Thursday, October 19, 2017

Biblia haijapotoshwa bali Waislamu ndio wamepotoshwa


Mungu wa Waislamu anasema:

Enyi mlio amini! Muaminini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha juu ya Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha kabla yake. (Al-Nisa 4:136)

Vilevile anasema:
Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. (Yunus 10:94).

Anasema kuwa aliteremsha vitabu kabla ya quran.
Tunajua kuwa anadai kwamba vitabu hivyo ni Taurati, Zaburi na injili.

Tuchukulie kwamba anachosema ni kweli.


Alipokuwa anatamka maneno haya kwenye mwaka 600 Baada ya Kristo, Agano laKale la Biblia tayari lilikuwa na umri wa MAELFU ya miaka; na Agano jipya lilikuwa tayari na MAMIA ya miaka.

Yafuatayo ni maswali muhimu ya kujihoji kwako ndugu yangu Mwislamu na kupitia hayo, utatambua kama kweli Biblia imepotoshwa au ni wewe umepotoshwa:

Mungu wako anasema kwenye Al-Nisa 4:136 kwamba muaminini yeye na VITABU alivyoteremsha KABLA (ya quran).
Hapo ilikuwa ni miaka 600 BAADA ya Yesu.
Hapo Biblia ilikuwapo tayari.


SASA MASWALI YANGU KWAKO NI HAYA:

1. Ile Yeremia 8:8 mnayopenda kuitumia kana kwamba kuthibitisha upotovu wa biblia ilishakuwapo au ilikuwa bado haijaandikwa? Wakati Mungu wenu akionyesha imani thabiti kwa vitabu hivyo, hiyo Yeremia 8:8 haikuwapo?

2. Kama tayari kwenye mwaka 600 BK Biblia ilishapotoshwa, nay eye akawaambia mkiwa na shaka muwaendee watu wa kitabu, je, alimaanisha muende ili mkapotoshwe?

3. Au alimaanisha alimaanisha wakafufuliwe akina Musa na Mitume wa Yesu ndipo muwaulize kwa habari ya mashaka yenu?

4. Lakini kama alimaanisha Wakristo na Wayahudi wa nyakati za Muhammad, je, unatambua kuwa hii maana yake ni kuwa, HADI MWAKA 600 BK biblia ilikuwa iko sahihi? Vinginevyo angewezaje kuwataka muende kwenye maandiko yaliyopotoshwa?

5. Na kama Biblia basi imepotoshwa (kama mnavyodai), je, unatambua kuwa jambo hilo linatakiwa LAZIMA liwe limefanyika BAADA ya mwaka 600 BK? Maana kabla ya hapo Biblia ilikuwa iko sawa.

……………
Sasa, haujui ya kuwa zipo Biblia LEO ambazo ni za tangu KABLA ya 600 BK?

Niishie hapo ili niwaachie wenye hekima wahukumu.
Ukipenda kudanganywa, ni wewe tu.
Yesu PEKE YAKE ndiye Njia, Kweli na Uzima.

Tafakari.
Chukua hatua.

No comments:

Post a Comment