Zaheed alizaliwa kwenye
familia ya Kiislamu. Baba yake na kaka zake wote walikuwa viongozi wa dini ya
Kiislamu. Zaheed naye alifuata mkondo uleule.
Mara baada ya kuhitimu
masomo ya dini na kukabidhiwa msikiti, chuki yake na kutokuwa na uvumilivu dhidi
ya Wakristo kulianza kujionyesha waziwazi.
Zaheed anasema, “Nilikuwa
nawakusanya vijana kwenye msikiti wangu na kuwachochea dhidi ya Wakristo.
Niliwaambia kuwa Wakristo ni makafiri. Niliwaambia waende wakawapige Wakristo
kwa fimbo na kwa nondo. Niliwaambia kuwa Allah anafurahi wakifanya hivyo.
Tulikuwa tukichoma moto Biblia tunazozikusanya.”
Zaheed anaendelea kusema,
“Lakini siku moja, nilijisikia tu nichukue Biblia moja niende nayo nyumbani.
Nilikuwa naisoma ili niweze kutafuta mambo yanayotatanisha ili niweze kuyatumia
dhidi ya imani ya Kikristo. Ghafla, nuru kubwa iliangaza kwenye chumba changu.
Halafu nikasikia sauti ikiita jina langu. Nuru ile ilikuwa kali sana. Iliangaza
chumba kizima. Ile sauti ikauliza, ‘Zaheed, kwa nini unanitesa?’ Niliogopa.
Sikujua cha kufanya. Nilidhani ninaota. Kwa hiyo nikauliza, ‘Wewe ni nani?’
Kisha nikasikia, ‘Mimi ni njia, na kweli, na uzima.’”
Zaheed anasema, “Kila
usiku, kwa siku tatu zilizofuata, ile nuru ilinilazimisha kukiri. Na usiku wa nne,
nilimkubali Yesu kama Mwokozi wangu.”
Kutokana na kile kilichotokea,
Zaheed alienda kwa ndugu zake msikitini ili kuwashirikisha kile ambacho
kilimkuta. Matokeo yake, kwa kuwa sasa alihesabika kuwa muasi wa dini yake ya
mwanzo, alikabidhiwa kwa askari.
Zaheed anaendelea kusema,
“Niliwekwa gerezani kwa miaka miwili. Na katika kipindi hicho chote, askari
walinitesa tena na tena. Wakati fulani walinining’iniza kwa nywele zangu kwenye
feni na kuniacha hapo. Wakati mwingine walining’oa kucha zangu wakitaka niikane
imani yangu katika Kristo. Lakini pamoja na kwamba niliteseka sana mikononi mwa
washitaki wangu wa Kiislamu, sikuwa na chuki dhidi yao. Maana miaka michache
iliyotangulia, nilikuwa mmoja wao.”
Zaheed anasema, “Wakati wa
hukumu yangu, nilipatikana na kosa la kukufuru. Na kulingana na sharia,
nilitakiwa kunyongwa. Walijaribu kunilazimisha kukana imani yangu kwa Yesu.
Waliniambia kuwa nikikubali, hawatanipiga tena, ningeachiwa huru. Lakini
nisingeweza kumkana Yesu. Muhammad hakuwahi kunitembelea mimi. Lakini Yesu
alinitembelea! Ninajua kuwa Yeye ndiye kweli. Kwa hiyo nilimwomba tu Mungu
nikitumaini kuwa na wao watafika mahali wamjue Yesu.”
Hatimaye iliwadia siku
ambayo Zaheed alitakiwa kunyongwa. Akiwa
hana hofu ya kifo, alijaribu hata kuwaambia askari habari za Yesu wakati
akipelekwa kwenye sehemu ya kunyongewa, maana tayari alishakubaliana na hali
yake – kwamba alikuwa ni wa kufa tu. Lakini Mungu alikuwa na mipango mingine
kabisa.
Kabla tu ya kunyongwa,
amri isiyotarajiwa ilitolewa na mahakama kwamba Zaheed aachiwe huru. Amri ile
ilisema kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha dhidi yake. Hadi leo, hakuna mtu
anayejua kwa nini Zaheed aliachiwa huru.
Zaheed anasema, “Sasa
najisikia kuwa Yesu alinitembelea mara mbili.
Kwanza, nilipokuwa mtesi wa watoto wake. Na pili, nilipokuwa niko karibu
na kunyongwa.”
Zaheed alibadili jina lake
na kuitwa Lazaro, ikiwa ni ishara ya kuponea chupuchupu kwenye mauti kama
ilivyokuwa kwa Lazaro wa Biblia aliyefufuliwa na Bwana Yesu.
Ingawaje Wakristo wengi
hawakumwamini mwanzoni, hivi sasa wamemkubali kama sehemu ya familia yao. Na
anasafiri kutoka kijiji hadi kijiji.
Zaheed anasema, “Naishi
kwenye nchi inayotawaliwa na mafundisho ya uongo ya Uislamu. Watu wangu
wamepofushwa. Nami nilichaguliwa na Mungu ili niwe sauti yake. Ninajihesabu
kuwa mateso niliyopitia si lolote si chochote ukilinganisha na furaha ya kumjua
Yeye – Njia, na Kweli, na Uzima!”
**********
Ndugu msomaji, Mungu yuko
kazini. Tumepewa muda huu mfupi katika maisha haya ili tuchague kumfuata Yesu
au tuamue kufuata dini – ziwe ni za Kikristo au za aina nyingine. Si kila mtu
atapata neema ya kutembelewa moja kwa moja na Kristo mwenyewe kama ilivyokuwa
kwa Zaheed. Msingi wa kuingia mbinguni ni kumwamini Yesu Kristo PEKEE!
Dini yako haitakusaidia
kamwe kuingia mbinguni. Yesu Kristo pekee ndiye Njia, na Kweli, na Uzima. Njoo
kwake LEO upate uzima wa milele bure.
Huenda unatamani kuja kwa
Yesu ila unaogopa kutengwa na ndugu zako. Ni kweli hayo yanaweza kutokea.
Lakini, kama ulivyomsoma au kumsikia Zaheed, na hivyo ndivyo ilivyo, kumjua
Yesu ndilo jambo kubwa na la milele kuliko kumkataa kwa sababu ya hofu ya
kutengwa na ndugu. Ndugu hawana mbingu ya kukupeleka. Yesu anayo mbingu.
Labda pia umetishwa
kwamba, ukiacha dini yetu hatutakuzika. Hii huwa ni sababu ya kuchekesha sana.
Kwani wewe ukifa, kama hawataki kukuzika, anayepata shida ni wewe au ni wao? Tangu
uzaliwe ulishawahi kuona watu wangapi walioacha kuzikwa kwa lengo la kuwakomesha?
Yesu ndiye Njia, na Kweli,
na Uzima. Anakuita leo. Anakungoja siku zote kwa upendo na shauku nyingi ili
akupe uzima wa MILELE alioandaa kwa ajili yako. LAKINI KUMBUKA, HATAKUNGOJA
MILELE! AMUA SASA!
Waweza kuniandikia maoni yako pia kupitia: ijuekweli77@yahoo.co.uk
Waweza kuniandikia maoni yako pia kupitia: ijuekweli77@yahoo.co.uk
asante kwa makala nzuri. Mungu wetu ni mwema kwa kila mtu.
ReplyDeleteAmen ndugu. Mungu akubariki. Songa mbele na Bwana Yesu.
ReplyDelete