Tuesday, February 19, 2013

Maisha ya Wanawake Katika Nchi za Kiislamu





Mwanamke wa Saudia aliyeamua kuumwaga
moyo wake wote


Ni jambo lililo wazi kwamba wanawake katika nchi za Kiislamu wananyanyaswa kupita kiasi. Maisha yao hayana uhuru wala amani kwa kuwa sheria za dini yao zinawakandamiza wao na kuwapendelea wanaume. Hata hivyo, baadhi yao wanatambua hali hiyo na wanapambana kujaribu kuibadilisha. Lakini, ni wazi pia kuwa mapambano yao hayo hayawezi kuwasaidia sana kwa kuwa huko ni sawa na kusema Quran ibadilishwe. Je, hilo linawezekana kwa nchi hizo? Maana tatizo si wanaume au serikali; tatizo ni maagizo ya Mungu wanayemwabudu.


Katika video hiyo hapo juu, tunamwona mwanamke mtangazaji wa kituo kimojawapo cha TV kule Saudi Arabia, akimhoji mwanamke mwingine, Bi. Buthayna Nasser, ambaye naye ni mtangazaji kwenye kituo cha TV. Mahojiano yanahusu mjadala uliokuwamo kati ya wanazuoni wa Saudia juu ya wanawake kuonyesha nyuso zao kwenye TV ya Saudia.


Bi. Buthayna Nasser anaonyesha jinsi anavyokerwa sana na unyanyasaji wanaotendewa wanawake na anaamua kusema yote yaliyo moyoni mwake. Kusema kweli maneno anayoongea ni maneno mazito yanayobainisha kilio kikubwa kilichomo, si tu ndani ya moyo wake, bali ndani ya wanawake wengi katika nchi za Kiislamu. Kama angejua tu kuwa uhuru kamili uko ndani ya Yesu Kristo, basi angeelewa ni wapi pa kukimbilia. Bwana Yesu na amsaidie mama huyu pamoja na wengine ili siku moja waweze kuijua njia ya kweli yenye uhuru na amani kamili.

Yafuatayo ni mahojiano hayo:


****************

Mtangazaji:
Je, kuonekana kwa wanawake kwenye TV kunaenda kinyume na sheria za Uislamu?


Mwanamume:
Tunachotaka ni wanawake kudhihirisha utamaduni wao na uwezo wao wa kufikiri. Tunachotaka ni wanawake wachangie kwenye kuleta maendeleo ya jamii. Lakini mwanamke anayesisitiza aonekane kwenye TV, anakuwa anasisitiza juu ya kuonekana kwa mwili wake. Kwa nini tunakuwa hatuwatendei haki wanawake kwa kusema kuwa tutanufaika tu kutokana na wao kwa kuwafanya waonekane mbele za watu wakiwa namna hii?


Mtangazaji:
(Kwa Bi. Buthayna). Ulijisikiaje uliposoma juu ya mjadala ndani ya Baraza la Shura la Saudi Arabia kuhusiana na kuonekana kwa wanawake kwenye vyombo vya habari?


Bi. Buthayna:
Kwa kweli, nilijisikia kutotendewa haki na nilijisikia hasira sana (indignation).


Mwanamume:
Juu ya suala la hijab, wanazuoni wote wa kidini wanakubaliana kwamba,  kama kuonyesha uso wa mwanamke kunaweza kusababisha vishawishi na mambo mengine, basi ni marufuku. Mbali na hivyo, hata pale waliporuhusu kuonyesha uso wa mwanamke, waliweka vizuizi  katika hili. Hata Shekhe Al-Albani alifanya hivyo. Mwanamke haruhusiwi kuonyesha shingo au nywele zake. Haruhusiwi kuonekana akiwa na vipodozi au mapambo ya vito (jewelry). Wasomi wote wa kidini wanakubaliana juu ya hili.


Bi. Buthayna:
Mheshimiwa, ninapoonekana kwenye TV, na ninapodai haki yangu ya kufanya wajibu wangu kwenye eneo hili la kiweledi (professional), ninadai kwamba uso wangu, ambao ni sehemu ya utambulisho wangu, lazima uonekane. Sitakubali kwa namna yoyote ile utambulisho wangu ufutiliwe mbali. Hawa ni akina nani ambao wanataka kuamua jinsi mimi ninavyotaka kuenenda? Kwa nini mnaniona mimi kuwa sistahili eti kwa sababu tu mimi ni mwanamke? Kwa nini kila wakati iwe ni sauti ya mwanamume inayoamua mimi nienende namna gani?

Mungu aliniumba mimi nikiwa sawa na ninyi kuhusiana na wajibu, hukumu na thawabu. Mnapofunga, nami ninafunga. Mnaposwali, nami ninaswali. Mkiiba, mikono yenu inakatwa. Na mimi nikiiba, mkono wangu unakatwa. Huu ni ushahidi mkubwa kabisa kwamba mimi sina tofauti na ninyi. Ninajua ninachokifanya. Ninajua namna ya kulinda heshima yangu. Walid alishangaa kwamba, mimi kama mtangazaji, nawezaje kuisema jamii ya Saudia kama iliyotiwa kasumba (brainwashed). Sishangazwi na Dk. Walid.

Tangu mtu anapokuwa na umri wa miaka sita au saba, tangu shule ya msingi hadi sekondari ya juu, anapokuwa na umri wa miaka ipatayo 18, na hata baadaye tunapoenda kwenye vyuo vikuu, kazi yetu ni kukariri, kukariri, kukariri tu.

Yeyote anayejaribu kubisha au kuhoji juu ya jambo lolote anaitwa na kuambiwa aombe msamaha kwa Allah. Anaambiwa kuwa kuuliza maswali kutampeleka jehanamu. Nyie mnaowatishia watu na jehanamu, ndio mliowaletea jehanamu hapahapa duniani! [Maelezo ya blogger: Bwana Yesu aliwaongelea viongozi wa dini washika sheria akisema kwamba: Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao. (Mathayo 23:4)] 

Mmepiga marufuku vitabu vyenye maarifa mbalimbali. Mmezizuia akili za watu kufanya kazi, kufikiri, kulinganisha na kuchagua mambo, licha ya kwamba ni Mungu ndiye aliyewapa akili hizohizo ili waweze kuzitumia kuchagua kati ya Mbingu na Jehanamu.

Bwana wetu alimheshimu mwanadamu kwa kumpatia uhuru wa kuchagua njia yake kwenye maisha haya ambapo matokeo yake yataonekana kwenye ulimwengu ujao. Matendo hupimwa kutokana na nia, kama alivyotufundisha Mwalimu aliye Mkuu; nia njema huchochea tabia.

Ndiyo mheshimiwa, tunakuwa ‘brainwashed’ kila siku, kupitia shuleni na kupitia kwenye madrasa za kukariri Quran.

Kila mara tunadai kwamba shule hizi zisiwe mahali pa kukariri, bali ziwe ni mahali pa kufundishia kwa ajili ya kutafsiri, na mahali pa kujifunza ufunguo wa lugha ya Kiarabu, ambayo ndiyo siri ya kuelewa Quran na maajabu yake. Yatosha kukariri kama  kasuku. Ndiyo, tunakuwa ‘brainwashed’, isipokuwa kwa wachache ambao Mungu amewaepusha na hilo.

***************


Haya ndugu msomaji wa blog hii. Naamini umemsikia Bi. Buthayna anavyoeleza kwa uchungu jinsi ambavyo baadhi ya wanadamu wanaweza kuwafanya wengine waishi maisha ya mateso hapa duniani. [Kumbuka kwamba huyu mwanamke si Mkristo; na wala haonyeshi dalili ya kwamba ana nia ya kuacha Uislamu.] 


Kila mtu ana maisha ‘mamoja’ tu! Lakini kuna watu ambao wanawapokonya wenzao maisha hayo ambayo ni ya thamani sana. Kisha wanawalazimisha kuwaza, kusema, na kutenda mambo ambayo wale wanaolazimishwa hawayataki. Ama kweli dini ni mzigo hasa! Unawalazimisha watu kushika dini si kwa sababu unataka waende mbinguni, bali ni kwa lengo la kujenga heshima ya jamii yako na heshima ya hiyo dini yako. Unachojali wewe ni hiyo dini yako iwe na 'jina' mbele za walimwengu 'at the expense of people's invaluable lives!!" 


Nadhani umeona alichosema huyo mwanamume hapo juu. Amesema: “Tunachotaka ni wanawake kudhihirisha utamaduni wao na uwezo wao wa kufikiri.” Yaani maisha yangu aliyonipa Mungu yatumike kuendeleza utamaduni?


Ndugu zangu, maisha ni zaidi ya utamaduni. Maisha ni zaidi ya dini. Maisha ni zaidi ya kila kitu.


Yesu Kristo anamwita kila mwanadamu aje apokee uhuru, furaha, amani, na hatimaye uzima wa milele baada ya ulimwengu huu.


Je, wewe uko kwenye dini kwa ajili ya kupata uzima wa milele au kwa sababu ya kulinda heshima ya dini hiyo? Je, wewe unampenda Mungu au unapenda dini?

Unaweza kusoma zaidi hapa

Usiache pia kusoma hapa.

Tafakari.

Jihoji.

Jichunguze.

Chukua hatua.


No comments:

Post a Comment