Friday, November 3, 2017

Je, ni kweli Ibrahimu alijenga kaabah?




Uislamu (au tuseme Muhammad), anadai kuwa Ibrahimu ndiye aliyejenga Kaabah.

Mtu anapochunguza kwa makini jambo hili, ni vigumu sana kuamini kuwa Uislamu uko sahihi. Badala yake mtu unasukumwa kuwaza kwamba yamkini Muhammad alianzisha hadithi kama hizi ili kujipa uhalali wa kuwa mtume.
 
Hebu tutazame hadithi ifuatayo kisha tutajihoji wenyewe maswali kadhaa:

Katika Sahih Bukhari Bk 4, Vol 55, No. 583 tunasoma:


Narrated Ibn Abbas: The first lady to use a girdle was the mother of Ishmael. She used a girdle so that she might hide her tracks from Sarah. Abraham brought her and her son Ishmael WHILE SHE WAS SUCKLING HIM, to a place NEAR THE KA'BA under a tree on the spot of Zam-zam, at the highest place in the mosque. DURING THOSE DAYS THERE WAS NOBODY IN MECCA, NOR WAS THERE ANY WATER So he made them sit over there and placed near them a leather bag containing some dates, and a small water-skin containing some water, and set out homeward.

Maana yake ni kuwa:
Amesimulia Ibn Abbas: Mwanamke wa kwanza kutumia “girdle” (sijajua ni nini hii) alikuwa mama wa Ishmaeli. Alitumia “girdle” ili kuficha nyayo zake Sara asizione. Ibrahimu alimleta yeye pamoja na mwanawe wakati alipokuwa angali anamnyonyesha, hadi karibu na Kaabah chini ya mti, mahali pa Zamzam, mahali pa juu kabisa kwenye msikiti. Katika siku zile hakukuwa na mtu yeyote Makkah, na wala hakukuwa na maji. Kwa hiyo, aliwakalisha chini mahali pale na kuweka karibu yao mfuko wa ngozi wenye tende, na kiriba kidogo cha maji, kisha yeye akarudi nyumbani.

Loh!

Mtu akisoma hivi anaweza kudhani kuwa labda Ibrahimu alitoka nao nyumbani na kwennda nao mwendo wa kama dakika 5 au kumi na kwenda kuwaacha mahali.

Lakini acha tujifunze mambo kadhaa ya msingi sana ndipo turudi kwenye hadithi hii.

1.     Ibrahimu hakuwa anaishi Saudi Arabia.
2.     Alikuwa anaishi Kaanani karibu na Beersheba.
3.     Huo ni umbali wa kilometa karibia 1,500.
4.     Enzi hizo hakukuwa na magari.

Sasa hebu fikiria hata wewe mwenyewe:

Mzee wa watu huyu anabeba mwanamke mwenye kitoto kinachonyonya kisha akasafiri nao umbali huo wote (yamkini ni safari ya miezi kadhaa) kwenda mahali ambako:
1.     alikuwa hajawahi kwenda
2.     hakukuwa na hata tone la maji
3.     hakukuwa na nyumba hata moja - maana
4.     hakukuwa na mtu hata mmoja

Kisha mzee huyu akawaacha hao wawili hapo na yeye akafunga safari kurudi zake tena kilometa 1,500 hadi Beersheba.

Hivi ni kweli?

Sasa kwa nini Muhammad alikuwa akitunga mambo ambayo ni dhahiri hayana ukweli kiasi hiki?

Bila shaka lengo lake lilikuwa ni kujaribu kuipa dini yake hadhi na uhalali kwa kuihusisha na watu muhimu kama Ibrahimu. Lakini pia Muhammad kwa kuwa alijiita mtume wa Mungu, alifanya kila juhudi kujiungamanisha na mitume wa kweli ili na yeye azidi kukubalika na wale waliomfuata.

Lakini ukweli ni upi?

Tunasoma katika Biblia Mwanzo 16:15-16

Hajiri akamzalia Abramu mwana wa kiume; Abramu akamwita jina lake Ishmaeli, yule mwanawe, ambaye Hajiri alimzaa. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka themanini na sita, hapo Hajiri alipomzalia Abramu Ishmaeli.

Kisha pia tunasoma Mwanzo 21:5
Naye Ibrahimu alikuwa mtu wa miaka mia, alipozaliwa mwana wake Isaka.

Maana yake ni kuwa wakati Isaka anazaliwa, Ishameli alikuwa na umri wa miaka 14. Hapa yeye na mama yake walikuwa bado wako nyumbani kwa Ibrahimu.

Tunajuaje hilo?
Tunajua kwa kuwa sababu iliyochochea wao kufukuzwa ilikuwa ni hii:

Mwanzo 21:8-9
Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya. Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka.

Yaani:
Isaka ameachishwa ziwa.
Hapa inawezekana ni miaka kati ya miwili hadi mitatu baada ya kuzaliwa.
Hapo ndipo huyu Ishmaeli alipomfanyia dhihaka Sarah.

Ina maana hapo Ishmaeli ana miaka kwenye 16 – 17.

Kutokana na dhihaka hiyo, ndipo Sarah akamwambia Ibrahimu:
Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka (mwanzo 21:10).

Na kesho yake Ibrahimu alipowaondoa nyumbani, hakuwasindikiza kokote:
Imeandikwa:
Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba. (Mwanzo 21:14)

Kumbe basi:

Si kweli kama asemavyo Muhammad kuwa Hajiri aliondoka wakati akimnyonyesha Ishmaeli. Na si kweli kwamba Ibrahimu aliwapeleka Makkah. Kwa hiyo, hata habari ya kwamba Ibrahimu aliwahi kufika Makkah ni uongo kabisa.

Ndugu Mwislamu,
Karibu kwa Yesu maana Yeye peke yake ndio Njia, Kweli na Uzima.

4 comments:

  1. hivi unadhani hiyo hadith umeipa tafsir swahihi?
    mh wadanganye mapunguwani wenzio
    hadith umefasir sivyo na badala yake umeenda kuuuga na kipande tofauti ili angalau uwaridhish kodoo.
    wewe ni kafiri na elewa you will not see the light if your heart will not leave from the ivil shadow
    jiulize ikiwa wanafunzi wa yesu hawajuwi kuhusu kufufuka kwa yesu na vile vile mpaka leo mmeongeza mengi ktk uokovu wenu kama kuzifanya baa pahala patakatifu pa kufungia ndowa' kuzikana kwa jeneza na suti ilihali bwege wenu alizikwa na sanda vile vile mme simama mkijitapa je dini yenu ni ip? ukristo si dini bali ni kitendo cha kupakwa mafuta

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi nilitarajia utaeleza usahihi wa hadithi ambayo unadai nimefasiri isivyo. Badala yake umekuja na porojo tu za miaka nenda rudi kwenye ulimwengu wa kiislamu.

      Delete
  2. Anachekesha sindano ishamuingia huyo mi nimekuelewa vizuri na nimefwatilia ni kweli

    ReplyDelete