Sunday, April 20, 2014

Je, Yesu Alitumwa kwa Israeli Peke Yake?




Waislamu “wanahubiri” kuwa Yesu  hakuja kwa ajili ya ulimwengu wote bali alikuja kwa ajili ya Wayahudi peke yao. Kisha wanasema kuwa Muhammad ndiye mtume sahihi kwa sababu huyo alikuja kwa ajili ya ulimwengu wote. Andiko wanalotumia kupinga utume wa Yesu kwa ulimwengu ni lile alilolisema Yesu wakati akiongea na mwanamke Mkananayo (yaani asiye Myahudi), ambaye alikuwa anaomba Yesu amponye mwanawe.

Imeandikwa:
Akajibu akasema,  Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:26).

Friday, April 18, 2014

Eti Wakristo Hula Mkate Wenye Mavi (au Mashonde)





Waislamu wanaojaribu kuitoa makosa Biblia bado wanaendelea na mahangaiko yao ya kujaribu kuipa uhalali quran kupitia upotoshaji mkubwa wa Maandiko ya Biblia. Kama kwaida, hawana hoja mpya wala za kufikirisha, bali ‘wana-recycle’ maswali yaleyale toka januari hadi desemba. Haya ni maswali ambayo yalibuniwa na watu fulanifulani, basi na wao wanayabeba bila hata ya kuchuja na kujua endapo yana ukweli au la. Hata hivyo, kila jambo wanalolisema kinyume na Biblia ni UONGO mtupu SIKU ZOTE - NA USHAHIDI WA UONGO HUO TUNAO WAZIWAZI!

Katika kitabu cha Ezakieli imeandikwa:

…. Nawe utakila kama mkate wa shayiri, nawe utakioka mbele ya macho yao juu ya mashonde yatokayo katika mwanadamu. (Eze 4:12).
[Maana ya mashonde ni kinyesi]

Monday, April 7, 2014

Je, Yesu alisema kuwa Yeye ni Mungu?




“Wahubiri wa injili” wa Kiislamu huwa wanapinga kuwa Yesu ni Mungu na unapowakatalia wanakwambia, “Lete andiko.” Maandiko yapo mengi sana ndani ya Biblia juu ya ukweli kwamba Yesu ni Mungu. Ni mengi mno!

Ukishawapa andiko, wanabadilika na kusema, “Nataka maneno aliyoongea Yesu mwenyewe.”

Hiki ni kigezo POTOFU na si cha kibiblia hata kidogo. Ukweli ni kwamba, Biblia YOTE ni Neno la Mungu. Haijalishi amezungumza Musa, Isaya, Yohana, Petro au Yesu mwenyewe. Imeandikwa:
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. (2Petro 1:21).


Hivyo, kudai kwao eti, “Nataka maneno aliyosema Yesu mwenyewe,” ni kigezo batili na kisicho na mantiki hata kidogo.

Wednesday, April 2, 2014

Eti Biblia inataja mashehe, kwa hiyo inaunga mkono Uislamu!




Wahubiri wa ‘injili’ wa Kiislamu wanaendelea kuhaha kuhalalisha quran kupitia Biblia. Nasema ‘kuhaha’ kwa sababu hakika kabisa wana juhudi kubwa mno lakini inasikitisha kwa sababu hakuna hata siku moja waliyowahi kusema jambo lenye ukweli kibiblia linalounga mkono quran kama wasemavyo wao – Mungu ni shahidi yangu. Mara waseme Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia; mara waseme Yesu aliposema kuwa ataletwa Msaidizi basi alimaanisha Muhammad, n.k. Ni kituko kimoja baada ya kingine. Na wanayemdanganya ni wao wenyewe pamoja na Wakristo wachache wasiojua Biblia.