Utangulizi
Rafiki yangu Ibra, amekuwa akinishambulia sana kwa kusema
kuwa Biblia ni kitabu kisichoaminika bali Quran ndiyo inayopaswa kuaminiwa.
Hoja yake kuu, kama ilivyo kwa Waislamu wengine wengi ni kwamba, Biblia
imeingizwa maneno ya kibinadamu kiasi kwamba yale ambayo Mungu aliyateremsha ni
kama hayapo tena leo.
Katika makala haya ninapenda tuangalie swali kwamba:
Je, ni kweli Quran ni kitabu ambacho hakijawahi kubadilika? Je, ujumbe wake
ndio uleule ambao aliteremshiwa Muhammad na Allah? Je, ni kitabu cha kuaminika
kuliko Biblia kama wanavyosema Waislamu?
Quran
iliandikwaje?
Ni jambo linalofahamika wazi kwamba Muhammad hakujua
kusoma wala kuandika, hivyo japokuwa aya za Quran ziliteremshwa kwake, si yeye
aliyeandika kitabu cha Quran. Badala yake aya hizi zilikuwa zikiandikwa kwenye
sehemu mbalimbali na wafuasi wake, kwa mfano kwenye mawe, mifupa ya wanyama,
majani ya miti, n.k., na hasa kwa kukaririwa na watu mbalimbali. Kwa hiyo, hadi
Muhammad anauawa (maana alikufa kwa kunyweshwa sumu – unaweza kusoma HAPA),
hakukuwa na kitabu cha Quran kama tukijuavyo leo. Hata hivyo, idadi kubwa ya
watu waliokuwa wamekariri aya nyingi za Quran waliuawa kwenye vita vya Yamama mwaka
632 BK – soma zaidi HAPA.
Hatimaye Abu Bakr, ambaye alikuwa ni khalifa wa kwanza,
alitoa agizo la kukusanywa kwa aya za Quran toka sehemu mbalimbali ili ziweze
kufanywa kitabu. Aliyepewa kazi hiyo aliitwa Zayd ibn Thabit. Zayd alikamilisha
kazi hiyo mwaka 634. Abu Bakr alibaki na kazi hiyo hadi alipokufa. Ndipo
ilikabidhiwa kwa khalifa Umar. Naye alipokufa, ilikabidhiwa kwa mjane wa
Muhammad aliyeitwa Hafsa.
Miaka takriban 20 baada ya kifo cha Muhammad, wakati wa
khalifa Uthman kulitokea mabishano juu ya namna sahihi ya usomaji wa aya za
Quran. Uthman aliagiza kuwa ile nakala ya Hafsa pamoja na maandiko mengine
mbalimbali ya Quran yakusanywe ili iweze kuandikwa nakala rasmi. Kazi hiyo
ilifanywa na Zayd ibn Thabit, Abdullah bin Az-Zubair, Sa’id bin Al-As na
Abdur-Rahman bin Harith. Hii ndiyo kazi ambayo imekuja kuzaa Quran iliyopo leo.
Baada ya kuikamilisha kazi ile, tunaambiwa katika Sahih
al-Bukhari 4987: “Uthman sent to every Muslim province one
copy of what they had copied, and ordered that all the other Qur’anic
materials, whether written in fragmentary manuscripts or whole copies, be
burnt.”
Yaani: Uthman alipeleka kwenye kila jimbo la Kiislamu
nakala moja ya Quran ile, na akaagiza kuwa maandiko mengine yote ya Quran, yawe
ni vipande vidogo vya miswada au nakala kamili, vichomwe moto.
Je,
waislamu wote waliikubali Quran ile?
Tunaposoma katika Sahih al-Bukhari
3808, tunaelezwa maneno aliyowahi kutamka Muhammad akisema: “Learn the
recitation of the Qur’an from four: from Abdullah bin Masud, Salim, Mu’adh bin
Jabal and Ubai bin Ka’b.”
Yaani: “Jifunzeni maneno ya Quran kutoka kwa watu wanne:
Abdullah bin Masud, Salim, Mu’adh bin Jabal na Ubai bin Ka’b.” – nadhani unaona
kuwa hapa Zayd ibn Thabit si mmoja wao.
Unadhani ni kwa nini Muhammad aliagiza kuwa watu wajifunze
Quran kutoka kwa hawa aliowataja? Nafikiri jibu ni kuwa kati ya wafuasi wake
wote, Muhammad alijua kuwa hawa ndio wenye Quran sahihi.
Nini basi kilitokea baada ya jopo la akina Zayd
kumaliza kazi yao? Abdullah ibn Masud, ambaye ni mmoja wa wale wateule wanne wa
Muhammad, alitamka maneno yafuatayo ambayo yamenukuliwa kwenye Ibn
Sa’d, Kitab al-Tabaqat al-Kabir, Vol. 2, p. 444:
“The people have been guilty of deceit in the reading of the
Qur’an. I like it better to read according to the recitation of him whom I love
more than that of Zayd Ibn Thabit.”
Yaani: “Watu wana hatia ya udanganyifu katika kusoma Quran.
Napenda zaidi kusoma kulingana na jinsi yeye [yaani Muhammad] alivyosoma,
ambaye ninampenda zaidi kuliko kusoma ile ya Zayd ibn Thabit.”
Haya ni maneno ya mtu aliyeishi pamoja na Muhammad, alisikia
Quran kutoka kwenye kinywa cha Muhammad na alitajwa na Muhammad kuwa watu
wanatakiwa kuzipata aya sahihi kutoka kwake! Maana ya maneno yake iko wazi –
kuwa Quran iliyoandaliwa na akina Zayd ni potofu.
Ibn Masud hakuishia hapo. Tunasoma katika Jami At-Tirmidhi 3104 kuwa ibn Masud
alitamka pia kuhusiana na kazi ya Zayd: “O you Muslim people! Avoid copying the
Musahaf and recitation of this man. By Allah! When I accepted Islam he was but
in the loins of a disbelieving man.”
Yaani: Enyi Waislamu! Epukeni kunakili msahafu wala kukariri
maneno ya mtu huyu. Kwa Allah! Wakati nilipoukubali Uislamu alikuwa bado kwenye
viuno vya mtu asiyeamini.
Je, kila aya
iliyotoka kwa Allah imo ndani ya Quran?
When
Ibn Umar—son of the second Muslim caliph—heard people declaring that they knew
the entire Qur’an, he said to them: “Let none of you say, ‘I have learned the
whole of the Koran,’ for how does he know what the whole of it is, when much of
it has disappeared? Let him rather say, ‘I have learned what is extant
thereof.’”
Yaani:
Ibn Umar – mwana wa khalifa wa pili katika Uislamu – aliposikia watu wakisema
kuwa waliijua Quran yote, aliwaambia: “Asiwepo mtu wa kusema, ‘Nimejifunza
Quran yote,’ maana awezaje mtu kujua Quran yote ni kiasi gani, wakati kiasi
kikubwa kimeshapotea?
Katika
Sahih Muslim 2286, tunasoma maneno
yafuatayo: Abu Musa al-Ash’ari sent for the reciters of Basra. They came to him
and they were three hundred in number. They recited the Qur’an and he said: You
are the best among the inhabitants of Basra, for you are the reciters among
them. So continue to recite it. (But bear in mind) that your reciting for a
long time may not harden your hearts as were hardened the hearts of those
before you. We used to recite a surah which resembled in length and severity to
(Surah) Bara’at. I have, however, forgotten it with the exception of this which
I remember out of it: “If there were two valleys full of riches, for the son of
Adam, he would long for a third valley, and nothing would fill the stomach of
the son of Adam but dust.” And we used to recite a surah which resembled one of
the surahs of Musabbihat, and I have forgotten it . . .
Yaani:
Abu Musa al-Ash’ari aliagiza waletwe wanaokariri kutoka Basra. Walikuja kwake
nao walikuwa mia tatu. Walikariri Quran, naye akasema: Ninyi ni watu bora
kabisa miongoni mwa wakazi wa Basra, maana ninyi ni watu mnaokariri (Quran)
miongoni mwao. Hivyo, endeleeni kuikariri. (Lakini kumbukeni) kwamba kukariri
kwenu kwa muda mrefu kusije kukafanya mioyo yenu iwe migumu kama ilivyokuwa kwa
wale waliokuwa kabla yenu. Tulikuwa tukikariri sura inayolingana kwa urefu na
ukali na (sura) Bara’at. Hata hivyo, nimeshaisahau, ukiacha hii ambayo
nakumbuka kidogo: “Kama kungekuwapo mabonde mawili yaliyojaa utajiri, kwa ajili
ya mwana wa Adamu, angetamani bonde la tatu, na wala hakuna kitu ambacho
kingejaza tumbo la mwana wa Adamu isipokuwa mavumbi.” Na tulikuwa tukikariri
sura ambayo ilifanana na mojawapo ya sura za Musabbhihat, na nimeshaisahau …
Haya
sasa. Wajuzi wa Quran walishasahau kile walichokuwa wanakifahamu. Lakini Abu
Musa analenga kuwaambia nini hawa watu 300? Anachowaambia ni kwamba:
“Nimewasikia mlivyokariri enyi watu wote 300. Lakini kuna sura mbili ambazo
hamzifahamu. Lakini tatizo ni kwamba hata mimi sizikumbuki. Zilishanitoka.”
Swali
kwa waislamu: Kama Quran ni ujumbe wa Mungu wa mbinguni, je, bado mna ujasiri
wa kusema kuwa ina kila kitu? Na inawezekanaje Mungu akaleta ujumbe ambao
alijua kuwa watu watausahau? Najua kuwa Quran pia inasema kuwa Mungu wa Quran
huwa anawasahaulisha watu wake aya (ambalo nalo ni jambo la ajabu – sijui
anakuwa anazileta za nini sasa?)
Abu
Ubaid katika kitabu kiitwacha Kitab Fada’il-al-Qur’an naye anatuambia maneno muhimu yafuatayo: A’isha
. . . said, “Surat al-Ahzab used to be recited in the time of the Prophet with
two hundred verses, but when Uthman wrote out the codices he was unable to
procure more of it than there is in it today.”
Aisha
alikuwa ni mke wa Muhammad mwenyewe. Hapa anasema: Surat al-Ahzab ilikuwa
ikisomwa wakati wa Mtume ikiwa na aya mia mbili, lakini Uthman alipoandika
kitabu hakuweza kupata zaidi ya ilivyo leo.
Sura
al-Ahzab ina aya 73 leo. Ina maana kuwa kuna aya 127 zenye ujumbe wa Allah
ambazo zilipotea. Je, bado utasema kuwa Quran ni kitabu cha kuaminika?
Tunasoma
pia kutoka Sunan Ibn Majah 1944 kuwa:
It was narrated that Aishah said: “The Verse of stoning and of breastfeeding an
adult ten times was revealed, and the paper was with me under my pillow. When
the Messenger of Allah died, we were preoccupied with his death, and a tame
sheep came in and ate it.”
Yaani:
ilisimuliwa kwamba Aisha alisema: “Aya inayohusu kupiga mawe na kunyonyesha mtu
mzima mara kumi ilifunuliwa, na karatasi hiyo ilikuwa chini ya mto wangu.
Wakati Mjumbe wa Allah alipokufa, tulikuwa tumebanwa na shughuli kifo chake, na
kondoo aliingia ndani na kuila.”
Swali
kwa Waislamu? Je, aya hii anayoisema Aisha imo kwenye Quran leo? Jibu ni kuwa
haimo. Ilikwenda wapi? Ililiwa na kondoo.
Je,
hoja yenu kwamba Quran tangu ishushwe na Allah haikuwahi kubadilika hata
kidogo; hata nukta; je, ni hoja ya kweli?
Je, kila alichosema Muhammad kiliandikwa kama alivyosema?
Muhammad alikuwa na waandishi ambao walikuwa pia wakiandika aya alizokuwa anapewa na Allah. Mmojawapo wa waandishi hao alikuwa ni Abdullah ibn Sarh. Hivi ndivyo anavyosema Abdullah kama tunavyosoma kutoka kwenye Al-Sira kilichoandikwa na al’-Iraq:
"I used to direct Muhammad wherever I willed. He would dictate to me 'Most High, All-Wise', and I would write down 'All-Wise' only. Then he would say, 'Yes it is all the same'. On a certain occasion he said, 'Write such and such', but I wrote 'Write' only, and he said, 'Write whatever you like.'"
Yaani: “Nilikuwa nikimuongoza Muhammad kokote nitakako. Yeye angeniambia ‘Aliye Juu Sana, Mwenye Hekima Yote’, na mimi ningeandika Mwenye Hekima Yote’ peke yake. Kisha angesema, ‘Ndiyo, hata hivyo ni sawa tu.’ Wakati fulani alisema, ‘Andika hivi na hivi,’ lakini mimi niliandika tu ‘Andika,’ naye akasema, ‘Andika chochote utakacho.’”
Je,
hivi mtu anawezaje kuwa na ujasiri wa kusema kuwa Quran ni kitabu
kinachoaminika? Kama kuna mambo mengi kiasi hiki ambayo yamepotea, utakuwa na uhakika gani kwamba unatimiza yote yanayotakiwa mtu ayafanye ili uweze kwenda mbinguni?
Kimsingi, Abdullah ibn Sarh yeye alipoona kuwa kumbe anaweza kuandika mambo na Muhammad akayakubali wakati yeye, Abdullah, anajua kuwa yametoka tu akilini mwake, aliamua kuachana na Uislamu na kumtoroka Muhammad!
Kimsingi, Abdullah ibn Sarh yeye alipoona kuwa kumbe anaweza kuandika mambo na Muhammad akayakubali wakati yeye, Abdullah, anajua kuwa yametoka tu akilini mwake, aliamua kuachana na Uislamu na kumtoroka Muhammad!
Tafakari
Jihoji
Chunguza mambo
YESU ANAKUITA AKUPE UZIMA
YESU ANAKUITA AKUPE UZIMA
.......................................................
Kwa ajili ya kupanua maarifa na ufahamu juu ya somo hili, soma pia makala yanayopatikana HAPA juu ya ugunduzi wa nakala za zamani sana za Quran zilizogunduliwa kwenye msikiti mmoja wa kale kule Sana'a, Yemen. Ukishamaliza kusoma makala haya, kama wewe ni Mwislamu, hautabaki kama ulivyokuwa kamwe!
Hii kali,Mungu akubariki mtumishi.
ReplyDeleteAmina. Bwana akubariki nawe pia Yusufu.
Deletesomo zuri
ReplyDeleteAmen ndugu. Bwana Yesu akubariki.
DeleteHizo hadithi zote ni za uongo hakuna hata hadithi moja hapo ni ya ukweli. Ni maneno ya Makafiri maneno ya uzushi tuonyesheni ni Aya ipi iliyosahauliwa? Mutupe na ushahid wenu? musilete hadithi za kikafiri za kuuzulia Dini ya Kiislam maneno ya uongo.
ReplyDeleteHa, Mzizimkavu hatimaye umerudi na kuonekana tena. Tangu tukutane mwaka jana; sijui mwaka juzi kabisa? Ulileta hoja kwamba Mkutano wa Nicea ndio uliotunga na kuingiza suala la Roho Mtakatifu kwenye Biblia. Nilikujibu na haukuonekana tena. Leo umezukia hapa. Karibu sana. Kumbe kina Sahih Muslim, Al-Sira, n.k. ni vitabu vya kikafiri?
DeleteRafiki yangu Mzizimkavu, HUWEZI KUSHINDANA NA KWELI. Hata ukikasirika hadi uwe mwekundu, itakutafuna na kukubwaga tu. Uislamu katu hauna msingi thabiti wa kusimamia. Umesimama juu ya mchanga. Na ni LAZIMA utaanguka tu mwishowe.
Kutoamini kwako; kuchukia kwako; n.k. hakubadili hali halisi. Quran haiaminiki kamwe na wala si Neno la Mungu Muumba wa vyote. SIO!!!
mzizimkavu mi nafatilia sana hii blog na ninajifunza mengi kiukweli hebu uthibitishie umma ya kwamba hadith hizo ni za kikafiri na za uongo ili tuweze kujua ukweli na pia utuambie ni kigezo au sababu gani inayotumika kukubali baadhi ya hadith na kubatilisha baadhi ya hadith ile hali quran tukufu inatuelekeza kusoma hadith. Kireri apa nawasilisha
ReplyDeleteUbarikiwe Kireri kwa kuwa na shauku na juhudi ya kuitafuta Kweli. Hata Maandiko yanasema: Heri wenye njaa na kiu ya haki maana hao watashibishwa. Mungu akufungulie mlango wa rohoni ili Yeye mwenyewe akupe uhakika wa upi ni ujumbe wake.
Deleterose...ahaaaa kumbe alinyweshwa sumu... eheeee kweri auaye kwa upanga ufa kwa upanga khaaa... aliwakosea nini hao wafuasi wake jamani. mhh alikuwa mwizi, muuaji au wakaona wampumzishe maana angewamaliza . khaa ehee Yesu wangu nisaidie kuijua kweri ili siku moja nije niuridhi ualme wa mbingu uliotuahidia
ReplyDeleteShalom dada Rose,
DeleteBwana akuzidishe katika kumjua Yeye aliye wa Pekee Mwokozi wetu wa milele.
Akushike mkono hadi mwisho wa safari; umalize kwa ushindi na ukamilifu ndani yake Yeye.
Unamzungumzia bwana Yesu
DeleteMbona mwenyewe alishindwa kujiokoa mpaka akatundikwa
Hakika moto unakusubiri,unapotosha umma kwa faida kidogo za kidunia?unasahau kuwa akhera ni ya milele na yenye kubakia?
ReplyDeleteYesu anakuita akakupe uzima...!
ReplyDeleteYeye mwenyewe alishindwa kujiokoa mpaka akatundikwa kwenye msalaba
Tafakari hayo maneno yako
Yesu anakuita akakupe uzima...!
ReplyDeleteYeye mwenyewe alishindwa kujiokoa mpaka akatundikwa kwenye msalaba
Tafakari hayo maneno yako