Mosab
Hassan Yousef ni kijana wa kipekee ambaye ana ushuhuda usio wa kawaida. Baba
yake ni mmoja wa waliokuwa viongozi wenye ushawishi mkubwa sana ndani ya kundi
la kijeshi la Hamas kule Ukanda wa Magharibi (Palestina). Mosab alikulia kwenye
familia iliyoshikilia Uislamu kwa nguvu sana.
Akiwa
na umri wa zaidi ya miaka 30 sasa [yaani wakati ushuhuda huu ukiandikwa], ni
mshirika wa Kanisa la Kikristo, Barabbas Road kule San Diego, Calif. Aliikana
imani yake ya Uislamu, akaiacha familia yake kule Ramallah na anatafuta hifadhi
ya kisiasa kule Marekani.
Hadithi
ya maisha yake inashangaza sana - uwe unakubaliana au hukubaliani na mtazamo
wake. Video ifuatayo inaonyesha mahojiano kati ya Mossab na kituo cha FOX News,
akieleza yeye mwenyewe namna Muislamu kutoka Ukanda wa Magharibi alivyogeuka na
kuwa Mkristo wa Pwani ya Magharibi.