Utangulizi
Rafiki yangu Ibra, amekuwa akinishambulia sana kwa kusema
kuwa Biblia ni kitabu kisichoaminika bali Quran ndiyo inayopaswa kuaminiwa.
Hoja yake kuu, kama ilivyo kwa Waislamu wengine wengi ni kwamba, Biblia
imeingizwa maneno ya kibinadamu kiasi kwamba yale ambayo Mungu aliyateremsha ni
kama hayapo tena leo.
Katika makala haya ninapenda tuangalie swali kwamba:
Je, ni kweli Quran ni kitabu ambacho hakijawahi kubadilika? Je, ujumbe wake
ndio uleule ambao aliteremshiwa Muhammad na Allah? Je, ni kitabu cha kuaminika
kuliko Biblia kama wanavyosema Waislamu?