Katika makala yangu niliyoipa kichwa kisemacho: Je, Muhammad Ametabiriwa Kwenye
Biblia? – Sehemu ya II, yaliyo hapa; ambayo
kimsingi ninaonyesha kimaandiko kwamba Muhammad kamwe hajatabiriwa kwenye
Biblia, rafiki yangu Ibra kwenye sehemu ya maoni (comments) umenipa changamoto
mojawapo ya muhimu sana.
Unasema: Mr. James, Kitu kibaya kwako ulichokiona
kimeandikwa ndani ya qurani ni juu kuwachinja watu waovu? Sasa kama ndio hivyo,
wewe hujasoma biblia au biblia hauijui vizuri. Unafanana na mtu wa kucopy na
kupaste.