Ka’aba
Katika sehemu ya 1 ya makala haya tuliangalia kuhusu asili ya Allah. Katika sehemu hii ya 2 tutaongelea kuhusiana na mji wa Makka na ka'aba, ambayo ni madhabahu kuu ya Uislamu.
Mji wa Makka ndio kitovu cha Uislamu duniani. Kwenye mji huu ndiko iliko Ka’aba, au kama wanavyoamini na kuiita Waislamu Bait – ul- Haram; au Bait – ul- Allah, yaani ‘nyumba ya Allah’ au ‘nyumba ya Mungu’. Na kila Mwislamu kokote duniani anatakiwa kuswali swala 5 kila siku huku akielekeza uso wake Makka iliko hiyo nyumba ya Mungu wao. Vilevile, kila mmoja wao anatakiwa kwenda Makka kuhiji walau mara moja katika maisha yake, maana hija ni moja ya nguzo kuu katika Uislamu. Kwa maana nyingine, Ka’aba ndiyo madhabahu kuu katika Uislamu.
Mji wa Makka ndio kitovu cha Uislamu duniani. Kwenye mji huu ndiko iliko Ka’aba, au kama wanavyoamini na kuiita Waislamu Bait – ul- Haram; au Bait – ul- Allah, yaani ‘nyumba ya Allah’ au ‘nyumba ya Mungu’. Na kila Mwislamu kokote duniani anatakiwa kuswali swala 5 kila siku huku akielekeza uso wake Makka iliko hiyo nyumba ya Mungu wao. Vilevile, kila mmoja wao anatakiwa kwenda Makka kuhiji walau mara moja katika maisha yake, maana hija ni moja ya nguzo kuu katika Uislamu. Kwa maana nyingine, Ka’aba ndiyo madhabahu kuu katika Uislamu.
Ka’aba ni nyumba ya umbo la takriban mchemraba ambayo, pamoja na vitu vingine vichache iliyo navyo, kuna kipande cheusi cha
jiwe ambacho kimejengewa ukutani kwenye kona mojawapo. Hivyo, Waislamu
wanapoenda Makka kuhiji huzunguka Ka’aba na pia kulibusu jiwe hilo, au kuligusa tu, na kama ikishindi kana, basi japo kulinyoshea mkono.
Zamani, Allah anasema, kuwa Muhammad alikuwa akitazama mbinguni wakati anapoomba [nadhani kila mwenye imani juu ya Mungu anaamini kuwa Mungu yuko juu – na huo kusema kweli nadhani ndio mtazamo sahihi kabisa].
Lakini Allah akamwambia mtume wake:
We have certainly seen the turning of your face, [O Muhammad], toward the heaven, and We will surely turn you to a qiblah with which you will be pleased. So turn your face toward al-Masjid al-Haram. And wherever you [believers] are, turn your faces toward it [in prayer]. Indeed, those who have been given the Scripture well know that it is the truth from their Lord. And Allah is not unaware of what they do. (sura Al Baqarah 2:144) – Sahih International Version.
Yaani:
Hakika tumeona jinsi unavyogeuzia uso wako [ewe Muhammad], kuelekea mbinguni, nasi hakika tutakugeuzia kwenye qiblah utakachokifurahia. Hivyo elekeza uso wako kwenye al-Masjid al-Haram. Na kila mtakakokuwa [enyi mnaoamini] geuzieni nyuso zenu kuelekea huko [mswalipo]. Hakika, wale waliopewa Maandiko wanajua vema kuwa ni kweli kutoka kwa Bwana wao. Na Allah anajua kile wafanyacho.
Allah anasema hafurahii sana Muhammad na Waislamu kugeuzia nyuso zao juu mbinguni (aliko Mungu muumba wa vyote – ajabu sana! Ajabu mno!), badala yake akaamuru wageuzie nyuso zao kwenye ka’aba wawapo popote wakati wa kuswali.
Pia anasema kuwa wale waliopewa Maandiko (yaani watu wa kitabu) eti wanajua fika kwamba jambo hilo ni kweli kutoka kwa Bwana wao!
We Allah wewe! Bwana wao yupi tena wakati wewe unasema ndiwe uliyesema na Ibrahimu ili akajenge ka’aba akitokea Kaanani – kilometa zaidi ya 1,000 kutoka Makka? [Tena basi Makka ambayo hata haikuwapo duniani hadi takriban kwenye miaka 400 baada ya Kristo - sasa sijui Ibrahimu alienda kujenga ka'aba porini kusiko hata na mtu mmoja]!! Ina maana kuna Bwana wao ambaye si wewe basi! Basi huyo Bwana wao ana Ibrahimu na Ishmael wa kwake; na wewe una Ibrahimu na Ishmael wa kwako, au siyo?
Kulingana na Quran, ka’aba
ilijengwa na Ibrahimu na mwanawe, Ishmael. Quran inasema kwamba:
Remember We made the House
a place of assembly for men and a place of safety; and take ye the station of
Abraham as a place of prayer; and We covenanted with Abraham and Isma'il, that
they should sanctify My House for those who compass it round, or use it as a
retreat, or bow, or prostrate themselves (therein in prayer). [Qur'an 2:125].
Yaani:
Kumbukeni, tuliifanya
Nyumba ile mahali pa kukusanyikia kwa ajili ya wanadamu na mahali pa usalama;
hivyo chukueni ninyi mahali pa Ibrahimu kama mahali pa swala; nasi tulifanya
agano na Ibrahimu na Ishmael, kwamba waitakase Nyumba Yangu kwa ajili ya wale
wanaoizunguka, au kuitumia kama mahali pa makimbilio, au kuinama, au kusujudu
humo (kwa swala).
[Allah anasema kuwa
aliifanya nyumba hii kwa ajili ya wanadamu, lakini waislamu hawaruhusu asiye
mwislamu, na hasa aliye Mkristo, kwenda kwenye ka’aba; au hata kupita juu kwa
ndege!! Inawezekana Allah anaposema ‘mwanadamu’ ana maana ya ‘mwislamu’!]
Kuhusiana na Ibrahimu,
hilo ni jambo ambalo tunawaachia Waislamu wenyewe maana sisi wengine tunaamini
na hata ushahidi wa kihistoria na kimaandiko unaonyesha wazi kwamba Ibrahimu
hajawahi kamwe kukanyaga mguu wake Uarabuni.
Kwa mfano, ufuatao ni
ushahidi mmojawapo juu ya jambo hili. Tunasoma kwamba:
Narrated Abu Dhaar: I
said, "O Allah's Apostle! Which mosque was built first?" He replied,
"Al-Masjid-ul-Haram." I asked, "Which (was built) next?" He
replied, "Al-Masjid-ul-Aqs-a." I asked, "What was the period in
between them?” He replied, “Forty years.” (Sahih Bukhari 4:55:636).
Yaani:
Imesimuliwa na Abu Dhaar:
Nilisema, “Ewe Mtume wa Allah! Ni msikiti upi ulikuwa wa kwanza kujengwa?”
Akajibu, "Al-Masjid-ul-Haram." Nikauliza, “Ni upi ulifuata?” Akajibu, “Al-Masjid-ul-Aqs-a.”
Nikauliza, “Ulipita muda gani hapo katikati?” Akajibu, “Miaka arobaini.”
Muhammad naye ana mambo! Al-Masjid
ul-Aqs-a ndiko hapo penye Ka’aba. Na
Al-Masjid-ul-Haram ni hekalu la Mfalme Sulemani kule Uyahudi.
Sasa,
hekalu la Yerusalemu lilijengwa na mfalme Sulemani kwenye takriban miaka ya 950
kabla ya Kristo (KK). Hii ni kusema kwamba, kama maneno ya Muhammad ni ya kweli
– na ninaamini kwamba hakuna mwislamu ambaye anaweza kukiri kuwa Muhammad ni
mwongo – basi, msikiti wa kwenye Ka’aba unatakiwa uwe ilijengwa kwenye 990 KK
(ukiongeza hiyo tofauti ya miaka 40).
Hilo
sio tatizo. Lakini shida inakuja unapomwingiza Ibrahimu. Ibrahimu aliishi takriban
miaka 2000 kabla ya Kristo. Tazama hapa. Hii ni kusema, aliishi miaka takriban
1050 kabla ya kujengwa kwa hekalu la mfalme Sulemani. Sasa, kama Ibrahimu wa
Muhammad aliyejenga Ka’aba aliijenga miaka 40 kabla ya hekalu la Sulemani, basi
NI LAZIMA awe ni Ibrahimu mwingine na Ishmael mwingine tofauti kabisa na wale
wa kwenye Biblia. Vyovyote iwavyo, hilo ni tatizo la Waislamu wenyewe
kulitatua. Ni kazi kwao kujiridhisha na kujithibitishia wao wenyewe kwamba,
kama wanataka imani yao itokane na Ibrahimu aliyeongea na Mungu wa Israeli,
basi hali ndiyo hiyo!
Kutokana
na ukweli huo hapo juu, tunabakia na uwezekano wa aina mbili: kwanza, kama
Muhammad yuko sahihi juu ya hiyo miaka 40, basi Allah ndiye aliyekosea au
aliongopa kusema kuwa Ibrahimu alijenga Ka’aba. Kama Allah yuko sahihi, basi Muhammad ndiye
aliyekosea au kuongopa kwamba Ka’aba ilijengwa miaka 40 kabla ya hekalu la
Sulemani. [Hata hivyo, kuna uwezekano kabisa huyu ni Ibrahimu mwingine kabisa.
Hebu tutafakari yafuatayo:
Hata kama ka’aba ilijengwa
na Ibrahimu (wa Biblia au mwingine tofauti), jambo moja ni dhahiri; kwamba wakati
Muhammad anatokea na kuanzisha dini yake, ka’aba ilikuwa chini ya wapagani wa
Uarabuni huku ndani na nje yake kukiwa na miungu zaidi ya mia tatu.
Ni mwaka 630 baada ya
Kristo (BK), ndipo Muhammad na wafuasi wake walitwaa mamlaka ya mji wa Makka na
kuifanya ka’aba kuwa sehemu ya kuabudia Mungu mmoja badala ya miungu zaidi ya
mia tatu. [lakini usisahau kwenye sehemu ya 1 ya makala haya tulibainisha
kwamba allah alikuwa ni mungu wa kipagani tangu maelfu ya miaka nyuma kabla ya
kutokea kwa Muhammad. Na unajiuliza; hivi asili ya ‘allah akbar’, yaani ‘allah
ni mkuu’ ni nini? Je, si kwa sababu kulikuwa na mamia ya miungu, na allah
akiwamo, ndiyo maana Muhammad akawa, kimsingi, anasema, “Hapana. Hiyo miungu
yote si kitu. Allah ndiye anayewazidi wote”? Huo ndio muktadha sahihi wa
kutamka maneno kama hayo, au siyo? Hilo ni wazo tu ambalo linahitaji utafiti
wako wewe unayemwamini Allah; maana mimi wala siamini kwamba Allah ndiye Mungu
wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.]
Basi turudi kwenye suala
la kuwapo kwa mamia ya miungu kwenye ka’aba wakati Muhammad anaingia. Hivi
ndivyo tunavyosoma:
Narrated 'Abdullah bin
Masud: The Prophet entered Mecca and (at that time) there were three
hundred-and-sixty idols around the Ka’aba. He started stabbing the idols with a
stick he had in his hand and reciting: "Truth (Islam) has come and
Falsehood (disbelief) has vanished." [Sahih Bukhari 3:43:658].
Yaani:
Imesimuliwa na Abdullah
bin Masud: Mtume aliingia Makka na (wakati ule) kulikuwa na miungu mia tatu na
sitini kuzunguka Ka’aba. Alianza kuichomachoma kwa fimbo aliyokuwa nayo mkononi
huku akisema: “Kweli (Uislamu) imeshakuja na Uongo (kutokuamini) kumetoweka.”
Ndugu
zangu waislamu, ka’aba wala haina uhusiano na Mungu Mkuu aliyeumba mbingu na
nchi. Ilikuwa ni madhabahu tu ya kipagani kwa ajili ya kuabudia mwezi, jua na
nyota.
Hivi
ndivyo tunavyoambiwa:
Narrated Abu Huraira: “In the year prior to the last Hajj of the
Prophet when Allahs Apostle made Abu Bakr the leader of the pilgrims, the
latter (Abu Bakr) sent me in the company of a group of people to make a public
announcement: 'No pagan is allowed to perform Hajj after this
year, and no naked person is allowed to perform Tawaf of the Ka’aba.'” (Bukhari V2, B26, #689 (V1, B8, No 365).
Yaani:
Imesimuliwa
na Abu Huraira: “Kwenye mwaka kabla ya Hija ya mwisho ya Mtume pale Mtume wa
Allah alipomfanya Abu Bakr kuwa kiongozi wa mahujaji, Abu Bakr alinituma pamoja
na kundi la watu wengine ili kutoa tangazo: ‘Hakuna mpagani anayeruhusiwa
kufanya Hija baada ya mwaka huu, na hakuna mtu aliye uchi anayeruhusiwa kufanya
Tawaf ya Ka’aba.
Sijui
ndugu msomaji kama unaiona maana ya maneno haya? Hiki ndicho tunachosoma humu:
1.
Waislamu
na wapagani walikuwa wakifanya hija pamoja kwenye ka’aba kwa miaka mingi hadi
hapo Abu Bakr alipofanywa kiongozi.
2.
Wakati
wawapo kwenye hija, wapagani walikuwa wakifanya Tawaf (kuzunguka ka’aba) wakiwa
uchi.
3.
Wapagani
walikuwa wakiabudu miungu yao ya kipagani kwenye ka’aba na waislamu wakimwabudu
Allah.
Ili
uone uzito wa jambo hili vizuri, hebu piga picha ya Hekalu la Sulemani
alilojenga Yerusalemu kwa ajili ya Yehova. Yaani humo ndani ya hekalu wawe
wanasali Wayahudi wanaomwamini Yehova na pia wapagani wanaoabudu jua, na mwezi
na nyota; tena wakiwa uchi!!!!!!!
Kwa
kuwa jambo hilo haliingii kamwe akilini; na haliwezekani, jibu ni moja tu: ni
Muhammad ndiye aliyeenda kuingilia madhabahu ya wapagani na si kinyume chake!
Na
ndiyo maana Muhammad alikuwa na ujasiri wa kutaka kuibomoa ka’aba. Hivi ndivyo
tunavyosoma:
Narrated Aswad: Ibn
Az-Zubair said to me, "Aisha used to tell you secretly a number of things.
What did she tell you about the Ka'ba?" I replied, "She told me that
once the Prophet said, 'O 'Aisha! Had not your people been still close to the
pre-Islamic period of ignorance (infidelity)! I would have dismantled the Ka'ba
and would have made two doors in it; one for entrance and the other for
exit." (Sahih Bukhari 1:3:128).
Yaani:
Imesimuliwa
na Aswad: Ibn Az-Zubaid aliniambia, “Aisha alikuwa akikusimulia kwa siri mambo
kadha wa kadha. Je, alikuambia nini kuhusiana na ka’aba? Nikajibu, “Aliniambia
kwamba, kuna wakati Mtume alisema, ‘Ewe Aisha! Kama watu wa kwenu wangekuwa
bado hawako karibu na enzi ya ujinga ya kabla ya Uislamu (ukafiri), ningebomoa
Ka’aba na ningejenga milango miwili; mmoja wa kuingilia na mwingine wa kutokea.’”
Hebu
piga picha hapa pia; kwamba Musa aliambiwa na Yehova atengeneze hema ya
kukutania. Akapewa maelekezo kwa undani sana ya namna kila kitu kinavyotakiwa kuwa, na akaambiwa afanye sawasawa na
alivyoonyeshwa na Yehova. Halafu anakuja kutokea mtume au nabii miaka mia
kadhaa inayofuata anasema, “Mimi naona katika nyumba hii Yehova alikosea kuweka
mlango mmoja. Inatakiwa milango miwili hapa.” Hivi inawezekana kweli?
Sasa,
kama kweli ni Allah ndiye alimwambia Ibrahimu na Ishmael wajenge ka’aba,
inaingia kweli akilini Muhammad kuja kusema angeweza kuibomoa na kuijengea
milango miwili?? Mwanadamu anaweza kumsahihisha Mungu?
Lakini
hilo linawezekana tu kama nyumba yenyewe haina uhusiano wowote na Mungu; kama
ambavyo ka’aba haina kamwe uhusiano wowote na Mungu wa mbinguni.
Duniani
leo kuna makanisa na mahekalu mengi, lakini tunapoongelea hema ya kukutania ya
Musa au hekalu la mfalme Sulemani, tunakuwa tunaongelea mahali pa pekee sana
ambako Mungu mwenyewe kibinafsi ndiye aliyetoa vipimo na kuchagua mahali pa
kujenga. Vivyo hivyo, kuna misikiti mingi duniani, lakini unapoongelea msikiti
wa kwenye ka’aba, basi ni allah mwenyewe (anayedaiwa kuwa ni Mungu wa Ibrahimu)
kujihusisha moja kwa moja na kazi hiyo. Sasa, hebu pia tazama picha hii hapa
chini, kisha ujiulize mwenyewe kama Mungu wa mbinguni anaweza kuagiza nyumba
yake ijengwe kwenye eneo lenye sifa hizi:
Nimekwambia
hapo mwanzo kwamba kwenye ka’aba kuna jiwe jeusi (wanaloliita Al-hajar
Al-aswad) ambalo waislamu hulibusu au kuligusa kama
sehemu ya ibada yao humo. Lakini tunaambiwa hivi kuhusiana na jiwe hilo:
Later, Umar said to the
black stone, "I know that you are a stone, that neither helps nor hurts,
and if the messenger of god had not kissed you, I would not kiss you."
(Sahih Bukhari, volume 2, #667).
Yaani:
Baadaye, Umar aliliambia
lile jiwe jeusi, “Najua kuwa wewe ni jiwe ambalo haumsaidii wala kumdhuru mtu,
na kama mjumbe wa mungu asingekubusu wewe, kamwe nisingekubusu.”
Hiyo
ndiyo hali ya Uislamu na waislamu hadi leo. Karibu kila kitu kwenye uislamu
kiko kinyume na hali halisi ya maisha; hata mioyo yao inakataa kuvikubali,
lakini wafanye nini sasa na wao wameshajiungamanisha na Muhammad? Anachosema Umar,
kimsingi, ni kuwa, “Moyoni najisikia kabisa kwamba hii habari ya kubusu jiwe ni
ubatili mtupu, lakini sina namna ya kuacha maana mtume amelibusu.”
Naamini
Waislamu wengi wanafikiri kuwa ka’aba iliyopo leo ndiyo hiyohiyo ambayo Allah
amewaambia kuwa ilijengwa na Ibrahimu na Ishmael. Lakini ukweli ni kwamba, ka’aba
ilishavunjwa na kujengwa zaidi ya mara kumi. Tazama hapa. Kwa hiyo, hii iliyopo leo ni
ujenzi wa hivi karibuni tu wa serikali ya Saudia.
Hitimisho
Ni kweli kabisa ka’aba ni
nyumba ya Allah, lakini KAMWE si nyumba ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Wala
Ibrahimu wa Israeli hajawahi kwenda Uarabuni kujenga ka’aba. Hii ilikuwa ni
madhabahu ya mungu mwezi, jua, nyota na miungu zaidi ya 360 iliyoabudiwa na
wapagani wa Uarabuni. Ukweli ni kwamba hii wala haikuwa ka’aba pekee. Zilikuwapo
ka’aba nyingi ambamo wapagani wa huko walikuwa wakiabudia miungu yao. Umeona mwenyewe
jinsi ambavyo wapagani hao walikuwa wakienda kuhiji Makka kwenye ka’aba tena
wakiwa uchi. Iweje leo useme kuwa mambo yaleyale; palepale kuwa ni mambo ya
kumwabudu Mungu aliyeumba mbingu na nchi?
Ndiyo maana Yehova
aliwaonya Waisraeli akisema: Basi
zishikeni amri zangu zote, na hukumu zangu zote, na kuzifanya, .... Nanyi
msiende kwa kuziandama desturi za taifa niitoayo mbele yenu; kwa kuwa wao
waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia. (Walawi 20:
22-23). Lakini ajabu ni kwamba Allah anasema kinyume kabisa. Kimsingi, anachosema kwa Waislamu ni kwamba: "Enendeni kwa kuzifuata kawaida za watu waliokuwa wanaishi Makka"!!!
Je, Mungu wa mbinguni anahitaji nyumba hapa duniani ili aweze kuishi humo? Hivi
kwa ukuu wake wote, Mungu huyu atakaa kwenye kachumba ambacho ndani yake hakuna
hata kitu?
Yesu Kristo anakuita akupe
uzima wa milele sasa. Muda unakimbia mbio!
Katika ulimwengu wa leo kupata taarifa si tatizo. Tunayo maktaba kubwa kuliko zote tangu kuumbwa kwa ulimwengu yenye kila taarifa uitakayo duniani - yaani Intaneti. Ni wewe tu kujua unataka nini.
Hoji mambo.
Chunguza.
Fanya utafiti.
Chukua hatua.
Safi Makala hii ni nzuri..
ReplyDeleteAmen mpendwa. Barikiwa na Bwana Yesu.
DeleteHalelluya Halelluya mtumwa wa Bwana Yesu! Nimebarikiwa sana na hii makala, ni kwa Utukufu na Upendo wa Mungu tu tunapata kuyajua haya kupitia kile ambacho Yeye Aliye Hai ameweka ndani yako.
ReplyDeleteHii ni Injili-Habari Njema ya wakati huu kwa hawa ndugu zetu ili kuona wanafunguliwa na hatimaye kuwa shuhuda nzuri kwenye shamba la Yesu, na wakati huohuo tunapata kuona Ukuu wa Mungu wa Ibrahim,Isaka na Yakobo ambavyo hauwezi hata kusogelewa na miungu hii inayoitwa mungu na walio nje ya Yesu. HAKIKA NIMEZIDI KUFUNGULIWA NA KUONA THAMANI YA WOKOVU NILIONAO, NAOMBA KWA ROHO MTAKATIFU AENDELEE KUNIIMARISHA, ASINICHOKE ILI NIFIKE KWAKE BABA YETU WA MBINGUNI NISIYE NA MAWAA.
Shalom brother Kishiwa. Mungu akubariki kwa kuendelea kusimama katika wokovu wake. Ni kweli kabisa unachosema, kwamba tunahitaji kuimarishwa na Roho Mtakatifu na pia kuuona uthamani mkubwa wa wokovu tuliopewa.
DeleteHakika inaumiza sana kwa wale ambao wako nje ya wokovu wakati huohuo wao wanaona wako sahihi KABISA huku wakiamini kwamba wanakwenda mbinguni - kumbe sivyo kamwe.
Bwana amimine ufunuo wake ndani ya mioyo yao, maana maandiko yanatuambia kwamba hakuna mtu anayeweza kusema Yesu ni Bwana isipokuwa kwa Roho Mtakatifu. Tuzidi kuwaombea wenzetu ambao hawajaona thamani ya wokovu.
Ubarikiwe sana.
Asante ndugu yangu James katika Yesu Kristo.
DeleteHebu na tusome kitabu cha Waebrania 4:1-2 "Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa. Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia."
Kutoka katika msitari 1b unaona neno "na tuogope." Kuogopa huku hakutufanyi tuende kwa Mungu kwasababu ya hofu! La hasha, bali Kanisa linaamshwa lisimame kuomba kwa rehema kwa kulia bila kuchoka ili kumletea Yesu wale waliofungwa. Na waliofungwa tunaona wakiandikwa hapo msitari 2b.
Kifungo hiki cha Waebrania 4:2b kimetokana na "imani", na wote tunaelewa kuwa imani chanzo chake ni kusikia maneno, lakini maneno haya ni wazi yametoka kwenye baraza la shetani, na ndiyo maana hayawezi kuchanganyika na maneno ya THAMANI YALETAYO UZIMA. Kwa hiyo hapa unaona INJILI inahubiriwa sana! Lakini shetani tayari amefanya mioyo ya hawa watu kuwa migumu kwa maneno aliyopandikiza ndani yao na Mungu anajua ndiyo maana analikumbusha KANISA kuingia GHARAMA kuona watu hawa wanafunguka.
Shida ipo ndani ya KANISA leo, limelala na limesahau wajibu wake. Limebakia likijihesabia haki na kuwa na ubinafsi ubinafsi tu, Yesu anaelewa kuwa siku moja kanisa linahitaji kupeleka HESABU ndiyo maana analiambia liogope, tukiangalia hali ilivyo leo pamoja na kwamba hakuna anayejua ni lini BWANA WETU YESU atarudi, lakini ishara zinaonyesha kuwa yu MLANGONI anapiga hodi. Tuamke na tufanye kazi tuliyoitiwa hawa mamilioni ya watu wanahitaji kufunguliwa!! Bila Kanisa hawana namna watatoka huko kwenye upofu == 2 Wakorintho 4:4 "ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu."
Kanisa Amka Amka Amka.
Barikiwa Mtumwa wa Bwana Yesu.
Nakubaliana nawe kabisa Revocatus kwamba kuna roho ya kujihesabia haki inayotufanya, hasa sisi tuliookoka, kuona kwamba sisi ndio tuna haki sana na mbingu.
DeleteUkweli ni kwamba, ni watu wachache sana ambao wanamkataa Mungu na kumkubali shetani huku wakijua kabisa. Asilimia kubwa sana ni kwa sababu ya vifungo vya rohoni vya giza ambavyo vinawafanya wasijitambue kuwa wako kwenye njia ya upotovu.
Lakini Kanisa lina mchango mkubwa sana sana sana wa kuwatoa humo kwa njia ya mahubiri na pia KUOMBA.
Sisi si wema kuliko wao hata kidogo.
Tomo wokovuni kwa neema tu si kwa haki yetu wenyewe.
Ubarikiwe brother.
Kaka naomba namba zko kwa 0762585005 barikiwa sana
ReplyDeletemasjid lharam ndipo ilipo kaaba na masjidi aqsa ndo hilo hekalu.kwa hiyo kwa hesabu zako hizo ilikuwa utoe 40 sio uongeze 40
ReplyDeleteKiomi, nimeona maoni yako. Asante kwa ufafanuzi. Nitayafanyia kazi. Mungu akubariki.
DeleteMbona sijaona kasoro yoyote hapo mimi maana hata hiyo miaka yenyewe sijui umesoma toka vitabu gan haujasema
ReplyDelete