Waislamu wanaojaribu kuitoa makosa Biblia bado wanaendelea na mahangaiko yao ya kujaribu kuipa uhalali quran kupitia upotoshaji mkubwa wa Maandiko ya Biblia. Kama kwaida, hawana hoja mpya wala za kufikirisha,
bali ‘wana-recycle’ maswali yaleyale toka januari hadi desemba. Haya ni maswali
ambayo yalibuniwa na watu fulanifulani, basi na wao wanayabeba bila hata ya kuchuja
na kujua endapo yana ukweli au la. Hata hivyo, kila jambo wanalolisema kinyume
na Biblia ni UONGO mtupu SIKU ZOTE - NA USHAHIDI WA UONGO HUO TUNAO WAZIWAZI!
Katika kitabu cha Ezakieli imeandikwa:
…. Nawe utakila kama mkate wa shayiri, nawe
utakioka mbele ya macho yao juu ya mashonde
yatokayo katika mwanadamu. (Eze 4:12).
[Maana ya mashonde ni kinyesi]
Hebu soma hoja mojawapo juu ya andiko hili
kutoka kwa mmoja wa hawa ndugu:
Wakristo hivi mnafaham yakuwa huo
Mkate una mavi? Mavi jamani mavi, mnalishwa mavi eti ni mwili wa mungu,
Someni ndani ya Biblia
imeandikwa mashonde, ila Maana yake
haswa ni mavi ya mwanaadam, hili
andiko
EZEKIELI 4:12
Nawe utakila kama mkate wa
shayiri, nawe utakioka mbele ya macho yao juu ya mashonde yatokayo katika
mwanadamu.
Mashonde maana yake ni mavi makavu, anaebisha afunguwe Biblia yake
sehemu ya maneno magumu.
Nyie kulenitu ila fahamuni mnakula mavi.
Mwisho wa
kunukuu.
Biblia inaongea
vizuri sana juu ya watu hawa:
Ndugu
zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili
yao, ili waokolewe. Kwa maana
nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.
Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao
wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. (Warumi 10:1-3)
Ni kweli
kabisa juhudi wanayo sana, tena sana! Lakini hebu chukulia mfano huu. Kila asubuhi
Bwana Juhudi huenda kutega upepo kwa kutumia tenga ili aweze kuupata. Na anafanya
hivyo kwa miaka yake yote anayoishi hapa duniani. Lakini inafika siku ambayo
amezeeka, hana nguvu na yuko tu kitandani. Je, atakapojiangalia na kujipima
katika kazi ile aliyofanya kwa miaka yake yote, kutakuwa na nini cha kumsaidia?
Ndicho hasa
wanachofanya hawa ndugu zangu Waislamu wanapojaribu “kutuhubiria” Biblia –
Mungu ni shahidi yangu – wanatega tu upepo kwa matenga!
Na kinachonishangaza
na kunisikitisha ni jinsi ambavyo huongea kwa ujasiri kana kwamba kile
wanachokisema kina hata chembechembe za ukweli!!
Basi hebu
tuone tenga lao limenasa nini kwenye Ezekieli 4:12. Tusome tena andiko hilo:
…. Nawe utakila kama mkate wa shayiri, nawe
utakioka mbele ya macho yao juu ya mashonde
yatokayo katika mwanadamu. (Eze 4:12).
Hapa Mungu
alikuwa amekasirishwa na wana wa Israeli kwa sababu ya uasi na dhambi zao. Kwa
hiyo akamwambia Yeremia:
Lakini wewe, mwanadamu,
tazama, watakutia pingu, nao watakufunga kwazo, wala hutakwenda nje kati yao;
nami nitaufanya ulimi wako ugandamane na kaakaa lako, hata utakuwa bubu, wala hutakuwa mwonyaji kwao; kwa kuwa wao ni
nyumba yenye kuasi. (Eze
3:25-26)
Kwa hiyo
Mungu akapanga kuwaadhibu. Lakini akataka kuwapa onyo kwanza ili kama wana
akili wageuke na kuacha njia zao mbaya. Na maonyo hayo aliyatoa kupitia
Ezekieli – kwamba afanye mfano wa kile ambacho kitawakuta kama wataendelea
kuasi.
Acha tusome
kabisa maneno hayo kikamilifu:
(Eze 4:1) Wewe nawe, mwanadamu, jipatie tofali uliweke
mbele yako, kisha, chora juu yake mfano wa
mji, yaani, Yerusalemu;
(Eze 4:2) ukauhusuru, ukajenge ngome juu yake, na kufanya
boma juu yake; ukaweke makambi juu yake, na kuweka magogo ya kuubomoa
yauzunguke pande zote.
(Eze 4:3) Kisha ukajipatie bamba la chuma,
ukalisimamishe liwe ukuta wa chuma kati ya wewe na mji huo; ukaelekeze uso wako
juu yake, nao
utahusuriwa, nawe utauhusuru. Hili litakuwa ishara kwa nyumba ya Israeli.
(Eze 4:4) Tena lala chini kwa ubavu wako wa kushoto,
ukaweke huo uovu wa nyumba ya Israeli juu yake; kwa kadiri ya hesabu ya siku
utakazolala juu yake, kwa kadiri hiyo utauchukua uovu wao.
(Eze 4:5) Maana nimekuagizia miaka ya uovu wao iwe kwako hesabu ya siku, yaani, siku mia tatu na
tisini; ndivyo utakavyouchukua uovu wa nyumba ya Israeli.
(Eze 4:6) Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu
wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa
nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia.
(Eze 4:7) Nawe utauelekeza uso wako, uelekee mazingiwa
ya Yerusalemu, na mkono wako utakuwa haukuvikwa nguo, nawe utatoa unabii juu
yake.
(Eze 4:8) Na tazama, nitakutia pingu, wala hutageuka
toka upande mmoja hata upande wa pili, hata utakapozitimiza siku za mazingiwa
yako.
(Eze 4:9) Pia ujipatie ngano, na shayiri, na kunde, na
dengu, na mtama, na kusemethi, ukavitie vyote katika chombo kimoja, ukajifanyie
mkate kwa vitu hivyo; kwa kadiri ya hesabu ya siku utakazolala ubavuni mwako;
yaani, siku mia tatu na tisini utaula.
(Eze 4:10) Na chakula chako utakachokula kitapimwa,
shekeli ishirini kwa siku moja; utakila kwa wakati wake.
(Eze 4:11) Nawe utakunywa maji kwa kuyapima, sehemu ya
sita ya hini; utayanywa kwa wakati wake.
(Eze 4:12) Nawe
utakila kama mkate wa shayiri, nawe utakioka mbele ya macho yao juu ya mashonde yatokayo katika mwanadamu.
(Eze 4:13) Bwana akasema, Hivyo ndivyo wana wa Israeli watakavyokula
chakula chao, hali kimetiwa unajisi, kati ya mataifa
nitakakowafukuza.
(Eze 4:14) Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, tazama, roho
yangu haikutiwa unajisi; maana tangu ujana wangu hata sasa sijala nyamafu, wala
iliyoraruliwa na hayawani; wala nyama ichukizayo haikuingia kinywani mwangu.
(Eze 4:15) Ndipo akaniambia, Tazama, nimekupa mashonde ya ng'ombe badala ya mashonde ya mwanadamu,
nawe utakipika chakula chako juu ya hayo.
Kwa sababu
ya kukariri vitu bila kujibidisha kutafuta ukweli, wahubiri hawa wa injili ya
Kiislamu inayotoka kwenye Biblia, wanadhani eti Ezekieli aliambiwa apike mkate kwa kuchanganya na mavi ya mwanadamu.
Pole yao!!
Ndugu
zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili
yao, ili waokolewe. Kwa maana
nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.
Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao
wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. (Warumi 10:1-3)
Lakini Biblia
inasemaje?
Nawe utakila
kama mkate wa shayiri, NAWE UTAKIOKA mbele ya macho yao JUU YA MASHONDE
YATOKAYO KATIKA MWANADAMU. (Eze 4:12)
Sijui Kiswahili
ni kigumu kwao? Hapa Ezekieli anaambiwa atumie mavi ya mwanadamu kama kuni za
kuokea; siyo kwamba ayachanganye ndani ya mkate!!
Na kwa
sababu lengo lilikuwa ni kuonyesha mfano wa yale yatakayowakuta watenda dhambi
hao, Mungu akafafanua maana ya jambo hilo:
Bwana
akasema, Hivyo ndivyo wana wa Israeli watakavyokula chakula chao, hali kimetiwa
unajisi, kati ya mataifa nitakakowafukuza. (Eze 4:13)
Maana yake
ni kuwa, wataondolewa kwenye nchi yao na kusukumwa kwenye mataifa yasiyomjua
Mungu; mataifa ya kipagani yanayoabudu miungu mingine; na huko wataishia
kunajisika, maana itawabidi wale chakula cha hayo mataifa.
Lakini kwa
sababu Ezekieli naye alijisikia vibaya kwa jambo hilo, ndipo Mungu akapunguza
ukali wa lile jambo:
Ndipo
akaniambia, TAZAMA, NIMEKUPA MASHONDE YA NG'OMBE BADALA YA MASHONDE YA
MWANADAMU, nawe utakipika chakula chako juu ya hayo. (Eze 4:15)
Acheni
kukariri ndugu zangu Waislamu!! Mnaelekea kuzimu!!
Nimalizie
kwa kuubainisha uongo wa walimu hawa (wa uongo) kwa kutaja mambo manne muhimu:
Kwanza: Mashonde
hayakutiwa ndani ya mkate bali yalitakiwa kutumika kama kuni za kuokea mkate.
Pili: Hili si
agizo la Mungu kwa Wakristo juu ya namna ya kupika mikate yao.
Tatu: Mkate huu
hauna uhusiano na ule unaotumiwa na ndugu zangu Wakatoliki kwenye meza ya
Bwana.
Nne: Jambo hili
lilifanywa kama adhabu kwa Israeli kutokana na dhambi – sasa je, mkate unaoliwa
Kanisani huwa ni kwa ajili ya adhabu?
Enyi
wahubiri wa injili wa Kiislamu, mnayemdanganya ni ninyi wenyewe wala
hamuwadanganyi Wakristo, maana kile mnachohubiri wala hakimo ndani ya Biblia. In
fact, HAMJAWAHI HATA SIKU MOJA KUSEMA NENO LA BIBLIA NA LIKAWA KWELI. YOTE HUWA
NI UONGO NA UPOTOSHAJI.
MBINGU
IPO MOJA TU! MUNGU YUPO MMOJA TU NA JINA LAKE MOJAWAPO NI “YESU”. NENO LA MUNGU
LIKO KWENYE KITABU KIMOJA TU – NACHO NI BIBLIA!!
Mnajihangaisha
bure kutega upepo kwa matenga!!
Na c ajabu huyu mtu akawa ni kiongozi wa msikitin
ReplyDeleteHawana tofauti. ni walewale tu
DeleteNa c ajabu huyu mtu akawa ni kiongozi wa msikitin
ReplyDeletetatizo wao wanasoma ili wapinge bila hata upembuzi yakinifu
ReplyDeleteUzuri ni kwamba Neno la Kristo ni upanga. Linakaa ndani yao na litawasumbua hadi wale waliokusudiwa watakapofunguka. Kazi yetu ni kupanda mbegu na kumwagilia. Bwana ndiye anayeotesha na kukuza.
DeleteYesu yeye alikula mavi ya ng'ombe sio ya binadamu? Dah! huyo Mungu ana roho gani? Hana huruma wala haki? Hivi kwani Mungu wenu ni yupi na anasifa zipi? Maana mpaka sasa sijaona mkristo mwenye kumjua Mungu. Wengine wanasema Yesu Mungu. siwaelewi. Lakini nadhani tatizo kubwa ni biblia na mapokeo ndio tatizo. Wakristo wote wanamfuata mafundisho ya paul.
ReplyDeleteshalom ndugu. asante kwa kutembelea blog hii na kutoa maoni yako - MAANA HYA NI MAONI KWELIKWELI. Post hii imeongea kwa ushahidi wa maandiko lakini wewe ulichotoa ni maoni tu ambayo hayana ushahidi wa hata andiko moja. Ni nani basi atakayeacha kufuata maandiko afuate maneno ya mtu yasiyo na support ya maandiko.
DeleteTunaheshimu maoni yako lakini tunasikitika kwamba hayana uzito wowote wa kutiliwa maanani.
Amina
ReplyDeleteAmina
ReplyDelete