Waislamu
“wanahubiri” kuwa Yesu hakuja kwa ajili
ya ulimwengu wote bali alikuja kwa ajili ya Wayahudi peke yao. Kisha wanasema
kuwa Muhammad ndiye mtume sahihi kwa sababu huyo alikuja kwa ajili ya ulimwengu
wote. Andiko wanalotumia kupinga utume wa Yesu kwa ulimwengu ni lile
alilolisema Yesu wakati akiongea na mwanamke Mkananayo (yaani asiye Myahudi),
ambaye alikuwa anaomba Yesu amponye mwanawe.
Imeandikwa:
Akajibu
akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea
wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:26).