Friday, April 5, 2013

Upande Mwingine wa Maisha Katika Nchi za Kiislamu




Hii si video ya kidini. Haielezei Ukristo wala Uislamu. Lakini ni video inayoonyesha maisha ya watu wa Irani ambayo ni nchi ya Kiislamu. Kwa jinsi ambavyo Uislamu unajinadi mbele ya ulimwengu, mtu ungefikiria kwamba watu wa nchi kama hizo wana furaha na utawala wa kidini wa nchi zao. Lakini je, hivyo ndivyo ilivyo?

Swali ni kwamba, kama hivyo sivyo ilivyo, viongozi wa nchi hizi wanamdanganya nani? Tawala ZOTE za kidikteta zina tabia moja – kufunika ubaya wao na kuonyesha mambo fulanifulani mazuri ili dunia idhani kuwa watu wake wana furaha; huku wakati huohuo wakiwazuia watu wake kujua mambo yanayoendelea kwenye ulimwengu nje ya nchi yao.

Unamdanganya nani? Kama unaonyesha picha ambayo katika hali halisi haiko hivyo, unayemdanganya ni mtu mwingine au unajidanganya wewe mwenyewe?

Manung’uniko na malalamiko ya watu katika nchi hizi yana maana moja kubwa kwamba – kutokana na ukweli kwamba hakuna mwanadamu anayependa kuamuliwa mambo yake - kuamuliwa aamini nini, kuamuliwa avae nini, kuamuliwa aende wapi, kuamuliwa asiende wapi, n.k., pale wanapokuja kugundua uhuru halisi ulio ndani ya Muumba wao na jinsi  Muumba wao (Yesu Kristo) anavyowathamini na kuwaheshimu, hapo ndipo wanapoachana na wakandamizaji wanaotumia maisha ya watu kwa faida ya wakandamizaji hao.

Unapoangalia na kusikiliza video hii, hiki ndicho unachoona na kutambua.
1.  Watu, na hasa kizazi cha vijana na wale waliozaliwa baada ya mapinduzi ya Irani, wamechoshwa na udikteta  wa watawala wa nchi hiyo.
2.  Watu wamechoshwa na imani kali ya kidini ambayo inawanyima uhuru na kuwafanya waishi maisha ya kitumwa.
3.  Watu wanafanya mambo kutokana na hofu ya kukamatwa na watawala na si kutokana na kumpenda Mungu au kupenda dini.
4.  Tawala za kidikteta zinawalazimisha watu kufanya mambo mbalimbali, si kwa faida ya watu hao, bali ni kwa lengo la kujionyesha kwa ulimwengu kwamba eti wananchi wanafurahia kuyafanya mambo hayo.
5.  Watu wanaamua kuasi dhidi ya tawala za kidikteta na kufanya yale ambayo mioyo yao hasa ndiyo inayoyataka.

Hakika kabisa, huko mbele tunakoelekea, Roho Mtakatifu anaenda kubomoa kuta zilizosimamishwa na watawala wa aina hii ili kwamba upendo wa Mungu utawale na kufungua mioyo ya wanadamu wanaoteseka chini ya makongwa ya kidini ya watawala madikteta.

Mwanadamu hawezi kushindana na Mungu aliyewaumba wanadamu kwa upendo mkubwa. Ni suala tu la majira na nyakati alizoziweka kutimia. Kibinadamu tunapoangalia hali ilivyo tunaweza kusema, “Nchi hizi haziwezi kamwe kubadilika.”

Lakini acha nikwambie kweli. Hata sasa kuna jambo la kushangaza sana linaloendelea kwenye ulimwengu wa Kiislamu ambalo si kazi ya mwanadamu, bali ni kazi ya Roho Mtakatifu mwenyewe!! Hakika kabisa!!

Misingi ya vifungo ndani ya ulimwengu wa Kiislamu inatikiswa na inaendelea kubomoka na Waislamu kwa mamilioni wanamgeukia Yesu Kristo – hata kule ambako hakuna hata mhubiri mmoja wa Kikristo.

Biblia inasema wazi:
Katika siku hiyo itakuwako madhabahu katika nchi ya Misri kwa Bwana, na nguzo mpakani mwake kwa Bwana.

Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa Bwana wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia Bwana kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi mwenye kuwatetea, naye atawaokoa.

Na Bwana atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua Bwana katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea Bwana nadhiri, na kuzitekeleza.

Naye Bwana atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa Bwana, atakubali maombi yao na kuwaponya.

Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hata Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri.

Katika siku hiyo Israeli atakuwa wa tatu pamoja na Misri na Ashuru, watakuwa baraka kati ya dunia;

kwa kuwa Bwana wa majeshi amewabariki, akisema, Wabarikiwe watu wangu Misri; na wewe Ashuru, kazi ya mikono yangu; na wewe Israeli, urithi wangu. (Isa 19:19 - 25).



Kama ilivyo kawaida ya Neno la Mungu, huwa halitanguki hadi yote yatimie. Hili nalo lazima litatimia! Ashuru ni eneo ambalo hivi leo ni nchi za Uturuki, Iraki, Irani na Syria.

Siku zinakuja ambapo hakutakuwako na Uislamu kabisa. Hii si kazi ya mwanadamu bali kazi ya Mungu mwenyewe aliyeumba mbingu na nchi na wanadamu ambao anawapenda mno mno.

Upinzani unaoonekana hivi sasa kana kwamba ni mkubwa sana utaendelea kuongezeka ili kwamba nguvu za Mungu zionekane wazi. Unapotazama kibinadamu ni lazima utasema, “Aa wapi! Yaani Irani au Saudi Arabia ije kuwa ni nchi inayomwamini Yesu Kristo kama Mungu na Mwokozi wa ulimwengu?!”

Kwa Bwana yote yanawezekana. Na kadiri upinzani unavyokuwa mkubwa kabisa, ndivyo utukufu wa Mungu unavyoonekana zaidi.

Unaweza kutazama pia HAPA

Pia HAPA.

Na HAPA.

Najua ni rahisi tu kusema hivi, "Ah, hakuna kitu kama hicho. Hizo ni propaganda tu za Wakristo. Hakuna Mwislamu wa kweli atakayeacha Uislamu na kuingia kwenye Ukristo. Wanaoacha ni wale wasioujua Uislamu sawasawa."

Watu wana mioyo. Na moyo wa mtu husema naye muda wote. Kila mmoja wetu anapambana na maisha haya huku tukijaribu kujaza utupu au uwazi fulani ulio mioyoni mwetu - lakini jambo hili haliwezekani kamwe. Baadhi wanajaribu pombe, wanashindwa! Wengine wanajaribu dawa za kulevya, uzinzi, biashara, na HATA DINI!!! Lakini yote ni kazi bure. Jibu ni moja tu kwa ajili ya moyo wa mwanadamu unaotafuta amani na furaha - YESU!!!

Njoo kwa Yesu leo.

Tafakari.

Chunguza mambo.

Chukua hatua.

6 comments:

  1. Nyinyi wakristo ni mashetani wakubwa, mnatia nguvu mikono ya watendao maovu. Sasa sikiliza neno la mungu linasemaje.
    '' Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.''
    (yer.23:14)
    Hizi ni dhama za utawala wa ufalme wa mungu ambao Yohana baptist na yesu walihubiri.
    3.2 "Tubuni, maana Ufalme wa mbinguni umekaribia."
    4.17 Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, "Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia!"
    10.7 Mnapokwenda hubirini hivi: `Ufalme wa mbinguni umekaribia.
    Unaposikia ufalme wa mbinguni, ni dunia kutawaliwa na amri za mungu!watu wanatakiwa wamwogope mungu.
    Ushetani wenu msilete ktk nchi za kislam. Ndoa za jinsia moja, mavazi ya nusu uchi, wizi, ulevi, madanguro, kuuwa maalbino,ujambazi uko uko!!!
    Halafu tambua ya kwamba, kwa uwingi wa wahumini, wakristo ni zaidi ya waislam na kadri miaka inavyoendelea idadi ya waislamu inaongezeka kwa nguvu zote kuliko imani yeyote duniani. Leo hii nchini uingereza inakadiriwa ifikapo mwaka 2030 litakua taifa la kiislam. Uwanja wa mpira wa arsenal (emirate) ni marufuku kupepea bendera ya uingereza kwa sababu ina msalaba.
    Ndugu yangu tunapotafuta ukweli wa mambo inabidi tujifunze kutoka kwa mungu au manabii. Tusikurupuke na kuwadharau wale waliotumwa na mungu badala yake tunakumbatia maagizo ya watu wa kawaida.
    Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; (Mt 11:29)
    Sasa sikiliza mafundisho ya Yesu. Usije ukawalaumu bure waislam.
    `5.17 "Msidhani ya kuwa nimekuja kutangua Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha.
    5.18 Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya Sheria itakayoondolewa,mpaka yote yametimia.
    5.19 Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katikaUfalme wa mbiguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine,huyo atakuwa mkubwa katika Ufalme wa mbinguni.
    5.20 Ndiyo maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa Mafarisayo na walimu wa Sheria, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
    5.21 "Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: `Usiue! Atakayeua lazima ahukumiwe.`
    5.22 Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwitandugu yake: `Pumbavu` atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.
    5.23 Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe,
    5.24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi ukatoe sadaka yako.
    5.25 "Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani, kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimuatakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
    5.26 Kweli nakwambia, hutatoka humo mpaka umemaliza kulipa senti ya mwisho.
    5.27 "Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: `Usizini!`
    5.28 Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazama mwanamke kwa kumtamani, amekwisha zini naye moyoni mwake.
    5.29 Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, ling`oe ukalitupe mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako,kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu.
    5.30 Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali. Afadhali zaidi kupoteza kiungo kimoja cha mwili, kuliko mwili wakowote uende katika moto wa Jehanamu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni jambo jema kwamba unaiamini Injili ya Bwana Yesu, Ibra, hata kama huwa unachambua sehemu zile ambazo, ama unaona kuwa zinaendana na Uislamu, au unaona zinakusaidia kuwakemea Wakristo wale ambao unaona wanapingana na Uislamu.

      Sasa, huyo Yesu unayemnukuu mara kwa mara anasema hivi: ... shetani akimtoa shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje? (Mt 12:26). Kama Wakristo tu mashetani, iweje tunamkemea shetani kwa Jina la Yesu na anatimua mbio?

      Lakini unasemaje kuhusu wewe ndugu yangu Ibra, unapoingia kwenye swala huwa unageukia kusalimia kushoto na kulia; huwa unamsalimia nani? Kama sikosei, je, huwa hamsemi kuwa kulia kwako kuna malaika na kushoto kwako kuna jini? [sina uhakika ni upande gani ni wa jini na upi ni wa malaika]. Na je, kushoto kwako si ndio kulia kwa mwenzio? Je, huyo wa kulia kwako ambaye wewe unamwita malaika, si ndiye ambaye mwenzako anamwita jini? Au je, jini na malaika wanaweza kukaa nyumba moja ya ibada kumwabudu Mungu yuleyule? Of course najua utasema kuwa kuna majini wazuri na wabaya. Hilo tunawaachia ninyi na yeyote anayependa kutafakari na kujiuliza. Je, si ninyi mnaosema kuwa majini ni ndugu zenu?

      Wakristo si mashetani bali ni maadui wa mashetani, na kwa Jina la Yesu Kristo, Mungu wa Miungu, shetani anashikishwa adabu. Kwetu sisi majini ni mashetani; na mashetani ni majini. WOTE LAZIMA WAPIGWE KWA JINA LA YESU; NA HICHO NDICHO KINACHOTENDEKA.

      Sasa, najua hatuwezi kukubaliana katika haya, lakini tumwachie kila msomaji aamue mwenyewe nafsini mwake kama kweli Wakristo wako karibu na ushetani au wako mbali nao.

      Nuru ya Bwana Yesu ikuangazie moyoni mwako, Ibra, katika Jina la Yesu.

      Delete
  2. Mr.James mimi nadhani wewe hujui Ushetani. SHETANI, ni yeyote aendae kinyume na matakwa ya mungu. Unaposikia Jina la shetani, maana yake ni muasi. Ukisikia kuasi, ni kupinga. Ukisikia kupinga ni kwenda kinyume na matakwa au taratibu zilizowekwa.
    Mr.James, sisi waislamu tunavikubari na kuviamini vitabu vyote vya mungu tulivyoorozeshewa kwenye kitabu kitukufu cha Al-quran (taurat, zaburi, injili n Al-quran).
    Lakini kwa bahati mbaya sana, vitatu vya mwanzo haviko katika hali yake ya asili. Mkono wa waandishi umekorofisha kila kitu.
    Kwa hiyo, neno likisema kweli sisi waislam tunaamini kwamba hapo imesema kweli, na likisema uongo tunaamini pia kwamba hapo pana uongo. Hii ni kutokana na kuingizwa na fikra za kibinadamu.
    Ninavyojua mimi, agizo lolote kutoka kwa mungu lafaa kutekelezwa. Usipotekeleza wewe unakuwa shetani.
    Vigezo kama hivi, vya kupinga au kwenda kinyume na matakwa au maagizo ya mungu vinawangukia upande wenu ndio maana mimi nawaita nyie Mashetani.
    Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu shetani aliyomuasi mungu alintumia paulo kuwadanganya watu ili waende kinyume na matakwa ya mungu. Kwa mfano:
    Yesu ktk Mat5:17-20 anasema yeye hakuja kutengua sheria na sheria hiyo haitatenguka mpaka siku ya mwisho.
    Paulo ktk waef 2:15 anadai sheria imetenguka.
    Kwa mistari hii nani wakumwamini? Jee! Yesu atakuwa muongo alipodai kwamba sheria haitatenguka mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka?

    Mw 17:9-26 Êxodus 12:48 Lv 12:3, mungu ameagiza watu wote watahiriwe. Ni amri kutoka kwa mungu.
    Paulo anasema nini katk wag 5:2 ''Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno.''

    Yesu amesema ktk mat 7:21-23
    21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
    22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
    23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
    Paulo wa tarso anasema vipi ktk rum 3:28 28 Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.
    Sasa nani kati ya hawa watu ni mkweli? Ndugu yako kuwa na imani tu bila ya matendo huwezi kupata uzima wa milele. Hizo ni imani ya kishetani. usidhani ya kwamba shetani hamjui mungu, shetani anamjua mungu na kumuogopa kabisa ila hatekelezi matakwa yake.
    Ufalme wa mungu unafanana na tawala zilizojaa hapa duniani, mfano wewe ni mtanzania, tanzania kuna katiba ambayo inabidi ifuatwe kwa mujibu wa sheria sasa ikatokea wewe ukazipinga zile sheria na kuziasi, moja kwa moja wewe ni shetani wa nchi na huku ungali unatambua ya kuwa wewe ni ntanzania halisi.
    Sisi waislam tunapotaka kuwanza kufanya jambo lolote tunaanza na kumlaani shetani asituingilie katika shughuli zetu kwa sababu shetani anakuwepo maeneo yote ili awapoteze binadam.
    Sasa wewe umemuona jirani yako wa upande wa kulia na kushoto, na yule anaeswali akiwa peke yake jirani anampata wapi?
    Sisi waislam siku zote tunatambua ya kwamba Nyie mnaejiita wakristo sio watu wa kristo, mlichofanya nyinyi, shetani mwenzenu paulo, kaliteka jina la yesu na kulipachika katika miungu ya kirumi, ili apate wafuasi wengi ndo maana akasema kuwambia warumi ktk rum 1:8 imani yenu inahubiriwa dunia mzima.
    Kwa kutambua hilo, hakuna hata agizo moja la yesu mnalolifuata, kama mnalo nitajie.
    Swala la majini waliosikia quran inasomwa wakaamini. Sasa basi kama hawa ni ndugu zetu, na nyie pia ndugu zenu si watakuwa wa kundi ambalo hawajaamini quran?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwamba shetani ni mtu yeyote anayeenda kinyume na mapenzi ya Mungu? HAPANA! Hii si maana ya kimaandiko. Shetani ni shetani na mwananadamu ni mwanadamu.
      ..................

      Kuhusu suala la Torati, Ibra, tatizo moja kubwa kwako linaloonekana ni kwamba hauelewi hasa maana ya maneno ya Yesu anaposema: sikuja kutangua torati.

      Na wala hasemi kuwa sheria haitatenguka mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka kama unavyosema wewe.

      Jambo hili nilishalieleza kwa mapana na kikamilifu vilevile huko nyuma. Lakini si vibaya kurudiarudia wakati mwingine, maana nayo ni njia mojawapo ya kumfanya mtu aelewe.

      Sasa basi, hebu tusome maandiko hayo kwa ukamilifu: Imeandikwa hivi: Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati na manabii; la sikuja kutangua, bali kuitimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu nan chi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. (Mt. 5:17-18).

      Wewe Ibra pamoja na Waislamu mnadhani kuwa Yesu anasema kuwa:” Msifikiri nimekuja kuwaambia muache kutimiza sharia za torati. Hapana, hadi mbingu zitakapoondoka, sharia zote katika torati ni lazima zitimizwe kama zilivyo.” Haya ndiyo mawazo yenu juu ya andiko hili.

      Hii KAMWE si maana ya andiko hili. Kile ambacho Yesu anasema ni kinyume chake kabisa. Torati ina maagizo pamoja na hukumu kwa yeyote ambaye anavunja hata agizo moja. Na kwa sababu wanadamu WOTE ni wenye dhambi, kwa maana nyingine ni kuwa, wanadamu wote tulikuwa chini ya hukumu ya Mungu. Tulikuwa tumehukumiwa kifo (mauti) – maana imeandikwa kwamba: Mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23).

      Kile ambacho Bwana Yesu anasema katika maandiko haya ni kuwa: Msifikiri kuwa Mungu atafumba tu macho na kusema, “Kwa kuwa mmetenda dhambi, basi nawasamehe tu. Njooni tu muingie mbinguni. Msifikiri ya kuwa nimekuja kutangua (kubatilisha) hukumu za torati. La hasha! Kila hukumu katika torati yote ni LAZIMA ilipwe. Hata nukta moja haitaachwa HATA YOTE YATIMIE. Kama umetenda dhambi mia, ni lazima zilipwe! Kama umetenda dhambi moja, ni lazima ilipwe! Hakuna kutangua hata amri moja!”

      Ndipo sasa Yesu alipoinuliwa msalabani akasema neno moja kubwa linalomaliza kila kitu. Alisema, “IMEKWISHA.” (Yoh. 19:30).

      Yote ambayo torati ilikuwa inayadai, Yesu ameshayatimiza KIKAMILIFU!! Kwa hiyo, badala ya kung’ang’ana na sheria ambazo kwa mwanadamu hazitimiziki, sasa tunaishi kwa neema na imani katika Mwokozi Yesu aliyetufia msalabani.

      Lakini wewe ndugu yangu,Ibra, hangaika uhangaikavyo na sheria zako zinazokutaka usile, usiguse, kunawa, kufuga ndevu, n.k., lakini mwisho wa yote ni kushindwa vibaya! Na licha ya hivyo, hapo unahangaika tu na mwili ambao utaoza na kuishia mavumbini, vipi mbona umetelekeza roho ambayo itadumu milele?

      Na kila mara nawauliza swali hili ambalo huwa hamjibu: Kama kunawa mwili ni sehemu ya ibada na kunakusaidia kwenda mbinguni, je, mwanao akiwa mwizi au mwongo, au mzinzi, utampeleka bafuni akaoge ili wizi wake uishe?

      Of course mnajua kuwa jibu ni hapana. Na sababu ni kuwa, wizi au uongo au uzinzi, haukai mwilini bali ni rohoni. Kwa hiyo, uoshaji wake unafanywa kwa aina nyingine kabisa ya maji - ya kiroho. Kunawa na kuoga kama sehemu ya ibada ni kupoteza wakati. Vivyo hivyo, kushika torati kimwili ni kupoteza wakati.

      Delete
    2. Ukubali,
      Usikubali
      YESU Atabaki kua ni BWANA WA MABWANA NI YEYE YULE YULE JANA,LEO NA HATA MILELE unapinga sababu ya kiburi cha uzima ila siku nafsi ikitengana na mwili ndipo utakiri kwa kinywa chako mwenyewe na kuambiwa hukumu imekwisha tolewa hakuna msamaha île upande sa kaburi....

      Ninaliheshimu,
      Ninalisifu na
      Kulitukuza jina
      Lake Takatifu
      AMEN.

      Delete
  3. MUNGU alie hai awape kufunguka fahamu wasioelewa ,waelewe na maandiko.
    Shetani mjinga sana,anajaribu kuficha ukweli kwa wanadam makin kashasahau kuwa anaeshndana nae ndie anaejua yote ubarikiwe mtumish James kwa kunijenga Roho yangu,
    Ubarikiwe pia mtumish Ibra maana ipo siku utamuona KRISTO kwa macho ya nyama kabla hujamaliza muda wako wa kukaa duniani.
    Kumbuka tu kuwa kuna mlango mmoja tu wa kuingia mbingu ya kweli ya kudumu..ambayo ni YESU KRISTO yohana 14:6.

    Nawapenda

    ReplyDelete