Friday, July 5, 2013

Je, Biblia Ina Vitabu Vingapi?




Vitabu 73 au 66?
Leo duniani kuna Biblia yenye vitabu 73 na yenye vitabu 66. Waislamu wamekuwa wakitumia suala hili kama silaha ya kushambulia Biblia kwamba ni kitabu kisichoaminika, wala hakiwezi kumfikisha mtu mbinguni.

Kwa mfano, ndugu yangu Ibra ambaye amekuwa msomaji na mchangiaji mzuri sana wa blog hii ameniuliza kama ifuatavyo:
James, naomba majibu kwa maswali yafuatayo:
-Biblia original kabisa iliyoandikwa na roho mtakatifu ina vitabuvingapi?
-Kitabu cha Danieli kina sura 12 au 14?
-Biblia yenye vitabu 73 na ile ya 66 ipi ya kweli? Je! Hapa kuna mkono wa roho mtakatifu au ubinadamu?
Ukweli unabaki palepale kwamba biblia sio kitabu cha kutegemea sana kwa mambo ya mungu. Hapa duniani biblia ninazojua mimi ziko zaidi ya tano. Na zote zimepishana kwa namba ya vitabu vilivyopo.
Sasa hapo mimi nabaki nashangaa, niamini biblia gani kati ya hizi? Ubabaishaji, kweli haimo.
Tafakari. Jihoji. Kweli imo ndani yako! Soma Qur'ani tukufu.


Hili analoongelea Ibra hapa ni jambo ambalo lipo. Kuna Biblia yenye vitabu 73 na yenye vitabu 66. Lakini je, humu kuna ubabaishaji unaoifanya Biblia isiaminike?

Biblia ya vitabu 73 inakubaliwa na Kanisa Katoliki na ile yenye vitabu 66 inakubaliwa na makanisa ya Kiprotestanti. Hii ni kusema kuwa, kiujumla, vitabu vyote vilivyopo kwenye Biblia ya Kiprotestanti vimo kwenye Biblia ya Kikatoliki; lakini ile ya Kikatoliki ina vitabu 7 zaidi.

Vitabu 7 zaidi
Vitabu 7 vilivyomo kwenye Biblia ya Kikatoliki, ambavyo havimo kwenye ile ya Kiprotestanti ni hivi vifuatavyo:
1.   Tobit
2.   Judith
3.   Maccabee 1
4.   Maccabee 2
5.   Wisdom of Solomon
6.   Ecclesiasticus (Sirach)
7.   Baruch

Vitabu hivi viliingiaje?
Baada ya Wayahudi kutawanywa na Mungu kwenye mataifa mbalimbali nje ya Israeli kutokana na dhambi, wengi wao walizaliwa wakati dola ya Ugiriki (Uyunani) iliyoenezwa na Alexander the Great ilipokuwa ndiyo dola kuu kwenye dunia ya wakati ule. Kwa hiyo, wengi wao hawakujua Kiebrania. Matokeo yake ilionekana haja ya kuwatafsiria Biblia ya Kiebrania (Agano la Kale) katika lugha waliyoijua, yaani Kiyunani.

Wataalamu takribani 70 walikutana katika mji wa Alexandria, Misri, kwenye mwaka 200 KK na kuandaa Biblia yenye vitabu vyote vinavyopatikana kwenye Biblia ya Kiebrania. Lakini pia waliongezea vitabu hivyo 7 tulivyotaja hapo juu. Biblia hii imekuja kukubaliwa na Kanisa Katoliki pia.

Vitabu hivi viliachwaje?
Kufuatia mwenendo usio wa kimungu uliokuja kujitokeza kwa miaka mingi ndani ya Kanisa Katoliki, baadhi ya watu, kama vile Martin Luther, walianza kuhoji mafundisho fulanifulani ya Kanisa Katoliki na pia vitabu hivyo 7 ambavyo havikuwamo kwenye Biblia ya Kiebrania. Mfano wa mafundisho yaliyohojiwa ni Kanisa Katoliki kusema kwamba mtu anaweza kutoa fedha kununua msamaha wa dhambi kutoka kwa Mungu kwa ajili yake au kwa ajili ya wafu wake, n.k.

Ilibainika kuwa vitabu hivi vina mafundisho potofu, hivyo haviwezi kuhesabika kuwa ni Neno la Mungu. Matokeo yake, Luther na wanamageuzi wengine waliamua kukubaliana na vitabu vilivyo kwenye Biblia ya Kiebrania na kuacha vile 7 vilivyoongezwa kwenye Biblia ya Alexandria (inayoitwa Septuagint).

Tofauti tu ni kwamba, Biblia ya Kiprotestanti ikawa ina vitabu 39 katika Agano la Kale ilhali ile ya Kiebrania ina vitabu 24. Hivi ni vitabu vilevile ila tu Biblia ya Kiebrania inaunganisha baadhi ya vitabu kama kitabu kimoja. Kwa mfano, vitabu 12 vya manabii ambavyo ni vidogovidogo (minor prophets), inavichukulia kama kitabu kimoja, lakini ni vitabu 12 tofauti kwenye Biblia ya Kiprotestanti.

Hebu sasa tuangalie vile vitabu ambavyo viliondolewa kwenye Biblia ya Kiprotestanti pamoja na baadhi tu ya upungufu wa vitabu hivyo uliosababisha kuondolewa kwake – lakini makosa na mapungufu yake ni zaidi ya haya yaliyoorodheshwa hapa:

TOBIT
Kitabu hiki ambacho kiliandikwa kwenye mwaka 726-722 K.K., kina mafundisho kadhaa kama vile hili linalosema:
For alms deliver from all sin, and from death, and will not suffer the soul to go into darkness. (4:8-11).

Yaani: Sadaka huokoa na dhambi zote, na kutoka kwenye mauti , na hazitakubali roho ya mtu iende gizani (yaani kuzimu).

Pia imeandikwa:
Prayer is good with fasting and alms more than to lay up treasures of gold: for alms delivereth from death, and the same is that which purgeth away sins, and maketh to find mercy and life everlasting (12:8-9).

Yaani: Kuomba ni kuzuri kama kukiambatana na kufunga na kutoa sadaka kuliko kujiwekea hazina ya dhahabu; maana sadaka huokoa na mauti, na pia hutakasa dhambi, na humwezesha mtu kupata rehema na uzima wa milele.

Kwa mtu yeyote anayemwelewa Bwana Yesu na mafundisho yake wala haihitaji ufahamu mkubwa sana kujua kuwa hiki si kitu cha kutoka mbinguni hata kidogo. Haya ni mafundisho kutoka sehemu nyingine kabisa!

Kwenye karne ya 16 Kanisa Katoliki lilikuwa likiuza msamaha kama tulivyosema hapo juu. Unaweza kusoma zaidi HAPA. Pia hadi leo, waumini wake hutoa fedha kiasi fulani kanisani ili wafu wao waweze kusomewa misa; ili kwamba, hata kama walikataa wokovu wa Kristo na wakafia dhambini, basi waweze kusamehewa na Mungu na kuingizwa mbinguni.

Lakini hata kwa akili ya kawaida tu, inawezekanaje kununua uzima wa milele na msamaha wa dhambi kwa kutumia fedha? Kama ingekuwa ni kweli, basi matajiri wote wangeweza kwenda mbinguni na maskini wote wakaenda motoni. Pia, kusingekuwa na haja ya kuishi maisha matakatifu. Cha msingi ingekuwa ni kuishi kama upendavyo mradi uwe tu na fedha za kutoa sadaka nawe utakwenda mbinguni moja kwa moja.

Je, tunaweza kweli kusema kuwa maneno haya kwenye Tobit yanatoka kwa Mungu wa mbinguni? Jihoji mwenyewe kama kitabu kama hiki kinafaa kuwamo kwenye Biblia.

Mfano mwingine uko kwenye sura ya 6. Tobias alikuwa amepumzika karibu na Mto Tigris. Akatokea samaki mkubwa ambaye alitaka kummeza. Kisha akatokea malaika ambaye aliongea naye maneno mengi. Lakini mojawapo ya meneno hayo ni haya:
If thou put a little piece of its heart upon coals, the smoke thereof driveth away all kinds of devils, either from man or from woman, so that they come no more to them. And the gall is good for anointing the eyes, in which there is a white speck, and they shall be cured (6:8-9).

Yaani: Ukiweka kipande kidogo cha moyo wake [yaani wa samaki] kwenye makaa ya moto, moshi utakaotoka unafukuza kila aina ya mashetani, ama kutoka kwa mwanamume au mwanamke, na hawatarudi tena. Na nyongo yake ni nzuri kwa ajili ya kuponya macho yenye madoa meupe.

Ninajiuliza kama asili ya fundisho hili si kulekule lilikotoka fundisho jingine ambapo mtu fulani aliambiwa kuwa nzi akitumbukia kwenye kinywaji basi bawa lake moja lina ugonjwa lakini bawa la pili lina tiba!

Hivi kweli unaweza kufukuza majini kwa kutumia moshi wa moyo wa samaki? Hata usipokuwa msomi wa Biblia, unawezaje kuamini kuwa kitabu kama hiki ni Neno la Mungu? Kinachoelezwa kwenye aya hizi ni ushirikina tu ambao siogopi kusema kuwa unatokea kwenye shimo la kuzimu!

Jambo jingine tunaambiwa kuwa Tobit aliishi wakati Waashuru walipoitwaa Israeli (722 KK) na pale Yeroboamu alipoasi ufalme wa Yuda (931 KK). Wakati huohuo tunaambiwa kuwa aliishi kwa miaka 158. Lakini ukweli wa kihistoria ni kwamba, tukio la Waashuru na lile la Yeroboamu yametenganishwa na kipindi cha miaka zaidi ya 800! Makosa ya aina hii ni sawasawa na yale yaliyo kwenye ile inayoitwa Injili ya Barnaba.

WISDOM OF SOLOMON
Kitabu hiki kinasema katika sura ya 11:17 kuwa Mungu aliumba ulimwengu kwa kutumia vitu vilivyokuwapo tayari (yaani kama mfinyanzi anavyoumba vyungu kwa kutumia udongo uliopo tayari). Hili si jambo la kweli. Tunafahamu kuwa Mungu aliumba ulimwengu kwa Neno lake tu. Alikuwa akitamka na vitu vinafanyika.

JUDITH
Kitabu hiki kinamwongelea mwanamke aitwaye Judith ambaye anafanya jitihada za kuwaokoa watu wa taifa lake, Israeli toka mikononi mwa maadui, yaani Waashuru. Lakini kinachotokea ni kuwa, Judith anakwenda kwa adui ambapo tunaambiwa:
"But Judith praying to the Lord passed through the gates, she and her maid. And it came to pass, when she went down the hill, about the break of day, that the watchmen of the Assyrians met her, and stopped her, saying: Whence comest thou! Or whither goest thou? And she answered: I am a daughter of the Hebrews, and I am fled from them, because I knew they would be made a prey to you, because they despised you, and would not of their own accord yield themselves, that they might find mercy in your sight. For this reason I thought with myself, saying: I will go to the presence of Holofernes, that I may tell him their secrets and shew him by what he may tell them, without the loss of the one man of his army. And when the men had heard her words, they beheld her face, and their eyes were amazed, for they wondered exceedingly at her beauty" (10:10-14).

Yaani: Lakini Judith baada ya kumwomba Bwana alipita kwenye lango, yeye na wajakazi wake. Ikawa aliposhuka kilima, wakati wa mapambazuko, walinzi wa Kiashuri walikutana naye, na kumsimamisha, wakasema: Unatokea wapi! Au unakwenda wapi? Naye akajibu: Mimi ni binti wa Kiebrania, nami nimetoroka kutoka kwao, maana nilijua kuwa watakuwa mawindo kwenu, maana waliwadharau, wala hawakuwa tayari kujikabidhi wenyewe kwenu, ili waweze kupata rehema machoni penu. Kwa sababu hii, niliwaza moyoni mwangu na kusema: Nitakwenda mbele za Holofenes, ili nikamweleze siri zao na kumwonyesha ni nini awaeleze, bila kupoteza mtu wake hata mmoja. Na wale watu waliposikia maneno yake, walimwona uso wake, na macho yao yalishangaa, maana walishangaa sana uzuri wake.

Alipofikishwa kwa Holofenes, alimwambia:
"For it is certain that our God is so offended with sins, that he hath sent word by his prophets to the people, that he will deliver them up for their- sins. And because the children of Israel know they have offended their God, thy dread is upon them. Moreover also a famine hath come upon them, and for drought of water they are already to be counted among the dead. And they have a design even to kill their cattle, and to drink the blood of them. And the consecrated things of the Lord their God which God forbade them to touch, in corn, wine, and oil, these have they purposed to make use of, and they design to consume the things which they ought not to touch with their hands: therefore because they do these things, it is certain they will be given up to destruction. And I thy handmaid knowing this, am fled from them, and the Lord hath sent me to tell thee these very things and will pray to God, and he will tell me when he will repay them for their sins, and I will come and tell thee so that I may bring thee through the midst of Jerusalem, and thou shalt have all the people of Israel, as sheep that have no shepherd, and there shall not so much as one dog bark against thee: because these things are told me by the providence of God. And because God is angry with them, I am sent to tell these very things to thee"(11:8-17).

Yaani: Maana ni hakika kwamba Mungu wetu ameghadhibishwa na dhambi zetu kiasi kwamba ametuma neno lake kupitia manabii wake kwa watu, kwamba atawatoa kwa sababu ya dhambi zao. Na kwa sababu wana wa Israeli wanajua kuwa wamemtenda Mungu wao dhambi, utisho wako uko juu yao. Pia, njaa imekuja juu yao, na kutokana na kukosekana kwa maji wanaweza kuhesabiwa miongoni mwa wafu. Na wanapanga hata kuua mifugo yao, na kunywa damu yao. Na hata vitu vilivyowekwa wakfu vya Bwana Mungu wao ambavyo Mungu amewazuia kuvigusa, katika nafaka, na  mafuta , hivi wamekusudia kuvitumia, na wanakusudia kula vitu ambavyo hawatakiwi hata kuvigusa kwa mikono yao: kwa hiyo, kwa kuwa wanafanya mambo haya, ni hakika watatolewa ili waharibiwe kwa kuwa wanayatenda haya. Na mimi mjakazi wako nikiyajua haya, nimekimbia kutoka kwao, na Bwana amenituma kukuambia mambo haya name nitamwomba Mungu, naye ataniambia ni lini atawalipa kwa uovu wao, kisha nitarudi na kukueleza ili kwamba niweze kukuleta katikati ya Yerusalemu, nawe utakuwa na watu wote wa Israeli, kama kondoo wasio na mchungaji, na wala hatatokea hata mbwa mmoja wa kukubwekea: maana mambo haya nimeambiwa na Mungu. Na kwa sababu Mungu amewakasirikia, nimetumwa kukueleza mambo haya.

Hapa Judith ana makusudi mazuri ya kuwaokoa watu wake. Lakini mbinu anayotumia ni kusema uongo mwingi tu! Tangu lini Mungu wa Biblia akahitaji uongo ili kutekeleza makusudi yake? Inaeleweka kuwa uongo unakubalika kwenye Uislamu kama unatumika kwa lengo la kuendeleza Uislamu (ambapo unaitwa Taqiyya. Soma HAPA ili kuelewa zaidi), lakini kwenye Ukristo uongo haukubaliki hata kidogo. Mungu wa Biblia hahitaji kutumia waongo ili kujenga ufalme wake. Uongo kwake ni dhambi ambayo malipo yake ni jehanamu ya moto!

Kutokana na uongo huu tunaambiwa kuwa Judith aliweza kumlewesha huyo mkuu wa maadui, akakata kichwa chake, akakiweka kwenye kikapu na kurudi zake kwenye mji wa Wayahudi alikotokea. Hatimaye Wayahudi waliwashinda Waashuru.
Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo hana haja ya mbinu kama hizi! Hana!!

Vilevile tunasoma katika sura ya 1:5 kwamba:
Now in the twelfth year of his reign, Nabuchodonosor king of the Assyrians, who reigned in Nineveh the great city, fought against Arphaxas and overcame him.

Yaani: Katika mwaka wa kumi na mbili wa kutawala kwake, Nabukodonoso mfalme wa Ashuru, ambaye alitawala Ninawi mji ule mkuu, alipigana na Arpaksa na kumshinda.

Shida ya andiko hili ni kuwa, kwanza Nabukodonoso hakuwa Mwashuri. Alikuwa ni mtawala wa dola ya Babeli kuanzia mwaka 605 hadi 562 KK. Na mji wa Ninawi ulishaharibiwa mwaka 612 KK. Ni matatizo yaleyale kama katika Injili ya Barnaba!  

ECCLESIASTICUS
Kitabu hiki kiliandikwa kwenye mwaka 180 KK. Ndani yake tunakutana na mafundisho yafuatayo:
"Bring not every man into thy house: for many are the snares of the deceitful ... Receive a stranger in, and he shall overthrow thee with a whirlwind, and shall turn thee out of thy own" (11:31, 36).

“Usimlete kila mtu nyumbani mwako: maana hila za wadanganyifu ni nyingi … mkaribishe mgeni ndani kwako, naye atakutupa nje kwa kisulisuli, naye atakutoa nyumbani kwako.”
"Do good to the humble, and give not to the ungodly: hold back thy bread, and give it not to him, lest thereby he overmaster thee. For thou shalt receive twice as much evil for all the good thou shalt have done to him..." (12:6-7).

Yaani: Mtendee wema aliye mnyenyekevu, wala usitoe kwa asiye mcha Mungu: uzuie mkate wako wala usimpatie asije akakutawala. Maana utapokea uovu mara dufu kwa wema wote utakaokuwa umemtendea …

Je, haya ndiyo mafundisho ya Bwana Yesu? Yesu anayesema usiwanyime watu vitu vilivyo katika uwezo wako? Yesu anayesema kuwa adui yako mpende na umwombee? Yesu anayesema kuwa uwakaribishe nyumbani kwako watu wasio na makao?

BARUCH
Ndani ya kitabu hiki tunakutana na mafundisho kama haya:
"O Lord Almighty, the God of Israel, hear now the prayer of the dead of Israel, and of their children, that have sinned before thee, and have not hearkened to the voice of the Lord their God … (3:4)

Yaani: Ee Bwana Mwenyezi, Mungu wa Israeli, sikia sasa sala za wafu wa Israeli, na za watoto wao, ambao wamekutenda dhambi, wala hawakuisikiliza sauti ya Bwana Mungu wao ….

Mbona mambo haya yanashangaza? Watu wameacha kumtii Mungu. Kisha wakafa kwenye dhambi zao. Sasa wanamwomba Mungu kutokea kuzimu. Je, nini maana ya Mungu kutuweka duniani? Je, hajatuweka ili tutii sheria zake tukiwa hapahapa? Kama mtu akifa huku ana dhambi, inawezekanaje akamwomba Mungu naye akasikiwa? Basi hakuna maana yoyote ya Mungu kutuweka hapa duniani!

MACCABEES 1 & 2
Vitabu vya Makabayo navyo vina mafundisho kadhaa ambayo ni kinyume na Biblia kwa ujumla. Ifuatayo ni baadhi ya mifano yake:

Kutokana na vita, askari wengi wa Kiyahudi waliuawa. Wakati wakuwazika, ilionekana kwamba ndani ya mavazi yao walikuwa wamebeba miungu ya kigeni, jambo ambalo ni dhambi.

Matokeo yake, Yuda Makabayo alifanya jambo kuhusiana na dhambi ile kwa ajili ya wale wafu. Imeandikwa:
And making a gathering, he sent twelve thousand drachmas of silver to Jerusalem for sacrifice to be offered for the sins of the dead, thinking well and religiously concerning the resurrection. (For if he had not hoped that they that were slain should rise again, it would have seemed superfluous and vain to pray for the dead), and because he considered that they who had fallen asleep, with godliness, had great grace laid up for them. It is therefore a holy and wholesome thought to pray for the dead, that they may be loosed from sins."

Yaani: Baada ya kukusanyika, alipeleka fedha elfu kumi na mbili Yerusalemu ili zikatolewe dhabihu kwa ajili ya dhambi za wafu, huku akiwaza vema na kidini juu ya ufufuo. (Maana kama hangekuwa na tumaini kwamba wale waliouawa watafufuka tena, ingekuwa ni kazi bure kuomba kwa ajili ya wafu), na kwa kuwa aliamini kuwa wale waliokufa katika ucha Mungu wana neema kubwa iliyowekwa kwa jili yao. Hivyo, ni wazo takatifu na kamilifu kuomba kwa ajili ya wafu, ili waweze kufunguliwa kutoka kwenye dhambi zao.

Ni mambo yaleyale ya kudhani kuwa tunaweza kununua wokovu wa Mungu kwa fedha. Je, ni kweli inawezekana? Haya ni mafundisho potofu?

Matokeo ya uamsho wa Kiprotestanti
Bwana Yesu alisema waziwazi kuwa: Nami nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda (Mathayo 16:18).

Pia alisema kuwa tutawatambua watumishi wake kwa matunda yao. (Mathayo 7:16).

Kwa nini katika hali ya kawaida tu mlokole anapofanya kosa anashambuliwa ZAIDI kuliko mtu mwingine anapofanya kosa lilelile?

Japokuwa washambuliaji hawatakiri waziwazi, lakini mioyoni mwao wanajua fika kwamba ulokole (wokovu) ni maisha tofauti kabisa na dini zilizozoeleka au zenye majina makubwa. Ndiyo maana utasikia:
·         Yaani hata walokole nao wanapigana?
·         Mlokole gani huyo analewa pombe?
·         Mlokole atakuwa huyo? Mbona kanidhulumu fedha zangu?, n.k.

Na wala hutaona kwenye magazeti wameandika: Mkatoliki/Mlutheri/ Mwislamu kakamatwa ugoni! Hiyo si habari inayoweza kuuza gazeti. Lakini je, huawahi kusoma: Mlokole kashikwa ugoni? Hiyo ndiyo habari. Ni kwa nini?

Wokovu ni jambo la kipekee sana. Wokovu ndilo jambo linalompa homa kali shetani na kuzimu yote. Je, si kweli kama Maandiko yasemavyo kwamba mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe?

Baada ya Yesu Kristo kuondoka duniani, kundi lile dogo la mitume na wafuasi wake walieneza Injili ya Bwana kwa bidii sana hadi ulimwengu wote ukataharuki. Hadi watu wakawa wanasema: Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako (Matendo 17:6).

Katika miaka ya mwanzo ya Ukristo, shetani aliinua mateso makali mno, kupita kiasi, ambapo Wakristo waliteswa na tawala za Kirumi – waliuawa kwa njia mbalimbali kwa kipindi cha takriban miaka 300. Soma HAPA. Lakini kama Bwana alivyokuwa ameahidi, milango ya kuzimu haikuweza.

Lakini shetani alipoona kuwa hawezi kuangamiza Ukristo kwa kuua watu kimwili, aliamua kubadilisha mbinu. Aliamua kuingia kanisani ili afanye kazi yake kutokea ndani.

Ndipo kilipoingia kipindi cha utawala wa Kanisa Katoliki kwa miaka zaidi ya 1000. Katika kipindi hiki, misingi ya kweli ya Ukristo ilitelekezwa na badala yake yakaingizwa mafundisho mengi ya yaliyo kinyume na Biblia isemavyo. Ifuatayo ni mifano michache:

  •      Hakuna anayeruhusiwa kufasiri maandiko isipokuwa viongozi wa Kikatoliki.

  •     Kuwaomba wafu watuombee kwa Mungu.

  •     Kuombea wafu wasamehewe dhambi.

  •     Masalia ya watakatifu (relics) – iwe ni nguo, mfupa, nywele, n.k.,  yana   nguvu fulani ya kimungu inayoweza kuwasaidia walio hai.

  •     Bikira Maria kuwa mwombezi wetu.

  •    Wafu kuwa toharani.

  •     Kutumia Kilatini kama lugha ya kuendeshea ibada.

  •     Kuzuia Biblia kutafsiriwa katika lugha za watu wa kawaida.

  •     Kuzuia watu wa kawaida (walei) kuwa na Biblia.

  •     Kutangaza kuwa mtu fulani ni mtakatifu.

  •     Kuzuia watumishi kuoa au kuolewa.

  •     Kusali kwa kutumia rozari.

  •     Kuuza misamaha ya dhambi.

  •     Kwamba bikira maria alipaa mbinguni mzimamzima, n.k.


Na jambo jingine ni hili sasa la kufanya mbinu ili ndani ya Biblia viingie vitabu ambavyo vina mafundisho potofu, ambayo ni kinyume kabisa na Injili ya Ufalme wa Mungu aliye hai. Mtu mwingine anaweza kusema kwamba, “Si ni wanadamu, tena wasomi, walioingiza vitabu hivi kwenye Biblia?” Shetani hawezi kuleta mapepo yake yakiwa na mikia na mapembe kuja kuandika vitabu. Anatumia wanadamu hawahawa – uwe umesoma au haujasoma. Shetani haogopi elimu ya mwanadamu; anamwogopa Yesu peke yake.

Kwa hiyo, vitabu hivi vilikubaliwa na Kanisa Katoliki kwa sababu vinaendana na baadhi ya mafundisho yao hayo ambayo yako kinyume na Biblia kwa ujumla.

Tunapoangalia mambo haya kiroho, ndipo tunapopata picha iliyo sahihi. Hii ilikuwa ni kazi ya ibilisi mwenyewe akijaribu kulivuruga kanisa ili watu wasiweze kujua Injili ya kweli ya Bwana Yesu na kuokolewa.

Lakini ukweli unarudi palepale – Bwana Yesu alishaahidi kuwa atalijenga Kanisa wala milango ya kuzimu haitalishinda!

Hatimaye kwenye karne ya 16 kukatokea wanamageuzi kama vile Martin Luther. Hawa walianza kuhoji mafundisho hayo ya Kanisa Katoliki yaliyokuwa yameota mizizi kwa karne na karne wakati ule.  

Na kwa kuwa mafundisho haya yalishaota mizizi mirefu, na hivyo ilikuwa ni jambo gumu sana kukubali kuyaacha – kama ilivyo hata leo - Kanisa Katoliki katika Mkutano wa Trent (Council of Trent) mwaka 1546, waliamua kutangaza rasmi kuwa vitabu hivyo ni sehemu ya Biblia Takatifu. Na kwa kweli Kanisa Katoliki limekuwa na historia iliyojaa upotoshaji mwingi kwa miaka mingi; wala sit u katika vitabu hivi saba.

Jambo la kujiuliza tu
Ukiyaangalia mambo haya yote kama sehemu ya historia ya mwanadamu, utakosa kuona picha ya upande wa pili, ambayo ni ya muhimu hata zaidi. Ukweli kabisa haya ni mambo ya kiroho zaidi kuliko ya kihistoria. Kama ambavyo Mungu yuko kazini kuleta wokovu, shetani naye yuko kazini kuleta mauti.

Mungu hayuko kazini kuleta wokovu kwa ajili ya Wakristo, bali yuko kazini kuleta wokovu kwa wanadamu wote. Vivyo hivyo shetani naye hayuko kazini kushindana na Wakristo bali na wanadamu wote.

Lipo swali la msingi sana kwangu ambalo huwa najiuliza mara nyingi: Kwa nini kuna kufanana sana kati ya Uislamu na Ukatoliki?

  • ·         Wote wanaombea wafu.

  • ·         Wote wanaomba kwa kutumia tasbihi.

  • ·         Wote wana utaratibu wa hija.

  • ·         Wote hawapendi watu wa kawaida wajue maandiko ya vitabu vyao vya dini bali waamini tu kile wanachoambiwa na viongozi wao wa dini (japo kwa Ukatoliki jambo hilo limekufa siku hizi).

  • ·         Wote wanawaaminisha wafuasi wao kuwa maneno ya Mungu hayawezi kueleweka wa watu wengine isipokuwa kwa watumishi wa Mungu peke yake (kwa Ukatoliki hili nalo limeisha).

  • ·         Wote hawataki mtu kuhoji mambo ya dini. (kwa Ukatoliki hili limekufa sasa pia)

  • ·         Wote wanawachukulia watu wanaohoji dini kuwa ni maadui, hivyo wanastahili kuadhibiwa [Ukatoliki uliita uasi – heresy; Uislamu unaita kukufuru. Matokeo yake watu hao wanatengwa (excommunication) au kuuawa] – jambo hili nalo kwa Ukatoliki limekufa siku hizi.

  • ·         Wote hawawapendi Wayahudi. (Hili nalo Ukatoliki umeshaliacha).

  • ·         Wote wanapenda wawe na usemi wa mwisho si tu kwenye mambo ya kidini, bali pia kwenye mambo ya kisiasa (Ukatoliki ndio uliokuwa unasimika au kuondoa wafalme kwenye hiyo miaka 1000 ya utawala wake).

Na ajabu ni kwamba, mambo haya yote ni kinyume kabisa na mafundisho na maagizo ya Bwana Yesu. Wala hayamo kamwe kwenye Biblia! Badala yake wanapenda kuyahalalisha kwa kusema kuwa ni mapokeo kutoka kwa mababa wa imani wa zamani. Je, yanatoka wapi?

Unaweza kuwa na majibu yako, lakini mimi pia nitakupa mtazamo wangu. Mambo haya yanatoka kuzimu! Shetani alikuwa na zigo lake la mitego alilotaka kulitua kwenye kanisa ili kuwanasa wanadamu wa kwenda naye jehanamu.

Alijaribu kwa miaka mingi tu kufanya hivyo kwenye Kanisa, na kwa kiasi fulani alifanikiwa kwa muda. Lakini upepo uligeuka. Mbinu yake iligundulika na hivyo vitabu vyake pamoja na hila zake nyingine zikaondolewa kwenye Biblia “ya Waprotestanti” baada ya akina Luther na manamagezuzi wengine kusimama kidete kwa neema ya Bwana.

Na hata leo hii, Wakatoliki wengi wanashtuka. Hicho kinachojulikana sasa kama ‘wanamaombi’ au ‘wakarismatiki’, hata kama mtu angepinga kwa namna gani, ukweli ni kwamba kinafanana au kinaegemea zaidi kwenye ulokole kuliko kwenye Ukatoliki asilia.

Kwa maana nyingine ni kuwa zigo hilo ambalo adui aliliandaa ili kuwapata wanadamu, ilishindikana kuliingiza kwenye Ukristo. Lakini ni wazi kwamba zigo hilo lilienda kutua zimazima kwenye Uislamu – maana ni mambo yaleyale ambayo shetani alijaribu kuyafanya kwenye Kanisa miaka mingi kabla ya Uislamu kuwapo duniani, ndiyo sasa ni sehemu ya Uislamu.

Hata watu wasiokuwa tayari kukiri ukweli wa mambo wanajua kuwa walokole ni watu maalum sana katika dunia hii. Kwa nini wanakuwa hivyo? Ni kwa sababu wanasimama na Injili ya Kweli ya Bwana wa uzima, Yesu Kristo.

Hitimisho
Ni wakati sasa turudi kwenye swali letu la msingi. Je, Biblia ya kweli ina vitabu vingapi? Je, ni 73 au ni 66?

Katika makala haya nimekupatia mtiririko wa kihistoria – kimwili na kiroho. Je, wewe unadhani jibu la swali hilo ni nini? Bila shaka makala inaonyesha wazi jibu langu. Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo akubariki.

38 comments:

  1. Hii blog ungeitangaza zaidi(hata mitandao mingine ya kijamii)...naamini hii ndiyo kweli maana kwa hii najiona ni huru..Mungu akubaliki Mtumishi wa Mungu..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amen mpendwa. Asante kwa ushauri na Bwana akubariki. Njia mojawapo pia, ukiangalia mwisho wa kila makala, chini ya jina langu, kuna link ambazo zinaruhusu msomaji ku-email makala, kuisambaza kwa njia ya twitter, kuisambaza kupitia facebook, n.k. Kwa hiyo, ukiguswa na makala yoyote, tafadhali tumia njia hizo kusambaza neno hili. Ubarikiwe.

      Delete
    2. +MUNGU SAIDIA SANA, Dunia inaozeshwa na watu kama hawa, waliopandikizwa sumu na yule mwovu, wale ambao uhayawani unawasonga, wamechanagnyikiwa, au labda kichwani upstairs zao zina shida, wengine husoma sana na kuchanganyikiwa kama Padre wa ujerumani aliyechanganyikiwa, SIKU MOJA MUNGU ATAHUKUMU, Tutaongea sana siku ya mwisho Kristo atakuja atauliza je mmelifuata tuna imani bado?, na atauliza kama kweli tuliilinda imani tuliyoachiwa na mitume, watajidai sana, wakati biblia iliandaliwa na Mababa wa Kanisa Mama, Kanisa la Mwanzo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, biblia ya Kristo haikuja karne ya 16 wakati wa padre fulani, wala siyo wakati wa karne ya 18 wakati wa mama fulani au william huko marekani, bali ni tangu karne za kwanza!, Padre Jerome kwa kutumwa na Kanisa aliandaa vitabu hivyo, kwa hiyo kaka jipange usianganywe?

      Delete
  2. napata kujifunza mambo mengi sana MUNGU AKUBARIKI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amina. Uzidi kubarikiwa na Bwana Yesu. Asante kwa kutembelea blog hii na kutoa maoni yako.

      Delete
    2. Hellow John nimefurahishwa na mtirirko wa uandishi wako pamoja na kunifanya nibaki katika kweli huru kwa kila aaminiye. Nakupongeza kwa mtazamo wangu kuueleza umma haya mambo kwani tuliowengi wengi huwa hatuna muda wa kufanya jinsi ulivyoonyesha na kufafanua ukweli. Nataka kukushauri na kuomba msaada kwako kuwa unaweza kunitumia masomo yako katika blog hii kwa ajili ya kujisomea na kwa ajili kuongeza imani katika maisha yangu kwani bwana ndie mkombozi wa kila mmoja kwa aaminiye kweli na uzima? naomba kuna maswali utanijibu in box samahani

      Delete
    3. Shalom, shalom ndugu
      Asante kwa kutembelea blog hii na kutoa maoni yako.
      Umeuliza kuhusu kukutumia masomo,

      Kutokana na ufinyu wa muda na wingi wa majukumu, sitaahidi kukutumia masomo haya kwa haraka maana inabidi niyacopy yote na kuyageuza kuwa file la pdf kwa mfano.

      Ila nafikiri wewe nikumbushe tena tu kama ukiona muda umepita. Nitajitahidi kufanya hivyo. Lakini inabidi unitumie e-mail yako. Unaweza kuniandikia ujumbe kwenye WRITE TO BLOGGER FORM iliyo juu kulia kwa blog hii ---- au kupitia: ijuekweli77@yahoo.co.uk

      Delete
  3. Eish!!! Nimekipata kitu ambacho tangu nizaliwe kimwili na kiroho sija wahi kukipat,najisikia kuongezeka kiimani;Mungu akujalie mtumishi,akuongezeye siku za kuishi ilia aendelee kuziookoa roho zilizo potea kupitia wewe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amen. Jina la Bwana libarikiwe. Neema ya Bwana wetu Yesu ni kuu. Tuwaombee na wenzetu ili kwamba neema hiyo iweze kuwafikia na wao wamjue Mungu wa kweli atupendaye sana.

      Delete
  4. MUNGU akubariki!.Uwe na sabato njema.

    ReplyDelete
  5. Tazama umenyoosha kidole kimoja na vingine viemekugeukia.Tuache sisi tunaomheshimu Bikira Maria tuendelee na wewe umesongwa na Roho ya usengenyaji
    kiasi kwamba huoni boriti lilo usoni kwako ambalo sasa limepelekea baadhi ya watumishi kulitumia jina la Bwana Yesu kinyume na mipango ya Mungu huku wakijiita walokole.Laukana ungelimuomba Mungu akuonyeshe nini kinachoendelea ya ndani ulokole na leo hii Biblia Takatifu imegeuzwa kuwa mtaji kwa watumishi waliarijiwa kuzimu na duniani.Bado unawakati mgumu sana pia tunageuza na shavu lingine uongezee makofi.Kila la heri!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante kwa maoni yako ndugu. Ni kweli kuna wanaojiita watumishi na wanatumia Neno la Mungu kwa faida yao. Na jambo hilo ni dhambi kwa sababu linakwenda kinyume na kile kilichoandikwa kwenye Biblia. Kwa hiyo, hata wao nao hakuna anayewaunga mkono.

      Sasa, kama tukiwasema kuwa wako kinyume na Biblia, tutakuwa tunafanya usengenyaji? Kwa nini unadhani kusema kuwa kusema suala la Bikira Maria ni usengenyaji?

      Basi tusaidie kulingana na Maandiko (Biblia) uhalali, kwa mfano, wa kumwita Bikira Maria mwombezi wetu. Jambo hilo liko wapi kwenye Biblia?

      Yesu alisema wazi kuwa: Mimi ndimi njia na kweli na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi. Je, maneno "kwa njia ya mimi" yanamjumuisha na Bikira Maria?

      Delete
  6. Ni masikitiko makubwa sana kwa wale wanaomsifu Bwana Yesu na kumpa maisha lakini wamemtengema Mama yake eti alikuwa mwanamketu! Poleni sana kwani mnamsikitisha mno Bwana Yesu.Leo wake wa baadhi ya wachungaji wanaheshiwa makanisani mwao kiasi kwamba hawafanyi shughuli ye yote ila hutumikisha wamama washirika kupika,kufua na usafi kwa ujumla huku wakizisahau familia zao na kusubiri uponyaji kwa kutumikishwa hivyo.Waamini wengine wamehamishia mali zao kwa Wachungaji eti watabarikiwa wakati wameacha familia zao hazina kitu na uduni wa maisha ukiwakabili wakati Pastor anajiachia na familia yake katika raha maana kila anachohitaji waamini wanajikuna wanapeleka.watoto wao wanakosa ada ila wa Pastor wanasoma Vyuo vikuu kwa sadaka zao na mali za waamini wasiojitambua.Kosa ukiingia moja kati ya makanisa hayo milangoni kuna mambo makuu ya kutisha ya kuzimu na maji ya visima vya kubatiziwa yanatoka kuzimu sasa wewe muumini huna bahati pia walala hoi hawana maana wala hawakumbukwi na wachungaji wao.Tena mwiko masikini kuketi kiti cha mbele kwa sababu sadaka yake ni ndogo sana haitunishi mifuko.Haya yapo sana tumeyashuhudia na sisi tunaosengenywa tumekuwa msaada pindi wanapokuwa taabuni kwani hakuna anaetoka kanisani kwake kumsaidia.Idadi kubwa ya makanisa leo hii ina sababishwa na umimi kiasi kwamba wachungaji wanakosona kuhusu sadaka na mapato ya kanisa hivyo wanatawanyika na kuanza makanisa huku wakitangaza mchungaji fulani hafai kabisa anajitajirisha mwenyewe na baadhi ya wazee wa usharika,siongopei haya yametokea eneo ninaloishi hata tukagundua kanisa lina pastor asie na ndoa na waumini wengi mno ila ni walokole kisa wanasali kanisa lile.Mtumishi wajibika kwa undani.Martin Luther aliufikiria sana mwili wake akaona bora aanzishe dhehebu lake ili akamilishe hitaji la mwili wake.Mwanadamu wa leo tamaa za mwili zimemiliki akili yake na angenda ya wakatoliki itawatenga sana na Mungu kwani usengenyaji umezidi kiasi kwamba sisi wakatoliki tunaonekana kama wapagani.sasa kasome Marko 9:38.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mpendwa wangu, kitu chochote kilicho kinyume na Biblia ni kosa. Haijalishi anayefanya ni mlokole, mlutheri au mkatoliki. Katiba pekee ya wokovu wetu ni Biblia. Suala la madhehebu ni jambo tu la kuturahisishia kukutana na kufundishana na kusaidiana ktk safari yetu ya kuelekea mbinguni.

      Kama wewe uko Katoliki na unaishi sawasawa na Biblia, utakwenda mbinguni tu. Kama wewe ni mlokole (hata kama ni mchungaji au askofu) na unaishi kinyume na Biblia hauendi mbinguni.

      Ukisikia walokole haina maana kuwa ndani yake hakuwa waasi. Wapo. Tena wanaweza kuwa ni wachungaji kama unavyosema. Lakini uasi huo hautokani na kuwa walokole. unatokana na kukosa utii kwa neno la Mungu. Na waasi wako kila mahali. hata Kanisa Katoliki si wapo?

      Tatizo kubwa ninaloliona mimi si kuwapo kwa waasi. Tatizo ni pale mambo yasiyo ndani ya Biblia yanapofundishwa na watumishi au na kanisa kana kwamba ni maagizo ya Mungu.

      Delete
  7. Acha kfuatilia sana vitabu vya kale soma Agano Jipya ambalo linaelezea habari za mwamke pekee dunia aliechaguliwa na Mungu kuubeba Uzao uliolta ukombozi,acha dhihaka zidi ya Mama Bikira Maria tena ufanye toba kwani unakufuru maamuzi ya Mungu.Bikira Maria tunamheshimu ila hatumuabudu wala kumtukuza maana ni mwanadamu mwenzetu.Na kwa maelezo ya Malaika Gabriel alimwambia umebarikiwa kuliko wanake woteeeeeeeeeeeeeeeeeee hivyo utaheshimiwa kwa namna ya pekee.Mpendwa tazama hekalu lako ambamo hukaa Roho Mtakatifu wa Mungu mna baraka laana?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unachosema kuhusu Bikira Maria kubarikiwa kuliko wanawake wote hilo ni kweli kabisa maana hata Biblia inasema hivyo kama ulivyosema. Na hiyo ndiyo kanuni ya msingi ya kupima roho. Si tumeambiwa tusiamini kila roho bali tuzijaribu kwanza? Unajaribuje sasa? Unajaribu kwa kuangalia kama inaendana an Biblia.

      Sasa, Kanisa Katoliki linasema kuwa Bikira Maria ni mwombezi wetu. Ni wapi kwenye Biblia ilikosemwa hivyo? Badala yake Biblia inasema kuwa mtu akifa anakuwa hajui CHOCHOTE tena kinachoendelea huku duniani. Hawezi kuwa mwombezi. Mwombezi ni MMOJA TU - Yesu Kristo.

      Delete
    2. Mbona mmeshindwa kukikataa kitabu cha ufunuo wa Yohana. Ebu Soma basi ufunuo!

      Delete
  8. Kaka James, nashukuru sana kwa kuendelea kutoa elimu sahihi kwa roho nyingi zilizopotea. kimsingi mambo mengi sana uliyoyaandika humu ni ya msingi na yana ukweli. Mimi mwenyewe ni mkatoliki toka kuzaliwa, nikimaanisha nimezaliwa kwenye familia ya kikatoliki na kukulia humo. ukweli ni kwamba familia nyingi za kikatoliki hawasomi Bibllia takatifu na kuitafakari kwa undani; kwa sababu ya malezi ndani ya kanisa wengi tumezoea kulishwa tu kama ulivyo sema na huo ndio ukweli; wengi tunaamini kila kitu kilichoelekezwa kwetu toka juu kwa kisingizio kuwa hili limetoka juu na hivyo hakuna mwenye haki ya kuhoji chochote zaidi ya kuichukua kama ilivyo. Namshukuru sana Mungu kwamba amenipa shauku ya kutaka kufahamu mambo kwa undani na kujua ukweli, kwani hata neno linasema tuijue ile kweli na kweli ndiyo itakayotuweka huru na si vinginevyo. katika kutafuta ukweli, nimekuja kugundua mengi sana na mengi bado nagundua hata kupita blog hii, namshukuru Mungu-nimefikia uamuzi ambao bado naendelea kumwomba Mungu aniongoze sawa sawa kuwa nitasimama katika neno la Mungu peke yake yaani Biblia, habari ya mapokeo, hayo yaliandikwa na mwanadamu kwa malengo na madhumuni yao wenyewe, na pengine ndio mpango wa shetani kama ulivyotoa angalizo.Napenda kumshauri huyo anonymous kuwa asipende kushikilia kila kitu kama kilivyo eti kwa sababu ameyakuta hivyo, Mungu katupa akili, utashi, uelewa na ujuzi wa kuhoji mambo-namshauri asiridhike na alichonacho bali apende kusoma, afanye tafiti kuhusu kile anachoamini kama kweli ni mpango wa Mungu-Yesu alisema, "Mimi ndimi njia, kweli na uzima, mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi" na ndivyo ilivyo, hakudelegate power kuwa tukiona kwakwe inakuwa ngumu tuombe kupitia kwa mama yake au kwa wafu (ambao wanatambulika kama watakatifu). Huo si mpango wa Mungu, na siamini kuwa maombi yangu yanaweza kufika kwa Mungu kupita kwao bali kwa kupitia kwa Yesu pekee. Hayo mambo mengine ni mpango wa shetani na kwa sababu wakatoliki wengi sana hawapendi kulisoma neno la Mungu na kutafakari na kuomba msaada wa roho Mtakatifu awaongoze, wengi wamekuwa wakishikilia na kuamini hicho wanachoamini kwa sababu ndivyo walivyovikuta na hakupaswi kuwa na marekebisho. ni wakati wa kumtafuta Yesu kwa nguvu zetu zote, kwa akili zetu zote na kwa utashi wetu wote, tuache kuamini kwa mazoea bali tutafute maarifa maana neno la Mungu lasema "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" ina maana wengi hawapendi kusoma, kutafakari, na kuhoji mambo kwa msaada wa Roho wa Mungu kama kweli wanachoamini kimetoka kwa Mungu au la. Mimi Binafsi Bikira Maria namheshimu kama mama wa mwokozi wangu Yesu, na ni mama aliyepewa heshima kubwa sana na Mungu lakini nachelea kusema kuwa hakuna popote palipoandikwa kuwa tuelekeze maombi yetu kwa Mungu kupita yeye. labda ndugu yangu huyu aje na ushahidi kamili kuhusu hili la kuonesha kuwa tunapaswa kuelekeza maombi yetu kwa Mungu kupitia wafu. Anachoeleza kaka James, namuunga mkono, si usengejaji bali ni kunyoosha ukweli na kutoa ukakasi ambao umetutanda kwa kipindi kirefu sana na bado tunaendelea kungangania.wokovu ni hapa duniani na Mungu anapendezwa zaidi na watakatifu waishio duniani neno la Mungu lasema hivyo. maana yake nini; usitegemee ukaishi maisha ya upotevu hapa duniani alafu ukifa utegemee utaombewa na walio hai ili usamehewe dhambi, kwa uelewa wangu hili si sahihi kutokana na neno la Mungu linavyoelekeza. Ukishakufa ndio umeondoka kama ulivyo na hakuna nafasi tena ya kubadilika, na ndio maana Yesu alipokuwa anaeleza habari ya tajiri na lazaro; aya moja inasema tajiri baada ya kuona mateso yanakuwa makali kule jehanam, alitamanni ndugu zake wapate habari kuhusu alipo kuwa waishi maisha mazuri ya kumpendeza Mungu wasije wakaishia kama wao,Yesu anatuambia nini hapa; anatueleza kuwa ukifa hakuna nafasi ya kubadilika na kuwa na hali tofauti na ulivyokufa, kama ulikufa mdhambi inabaki hivyo, kama ulikufa mtakatifu inabaki hivyo.nafasi pekee ya kubadilika na kujiweka nafasi ya kuokoka ni hapa hapa duniani tungali hai. ukishakufa huna nafasi hiyo tena,

    Tumsifu Yesu Kristu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Milele amina Henry. Ashukuriwe sana Bwana Yesu na Roho Mtakatifu kwa kukupa mwanga wa Injili wa ajabu namna hii. Mambo uliyoyasema humu ni makubwa sana kiasi kwamba hata sina cha kuongezea bali Neno hilo ambalo Bwana ameweka ndani yako lizidi kukua na kuzidi hadi utimilifu wa Kristo.

      Ni kweli kabisa KATIBA YETU NI BIBLIA. Kama jambo halimo humo na kuna mtu analifundisha, basi hatuna kabisa sababu ya kulikubali. Ni hatari sana kwetu kuruhusu mafundisho yaliyo nje ya Biblia kuingia mioyoni mwetu.

      Ubarukiwe sana Henry.
      Endelea kusonga mbele katika Neno/katika Kristo.

      Delete
  9. Kaka James, nashukuru kwa kunitia moyo katika safari ya kuuendea ukweli na uzima. naomba usinisahau kila siku ya maombi yako, uiombee familia yangu tafadhali ili Mungu azidi kutuongoza kwa neema zake. Hakika katika kusimamia ukweli changamoto ni nyingi na ndiomaana nakuomba uniombee/utuombee ili Yesu atuongoze katika ile kweli.

    Pia katika sala zako, naomba uwakumbuke wakatoliki wote na wale wote wanaoamini ktk mafundisho ya upotoshwaji bila kujisumbua kutafuta ukweli, ni kama wamefungwa na wanaridhika na kila wanachoambiwa. Naamini sala na maombi pekee ndio yenye uwezo wa kuzifungua roho zilizofungwa.

    Mungu akubariki sana kaka James kwa kueneza injili yake kwa watu hasa wale ambao bado hawajamjua vizuri.

    ReplyDelete
    Replies
    1. amen Henry. ubarikiwe na Bwana na Nuru yake uendelee kuangaza kwako (maana Neno lake ndiyo taa ya miguu yetu katika safari hii tuliyo nayo).

      Delete
  10. Ndugu yangu James umekuwa mwalimu mzuli sana katika kufundisha watu, lakini neno la Mungu linatuonya kujipiga kifua. Mimi ni Mkatoliki ila nazani nawe ni mlokole kama sijakosea. Ningependa kujua ina maana yote mnayofanya katika Ibada yameandikwa kwenye Biblia??????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tumsifu Yesu Kristo ndugu yangu. Ni kweli mimi ni mlokole. Ninaamini kabisa wako wakatoliki wengi watakaoingia mbinguni kwa Bwana Yesu; na ninaamini wako walokole wengi watakaoingia jehanamu.

      Pia nakubaliana kabisa na wewe kuwa yako mambo mengi yanayofundishwa kwenye makanisa ya wokovu ambayo hayajaandikwa kwenye Biblia.

      Mtazamo wangu hata hivyo (japo huenda nimekosea bila kujua na nitashukuru ukinisahihisha) ni huu: Kama kuna jambo ambalo liko ndani ya Biblia TAYARI halafu akaja mtu anafundisha jambo ambalo: 1. haliko kwenye Biblia 2. Linapingana na jambo lililoko kwenye Biblia, basi, fundisho hilo ni la uongo na halitakiwi kuaminiwa.

      Kwa mfano, fundisho la kwamba Bikira Maria ni mwombezi wetu; au kwamba watakatifu (yaani wafu) wanaweza kutuombea ni kinyume kabisa na maandiko ambayo tayari yamo kwenye Biblia:

      (Mhu 9:5) kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala HAWANA IJARA TENA; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.


      (1Tim 2:5) Kwa sababu Mungu ni mmoja, NA MPATANISHI KATI YA MUNGU NA WANADAMU NI MMOJA, Mwanadamu KRISTO YESU.

      Lakini kuna mambo ambayo hayajatajwa kwenye Biblia, yanafundishwa na hayaleti upinzani wowote na Biblia; na ni mazuri. Je, kuna tatizo kuhusu hayo? Mimi nadhani hakuna.

      Kwa msingi huu ninaousema, hata kama kuna makanisa ya kilokole ambayo yanafundisha mambo yaliyo kinyume na Biblia, ni kosa vilevile. Mimi sitetei ulokole au kupinga ukatoliki. Mimi sikubaliani na mafundisho ambayo kiukweli ni potofu.

      Ubarikiwe na Bwana

      Delete
    2. Kwa mfano, fundisho la kwamba Bikira Maria ni mwombezi wetu; au kwamba watakatifu (yaani wafu) wanaweza kutuombea ni kinyume kabisa na maandiko ambayo tayari yamo kwenye Biblia:

      (Mhu 9:5) kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala HAWANA IJARA TENA; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Endelea mstari wa sita "Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lolote LILILOFANYIKA chini ya jua" Mathayo 17 kuanzia mstari wa kwanza pale hadi wa nne tunaona Musa na Elia wakimtokea Yesu. Ngoja nikuulize swali, Kama mhubiri isemavyo "HAWANA IJIRA TENA" kutokana na huo mfano unasemaje hapo??? Na kuhusu Bikira Maria nitakuuliza

      Delete
    3. Kwanza ningependa kujua maana ya IJARA

      Delete
    4. ijara maana yake mshahara au malipo. Hii ni kusema kuwa sisi tulio hai tukiamini au tukiomba, Mungu "anatulipa" yaani anatujibu. Bwana Yesu anasema: Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. (Ufu 22:12).

      Hii ina maana anakuja kulipa ujira (au ijara) kwa YALE YALIYOTENDWA NA MTU ANGALI HAI, SIO AKIWA AMESHAKUFA. MFU HANA IJARA TENA!!

      Yaani, mfu hawezi akaomba akakuombea akajibiwa. YESU HANA MSHAHARA/MALIPO/IJARA/UJIRA KWA AJILI YA WAFU.

      Delete
    5. Vivyo hivyo, huwezi ukamwombea mfu na akaingiziwa malipo kwenye akaunti yake ya mbinguni. UKIFA AKAUNTI HIYO INAFUNGWA!!

      Delete
    6. Umeniuliza kuhusu Musa na Eliya; nikisoma kuhusiana na wao, sioni kama walitokea huku ili kuja kunenepesha "akaunti" zao za mbinguni.

      Kumbuka kuwa, ninaposema hawana ijara, simaanishi kuwa hawako hai. Kufa ni kuvua tu hili gwanda la nyama na mifupa na kuvikwa mwili mwingine wa kiroho - na bado mtu anaendelea kuwa hai kabisa - tena zaidi ya sasa.

      Lakini kutokuwa na ijara inamaanisha tu kwamba kile ulichovuna katika maisha yako hapa duniani hakibadiliki tena kuanzia pale unapokufa. Na ndiyo maana hata fundisho la watu kuwa toharani ni la uongo na kuwapa watu matumaini ya upotovu na ya hatari.

      Delete
    7. Ndugu yangu James tafakari kwako ni ngumu sana na sipendi kulumbana katika Imani, cha muhimu amini unachoamini, usizani Mapadri kusomea Upadri zaidi ya miaka saba ni jambo dogo. Ila nakuambia ujue kuwa Wakristu Wakatoliki hawakatazwi kusoma Biblia hata siku moja. Tangia nimezaliwa mpaka leo ninaishi kwa kusoma Biblia. Kanisani tunaenda kupewa tafakari tu ya neno la siku na tafakari zaidi ni wewe na nafsi yako. Sitaki kuzungumza chochote kuhusu walokole bt nakusihi usimhubiri Yesu kwa kujiona mwema kama unavyodai wewe kwa maneno yako haya " Kwa nini katika hali ya kawaida tu mlokole anapofanya kosa anashambuliwa ZAIDI kuliko mtu mwingine anapofanya kosa lilelile?

      Japokuwa washambuliaji hawatakiri waziwazi, lakini mioyoni mwao wanajua fika kwamba ulokole (wokovu) ni maisha tofauti kabisa na dini zilizozoeleka au zenye majina makubwa. Ndiyo maana utasikia:
      · Yaani hata walokole nao wanapigana?
      · Mlokole gani huyo analewa pombe?
      · Mlokole atakuwa huyo? Mbona kanidhulumu fedha zangu?, n.k.

      Na wala hutaona kwenye magazeti wameandika: Mkatoliki/Mlutheri/ Mwislamu kakamatwa ugoni! Hiyo si habari inayoweza kuuza gazeti. Lakini je, huawahi kusoma: Mlokole kashikwa ugoni? Hiyo ndiyo habari. Ni kwa nini? Yesu angekuwa anahubiri kama nyinyi watu wangemkataa zaidi.Samahani lakini kama nimekuuzi, Na kuhusu Bikira Maria hatumwabudu ila tunaheshimu heshima yake kama Mama aliyemzaa mkombozi wetu Yesu, Pia Rozari unayosema haipo kwenye Biblia ni kweli kabisa, lakini sisi tunasali Rozari kufuata waliotutangulia maana walijibiwa maombi yao. Tena nakuambia Rozari ina nguvu sana ya Mungu, mimi mwenyewe nimeshuhudia hilo. Mungu akubariki sana kwa kazi yako lakini usiongee vitu usivyovijua unakuwa unakufuru

      Delete
  11. Kwa aliye uliza kuonekana kwa Musa na Eliya kunakotajwa katika Math 17 wakati biblia imetaja wafu hawana ijara tena:

    KWA UFUPI: Tukio hili limetajwa na waandishi watatu yaani Mathayo, Marko na Luka, kila mmoja kwa ufahamu na ufafanuzi wake, Luka katika 9:31 kuna kitu anaongezea pale; “walioonekana katika utukufu, wakanena habari za kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemu”.
    Tukuo lile Ilikuwa kiwakilishi cha cha kitakachofuata baada ya hitimisho la safari ya ukombozi wa mwanadamu. Ebr 9:28 “kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu”.

    Alionekana katika utukufu - aliwakilisha utukufu atakaokuwa nao atakapokuja mara ya pili ambao ni utukufu wa baba yake na malaika watakatifu, Math 25:31.

    Musa - alitokea kuwakilisha watu wenye haki watakaofufuka katika ufufuo wa kwanza. 1 kor 15:52
    Eliya - aliyepewa hadhi ya kutoonja mauti, akachukuliwa mbinguni bila kufa, alikuja kuwakilisha watakatifu watakaotwaliwa wakati wa kurudi kwake yesu mara ya pili bila kuonja mauti 1 kor 15:51 1Thes 4:15

    NB: Lakini ujue kuwa japo Musa alipitia mauti hayuko kaburini akisubiri kufufuliwa, itakumbukwa kuwa tangu mapema Musa alijua jina lake limeandikwa katika kitabu cha uzima Kut 32;32, Yesu mwenyewe (ambaye wakati mwingine hutajwa kama Mikael- malaika mkuu Dan 12:1, Uf 12:7) alishamtoa kaburini, yuda 1:9

    ReplyDelete
  12. Msikubal kubishana na wajinga, kwa maana kuna wajinga wengne hawajui na hawajui kwamb hawajui na hawatak kutaka kujua. Je, mwerevu ukibishan na mjinga hipi itakuwa tofaut ya mjinga na mwerevu? Ndugu zangu tafuten kuelewa na si kubishan. Tumsifu yesukristo

    ReplyDelete