Katika makala haya,
ninajibu hoja zako rafiki yangu Ibra, ambazo umezitoa kwenye sehemu ya
‘comments’ kwenye makala yangu mengine yenye jina: Je,
Yesu aliagiza wafuasi wake wawaue maadui wa Yesu? Unaweza kusoma HAPA.
Ninatoa majibu yangu kama
makala tofauti kwa sababu kuu mbili. Kwanza ni kuwapa fursa watu wengine waweze
kujifunza kutokana na mjadala wetu na hata kuchangia au kutusahihisha pale
tunapokosea. Pili, kutokana na urefu wa majibu yangu, ni rahisi kuyatoa kama
makala kuliko maoni (comments), maana maoni ya mara moja hayatakiwi kuzidi
herufi takribani 4,000 hivi.