni moja tu – kwamba hiyo ni sinema ya uongo!

Sasa, suala la yubile ya kila miaka 100, kwa mara ya kwanza, lilikuja mwaka 1300. Halafu waislamu mnataka kuwaambia watu kuwa injili ya Barnaba iliandikwa na mtume aliyeishi na Yesu kwenye karne ya Kwanza, yaani miaka 1300 kabla ya jambo hili linalohusiana na yubile ya kila miaka 100 kutokea. Au huyu mheshimiwa 'barnaba' alikuwa anaongea kinabii?

Kwa msomaji unayependa KWELI, hili linakuonyesha kitu gani? Bila shaka jibu liko wazi kwamba mwandishi wa injili hii aliishii baada ya mwaka 1300. Amka!!!

Barnaba wa karne ya 1 asingeweza kamwe kuandika au kusema jambo kama hili; na zaidi ya yote Yesu…?!

6.  Katika sura ya 178, injili ya Barnaba inatuambia kuwa ili ufike paradiso ni lazima uvuke mbingu 9. Ikimaanisha kuwa, paradiso ni ya kumi. Imeandikwa: Truly I say to you that the heavens are nine, ……. And truly I say to you that paradise is greater than all the earth and all the heavens together.

Katika karne ya 14 kule Italia kulikuwa na mshairi maarufu aliyeitwa Dante Alighieri. Katika mojawapo ya vitabu vyake, Dante anazungumzia jambo hilihili. Yaani anasema kuwa ili kufika paradiso unatakiwa kuvuka mbingu tisa!!! Unaweza kusoma HAPA.

Na inajulikana, kama nilivyosema mwanzo wa makala haya kuwa, nakala za zamani kabisa zinazojulikana za injili ya Barnaba ni mbili – moja ya Kiitaliano na nyingine ya Kihispania. Na hizi zinajulikana kuwa ni za kwenye takriban karne ileile ya Dante. Waswahili wanasema, mwenye macho haambiwi tazama!!

7.  Sura ya 193 ya Injili ya Barnaba inaongelea juu ya kifo cha Lazaro ambaye alifufuliwa na Yesu. Kisha Yesu anasema kuwa saa yake (ya kufa) ikifika naye atalala vilevile kama Lazaro na atafufuliwa mara moja. Imeandikwa: 'My hour is not yet come; but when it shall come I shall sleep in like manner, and shall be speedily awakened.'

Lakini unapofika kwenye sura ya 216 na 217, wakati ambapo Yesu amekamatwa ili auawe, tunaambiwa kuwa Mungu alimwondoa kimiujiza (kama Quran inavyosema) na badala yake mungu huyu (anayeonekana kuwa ni mwongo) akamvika Yuda sura ya Yesu na Yuda akauawa kwa kuwa watu waliomjia Yesu walidhani kuwa Yuda ndiye Yesu.

Swali ni kuwa, je, si Yesu katika sura ya 193 ndiye aliyesema kwamba angekufa na kufufuliwa? Mbona basi Mungu anamkimbiza na kumficha badala ya kutimiza lile ambalo Yesu alilisema?

Mwenye macho haambiwi tazama!!

8.  Sura ya 54 inasema kuwa mafarisayo walikuwapo wakati wa nabii Eliya. Lakini historia inaonyesha kuwa Mafarisayo walitokea kuanzia karne ya pili kabla ya Kristo. Soma HAPA au kwingineko.

Lakini nabii Eliya aliishi kwenye karne ya 9 kabla ya Kristo. Soma HAPA. Hiyo ina maana kuwa aliishi takriban karne 7 kabla mafarisayo hawajatoke. Sasa iweje huyu barnaba atuambie kuwa mafarisayo walikuwapo nyakati za Eliya?

9.  Sura ya 80 inatumbia kwamba Danieli alichukuliwa na Nebukadreza kupelekwa Babeli akiwa na miaka miwili. Imeandikwa: Daniel as a child, with Ananias, Azarias, and Misael, were taken captive by Nebuchadnezzar in such wise that they were but two years old when they were taken; and they were nurtured among the multitude of idolatrous servants.

Unaposoma Biblia inatuambia kwamba: Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha. (Dan. 2:1).

Matokeo yake Nebukadreza alitaka waganga na wataalamu wa kutafsiri ndoto wamwambie maana ya ndoto ile. Kila mmoja alishindwa lakini Danieli alitafsiri ndoto ile baada ya kumwomba Yehova.

Matokeo yake, Biblia inasema: Ndipo Nebukadreza, mfalme, akaanguka kifudifudi, akamsujudia Danieli, akatoa amri wamtolee Danieli sadaka na uvumba. Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii. Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli. (Dan. 2:46-48).

Sasa, Nebukadreza aliota ndoto hii akiwa katika mwaka wa pili wa kutawala kwake. Kama alimchukua Danieli kutoka Israeli katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake, hiyo ina maana kwamba, Danieli alitafsiri ndoto ile akiwa na miaka mitatu; na pia alifanywa kuwa liwali (mbunge) akiwa na miaka hiyohiyo mitatu!

10.              Jambo jingine ambalo ni kichekesho kikubwa kuhusiana na hii injili ya Barnaba ni kuwa Yesu hakuwahi kuwa na mtume aliyeitwa Barnaba. Mitume wa Yesu wanajulikana. Unaweza kusoma Mathayo 10:2-4; Luka 6:13-14.


Sasa, Barnaba ni nani? 

Huyu alikuwa ni mwanafunzi aliyemwamini Yesu baadaye wakati Yesu tayari alishafufuka na kupaa kurudi mbinguni. Wakati mitume alioacha Yesu walipohubiri injili ya Yesu, mmoja wa watu waliosikia na kuiamini na kuokolewa alikuwa ni Yusufu (Joseph), mwenyeji wa Kipro (Cyprus).


Huyu aliuza shamba lake akaleta fedha kwa mitume ili wenye uhitaji waweze kugawiwa. Mitume walimpa jina la Barnaba likiwa na maana ya ‘mwana wa faraja.’


Imeandikwa: Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji. Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro, alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume. (Matendo ya Mitume 4:33-37).

Kwa hiyo, Barnaba hakuwa mmoja wa mitume wa Yesu!


Je, unadhani baada ya ushahidi huu kidogo (maana upo zaidi) bado utashikilia kuwa Injili ya Barnaba ni ya kweli? Unafikiri ni nani aliiandika? Kama umewahi kuisoma injili hii, ni kitu gani kitakachokufanya upinge hoja kwamba injili hii iliandikwa na mwislamu aliyeishi Italia katika karne ya 14, 15 au 16 ambaye alikuwa anajaribu kumhalalisha Muhammad kama ambavyo ninyi Waislamu mmeendelea kufanya hadi hivi leo – maana injili yenyewe 'inamfagilia' Muhammad?

Waswahili husema: Mwenye macho haambiwi tazama na pia sikio la kufa halisikii dawa. Je, wewe ni mwenye macho au ni sikio la kufa?

Jiponye mwenyewe.

Utadanganywa hadi lini?

Tafakari.

Hoji mambo.

Chukua hatua.

21 comments:

  1. ok pole kwa kuumiza kichwa ili kupata ukweli wa mambo magumu kama haya

    ReplyDelete
    Replies
    1. amina. tuendelee kupeleka Keli ya Kristo ili watu watoke gizani

      Delete
    2. rudi tena mafunzoni.... nahisi unajaribu kufumba macho kukwepa kuona ukweli. lakini kama wataka kujua ukweli isome qur ani vizuri soma injili ya barnaba soma na biblia..


      Delete
    3. Nakala ya Injili ya miaka 1500 iliyopita na ambayo imepatikana tena katika kanisa moja nchini Uturuki baada ya kupotea kwa muda wa miaka 12, ina utabiri wa kuja Mtume wa Uislamu, Nabii Muhammad SAW baada ya Masihi Issa yaani Yesu AS.
      Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, nakala hiyo ya zamani sana ya Injili imeandikwa kwa lugha ya Kiarami na vyombo vya habari vinasema kuwa, ilikuwa imefichwa kwa muda wa miaka 12.
      Tayari viongozi wa Vatican wameonesha hamu kubwa ya kuipata Injili hiyo na Papa Benedict wa 16 ametoa mwito wa kufanyiwa uchunguzi maandishi ya Injili hiyo.
      Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni wa Uturuki, Ertuğrul Günay amesema kuwa, bei ya Injili hiyo ni dola milioni 22 za Kimarekani na kwa vile utabiri wa kuja Mtume Muhammad SAW unapatikana kwenye Injili hiyo yenye lugha ya Nabii Issa AS, ilikuwa imefichwa ili watu wasiione.
      Amesema maneno yaliyomo kwenye Injili hiyo ya miaka 1500 iliyopita yanafanana sana na maneno ya Qur'ani Tukufu na kiujumla maneno yake yanakaribiana sana na mafundisho ya Uislamu.
      Sehemu moja ya maneno yaliyomo kwenye Injili hiyo yanamtaja Yesu kuwa ni mwanadamu na kumnukuu Nabii huyo wa Mwenyezi Mungu akisema kuwa, Mtume atakayekuja baada yake anaitwa Muhammad. Sehemu ya maneno ya Injili hiyo ya miaka 1500 iliyopita yana maana isemayo: Kuhani mmoja alimuuliza Masihi Yesu kuhusu mtu atakayekuja kuchukua nafasi yake na Yesu akajibu: "Muhammad (SAW) ndilo jina lake lililobarikiwa, anatoka katika kizazi cha Ismail, baba yangu Mwarabu."
      Waziri wa Utamaduni wa Uturuki pia amesema, tayari Papa Benedict wa 16 ametuma maombi rasmi ya kutaka wapatiwe Injili hiyo iliyopatikana kwenye visiwa vya Uturuki vilivyoko kwenye bahari ya Mediterranean. Imeelezwa kuwa watu waliopatikana na Injili hiyo walikuwa wana nia ya kuiuza kimagendo na hivi sasa wanashikiliwa katika mahakama za Uturuki.
      Wakati huo huo kasisi Ihsan Uzbek, mmoja wa viongozi waandamizi wa Kikristo nchini Urutuki amesema kuwa Injili hiyo ni ya zama za mtakatifu Barnaba aliyeishi na Nabii Issa na ambaye alikuwa mfuasi wake wa karibu.
      Huko nchini Uturuki nako kumetolewa mwito wa kufanyika uchunguzi wa kitaalamu wa kuweza kujua tarehe hasa ilipoandikwa Injili hiyo.
      Habari zinazofanana: Uturuki kuonyesha Injili inayotabiri kudhihiri Mtume Muhammad SAW.

      Delete
    4. Uislamu ni maneno tu hakuna matendo kwa huyo Mungu wake--- MANENO TU NA AHADI HEWA------------- Yesu yuko kazini usiku na mchana na tunaona matendo yake sawasawa na ahadi alizotoa miaka 2000 iliyopita.

      Hatuna haja na allah. Hakuna mtume aliyeitwa Barnaba.

      Sasa kwa nini wewe unatoa HITIMISHO ilhali unasema hiyo "injili" wanataka kuifanyia uchunguzi? Au tuseme uchunguzi tayari.

      Kufanana na quran si tatizo, maana hata "injili" ya barnaba nayo ni quran tupu humo ndani.

      ALLAH ANAHANGAIKA!!!!!!!!!!!!!

      Delete
    5. BARNABA Aliokoka kwa kuhubiriwa na wakina Petro, sasa aje aandike kupinga na kumuweka Muhammad ndani take duu! Changa la macho hili, injli hazitofautiani hata siku moja.

      Delete
  2. Ahsante sana kuchambua injili hii ya Barnabas ambayo hakika ni kanyaboya kama Quran ilivyokuwa kanyaboya. Uandishi wa Quran hautofautiani na Barnabas. Hii inakueleza tu kuwa aliyeandika Barnabasa alikuwa na elimu ya Quran ila akataka kuihalalisha Quran kwa kuweka imani ya Quran kwenye kitabu hiki akakikiita kitabu cha Kikristo kuwapotosha watu. Waislamu mnapotea na mnapotezwa hivi hivi na watu wanaowalaghai. Huu ulaghai uliotumika kuandika Barnabas hata Quran imetumika tu huo ulaghai kuiandika.

    ReplyDelete
    Replies
    1. amen. ulichosema ndugu ni cha kweli. Biblia haina mtu wa kui-challenge hata kidogo. Hilo ni NENO la Mungu wa kweli.

      Delete
  3. Ndugu James John

    Umefanya vyema kuijadili injili feki ya barnaba hapa. Lakini ili usionekane kuwa "asiyemwaminifu" katika Habari ya Uinjilishaji ni vyema kujifunza kwanza jambo kabla hujaliweka ili usionekane mpotoshaji kama nabii wa uongo mohamad.

    Kanisa Moja Takatifu Katoliki La Mitume Halifundishi kama Ulivyosema katika nukuu Hii
    "Kuna mambo mawili makubwa ambayo huwa yananishangaza sana kuhusiana na masuala ya kiroho. Kwanza ni jinsi ambavyo wakuu wa dini wa Kanisa Katoliki wanavyotumia miaka na miaka kusomea dini na Biblia, kisha wanakuja kuishia kufundisha mambo yaliyo nje ya Biblia!!! Kwa mfano, wanawaambia waumini wao kuwa wafu wanatuombea kule mbinguni au kwamba unaweza kufanya misa huku duniani halafu ndugu yako aliyekufa akiwa na dhambi na, kwa ridhaa yake alikataa wokovu, eti atasamehewa dhambi na Mungu atamuingiza mbinguni!!!


    Si kila mfu hutuombea ila WATAKATIFU TU. Mama Bikira Maria, Mtakatifu Stephano, Paulo, Petro, Yuda Thadeus, Baba Mt. Yohane Paul wa Pili na Watakatifu wengineo wengi hawa ndio ambao hutuombea kwani Wapo karibu na Mungu Mkuu. Na hii Ni Neema ya Mungu Kwa wanadamu Wote wenye Mapenzi Mema na Ni Fundisho Lenye Uongozi wa Roho Mtakatifu.

    Si Kila mfu huombewa. Kanisa huwaombea wale waliokufa katika hali ya Neema wakiwa na Tumaini La Ufufuko kwa njia ya Yesu Kristu Bwana Wetu. Kama mtu hakufa katika hali ya neema, yaani iwe alikufa katika hali ya dhambi mf. katika ujambazi, kujiua, mafarakano, ulevi n.k huyu hatumuombei kwani amekwisha hukumiwa.

    Kanisa Linafundisha watu kujitahidi kuishi kitakatifu kama wafuasi waaminifu wa Yesu Kristu kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu.

    Ndugu James Nirudie kukukumbusha Kujifunza kwa bidii kutoka Kwa Wakristu popote Ulimwenguni ili uweze Kuinjilisha katika Uaminifu kwa Bwana wetu Yesu Kristu na kwa Kanisa lake Takatifu.

    Wako Katika Umoja wa Yesu Kristu
    Innocent Julius
    Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo
    Kanisa Moja Takatifu katoliki la Mitume.
    Kijenge, Arusha, Tanzania

    ReplyDelete
    Replies
    1. shalom shalom Innocent

      Nakushukuru kwa maoni yako ambayo nayaheshimu.
      Asante pia kwa angalizo lako.
      Ningependa kuanza kujifunza kutoka kwako.

      Tafadhali naomba unithibitishie KIMAANDIKO juu ya ukweli wa hayo uliyoyasema yaani watakatifu wanaostahili kuombwa; na wale wabaostahili kuombewa.

      Asante na Bwana akubariki.

      Delete
    2. Shalom Ndugu

      Kwanza nitoe angalizo tena.
      Mungu Mwenye - Enzi ndiye Mpaji wa Vyote m.f Uzima, Msamaha, Mali n.k. Mahitaji yetu yote Mungu ndiye anayetupatia tumuombapo.
      Kwa watakatifu TUNAOMBA WAUNGANE NASI KATIKA SALA NA MAOMBI YETU, yaani WATUOMBEE. Ndiyo Maana Utasikia Mkatoliki anamtaja Mtakatifu Fulani kisha anasema UTUOMBEE.

      Kamwe hatuwaombi watakatifu wafu, Kwani tunaamini wote walio Mbinguni wana Uzima Tele zaidi Yetu.Bwana Mungu wetu si wa wafu bali wa walio hai.
      Maombi ya Mtu mwenye haki yana nguvu sana Yak 5:16. Hao walioko Mbinguni ni wenye haki kwa sababu kisicho safi hakiwezi kuingia mbinguni Ufunuo 21:27.
      Watakatifu Mbinguni ni sehemu ya Mwili wa Kristu hivyo hawatengwi nasi tulio pia sehemu ya Mwili wa Kristu kwa Kifo\Mauti ya kimwili, bali wanatuzunguka kama wingu kubwa la mashahidi Waebrania 12:1
      Wanasimama katika Ufalme wa Mungu na kutolea Maombi yetu Kwake Ufunuo 5:8, na kufanya tuwe na utulivu katika kukaza mwendo kuifikia taji.
      Washiriki katika Mwili wa Kristu wakiombeana ni jaambo linalompendeza Mungu 1 Tim 2:1-4 na Ndivyo alivyoamrisha katika amri ya mapendo Yohana 15:17.
      Watakatifu walio Mbinguni wana Mapendo thabiti, sasa kwa nini wasituombee? Kristu Ni Mzabibu, Nasi tuu Matawi; Kama sisi na watakatifu twaungana naye, basi sote twashikamana kwa pamoja bila kutengwa.
      Mtakatifu Paulo Mtume na Shahidi wa Yesu Kristu aliuliza 'je Jicho laweza kuuambia Mkono 'sikuhitaji'?" Hivyo nasi hatuwezi kusema hatuhitaji maombi ya ndugu zetu katika Kristu walio hapa duniani na hata walio mbinguni. Tukijua kuwa Wokovu ni kwa familia ya Mungu/Taifa la Mungu.
      Na Kwa kuwa sote tuu taifa la Mungu, Hivyo Ni Vyema kuziombea Roho za Marehemu wetu waliokufa katika Kristu.

      Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu Akubariki

      Wako Katika Umoja wa Yesu Kristu
      Innocent Julius
      Parokia ya Watakatifu Petro na Paulo
      Kanisa Moja Takatifu katoliki la Mitume.
      Kijenge, Arusha, Tanzania

      Delete
    3. Amina Innocent. and James. Nimejifunza mengi mno. It was worthy my time. Mungu awabariki.

      Delete
  4. Innocent rudi jifungie ndani soma tena Biblia yako,upagani umeingizwa Karoliki,shtuka

    ReplyDelete
  5. napenda kujua tofauti ya wakristo na wakristu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shalom Klauss
      Tofauti ya maana hakuna bali ni namna tu ya utamkaji. Wakatoliki wanapendelea kutumia Kristu na protestants wanapendelea Kristo. Lakini yote yana maana ileile.

      Delete
  6. Hahahahahahaha. Eti nakala imegunduliwa ilikuwa imepotea miaka 12. Kabla ya miaka12 mbona hatukuisikia. Wanatengeneza ushahidi

    ReplyDelete
  7. James kuwa makini na kitu imani, hivyo usipate shida sana... eleza kwa kiwango chako na kufunuliwa na roho.. kwa nini roho.. James yamekuwepo mafundisho ya ajabu yakutisha yakusikitisha na hata KUCHEKESHA, Biblia inatamka wazi na bila ubishi roho ikishamtoka mtu haina uwezo wa kutubu tena.. Mungu akasema kunatofauti gani ya kufa mnyama na kufa binaadamu maana jinsi afavyo huyu ndivyo afavyo huyu? nani alikwambia Mwanaadamu anapokufa roho yake huenda juu naya mnyama henda chini nani kakwambia? lakini leo ypo mtu mmoja kwa kuchafua tu imani za watu wengine kadai amekwenda kuzimu akamuon Marti Lutha, Kanumba na wengine (kasoro YUDA)eti wnanakula nyama za watu.. ahera kunapikwa akamchukua mwanamuziki maarufu duniani aliyefariki takribani miaka 5 iliyopita akapita pori kwa pori akampeleka mbinguni jamani... LABDA MBINGU YA DSM... si mbingu Yesu aliyoiongelea... Comedian tupu zile picha za horror tulizozoea kuziona zimehamia kwenye mafundisho... inafikia mkuu wa kanisa Katoliki anatamka wazi kisa cha Hawa kula tunda bustani ya edeni ni kisa cha habari bandia BBC nukuu... Injili ya Barnaba ni Propaganda... muombe roho akufunulie.

    ReplyDelete
  8. Mtakuja jua ukweli siku mkitolewa roho zenu

    ReplyDelete
  9. Kama watu wanaweza chambua hili tuliweke na hili tusiliweke inamaanisha nini? Kwamba biblia ilichambuliwa kwanza na kuonwa na watu kwamba hili linafaa tuliweke na hili halifai. Kwa ninavyojua mimi maneno ya Mwenyezi Mungu hayapangiwi na mwanadamu. Tuzidi kufanya uchunguzi ili tuweze kuitambua njia iliyonyooka.

    ReplyDelete
  10. Umesema neno masihi na kiristo ni kitu kimoja. Sio kweli. Kristo ni jina la yesu.

    Nukuu ktk bibilia, Yule mwanamke akasema "najua kua yuaja masihii aitwae kristo. Kwamantiki hio kristo ni jina la yesu yaaninyesu kristo.

    ReplyDelete
  11. Msipate shida, neno la Mungu linanguvu wala haliitaji kutetewa. Kama kanisa lako au dini yako ina mafundisho potovu haiwezi kuwa na nguvu za Mungu hata kutoa pepo kwa Jina lake Yesu. Mtaishia kutumia akili zenu wenyewe huku mafundisho yenu yaki lenga kuhalalisha tamaa za miili yenu.
    1. Kwa Habari ya kuombea wafu ni uzushi ulioingia kanisani(Luka 16: 19-31) Usipoishi maisha ya kumpendeza Mungu hapa duniani huwezi ingia mbinguni.

    2. Kwa waislamu;
    Kama tulivyo wakristo, waislamu nao wanadai kumuabudu Mungu wa wayahudi. Lakini Biblia haipingani na kitabu cha wayahudi lia Quran inapingana kwa mambo mengi. Hakuna nabii aliyetumiwa na Mungu akashindwa kuandika au kusoma alichoambiwa na Mungu. Mohamed yatima(mkoresh) aliye lelewa na mjomba wake anapata ajira kwa mwanamke Tajiri Kisha anamuoa na kuanzisha uislamu ambao baadae watu wa mecca walipopingana na uislamu Mohamed anaamua kuhama na kwenda Medina akawateka watu wa Medina na kuwafanya watumwa. Jeshi lake lilipopata nguvu akarudi kuivamia mecca na kuiteka Kisha akaua wayahudi wengi lakini mwanamke myahudi alipika chakula akaweka sumu kulipa kisasi cha mauti ya mume wake na watu wake. Mohamed akala, akaanza kuumwa na mwisho akafa mikononi mwa Aisha binti aliyemuoa akiwa na miaka 9. Soma Quran utajua ukweli wa dini hii ya mpinga kristo.
    Kama huelewi kiarabu ingia yutube andika Christian prince, huyu ni muarabu anaichambua Quran kwa kina.

    ReplyDelete