Sunday, March 17, 2013

Biblia na Quran ni Vitabu Vyenye Nguvu Sana



Historia ni kama ghala kubwa ambamo kumehifadhiwa kila kitu. Tunapochungulia kwenye ghala hili, tunaweza kujifunza kuhusiana na wapi tumetokea, na hatimaye wapi tuliko na kule tunakoelekea.

Bila shaka Biblia na Quran ni vitabu viwili ambavyo vina umuhimu mkubwa sana kwa wanadamu na ulimwengu. Hivi ni vitabu ambavyo ndivyo vinavyoumba maisha halisi ya idadi kubwa sana ya watu. Haya si tu maisha ya kula, kunywa na kuvaa hapa duniani, lakini pia vinaaminika kuwa vimebeba hatima ya milele yote kuhisiana na kila mwanadamu.

Ni wazi kwamba hakuna mwanadamu anayeweza kuamini na kutumainia kitu kisicho cha kweli kama anajua kuwa kitamletea hasara, na hasa kupoteza uzima wa milele. [Lakini hata kama atakiamini ilhali anajua kuwa si cha kweli, basi huyo anakuwa anataka faida fulanifulani za muda mfupi; yaani hata huyu naye hawezi kuamini kitu kwa lengo la kupata hasara].

Kwa mtu anayethamini na kuitafuta kweli, bila shaka atakuwa tayari kujifunza kutoka kwenye historia.


******************


Biblia na Quran zinatofautiana katika mambo mengi, lakini napenda nizungumzie machache, ambayo naamini yanaweza kutusaidia kujibu swali hili kwamba: Kati ya Biblia na Quran, kitabu kipi kinastahili kuaminika?

KUHUSU BIBLIA
Zifuatazo ni sifa za Biblia:

Idadi ya waandishi
Biblia ni kitabu kilichoandikwa na waandishi takribani 40. Waandishi 30 waliandika Agano la Kale na waandishi 10 waliandika Agani Jipya.

Nyakati
Waandishi wa Biblia waliishi katika nyakati tofautitofauti.

Kwa muda gani?
Kuanzia wakati wa Musa hadi wakati wa akina Paulo na Yohana, ilichukua miaka zaidi ya 1500 kupata kila kitu ambacho ndicho kimekuja kuwa Biblia hii tunayoifahamu.

Aina ya waandishi
Biblia haikuandikwa na watu wa aina moja. Badala yake kulikuwa na aina mbalimbali za watu. Kulikuwa na wafalme, kwa mfano Sulemani hadi watu wa chini kabisa, kama vile akina Petro ambao walikuwa ni wavuvi waishio kijijini.

Lugha
Kwa asili, Biblia iliandikwa kwa lugha mbalimbali, yaani Kiebrania, Kiaramu na Kigiriki. Baadaye ndipo lugha hizi zikaja kutafsiriwa katika lugha karibu zote duniani hivi leo.

Mitindo ya uandishi
Biblia imeandikwa kwa mitindo mbalimbali ya uandishi. Kwa mfano:

  • Historia au masimulizi - Kutoka, Hesabu, Yoshua, Nyakati, n.k.
  • Sheria – Walawi na Kumbukumbu la Torati
  • Ushairi – Wimbo Ulio Bora na maombolezo
  • Unabii – Yeremia, Ezekieli, Habakuki, Yoeli, Malaki, Danieli, n.k.
  • Nyaraka au barua – Warumi, wakorintho, Waefeso, Yakobo, Petro, n.k.
  • Mafunuo – Ufunuo

Jinsi ujumbe ulivyokuja
Ujumbe wa Biblia ulikuja kwa njia mbalimbali ambazo ni za kawaida kabisa. Kwa mfano:

  • Mungu kuongea moja kwa moja na wanadamu. Mathalani aliongea na Adamu (Mwa. 2:16-17), Nuhu (Mwa. 6:13-21), Ibrahimu (Mwa. 12:1-3; 22:1-2) na Musa (Kut. 3:4; 4:16).
  • Kwa njia ya maono. Kwa mfano, alisema kwa njia ya maono na Ibrahimu (Mwa. 12:7; 15:1), Yakobo (Mwa. 46:2; 28:12-17), Isaya (Isaya 6:1-10), Ezekieli (Eze. 1:1-28; 10:1-22), n.k.
  • Kupitia historia ya kawaida ya maisha ya Waisraeli. Ndio maana historia hiyo imeandikwa na sisi tunajifunza kweli za kiroho kupitia maisha yao ya kimwili.

HII MAANA YAKE NI NINI?

Maana yake ni kuwa, kwa vile Biblia imeandikwa kwa muda mrefu sana, na watu wengi, na watu tofauti, ambao hawakujuana, walioishi nyakati tofauti, walioishi sehemu tofauti, waliokuwa na elimu na vyeo tofauti, basi tungetarajia kuwepo na mgongano, msigano, na tofauti kubwa kabisa katika ujumbe wake. Isingewezekana kabisa kibinadamu:

  • Kuwepo na ujumbe unaofanana kwa watu wote hao
  • Kuwepo na mtiririko safi unaoendana kimantiki na kukubaliana kabisa na majira na nyakati

Maana yake nyingine ni kwamba, ukweli huu unatoa ishara ya wazi kwamba Biblia imetoka kwenye chanzo kimoja tu. Wanadamu walioandika walikuwa wanatumiwa kama vyombo tu na huyo  Mwandishi halisi ambaye ni Roho Mtakatifu. Ndiyo maana ujumbe wa watu wote unaendana na kukubaliana sawasawa licha ya tofauti zao kubwa namna hiyo.

KUHUSU QURAN

Quran ni kitabu ambacho, kama inavyoshuhudia Quran yenyewe, kilitokana na kushuka kwa aya kutoka kwa Allah. Aya hizi alipewa Muhammad, ambaye sasa kutoka kwake zilifika kwa wanadamu. Kwa hiyo, yafuatayo ni mambo kuhusiana na Quran pamoja na ujumbe wake:

Idadi ya waandishi
Quran imeandikwa na mwandishi mmoja tu. Kama alipokea kweli hicho anachosema au hakupokea ni vigumu kuthibitisha.

Nyakati
Kwa kuwa mwandishi ni mmoja, basi aliishi kwenye wakati mmoja tu alipokuwa hai.

Kwa muda gani?
Muhammad alipokea aya za Quran kwa muda wa miaka 23 tu.

Aina ya waandishi
Kwa vile ‘mwandishi’ wa Quran ni mmoja tu, hatuwezi kuongelea suala la aina za waandishi. 

Lugha
Lugha iliyotumika kuandika ujumbe wa mwanzo wa Quran ni moja tu.

Mitindo ya uandishi
Kwa ujumla Quran ina aina moja tu ya uandishi, ambayo ni aina ya unabii.

Jinsi ujumbe ulivyokuja
Ujumbe wa Quran ulikuja kwa njia tofauti na ule wa Biblia. 

Ubada bin Samit reported that when wahi descended upon Allah's Apostle (may peace be upon him), he felt a burden on that account and the colour of his face underwent a change. (Sahih Muslim, Vol. 4, p. 1248).

[Tafsiri: Ubada bin Samit alisema kwamba wakati wahyi alipomshukia Mtume wa Mwenyezi Mungu (amani iwe juu yake), alijisikia mzigo kutokana na hali hiyo na rangi ya uso wake ilibadilika. (Sahih Muslim, Vol. 4, 1248)]

Verily, al-Harith Ibn Hisham said: O Apostle of Allah! how does revelation dawn upon you? The Apostle of Allah, may Allah bless him, said: Sometimes it dawns upon me in the form of the ringing of a bell, and that is very hard on me; (ultimately) it ceases and I remember what is said. Sometimes the angel appears to me and speaks and I recollect what he says. Ayishah said: I witnessed the revelation dawning upon him on an extremely cold day; when it ceased, I noticed that his forehead was perspiring. (Ibn Sa'd, Kitab al-Tabaqat al-Kabir, Vol. 1, p. 228).


[Tafsiri: Hakika, al-Harith Ibn Hisham alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ufunuo huwa unakujaje kwako? Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ambariki, alisema: Wakati mwingine huja kwangu kama vile sauti ya kengele, na hii huwa ngumu sana kwangu; (hatimaye) unakoma na mimi ninakumbuka kile kilichosemwa. Wakati mwingine malaika hunitokea na anaongea na mimi nami hukumbuka yale aliyosema. Ayishah alisema: Nilishuhudia ufunuo ukimjia katika siku ambayo ilikuwa ya baridi kali sana; ulipomalizika, niliona kwamba uso wake unatoka jasho. (Ibn Sa'd, Kitab al-Tabaqat al-Kabir, Vol. 1, uk 228.)]

The Prophet added, "The angel caught me (forcefully) and pressed me so hard that I could not bear it any more. He then released me and again asked me to read and I replied, 'I do not know how to read.' Thereupon he caught me again and pressed me a second time till I could not bear it any more. He then released me and again asked me to read but again I replied, 'I do not know how to read?' Thereupon he caught me for the third time and pressed me, and then released me and said, 'Read in the name of your Lord, who has created (all that exists) has created man from a clot. Read! And your Lord is the Most Generous." Then Allah's Apostle returned with the Inspiration and with his heart beating severely. Then he went to Khadija bint Khuwailid and said, "Cover me! Cover me!" They covered him till his fear was over and after that he told her everything that had happened and said, "I fear that something may happen to me." Khadija replied, "Never! By Allah, Allah will never disgrace you. You keep good relations with your Kith and kin, help the poor and the destitute, serve your guests generously and assist the deserving calamity-afflicted ones." (Sahih Al-Bukhari, Volume 1, Book 1, Number 3).

[Tafsiri: Mtume aliongeza, "Malaika alinikaba (kwa nguvu) na kunikandamiza kwa nguvu sana kiasi kwamba sikuweza kustahimili zaidi. Kisha aliniachia na kwa mara nyingine akaniambia nisome, nami nikamjibu, 'Mimi sijui kusoma.' Hapo alinikaba tena (kwa nguvu) na kunikandamiza kwa nguvu sana kiasi kwamba sikuweza kustahimili zaidi.  Aliniachia na kwa mara nyingine akaniambia nisome, nami nikamjibu, 'Mimi sijui kusoma.' Hapo alinikaba tena na kunikandamiza na kuniachia kisha akasema,  Soma kwa jina la Mola wako ambaye ameumba (vyote) Amemuumba mtu kwa bonge la damu. Soma! Na Mola wako ni mwingi wa ukarimu." Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu alirudi na wahyi huku moyo wake ukidunda kwa nguvu. Kisha akenda kwa Khadija binti Khuwailid na akasema, "Nifunike! Nifunike!" Nao wakamfunika mpaka hofu ilipomwishia na baada ya hapo akawasimulia kila kitu kilichomtokea na akasema, "Naogopa kwamba kuna kitu kinaweza kunitokea." Khadija alijibu, "Hapana! Kwa jina la Allah. Allah hawezi kukuaibisha. Una uhusiano mzuri na ndugu zako, unasaidia walio maskini na fukara, unawafanyia ukarimu wageni wako na kusaidia wenye misiba wanaostahili." (Sahih Al-Bukhari, Volume 1, Kitabu 1, Namba 3)]

………………………

Desturi za Kiislamu ziko kinyume na matumizi ya kengele kwani zinatajwa kuwa ni vyombo ya shetani. Desturi hizi hata zinasema kwamba malaika hawawezi kuwasaidia wale wanaobeba kengele. Ona mifano ifuatayo:

  • Abu Hurairah alisimulia kwamba Mtume (amani iwe juu yake) alisema: kengele ni ala ya muziki ya Shetani. (Sahih Muslim, Kitabu 024)

  • Imesimuliwa na Umar ibn al-Khattab: Ibn az-Zubayr alisema kwamba mteja wao mwanamke alimpeleka binti wa az-Zubayr kwa Umar ibn al-Khattab akiwa amevaa kengele miguuni mwake. Umar alizikata na kusema kwamba alikuwa amesikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (amani iwe juu yake) akisema: Kuna shetani katika kila kengele. (Sunan Abu Dawud, Kitabu 34)

  • Abu Hurairah alisema kwamba Mtume (amani iwe juu yake) alisema: Malaika huwa hawamsindikizi msafiri ambaye ana mbwa na kengele. (Sahih Muslim, Kitabu 024)

  • Imesimuliwa na Ummu Habibah: Mtume (amani iwe juu yake) alisema: Malaika huwa hawaongozani na watu wanaosafiri huku wana kengele. (Sunan Abu Dawud, Kitabu 14)

…………………………..

Swali linalokuja kwetu ni kwamba, mtume alipoulizwa ni vipi huwa anapokea wahyi (ufunuo), mojawapo ya njia alizozitaja ni kwamba, upo ufunuo ambao huja kwa sauti kama za kengele. Na hapa anasema kuwa kengele zinahusiana na shetani. Hapo inakuwaje?

Hitimisho
Rafiki uliyesoma makala haya, unapolinganisha vitabu hivi viwili (Biblia na Quran), unadhani ni kipi kinastahili kuaminiwa?

Siulizi kwamba unaamini kipi? Maana nadhani tayari unacho kile unachokiamini. Lakini swali langu ni kwamba, Kipi kinastahili kuaminiwa?

Tafakari 

Hoji mambo

Jiulize 

Chukua hatua.


12 comments:

  1. Mr.James,
    Idadi ya waandishi,
    Nyakati
    Aina ya waandishi
    Lugha
    Mitindo ya uandishi
    Jinsi ujumbe ulivyokuja
    Hakuifanyi kitabu fulani kiaminike na kingine kisiaminike, bali inategemeana na kile kilichoandikwa ndani yake.
    kwa hiyo kipimo halisi ni je, biblia ni neno la mungu, ili kiaminike?
    Luka 1:1-3.”Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa kati yetu,kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu.”
    Hapa tunajifunza mambo yafuatayo;
    i.Luka mwenyewe anakiri kuwa watu wengi wametia mikono yao na kutunga kwa taratibu kwa kadiri walivyosikia wala si kwa ufunuo wa Roho Mtakatifu kama Wakiristu wanavyodai.
    ii.Luka anakiri kuwa yeye mwenyewe hakuwa shahidi aliyeshuhudia kwa macho yake na maelezo aliyoyakusanya yalitokana na mashahidi walioshuhudia kwa macho na si kuwa alifunuliwa na Roho Mtakatifu kama wakiristu wengi wanavyoaminishwa na viongozi wao. Kwa kuthibitisha hili, la waandishi kwamba hawakuongozwa na roho mtakatifu angalia wanavyotafautiana:
    1,je Yuda alikufaje?(a)(MATHAYO 27:5) “Alijinyonga”(b ).(MATENDO 1:18) “Alianguka kwa kasi akapasua matumbo”
    2.Yesu alipokuwa anapita Forodhani alimwona nani ameketi? (a)Lawi wa Alfayo (MARKO 2:14; LUKA 5:27) (b)Matayo (MATAYO 9:9)
    3.Tofauti na Yesu je kuna mwingine aliyepaa kwenda mbinguni? (a) (YOHANA3:13) Hapana(b) (2 WAFALME 2:11)Ndiyo Eliya alipaa kwa upepo wa kisulisuli.
    4.Je Yesu akijushuhudia mwenyewe ushahidi wake ni kweli? (a)(YOHANA 5:31)Si kweli. (b) (YOHANA 8:14)Ni kweli.
    5.Je Yuda alimbusu Yesu ili wamsulubishe? (a) (MATAYO 26:48-50)Ndiyo. (b)(YOHANA 18:3-12)Hapana hakumsogelea kabisa.
    6.Je Yesu alijichukulia msalaba wake mwenyewe mpaka Golgotha? (a) (YOHANA 19:17)Ndiyo. (b) (MATAYO 27:31-32)Hapana
    7.Je nani alimwambia Daudi akawahesabu Israeli?(a)(2 SAMWELI 24:1)Bwana (b) (1 M/NYAKATI 21:1)Shetani
    8..Wana wa Hashumu ni wangapi? (a) (EZRA 2:19)mia mbili ishirini na watatu. (b) (NEHEMIA7:22)Miatatu ishirini na wanane
    9.Ni lipi jina la mama yake mfalme Abiya(a) (2 M/NYAKATI 13:2)Maaka binti Urieli wa Gibea. (b) (2 M/NYAKATI 11:20)Maaka binti Absalomu.Lakini Absalomu alikuwa na binti mmoja tu naye ni Tamari(2 SAMWELI 14:27).
    10.je Simoni Petro alipataje kujua kuwa Yesu ndiye Kristu? (a) (MATAYO 16:17) Alifunuliwa na Baba kutoka mbinguni. (b) (YOHANA 1:40-41)Aliambiwa na ndugu yake Andrea.
    Je Yesu alistahili kurithi kiti cha enzi cha Daudi? (a) (LUKA 1:32)Ndiyo, malaika alimfunulia Mariamu. (b) Hakustahili,kwa sababu Yesu ni katika kizazi cha Yehoyakimu,angalia ( MATAYO 1:11,1 M/NYAKATI 3:16) Na Yehoyakimu alilaaniwa na Bwana kuwa hatakuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Daudi (YEREMIA 36:30).Mhh!!Ajabu ya mungu wa Biblia hii.
    Je Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake?(a) (MWANZO 1:26)Ndiyo;(b)(ISAYA 40:18,25)Hapana, Mungu hafananishwi na chochote.(c)(ZABURI 89:6) Hapana.
    Kuna aya mbili zinazotofautiana juu ya uumbaji zinazopatikana katika kitabu cha mwanzo: Katika sura ya kwanza imeandikwa kwamba uumbaji ulichukua siku sita. Ajabu ni kwamba katika sura ya pili, imeandikwa kwamba Mungu aliifanya kazi hii kwa siku moja (2:4). Tukiendelea na mikorogano hii iliyofanywa na waandishi ni juu ya ukweli kwamba Adam alikuwa ni kiumbe wa mwisho kuumbwa (1:27) wakati katika aya ya pili imeandikwa kwamba alikuwa ni kiumbe wa kwanza kuumbwa kabla ya kiumbe kingine chochote (2:4-9).
    Je Mungu anaweza kuwa msahaulifu kiasi hiki? hapana hii inaonesha hawa waandishi wa Biblia hawakutumwa na Mungu sbb angewatuma basi wasingetofautiana.
    -Je ewe Ndugu Mkiristu bado unaendelea kuamini kuwa Biblia ni neno la Mungu?
    -Je inayumkinikaje liwe neno la Mungu ambalo halikutoka kwa Mungu(si ufunuo) bali ni kwa kutunga na kusikia tu kwa watu? Tafakari bado unayo nafasi!
    -Isomeni Biblia lakini pia isomeni Quran ambayo haina kasoro ndani yake inshaallah mtapata mwanga!Allah anatuambia Quran imenyooka sawasawa haina kasoro (sura 17:1-2).

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mpendwa Ibra, wewe ni fundi kwelikweli wa kuuliza maswali lakini hata siku moja hujawahi kujibu maswali ambayo mimi nimeyauliza kuhusiana na Uislamu. Niseme tu kuwa sijawahi kuona maoni yako wewe binafsi kama wewe tangu tufahamiane mtandaoni. Kila mara huwa unachukua maoni ya watu wengine na kuyaweka hapa. Kwa mfano, haya maswali unayouliza hapa ni maswali ambayo yako kila mahali kwenye intaneti na mtu yeyote aki-serch anayakuta. Vivyo hivyo, majibu yake nayo yapo kila mahali. Kama lengo la mtu ni kutafuta majibu haya, yanapatikana kwa wingi sana.

      Lakini mimi ningependa siku moja utoe maoni yako wewe kama Ibra na hasa juu ya maswali ambayo huwa nauliza kama makala au ninayokuuliza wakati wa kujibu maswali yako.

      Kuhusu maoni haya hapa, SI KWELI HATA KIDOGO kwamba eti idadi ya waandishi, aina, lugha, n.k., havifanyi kitabu kisiaminike. HILO SI KWELI HATA KIDOGO. Siku zote tunaamini ushahidi wa watu wengi na si wa mtu mmoja. Siku zote tunaamini zaidi jambo ambalo limetokea kwa watu wasiofahamiana; au walioishi nyakati mbalimbali kuliko watu wanaofahamiana.

      Jambo la mtu mmoja peke yake halina nguvu kama halikuthibitishwa na mtu wa pili na wa tatu au zaidi. Hata wewe ukitaka kuniuzia nyumba yako, hutaamini tu kwamba nitakulipa; au mimi sitaamini tu kwamba hutakuja kunikana - ni lazima kila mmoja wetu ataleta shahidi mmoja au zaidi. Huo ndio ukweli na hali halisi na hata wewe unajua.

      ...............

      Kuhusu hayo maswali uliyouliza juu ya Biblia, hebu copy link ifuatayo na u-search kwenye Google, utapata pa kuanzia: http://www.answering-islam.org/Bible/index.html#canon

      ...............

      Lakini wakati huohup, Ibra rafiki yangu, nitafurahi na nina shauku sana kuona siku moja MAONI au MAJIBU YAKO BINAFSI kuhusiana na maswali ambayo huwa nauliza.

      Ubarikiwe na Bwana Yesu.

      Delete
    2. rose... naomba niongezee unajua hawa wenzetu wanasema kuwa Mungu ni mmoja ila dini ni tofauti.. ila mimi kwa hilo nakataa maana Mungu aliyeumba mbingu na nchi haruhus fujo maana anasema uhai ni wa kila kiumbe humu duniani ni wake maana ndie aliyetuwekea hivyo hakuna mtu anayeruhusiwa kuutoa lakini mungu wao yeye anawaruhusu kuua chuki visasi na mambo ya aina hiyo. hivyo basi Mungu wa bible sio mungu wa quran wana tofauti kubwa sana. na ndo maana hawatakaa waelewe hawa enyi ndugu zetu karibu kwa Yesu kuna raha sana.

      Delete
    3. NI kweli kabisa Rose, Mungu haruhusu fuji au ghasia. Mungu ni wa amani, upendo na masikilizano. Huyo ndiye Mungu wa kweli.

      Bwana Yesu akubariki

      Delete
  2. Ndugu yangu, sisi waislamu hata ukimuona mdogo, tumejaaliwa kupata ufahamu wa mambo ya mungu. Sasa tunapotafuta ukweli wa mambo ya mungu, tunarejelea kwenye vitabu vya mungu, kwa hiyo neno la mungu hawatolei maoni, utapotosha.
    Wewe kama mada inakushinda ifunge blog yako! Oh mara kakopi kwenye intaneti mara nini hata kama yana ukweli?
    Sasa wewe si unajifanya unawafahamu sana waandishi wa biblia, basi nitajie nani kaandika taurati ya musa?
    Nani kaandika injili ya yesu?
    Quran sio kitabu cha historia, ndio maana hawakalii vikao.
    Quran ina pumzi ya mungu, tofauti na biblia!
    Waandishi wengi mungu ameona ufedhuli walioifanyia taurat yeremia 8:8.
    ...ninenalo silineni agizo la bwana...mambo haya sisi hatuitaji
    Mr.James, ina maana wewe ukienda shambani, njiani ukamuona kwa mbali simba amepanda juu ya mti na wewe upo peke yako tu. Je, tukio hilo litashindwa kuwa la ukweli kwa sababu halikushuhudiwa na watu wengine?
    Bado mimi nipo palepale, waandishi na mambo mengineo niliyoorodhesha hapo juu halifanyi neno kuwa la kweli.
    Maswali unayoniuliza wewe, hayapo kwenye mada. Mimi ninakujibu kulingana na mada zako uliweka hapa. Ukutaka chagua mada weka hapo juu nitakujibu. Majibu utayapata kutoka kwenye vitabu husika.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shalom Ibra,

      Unaniuliza nani kaandika taurati. Nadhani unamaanisha kuwa ni mwanadamu gani kaiandika. Biblia inatuambia kuwa ni Musa. Lakini hilo huenda si jambo la msingi sana. Cha msingi ni kuwa ujumbe wa Biblia umetoka kwa Roho Mtakatifu – iwe ni kupitia kwa Musa, kwa Paulo, au watu ambao hawakutajwa majina yao.

      Kuhusu Yeremia 8:8 sikutarajia kuwa utatumia tena andiko hilo kwa jinsi hii. Nilishakujibu swala hilo. Kama hukulisoma, basi nenda tena kwenye makala yangu yasemayo: Majibu Yangu kwa Ibra – Sehemu ya 2 kwenye blog hiihii.
      Kuhusu Paulo kusema “Ninenalo silineni agizo la Bwana” wewe unataka kutuaminisha kama kwamba anaongelea mafundisho yake yote kuwa si maagizo ya Mungu. Hapo alikuwa anaongelea jambo moja tu akitoa ushauri na ndiyo maana anaweka wazi kuwa huo ni ushauri wake binafsi. Huo si ushahidi kuwa Biblia si neno la Mungu.

      Kuhusiana na suala kwamba ukiona jambo ukiwa peke yako hakulifanyi kuwa la uongo, hiyo ni kweli kabisa wala sipingani na wewe. Lakini nitakachofanya mimi ni kukupima katika mambo mengi ili nikuweke katika kundi la kukuamini au la.

      Ninapopima maneno YOTE ya Muhammad katika Quran jumla yake inanipa jibu kwamba hayo si maneno ya Mungu aliyeumba mbingu na nchi hata kidogo.

      Mimi siwezi kumwamini Muhammad kwa sababu mafundisho yake yanaleta matatizo badala ya masuluhisho. Ndiyo maana kila mahali wanakomfuata na kumwamini, ni fujo, kuna chuki, watu wanauawa, watu hawaruhusiwi kuuliza maswali, n.k.

      Hayo yanayofuatwa ni maneno yake peke yake na Mungu wake (ambaye si Mungu wa Biblia, of course). Huo anaosema ni mafunuo kutoka kwa Mungu (Allah), alipewa yeye PEKE YAKE. Hana support ya mtu mwingine kuhusiana na maneno yake.

      Lakini ninaposoma Biblia ambayo, kuna mtu aliongea jambo, halafu miaka zaidi ya elfu tatu baadaye wengine wanakuja kusema ya kwao na ninakuta kwamba wanaoana kabisa katika yale wayasemayo, na jumla ya maneno yote ni AMANI, UPENDO, MAELEWANO, KUSAMEHE – basi sina haja ya kumwamini mtu MMOJA ambaye jumla ya maneno yake ni kinyume na hayo.

      Delete
  3. James, neno la mungu lina nguvu, likisimama halianguki wala kutikisika. Ni ngao kwa waminio. Mimi nilijua ya kwamba swali hili halitajibika. Ndio maana sisi tunasema, BIBLIA SI NENO LA MUNGU, kutokana na jinsi inavyojikanyaga.
    BIBLIA inasema TAURATI imeandikwa na Mussa. Sasa kama ni yeye aliyeandika, nani basi, aliyetangaza kifo cha Musa? Swali hili lazima lijibiwe!
    Na kuhusu yer.8:8, maelezo yako uliyoyatoa ni mengi mno lakini hayana ukweli wowote. Yale ni mawazo yako tu. Kutokana na maelezo yale nimeshapata fununu kwamba kumbe wewe hujui kitu na unajaribu kufanya makosa yaleyale yaliyofanywa na wenzako wa nyuma kwa kuuficha ukweli na kuhubiri uongo. Andiko linasem hivi, nikianzia na aya ya 7; "7 Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za Bwana.
    8 Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo."
    James! Aya ya 7 mungu, anawasikitikia watu wake, kwa kukosa ujuzi wa amri zake. Hapa aina maana kwamba walikosa tafsiri, hapana. Bali neno lenyewe la uzima kutoka kwa mungu, waandishi walipotoa kwa manufaa yao kama ulivyodai wewe mwenyewe. Na ushahidi wa jambo hili tumeliona jinsi kauli zinavyogongana juu ya mwaandishi wa Taurati.
    Lakini, kwa nini sisi tunasema BIBLIA SI NENO LA MUNGU? Hapa lazima uthibitisho upatikane ili watu wengine wapate kujifunza na kujua ile kweli aliyosema bwana Yesu.
    Katika timotheo wa 2, 3:16 tunasoma:
    "16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;"
    Katika ufunuo 22:18-19 tunasoma:
    "18 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki."
    Kwa nini nimetoa aya hizi? Kwa sababu nataka kujua kutoka kwa mkristo yeyote, kwamba Biblia kama kweli maneno yake ni pumzi ya mungu na hayaruhusiwi kuongeza wala kupunguza, na Roho mtakatifu alikuwa pamoja na waandishi, sasa iweje yatokee yafuatayo:
    Ukisoma kwenye Matayo 18:11; Mark 9:44; Mark9:46; Mark 15:28; Luk23:17; Yoh5:4; Matend24:7; Matend28:29....nk. Hakuna kitu kilichoandikwa. Inavyoonyesha, maandishi yameondolewa. Sasa nataka kujua, kwa kuwa roho mtakatifu alikuwepo wakati hawa wandishi wanafanya kazi yao ya kuandika neno la mungu, ni nani basi kaondoa miujumbe ya aya nilizokutajia hapo juu? Na kama zilikosewa, ni nani huyo mwenye makosa kati ya mwandishi na roho mtakatifu? NDIO MAANA TUNASEMA, BIBLIA SI NENO LA MUNGU.
    Ebu sasa tusome kitabu cha Samweli I, 13:1 kupitia biblia tafautix2 kama ifuatavyo:
    SWAHILI HOLY BIBLE
    "1 Sauli alikuwa na umri wa miaka kadha wa kadha hapo alipoanza kutawala;naye akatawala miaka kadha wa kadha juu ya Israeli." Maelezo ya aya hii, inasema miaka ya huyo sauli haijulikani. Sasa swali, ni mungu gani huyo asiejuwa miaka ya mtumishi wake? NDIO MAANA TUNASEMA BIBLIA SI NENO LA MUNGU.
    BIBLICA
    "Sauli alikuwa na miaka thelathini, alipokuwa mfalme, akatawala Israeli miaka arobaini na miwili." Andiko hili linatofautiana na la mwanzo. Swali linakuja roho mtakatifu ni kigeugeu?
    MASHAHID WA YEHOVA
    1Sauli alikuwa na umri wa miaka [?] alipoanza kutawala, naye akatawala miaka miwili juu ya Israeli." Swali linabaki paleple, kwamba huyu roho mtakatifu alikuwepo wapi?
    KATOLIKI BIBLE
    Saul was . . . years old when he became king, and reigned over Israel for . . . Years.
    NDIO MAANA TUNASEMA, BIBLIA SI NENO LA MUNGU. Kwa makosa kama hayo halafu ulete madai ya kwamba biblia imeandikwa kwa msaada wa roho mtakatifu.
    Biblia ingeandikwa kwa msaada wa roho mtakatifu isingekuwa na mapungufu llukuki ya namna hiyo. Hivi sisi waislaamu tuone ukweli ndio tuwache? Kazi kwako!

    ReplyDelete
  4. Jambo jingine Yesu alisema, usiwahukumu wenzako na wewe utakuja kuhukumiwa. Sasa mimi nataka uniakikishie kwa maandiko juu ya wasiwasi wako kwenye uislamu. Kwa sababu, ujio wa uislamu manabii wote waliontangulia muhammad walibashiri. Tumeona jinsi gani mungu alivyotutangazia juu ya ujio wa sheria motomoto,; Yesu nae alisikika katika mahubiri yake akisema ya kwamba, ufalme wa mbinguni umekaribia, na akawagiza tena wanafunzi wake akiwambia walihubiri hilo neno. Tumemsikia yesu akiwaambia jamaa zake juu ya kuondolewa kwa ufalme wa mbinguni kwao na kupewa taifa jingine.
    James jamaa yangu, mambo haya mbona unafanyia mzaha vipi wewe? Ni nini kinakutatiza kwenye quran? Sema tukusaidie mwisho wa siku utabakia peke yako na imani yako feki ambayo hakuna kwenye kitabu chako tegemezi wapoandika. Yaani wewe upo hewani tu huku ukijiaminisha kwamba umeokoka.
    Wazungu mnaowategemea sasa hivi wanaingia kwa fujo zote kwenye dini ya haki.
    Siku hizi uingereza mfanyakazi yeyote haruhusiwi kuingia ofisini akiwa na rozali.
    Uwanja wa mpira wa Arsenal, ni marufuku kuingia bendera ya uingereza ambayo inaitwa bendera ya king james. NARUDIA KUSEMA NENO HILI KWAMBA MASHARIKI YA KATI, NDIKO IMANI ZETU ZILIKOCHIMBUKA NA NABII MUHAMMAD (SWA) NI WA MWISHO KUJA KATIKA MAENEO HAYO AMBAYO YALITAWALIWA KWA NGUVU ZOTE NA UYAHUDI NA UKRISTO, LEO HII KUNA IMANI MOJA IMETAWALA ZAIDI YA 95%. NI IPI HIYO?
    James! Quran ni kama kifurushi cha mpangilio wa maisha ya wanadamu ulimwenguni kote. Ndio maana kuna nchi kama saudia na kwengineko wanakitumia kama katiba ikiwa na maana kwamba nchi hizo zipo chini ya taratibu za mungu kwa maneno mengine nchi hizo wanaishi kwa kutegemea amri za mungu ambao ni ule ufalme uliohubiriwa kukaribia na yesu. Kwa hiyo, quran ni ufalme wa mbinguni. We ukizini, ukiiba, ukifanya chochote kile kibaya, unahukumiwa kulingana na uzito wa kosa lako.
    Habari kama hii, Wayahudi walipewa lakini mungu akawanyang'anya na kuwapa Waarabu, ambao wanasimamia kidete hili taratibu zote za mungu zifuatwe.
    James, tambua ya kwamba waislaam wanagombanishwa na mataifa yenye ukristo mwingi, wakiwa na lengo ya kuubomoa uislam. Kama umewahi kusikia vita vya cruzade, kwamba mpaka leo hii vita hiyo ipo. Mfano, hapa kwetu tanzania, walokole wanawaona wakatoliki wamepotea. Iweje leo hii uwepo umoja wa wakristo bila kujali wana imani gani. Lengo lao ni hilo kuupiga vita uislaam na mbinu za aina mbalimbali zinatumika lakina wanashindwa kuusambaratisha, badala yake unazidi kuongezeka kwa kasi ya umeme na siku za hivi karibuni, baada ya 11 september 2011, nchi za magaribi tunaona jinsi gani watu wanavyokumbatia uislaam.
    Huko ulaya na America makanisa yanaisha kwa kuwauzia waislaam wafanye miskiti. Sasa tangu kichwa chako kimeota nywele umewahi kusikia msikiti umeuzwa? Huko USA professor mmoja wa chuo cha biblia cha havard unniversity kaachana na ukristo. Sasa wewe, na huyo professor wa biblia nani zaidi mpaka wewe useme hujaona fundisho lolote la maana kwenye quran?
    Hapo kwenye kipengele cha uungu umesema kweli kwamba mungu wenu nyie na sisi tofauti. Kwa sababu, mungu wenu nyinyi ni yesu lakini wakwetu sisi ni yule ambae yesu alikuwa anamuomba pindi afanyapo ibada zake. Sasa tatizo liko wapi? Nyinyi kaeni na mungu wenu yesu na sisi, yaani pamoja na yesu, tupo pamoja na mungu wetu.
    Msamaha, upendo, amani kwa waislaam mungu ametuimiza.

    ReplyDelete
  5. Mwisho kabisa nataka niseme neno moja kwamba, jambo kama hulijui halifai kutolea maelezo badala yake, waulize wale wenye ufahamu. We unaona siku zote, waislaam wakiwa katika mihadhara wakijadiliana na wakristo na watu wengine juu ya kutangaza dini ya kiislam kwa kuomba waulizwe maswali, halafu wewe unapayuka hapa na kudai waislaam hawaruhusu maswali. Na yule shehe kwenye channel 10? We unakaa wapi porini?
    James! Ukipita mitaani, utasikia tu maneno kama haya: huo sio uislaam bwana, ha mshikaji he! kuwa muislaam bwanaa usifanye hivyo!...nk. Maneno kama haya hayaongeleki na waislaam pekee, hata wakristo pia,,utawasikia wallahi...
    Hii yote ni kutokana na upendo na amani ya kweli tunayoishi sisi waislaam. Kila jambo tulitendalo lazima, tujiulize kitabu chetu kinasemaje.
    Sasa nyinyi wenzetu ni tofauti, mnahubiri upendo na amani lakini kweli haipo. Tazama Luther baada ya kubadilika na kutawala ujerumani, aliwauwa watu wapatao 100000 wa imani ya ubatizo. Hii ndio mbaya! Ya Muhammad ipo kwenye taratibu na haruhusiwi mtu yeyote kutekeleza licha ya wale wenye ujuzi wa kutafsiri sheria. Yaani kama akina yesu tu!

    ReplyDelete
  6. Achani bwebwe twende kwenye practical.

    Aitwe hapamtu mwenye mashetani Huyu atumie muhamadi. Na huyu atumie yesu majibu yakipatikana ndio dini yabkweli simple

    ReplyDelete