Ishmaeli na mama yake (Hajiri)
wanafukuzwa nyumbani kwa Ibrahimu
Katika makala yangu yenye kichwa
kisemacho: Je, Muhammad Ametabiriwa Kwenye
Biblia? – Sehemu ya II, ndugu yangu Ibra amenipa changamoto kadha wa kadha
ambazo naziheshimu na nimezitafakari vizuri. Unaweza kuzisoma kwa ukamilifu
wake kwenye sehemu ya ‘comments’ mwisho kabisa wa makala yaliyo hapa.
Mjadala wangu na Ibra
unatokana na hoja yake kwamba Muhammad
alitumwa kwa watu wote lakini,
Ibra anasema, Yesu alitumwa kwa ajili ya
wana wa Israeli tu, kitu ambacho mimi nimemweleza kuwa si kweli kwamba Yesu
alitumwa kwa Israeli tu. Hoja zake na majibu yangu viko kwenye sehemu ya hiyohiyo ya maoni
(comments) mwishoni mwa makala yaliyo
hapa.