Showing posts with label waislamu wanaokoka. Show all posts
Showing posts with label waislamu wanaokoka. Show all posts

Tuesday, January 15, 2013

Hata Saudi Arabia Bwana Yesu Ameingia


Mhalifu wa kidini akihukumiwa kwa mujibu wa sharia
[Kama unachofanya ni kizuri; ni cha Mungu, kwa nini ufiche uso?]

Waislamu Wanazidi kukutana na Yesu

na Grantley Morris
‘. . . shuhuda zaidi na zaidi zinakuja kutoka kwenye nchi zilizofungwa juu ya Mungu anavyowapa Injili Waislamu kwa namna isiyo ya kawaida kupitia ndoto na maono. Miongoni mwa maelfu ya waamini katika Irani katika miaka michache iliyoisha, zaidi ya nusu yao wamekuwa waamini baada ya Yesu mwenyewe kuwatokea katika ndoto au maono.’ Wendell Evans wa the Billy Graham Center’s Institute for Muslim Studies anazungumzia juu ya wingi wa ndoto na maono yanayoripotiwa kuhusu Kristo miongoni mwa Waislamu . . .’

Kuzimu

Abdullah alikuwa Mwislamu mwaminifu. Aliishi umbali wa kama saa moja hivi kwa mwendo wa gari kutoka Makka. Alikuwa akiswali mara tano kwa siku, na mara kwa mara alitembelea Makka.

Kama ilivyo kwa Waislamu wengi, Abdullah alifundishwa kuwa Wakristo wana pepo wachafu na kwamba anatakiwa kujiepusha nao.

Usiku mmoja Abdullah aliota ndoto kwamba yuko kuzimu, anaungua moto. Asubuhi iliyofuata, akiwa ana wasiwasi mkubwa, aliomba kwa Allah, ‘Nimefanya kila kitu vizuri; kwa nini niende motoni?’ katika ziku zilizofuata, aliendelea kupata wasiwasi zaidi.

Sunday, January 13, 2013

Jambo la Ajabu Linaendelea Kwenye Ulimwengu wa Kiislamu




Makala haya yanaelezea mahojiano yaliyofanywa na mtangazaji wa CBN, Chris Mitchel, kuhusiana na kile kinachoendelea katika ulimwengu wa Kiislamu, ambao kwa karne nyingi umekuwa ukipinga kabisa Injili kuhubiriwa kwenye sehemu hiyo. Mahojiano haya yanaonyesha jinsi ambavyo Bwana Yesu mwenyewe anabomoa kuta na vizuizi kwa namna ambayo hata tawala za kiimla zinazotumia mahakama, hukumu za kifo na sheria kali kuzuia Injili kuwafikia watu, hawana tena la kufanya. Ni wakati wa Waislamu kujihoji na kumpokea Mwokozi wao ambaye aliwafia msalabani.

Mwanamke Mwislamu Aliyemkimbilia Yesu Kristo


Hii si picha ya Siti mwenyewe. Ni picha tu kutoka kwenye mtandao.

Ushuhuda wa Siti Zainab

Assalam-mualaikum.

Jina langu ni Siti Zainab. Mimi ni mwanamke wa Kiislamu kutoka Malesia, kusini mashariki mwa Asia.  Nilizaliwa kwenye familia ya Kiislamu, iliyokuwa ikifuata taratibu za Kiislamu kwa nguvu sana. Tokea mwanzo, nilipata elimu ya Kiislamu ambayo ilikuwa imara na ya ndani sana.

Pamoja na elimu yangu ya msingi, nilipelekwa pia kwenye madrasah ya Kiislamu, yaani shule ya dini, na nikaanza kusoma na kukariri Quran tangu mapema; huku nikijifunza maadili na misingi ya Uislamu wa Kisuni, kutoka kwa walimu waliobobea wa Kiislamu. Huko nilijifunza kumwogopa na kumtii Allah s.w.t. na pia kufuata mafundisho na mifano ya Mtume Muhammad (hususani yale yaliyo kwenye Hadithi zinazokubalika). Pia nilikuwa nina uwezo wa kusoma Quran yote, jambo ambalo liliwafurahisha wazazi wangu. Kwa kifupi, nilikuwa nina msingi imara na imani ya ndani ya dini kama Muslimah mwaminifu na aliyejitoa kwa moyo wote.