Friday, December 28, 2012

Kuna Jambo la Ajabu Linaendelea Kwenye Ulimwengu wa Kiislamu




Takribani miaka 800 kabla ya Kristo, Mungu wa Israeli alisema kupitia nabii Yoeli kwamba:

Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.

Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi.

Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.

Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana. (Yoeli 2:28-32).

Thursday, December 27, 2012

Shekhe Zaheed Ampokea Yesu Kristo





Zaheed alizaliwa kwenye familia ya Kiislamu. Baba yake na kaka zake wote walikuwa viongozi wa dini ya Kiislamu. Zaheed naye alifuata mkondo uleule.


Mara baada ya kuhitimu masomo ya dini na kukabidhiwa msikiti, chuki yake na kutokuwa na uvumilivu dhidi ya Wakristo kulianza kujionyesha waziwazi.


Zaheed anasema, “Nilikuwa nawakusanya vijana kwenye msikiti wangu na kuwachochea dhidi ya Wakristo. Niliwaambia kuwa Wakristo ni makafiri. Niliwaambia waende wakawapige Wakristo kwa fimbo na kwa nondo. Niliwaambia kuwa Allah anafurahi wakifanya hivyo. Tulikuwa tukichoma moto Biblia tunazozikusanya.”